JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Leo nimeona video ambao imewekewa sauti ya mtu akisema wametumiwa video hiyo kwenye group la shule ya Themihill, video hiyo inaonesha mtu akifungua kitu kinachoonekana kama pen (kalamu) ambacho ndani yake kina risasi na baadaye kufyatuliwa. Anayeelezea video hiyo anadai pen hizo zinagawiwa mashuleni na kuuzwa huku akionesha hofu ya watoto kuuana au wao wenyewe kujidhuru kwa peni hizo. Ningependa kufahamu ukweli kuhusu video hiyo.
Wakuu, Nimekuja na swali hili baada ya jamaa mmoja kusema jambo hili sio la kweli, lakini mimi pia nimeshawahi sikia hii, bi mkubwa alituhadisia kuna ndugu yao mmoja aling'atwa na mbwa mwishowe alipokaribia kwenda kwenye ulimwengu mwingine alikuwa akibweka kama mbwa. Naamini hata wewe unayesoma hapa umeshawahi kusikia kuhusu hili. Je, suala hili ni kweli au stori tu za mtaani wataalamu wa JamiiCheck?
Wakuu, Kuna video nilikutana nayo huko mtandaoni (nimeangalia sijaiona), huyo dada alikuwa anasimulia jinsi rafiki yake alivyokufa baada ya kung'atwa chura. Chura huyo alikuwa ndani ya kiatu chake, wakati anavaa hakumuona, basi huyo chura akamng'ata kwenye kidole baada ya kushtuka (unajua jinsi wadada tunaogopa wadudu) akamtoa kwenye kiatu na kuvaa na kuendelea na kazi zake. Baada ya siku mbili yule dada akaumwa, homa kali ikamshika kumpeleka hospitali ndio ikaonekana ni hiyo sumu ya chura, na imeshambaa mwilini kiasi ambacho hakuna msaada tena. Mwisho dada alikuwa anakoroma kama chura (kama vile inavyotokea mtu aking'atwa na mbwa mwenye kichaa) mwishowe akafa. Sasa wakuu mimi nauliza, hawa chura tunaopishana nao majumbani ndio...
Back
Top Bottom