JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Tulianza na shopping mall Dodoma, sasa tena ni kiwanda cha Tumbaku. Yasemekama wahusika ni wale wale! Ukiingia mjini Morogoro, umbali kidogo kutoka mzunguko wa Msamvu kuelekea Iringa, unakutana na daraja la reli na pembeni yake unakuta shughuli za ujenzi wa kiwanda kipya cha Tumbaku. Eneo hili kwa miaka mingi lilieleweka ni eneo la wazi, na kwa sheria zetu za ardhi, hakuna aliye na madaraka ya kubadili matumizi ya eneo la wazi.
Wakati napitia pitia mitandaoni kutafuta style mpya kwa ajili ya shangazi yenu ndio nikakutana na hili bandiko kuwa aina ya kujamiiana huku mwanamke akiwa amemkalia mwanaume juu ('woman on top' or 'cowgirl' or 'reverse cowgirl'), hatari kwa afya ya mwanaume kwani hupelekea maumivu makali kwani hupekelea fracture ya uume kwa asilimia kubwa wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Inashauriwa mwanaume ndio akae juu ili kupunguza uwezekano wa kupata madhara.
Kuna wazandiki huwa nawashangaa wanavyoponda pombe. Pombe haina madhara kama wanafiki wanavyotuaminisha. Pombe ni nzuri ukinywa kistaarabu, ina faida lukuki, ukibisha muulize Albert Chalamila. Tafiti zinasema kuwa beer zinasaidia kujilinda na magonjwa ya moyo. Kama mnavyojua magonjwa ya moyo yanaondoa watu kimya kimya hivyo mimi nawashauri tunywe beer kujilinda na magonjwa ya moyo. Hata Biblia inasisitiza tunywe pombe tufurahie, na mkituona tunakunywa pombe msitukwaze. Too much of anything is bad, but too much good whiskey is barely enough
Licha ya kufanya makubwa kwa muda mfupi ndani ya Mhula wa Kwanza, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ametangaza hataomba muhula wa pili kwenye uchaguzi mkuu wa baadae 2026. Hapa Tanzania hakuna chochote kafanya na bado chawa wanataka aongeze muda mpka 2030! Tamaa na Uroho wa Madaraka. Tazama video hii ujionee mwenyewe. Video ya Rais Hakainde Hichilema akisema hatagombea tena mwaka 2026.
Baada ya Singida Fountain Gate FC kupoteza mchezo wao wa Ligi ya NBC Premier League wakiwa nyumbani dhidi ya Simba, kupitia mitandao ya kijamii walitoa malalamiko yao wakiituhumu TFF na Ligi ya Bodi kuwapangia refa kwenye michezo wanayokutana na Simba ambaye amekuwa akiibeba timu ya Simba SC baada ya kupewa maelekezo maalum ya kuwabeba Simba. Singida FG wamedai kuwa katika michezo ambayo refa huyo amekuwa akichezesha dhidi ya Simba basi yeye ndiye huibuka Man Of The Match, hivyo wamezitaka taasisi hizo zinazosimamia ustawi wa mpira wa miguu nchini kutolea ufafanuzi.
Nimeona mjadala kuhusu mihula anayoruhusiwa kugombea makamu aliyeshika madaraka ya Urais kutokana na kuchukua kiti katikati ya muhula baada ya Rais aliyekuwepo madarakani kushindwa kuendelea aidha kwa kufariki akiwa madarakani, kujiudhuru au sababu za kiafya. Mjadala umechagizwa na kauli ya Sophia Mjema aliyesema Rais Samia ni hadi 2035, huku wanaharakati wakipinga vikali kuwa hana sifa ya kugombea mihula miwili tena. Je, ukweli ni upi?
Salaaam Wakuu, Nimeona katika sehemu mbalimbali picha zikisambaa zikionesha nembo inayotumika kwenye Podium ya Rais Samia haina bibi na bwana kama ambayo alikuwa anaitumia Rais Magufuli. Hili limekaaje Wakuu tunaomba ufafanuzi. Nembo anayotumia Rais Samia ikiwa haina Bibi na Bwana Nembo aliyokuwa akiitumia Hayati Magufuli ikiwa na Bibi na Bwana
Aprili 27, 2023, akaunti ya Mtandao wa Twitter inayotumia jina la MainLandAfrica iliweka chapisho linalodai kuwa Bilionea wa Marekani Dan Friedkin amekodisha takriban Ekari 6,000,000 za ardhi nchini Tanzania. Chapisho hilo lilienda mbali zaidi kwa kudai kuwa Friedkin ni mmiliki wa Ekari zingine 25,000 za ardhi zinazounda pori la Akiba la Mwiba. Wanaojua kuhusu huyu jamaa watupe details anafanya biashara gani na ardhi kubwa kiasi hicho?
Tetemeko la aridhi nchini Morroco limeua zaidi ya watu 5000, kuna kijiji kimoja cha mlimani chote kimefutwa na tetemeko isipo kua majengo mawili tu, hayo majengo mawili ni msikiti wa kijiji na nyumba ya huyu alio jenga huo msikiti, hiivi hili lina uhusiano wote na Imani au ni ecological force tu, wenye uelewa mambo theology na geography tuambieni.
Back
Top Bottom