Wajue matapeli kumi mahiri waliowahi kuisumbua dunia

Bitoz

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
30,823
126,536
Umewahi kuombwa assist na msela fulani hivi aitwaye Rainyundo ? kama tayari kausha tu aisee ..........
Jamaa alikuwa na marafiki wengi humu JF Ila ujanjujanja umemponza na huo ndo umekuwa kama mwisho wa ID yake

Tapeli ni tapeli tu haijaishi iwe alidanganya,alikopa,alitoa tiba feki, n.k .....
Wazee wengine matapeli wa humu JF wanaotajwatajwa sana ni Mzizi uliokauka i,Kelvin Isaisa,na Mtu mwepesi
Kitaifa tunaye Dr Manyaunyau
Mwizi ni mwizi tofauti kati ya tapeli na jambazi ni kwamba tapeli anatumia akili na maneno matamu kudanganya watu wakati jambazi anatumia nguvu na silaha kupora
Sasa tuwaone wazee kumi maarufu wa kupiga assist enzi hizo yaani matapeli/wadanganyifu
Naandika kiufupi zaidi maana nikiandika kinagaubanga tutakesha bure

..........................................................................
10/Bernard Cornfield
104559050f80cdcb46200dc598138f15.jpg
8428263fba48feb9841c617164bb96a9.jpg


Alizaliwa mwaka 1927

Alikuwa mfanyabiashara na mzee wa bima aliyewekeza Marekani...

Alizaliwa nchini Uturuki na alipoingia Marekani akaanza kifanya kazi za kijamii Social Worker hapo ndio akatengeneza jina lake kama msela Rainyundo alivyoanza kwa kutengeneza marafiki humu Jf kea kumchangamkia karibu kila mtu...... Ilikuwa ni miaka ya 1850
Alifanya utapeli mwingi ila anakumbukwa zaidi baada ya kufungua kampuni nchini Canada iitwayo International Overseas Service(IOS) ila ofisi akaweka Geneva Uswis yaani amesajili kampuni huku halafu biashara anafanya kule halafu hapohapo anapiga mpunga pia huko Ufaransa kwa kampuni hiyohiyo moja ni km mkasa wa Richmond huku Bongo

Akapiga mkwanja mrefu kijanjajanja ila akadakwa mwaka 1973 na kutumikia miezi 11 jela huko Uswis ila akaachiwa huru baada ya kulipa USD 600,000 baadaye na kuishia kuishi maisha ya kawaida tu na mwisho wa siku akafariki dunia 1995 nchini Uingereza kwa kiharusi

9/Robert Hendy--Freegard

d05a42fdd9364aba04a5fb23aee3ee96.jpg
4c7346e0af3c9e0598b85ef2b39b97ca.jpg
Ni

Mwingereza aliyezaliwa mwaka 1971

Huyu jamaa aliwapiga Waingereza wengi assist kwa kujifanya ni jasusi wa M15 Scotland Yard yaani tuseme sawa na mbongo ajifanye ni Mwanausalama wa Taifa

Jamaa alikuwa anafanya biashara ya kuuza magari na kutumia mwanya huo kukutana na wateja kisha kuwatapeli kwa kujifanya ni mtu wa M15 Scotland Yard

Hakuishia hapo tu alitafuta hadi demu wa kujifanya mkewe na kupiga nae pesa kimagumashi

Aliwekewa mtego na kunaswa mwaka 2002 baada ya Scotland Yard kushirikiana na FBI kumsaka na kumtia mbaroni na kuwa maarufu ghafla ulimwenguni

8/James Hogue

67be2789e4552cab582b436088600ae9.jpg
2230942663ce90a2d55ae425f442b61a.jpg


Alizaliwa 1959
Huyu bwana alifanya udanganyifu wa vyeti ili asome Princeton University kama alichofanya Daudi Bashite huku bongo ila huyu mzungu ndo kiboko

Kwanza kabisa alitengeneza/iba vyeti vya marehemu wa miaka 16 aliyekuwa mwanafunzi wa Sekondari huko Nevada kisha akajifanya pia ni yatima kwa vyeti vingine na kufanikiwa kugusa "Mlimani" tena kwa kusoma kwa ufadhili kama mtoto yatima na hivyo kupiga assist sehemu kibao

Ila hauridhika kwani mwaka wa kwanza tu akaharibu baada ya kuiba baiskeli hivyo mwisho wa siku utambulisho wake halisi ukagundulika mwaka 1991

