Tajirika na Kilimo cha Nyoka: Tuwapende na kuwatumia Nyoka badala ya kuwaua

undefine

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
442
1,011
Screenshot from 2017-04-28 13-31-54.png

Kilimo cha nyoka ni moja ya kilimo yenye faida sana ,mmoja anaweza akaanzisha kilimo hichi ukizingatia thamani ya "snake venom" ipo juu sana.Sumu ya nyoka inatumika kwa wingi kwenye viwanda vya famasia na viwanda vya vipodozi hivyo thamani ya "snake venom " ipo juu sana kutokana na uhitaji wake.
Angkor-Night-Market-BBQ-Snake-1024x768.jpg

Gram moja ya "snake venom " kwa soko la kimataifa inauzwa $1880 ,na kwenye soko la Afrika kusini inauzwa kwa makadirio ya Rand 25,000

*Kama unafikiria kuanzisha shamba lako la nyoka ,yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili uweze kupata faida ya kutosha kutokana na venom wanayozalisha Nyoka

1.zingatia hali ya joto na hewa .
image016(2).jpg

Nyoka wanahitaji joto ya kiwango cha 24-29 degrees Celsius nyakati ya siku na 21-24 nyakati za usiku,

2.mabanda na nyumba za nyoka zinahitaji kusafishwa mara kwa Mara

Hali hiyo itasaidia kukuza uzalishaji wa nyoka kwa wingi.Nyoka wanahitaji kuwekwa mahali salama kuzuia matatizo yeyote ile ya kiafya kuwapata.

3.Nyoka kwa kawaida hula panya 3-4 na hulishwa kwa wiki 3-4 .Nyoka hula panya walio hai lakini wanaweza kula waliokufa pia ,Nyoka hupenda kucheza na panya mwanzo kabla ya kuwala hivyo ni vema kuwapatia walio hai.


Faida 3 za ufugaji wa nyoka

1.uzalishaji wa venom ambayo ukiuza unapata kiasi kikubwa cha pesa.

2.hupunguza na kutokomeza wadudu waharibifu kama panya nk.Nyoka chakula chao kikuu ni panya hivyo husaidia kutusafishia shamba au nyumba kwa kuwamaliza wadudu hawa.

Dawa ya kuua sumu ya nyoka itengenezwayo kutoka kwa sumu ya nyoka, yaani anti-venom, ndiyo tiba bora pekee ya kuumwa na nyoka.
chinas-snake-village-breeds-more-than-3-million-snakes-a-year.jpg

**Mwisho nawashauri ndugu zangu sio kila tukiwaona nyoka tunawaua ,nyoka ni rafiki zetu na sio maadui.Tuwatumie ipasavyo watatusaidia sana.
 
Sasa banda la nyoka unasafishaje? Na ukiwa unafuga unaweza kukaa nao karibu kabsa? Uogopi kung'atwa
Unawahamisha unawaweka kwenye beseni special ,vifaa za kuwabebea nyoka kama fimbo zilizochepuka zenye kibanio kuwakamata nyoka shingoni na unawahamisha kisha unawarudisha

Hukai nao karibu bali unawapa Huduma na kuwapa matunzo vizuri
 
Umeongea point sana mkuu, ila nadhani kunatakiwa taarifa zaidi.

Una uzoefu kidogo juu ya hii kitu mzee nikukontakti?
Nimeingia mwezi February hivyo sina uzoefu ya mauzo ila nimekuwa nafuatilia uhitaji,soko na namna ya kutoa venom,kuhifadhi nk

Labda nikupe uzoefu ya namna ya kuwafuga ..

2 1/2 nipo kwenye hii kilimo ,
Muhimu nikutafuta littre ya hii kitu
 
Nimeingia mwezi February hivyo sina uzoefu ya mauzo ila nimekuwa nafuatilia uhitaji,soko na namna ya kutoa venom,kuhifadhi nk

Labda nikupe uzoefu ya namna ya kuwafuga ..

2 1/2 nipo kwenye hii kilimo ,
Muhimu nikutafuta littre ya hii kitu
Nitashukuru sana mkuu na vipi initial cost zake?

Faida au gharama ya kuuza ni sawa kwa sumu zote au inategemea na aina ya nyoka?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom