FUTURE HUNTER
JF-Expert Member
- Apr 30, 2018
- 2,022
- 2,589
Hivi kuna hatua gani zinatakiwa kupitia ili kuvikataa hivi vyama vya wafanya kazi?
Penye ukweli uongo ujitenga!Kwa niaba ya Wafanyakazi wote Tanzania, nachukua fursa hii kumpongeza sana Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona na kusikia kilio cha Wafanyakazi.
Niwaombe sasa Viongozi wa Vyana vya Wafanyakazi kutumia hii Momentum aliyoianzisha spika tuone matamko na kauli za kumuunga mkono spika.
Ukiisoma sheria ya kuunganisha mifuko, kama unazo akili ndogo za kutosha kutambua nyeupe na nyeusi basi hutapeleja lawama kwa wabunge pekee (ingawa bado wanalaumiwa kidogo) kwani utaona kila eneo lililotaja fao fulani, sheria inaeleza kuwa kanuni (kikokotoo) kitakuwepo kwenye kanuni zitakazotungwa na Waziri mwenye dhamana.
Pamoja na ukweli huo, niwaombe Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi kuanzia Jumatatu muanze kutoa kauli za kumuunga mkono Spika na kueleza nini hasa hitaji la Wafanyakazi lakini pia mukiangalia mustakabali wa mifuko yenyewe ili isitokee wafanyakazi wakataka kulipwa kiasi kikubwa cha mafao huko mifuko ikishindwa hata kujiendesha na kudumu kwa vizazi vingine.
Ushauri wangu wa upande wa Serikali ni huu: Serikali yangu sikivu, huu ni muda muafaka wa Serikali (wataalamu) kukaa na wawakilishi na viongozi wa vyama vya wafanyakazi hasa vyama vya watumishi wale ambao hasa wameguswa na hizi kanuni ba kuweza kufanya actural valuation ya mifuko kwa pamoja na kuhakikisha wafanyakazi kupitia wawakilishi wao wanaelewa thamani hasa ya mali za mifuko na uwezo wa mifuko katika kujiendesha na kulipa mafao wastaafu waliopo na wanaokendelea kustaafu.
Hivi sasa Serikali hamueleweki kutokana na ukweli kwamba, haya mambo mumeyafanya sirini kana kwamba Wafanyakazi hawataelewa na wakielewa hawatapinga!!! That was very wrong!!! Kutana na wafanyakazi na ujadiliane nao na uhakikishe wameelewa na wanakuwa sehemu ya maamuzi mtakayofikia.
Namalizia kwa kumpongeza tena Mhe spika kwa maneno yake ya busara juu ya sakata hili na niwaombe tena viongozi wa vyama, mpeni Spika na wabunge ushirikiano na pia Jumatatu kila mmoja kwa staili yake toeni kauli za kumpongeza spika na wabunge na muwaombe wabunge hasa wa Chama Tawala walichukulie uzito suala hili kwani limegusa ndani sana katika mtima wa Mfanyakazi.
Nawasilisha
Hao ni mavi sio viongoziOngeeni kwa busara basi, na acheni kutumia maneno ya kejeri na dharau kwa viongozi.
Halafu sio wafanyakazi wote wanaoupinga huu mpango wa mafao.
Kumbuka hao pia wana haki yao ya kuupata huu mpango.
Pole sana ndugu.Hao ni mavi sio viongozi
Kuna suala hapa ambalo ni very technical! Unajua Wafanyakazi wa Tanzania wapo katika makundi mawili linapokuja suala la Mafao ya Uzeeni. Kuna wale waliopo katika Sekta binafsi ambao wanatumia mfuko wa NSSF na wapo Watumishi wa Umma.Salaam TUCTA ukiwa mwavuli wa vyama vya wafanyakazi TALGWU, TUGHE, CWT, RAAWU, TUICO, nk
Salaam hizi nazituma kwenu nikiwa sehemu ya jamii ambayo kupitia makato ya 2% ya kila mwezi mnazichukua pasipo kutimiza wajibu wenu
Naomba kufahamu fedha mnazowakata wafanyakazi kila mwezi mnazitumia kufanyia shughuli ghani?
Je mlishirikishwa wakati wa kutunga sheria na kanuni mpya za mafao? endapo hamkushirikishwa kwanini mmekaa kimya katika hii sintofahamu na mkanganyiko wa kanuni mpya zenye lengo la unyonyaji kwa mfanyakazi maskini wa nchi hii??
Endapo mlishirikishwa tungependa kujua mlitoa mchango gani kwenye vikao? au mnaridhika na hali ilivyo sasa?
Mnaposema kwa mtumishi anayepokea 1,000,000 kwa mwezi aliyefanya kazi miaka 35 kwa kikokotoo cha zamani mkupuo anapokea 71,612,411 na mafao ya kila mwezi ni 371,847 halafu kwa kujisifu mnasema kikokotoo kipya mkupuo anapokea 35,806,205 na mafao ya mwezi ni 557,771 eti kuna ongezeko lakiasi cha 185,924 mnatumia vigezo gani?