7/Eduardo de Valfierno
d5e8ff95cc4c660e50716ac7728dcf4a.jpg
b33e3ace6487a1e6e5e16bba2cf100d9.jpg

Huyu ni tapeli wa Kiargentina

Huyu bwana ndiye aliyefanikisha kuibiwa kwa picha maarufu iliyochorwa na nguli Leonardo Da Vinci iitwayo Monalisa

Alijifanya yeye ni Marquis na kisha kuwatafuta watu na kuwalipa halafu wakaiba picha ikiwa Makumbusho mwaka 1921
Baada ya aliyemtuma kuiba na kusepa huyu jamaa akala kamisheni na watunzaji wa makumbusho na kutoa kopi 6 za picha hiyo

Na msala ulikuwa mrefu kiasi ni ngumukjuuelezea wote

6/Soapy Smith
29686da3e0c57aa93065845008eaee1b.jpg
cbcacb41f9ff2c8988f95345448a0613.jpg

Alizaliwa nchini Marekanimwaka 1860

Alikuwa ni msanii,tapeli na pia alimiliki genge lililokuwa lokijihusisha na Organised Crimes nchini humo

Umaarufu wake wa kitapeli ulitokana na kubuni na kuanzisha biashara iitwayo "tripe and keister" katika kona zenye msongamano mkubwa wa watu mtaani kisha kuuza keki za sabuni(keki feki zilizotengenezwa kwa sabuni) na kukusanya makumi kwa mamia ya watu kisha kuanza ujanjaujanja wapromosheni

Pia alisubiri watu wakusanyike kwa wingi na kuwatapeli kwa mbinu za maneno matamu yaliyotukuka
ila mwisho wa siku aliondoka na mpunga mrefu

5/George Parker
861586097424e70ca54101e49023519b.jpg
c88ddad90da59977ee0566d0b815f543.jpg

Alizaliwa mwaka 1870
Huyu ni mmoja wa tapeli maarufu katika historia nchini Marekani ....alifanikiwa hadi kuwatapeli watalii kwa kuwauzia mji(ardhi) ya jiji la New York

Hakuishia hapo, alifanikiwa kuliuza daraja maarufu la Brooklyn Bridge mara mbili kwa wiki kwa kipindi cha miaka kadhaa
Alifanikiwa kuwatapeli watu kibao pia kwa kuwauzia Madison Square Garden na utapeli mwingine kibao ambao naweza kujaza page nzima hapa
Baada ya kuisumbua sana New York alikuja kukamatwa na kutupwa jela maisha
Huyu kwangu ndo tapeli mahiri kuwepo nchini Narekani

4/Victor Lustig
552c0f98bb7076b43bc337f604d49458.jpg

Tapeli huyu alizaliwa mwaka 1890 na kufariki dunia 1947

Alikuwa ni tapeli maarufu ....alifanya utapeli mwingi ikiwemo kuwauzia wasafiri ndani ya meli viboksi feki vya kutengenezea pesa(money print) alivyovitengeneza kwa ustadi mkubwa

Alikuwa na maneno matatu,mtu snart kimavazi, mjanjamjanja

Tukio lilimpaisha zaidi ni alipofanikiwa kuwatapeli wafanyabiashara wakubwa wa chuma kwa kuwauzia mnara wa Paris Paris Elffel Tower mara mbili kwa kuwapa tenda feki ya kuubomoa ili wachukue vyuma chakavukiasi kwamba walipogundua wametapeliwa waliona aibu hata kutangaza kwamba jamaa kawapiga assist.....ilikuwa ni aibu kwa watu wa hadhi yao

Jamaa alikuwa na kanuni yake maarufu ya utapeli(kutolewa,kuwa smart,kutokuwa mwongeaji kupitiliza)
Kanuni hii hadi leo matapeli wabobezi wanaitumia

3/Joseph Well
e7126e22e0f7c4b0db938262429c0499.jpg

Tapeli huyu alizaliwa mwaka 1877 na kufariki dunia 1975

Alikuwa ni tapeli maarufu karne ya 20....kafanikisha utapeli kkibao ukiwepo wa USD 8 Milioni

