Profesa Baregu; "Zamani Tulikuwa Tunafuta Ujinga Kwa Watu Wazima, Siku Hizi Wajinga Wengi Ni Vijana."

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Wakuu habari,

Utii ukizidi unakuwa uoga, na uoga siku zote huzaa unafiki na kujipendekeza, na mwisho ni mauti - Mwl. J.K. Nyerere

Dharau za Magufuli kwa wafanyakazi kunajenga tabia ya kutojiamini kwa wafanyakazi, kujiona kuwa wateswa, watengwa na kushuka kwa kiwango cha uzalendo. Zaidi, kunapunguza kwa kiasi kikubwa ufanisi wa kazi maofisini na kupungua kwa ubora wa huduma za kijamii kama elimu na afya. Kwa sababu ya kuogopa kutekwa na kupotezwa, kunaweza kusiwe na migomo, lakini migomo baridi inaweza kutokea, na zaidi, kudorora kwa huduma za kijamii (zaidi afya na elimu).

Mnaomshangilia Magufuli kwa dharau hizi anazowaonesha wafanyakazi, mjitathmini! Hakuna taifa linajengwa na wanyonge. Taifa linajengwa na wafanyakazi, wenye afya bora na elimu bora.

Kwenda kazini sio kazi. Kutekeleza ratiba ya kazini sio kazi. Kazi ni kuifanya kwa moyo, nguvu, ari na hiari. Lakini serikali ya Magufuli imepuuza wafanyakazi. Sasa tutarajie malalamiko mengi mahospitalini na kwengineko.

Sio heri, lakini ni shari iliyoandaliwa kwa nguvu zote, na wenye nguvu.

Kama Uchumi Wetu Unakua Kama Unavyotuambia Tuvumilie Nini? Mambo Gani Ni Mabaya Kwa Sasa Wakati Uchumi Wetu Unakua Kwa Kasi?

Mwenge Haujawai Kuwa Tunu Ya Taifa Hili, Tunu Za Taifa Ni UTU, UZALENDO, UADILIFU, UMOJA, UWAZI, UWAJIBIKAJI Na LUGHA YA TAIFA!!

Nyerere Hakua Muoga Alijibu Hoja Kwa Hoja Ndio Maana Hakupiga Marufuku Maandamano Wala Kuminya Uhuru Wa Kutoa Mawazo.

DMFNyiHX4AAKUef.jpg


".Nchi Yetu Imeingia Kwenye Utelezi Mwingi Kuelekea Dola Ya Kidikteta."→ Tundu Lissu

mr mkiki.
 
Professa Beregu anajisahau sana. Amezoea kuwalaghai wazungusha mikono wenzake lakini anasahau CHADEMA wamebadili KATIBA na kuwa na mwenyekiti wa maisha au huo uzalendo? Na walimpataje mgombea urais? Dr Slaa apojaribu kuhoji nini kilimpata?
 
Huyo professa ndiye aliyewabadili vijana wa bavicha na kuwa wavivu wa kuhoji.
 
Professa Beregu anajisahau sana. Amezoea kuwalaghai wazungusha mikono wenzake lakini anasahau CHADEMA wamebadili KATIBA na kuwa na mwenyekiti wa maisha au huo uzalendo? Na walimpataje mgombea urais? Dr Slaa apojaribu kuhoji nini kilimpata?
Katiba mpya itapatikana baada ya kunyooshana na kunyoosha nchi.
 
Back
Top Bottom