Mbona hamtolei mfano mtumishi mwenye kima cha chini anapokea kiasi gani? Je endapo huyo mtumishi atafariki miaka 3 baada ya kistaafu na wategemezi wake kulipwa hiyo miaka 2 hicho kiasi kinachobaki mnakipeleka wapi?
Je mnadhani bado tunahitaji kuwa na vyama vya wafanyakazi ambavyo vipo kwa maslahi ya waajiri badala ya wafanyakazi wenyewe?
JITAFAKARINI SANA NA CHUKUENI HATUA KABLA HII FAMILIA YA WANUONGE HAIJAAMUA KUCHUKUA HATUA
Nawewe ni wale wale wa Lumumba...mtu kama kaitumikia serikari takribani miaka 30 na mzigo wake maximum ni 80 au 90 million apewe yote....huu ni udictator wa live wa kupora fedha za wastafu..hii haikubaliki mzee serikari yako haina nia njema kabisa na wastafuKuna suala hapa ambalo ni very technical! Unajua Wafanyakazi wa Tanzania wapo katika makundi mawili linapokuja suala la Mafao ya Uzeeni. Kuna wale waliopo katika Sekta binafsi ambao wanatumia mfuko wa NSSF na wapo Watumishi wa Umma.
Julai 2014 SSRA walileta kanuni mpya kwa mifuko yote na mbayo ndiyo sasa imerejeshwa tena ya 1/580, 12.5 na 25%. Kusema ukweli hali iliyokuwepo kwa Wanachama wa NSSF kabla ya ujio wa kanuni hizo ikikuwa mbaya kuliko neno lenyewe MBAYA!!! Yaani Mfanyakazi aliyetumikia Taifa lake kwa Miaka 30 na ambaye amestaafu akiwa na Mshahara wa Tsh. 1,000,000.00 alilipwa mafao ya Mkupuo kiasi cha Tsh. 12,600,000.00 na alipata malipo ya kila mwezi ya Tsh. 525,000.00
Baada ya kuanza kutumika kwa kanuni za mpya Julai 1, 2014 Wastaafu wa NSSF wakawa wanalipwa pensheni bora zaidi. Mfano huyu aliyekuwa amepokea Tsh 12,600,000 kama mafao ya Mkupuo analipwa Tsh. 23,275,862.07 sawa na ongezeko la 84.73%! na malipo ya kila Mwezi anapokea Tsh. 465,517.24 sawa na punguzo la 11.33% pekee ikilinganishwa na kanuni ya zamani!
Kwa maelezo hayo hapo juu, ni vyema Watanzania wote kukaelewa haya yafuatayo:
1. Haitowezekana Wafanyakazi wanachama wa mfuko wa NSSF wakaungana na wenzao wa Umma (Waliokuwa PSPF na LAPF) katika kupinga ujio wa hii kanuni mpya. Wao tayari ujio huu uliwatoa Jehanam na kuwafikisha Duniani. Sasa waungane na wenzao waliokuwa mbinguni na wanalalamikia kushushwa duniani!!!? Hiyo kiuhalisia haitawezekana!
2. Hata kama vyama vya Wafanyakazi ni bora kiasi gani, katika hali kama hii niliyoeleza katika Na. 1 hapo juu, hawataweza kupata sauti ya pamoja ya Wafanyakazi wa Tanzania.
3. Jambo kubwa hapa ni kuangalia ni namna gani Serikali itaweza kuelimisha Wafanyakazi wa Umma kwa kuwaeleza kwa uwazi sababu hasa za kuleta vikokotoo hivi kwenye scheme ya Utumishi wa umma na siyo vinginevyo!
Taifa kwa sasa linahitaji watu wenye busara sana kuweza kutuliza hali iliyopo kwa wafanyakazi kwani kila kona ya nchi wanaonekana (Watumishi wa Umma) wakiwa katika msononeko mkubwa na kuvitupia lawama vyama vyao. Hii haitasaidia, jambo la msingi ni Serikali irejee katika meza ya duara na Wawakilishi wa wafanyakazi au kujikita katika kutoa elimu ya sababu za uwepo wa Kanuni hizi ili wafanyakazi waondokane na mawazo waliyonayo hivi sasa na waelewe kuwa pamoja na kupunguzwa kwa % ya malipo ya mkupuo, lkn Serikali inayo sababu za msingi za kutaka kukuza mfumo endelevu wa hifadhi hasa wakati huu ambao tayari viashiria vilishaonesha kuwa PSPF na LAPF zilikaribia kufa.
Ni vyema wafanyakazi tukaacha mihemko na hasira zinazochanganyika na hisia za kisiasa na kuangalia dhamira ya Serikali kabla ya kulaumh kwa hili lililotokea.
Wanaogopa kuitwa ikuluniinaniumiza sana viongozi tuliowachagua wamekaa kimya wakati serikali ikiwapora watumishi wake penshen wasiostahili.. hivi hakuna hata kukeme au kuilaani kinachoendela hakuna. wote wamekaa kimya. kuna haja gani ya kuwa na vyama vya wafanyakazi tz?
unastaafu badala ya kupewa penshen ya 100% badala yake unapewa 25%? kemeeni hili jambo itisheni midahalo, haya ni machungu yanayotupata