Alikuwa akikusanya madeni pamoja na wafanyakazi wenzake kisha kuweka kitu kibindoni kidogo kidogo pamoja na kutoa risiti fe
ki Jamaa alikuwa bonge la tapeli kiasi akiwa kitaa alikuwa akibadili jina karibia kila siku mara Dr fulani, mara sijui mchungaji
Keshatapeli watu kibao ikiwemo kujifanya mwekezaji wa kampuni kubwa ya bisshsra ya mafuta na kujiingizia mabilioni ya pesa

2/Charles Ponzi
f7ce6a09abfdf182ed4a408142697c14.jpg
75fd114e044ed9bda1496fedbec5f16c.jpg

Tapeli huyu alizaliwa mwaka 1882 na kufariki dunia 1949

Alikuwa ni mhamiaji/mzamiaji wa Kitaliano aliyeishi nchini Marekani na kuwa miongoni mwa matapeli wakali wa muda wote duniani
Usishangae umaarufu wa neno Ponzi kwenye Make Money Fast Schemes kwenye mitabdao ya kijamii....ni sababu ya huyu tapeli
Ukiitwa Ponzi pigana......

Ni msomi wa Chuo Kikuu kutoka Rome nchini Italia ila akatumia maarifa yake kuwapiga watu assist/utapeli wa kufa mtu ....amewahi kufanya kazi nchi nyingi na kuishia kuachishwa kazi kutokana na utapeli mfano alianza kufanya kazi mgahawani Marekani ila akaachishwa kutokana utapeli dhidi ya wateja
Huyu ni tapeli wakimataifa

1/Frank Abagnale
80e6af5ce5a19b0c0807b605abf94010.jpg
c51814623f42fd09c7e76647f1b3018f.jpg

Alizaliwa mwaka 1948
Alikuwa ni msanii,tapeli wa risiti(cheque) n.k
Miaka ya 1960's alifanya bad cheques katika nchi mbalimbali duniani kwenye mabenki makubwa zenye thamani ya USD 2.5 Milioni
8e3126f5443f2d40c7b52ddba92f7312.jpg


Hii ni filamu inayoelezea madudu ya cheki feki aliyoyafanya

Utapeli mwingine maarufu ni alipotengeneza "pay in slip" feki ya akaunti ya bank na kufanikiwa kuiba USD 40,000 na fasta kuingia
Tapeli huyu alisifika kwa kupenda vimwana hivyo kufikia hadi hatua ya kujifanya ni rubani kwa kuvaa mavazi ya kirubani na kufoji kitambulisho cha shirika kubwa la usafiri wa anga duniani

.

.
Mwisho
The Bitoz
 
Kwani walianzisha kilimo mkuu
Au mbegu walipanda wapi ?

huyo ontario ni balaa.... ana maneno matamu kama asali.... ni dogo wa miaka 23.. kamaliza udsm mwaka jana... na akaja humu na kutapeli maelfu ya mababa wenye ndevu zao..


mara ya mwisho alionekana beach za south africa akila bata.. yupo na mtoto mkaliii.. mrembo na mbichiii na bikra yake ndani


inasemekana alipiga watu zaidi ya milion 300 humu in 5 months
 
huyo ontario ni balaa.... ana maneno matamu kama asali.... ni dogo wa miaka 23.. kamaliza udsm mwaka jana... na akaja humu na kutapeli maelfu ya mababa wenye ndevu zao..


mara ya mwisho aliobekana beach za south africa akila bata..


inasemekana alipiga watu zaidi ya milion 300 humu in 5 months
Hahahaaa
Mkuu kwani alianzisha kitu gani hadi kutapeli watu ?
Mimi ndio nasikia kwako tu
 
huyo ontario ni balaa.... ana maneno matamu kama asali.... ni dogo wa miaka 23.. kamaliza udsm mwaka jana... na akaja humu na kutapeli maelfu ya mababa wenye ndevu zao..


mara ya mwisho aliobekana beach za south africa akila bata..


inasemekana alipiga watu zaidi ya milion 300 humu in 5 months
Humble African
 
alikuja na biashara ya ku download hela mtandaoni... unakaa na laptop yako tu chumbani kwako na wine au bia unaanza kudownload ma dola mtandaoni.. wabongo wanavyopenda vya bure wakajaaa kutokea kila upande nchi nzima... humu kulikuwa hakukaliki
Mkuu yaani watu walidownload pesa mtandaoni mkuu wakati akina sisi tunahangaika kufuga tu kuku ?

Kama bado wanadownload pesa nishtue na mimi nizame jumla

Au ishakufa hiyo kitu ?
 
Back
Top Bottom