Nala: Ijue benki ya kidijitali kutoka Tanzania

Arthurtz

Senior Member
Feb 10, 2017
151
121
Habari zenu wanaJAMII

Kwa wale ambao pengine wanamfahamu BENJAMIN FERNANDES ama umekuwa ukimfuatila katika kurasa zake za mitandao ya kijamii hasa Instagram na Facebook. utakuwa umekutana na startup yake kwa jina la NALA

Kama bado hujajua Nala App Ni nini hasa basi ungana nami katika Uzi huu. Ili niweze kukufahamisha machache katika mengi juu ya NALA

Ni nini NALA
NALA ni bank ya digital iliyotengenezwa mahususi kwaajili ya watanzania na waafrica hasa wale wale sub Saharan countries na inayoendana na matumizi na maendeleo ya mtanzania.
Imekuja hasa kutatua baadhi ya changamoto (sio zote) zilizopo katika mfumo wa Sasa wa malipo ya simu yaani mobile payments (m-pesa, Tigopesa, Airtel money etc)

Changamoto hizo ni nyingi naamini ninyi pia mnazifahamu. Hapa nitazitaji baadhi na kuona jinsi gani NALA imezitatua

1. Mlolongo mrefu wa USSD
Hili wote tunalishuhudia jinsi gani tumekuwa tunapitia mlolongo mrefu wa USSD tunapofanya miamala mbali mbali katika simu zetu kama vile kulipa bill, kutuma pesa, kutoa pesa, kununua muda wa maongezi na hata kulipia vingaamuzi vyetu.
Mfano.
Mtu anayetaka kununua umeme (luku) katika mtandao Fulani itabidi afuate hatua zifuatazo na kwa kila hatua akisubiri kwa sekunde. Baada ya kuBonyeza *150*XX# itabidi aendelee kupitia hatua hizi sita (6) Hadi kukamilisha muamala

Z9wPLKxnmQX5i5h9s_Xvqp3HMDztFmQGQpU4f5G9X-8eYz2s--5vmrrtYbcsm___YgXNHzOE6l23J4-iVmttj34K0_yaZwIkgHEYcebQ3LOe0uubG9EffIy6dYZcPbdEu9mhoI18


Huo Ni mtandao wa kwanza mwingine huu

rgzcOQQQetOMY6hysTjVykh-LqGYkLbgt5B8iwHmYIeYKS4qdfiCV9oTtXKLoBCQLeaYJDI1qL51dmcNfRVy8PXhAA_nlUSgQ-lk6VvRveUL44S3sxIAVYpf2eGUOGRqYcTNGgZU


Si kwa mitandao hii miwili karibu mitandao yote hali ipo kama hivi. This is very poorly designed menu that requires you to enter string of numbers which introduce more possibility for errors. Hi ni changamoto ya kwanza


2. Orodha ya miamala/ Taarifa fupi
Mfumo uliokuwepo Sasa Ni vigumu Sana kupata historia ya matumizi yako ya pesa hasa miamala ulofanya ( na maanisha Taarifa fupi ). Na hata ukihitaji hiyo Taarifa fupi itakubidi ulipie 50 Tzs ama zaidi na bado huweza kuletewa miamala yote.

3. Kutumia muda
Hadi kukamilisha mualama itakuchukua muda kwa sababu mfumo ni mrefu na complex. Hizo ni baadhi tu.


Ok Sasa ngoja tuone NALA imekuja na nini hasa ama imetatua vipi changamoto tajwa hapo juu

  1. Hakuna tena mlolongo mrefu wa USSD
Nala imeondoa kabisa mlolongo mrefu wa USSD katika kufanya transaction. Kwa mfano ukiwa na NALA ukitaka kumtumia mtu pesa you simply opens the app, clicks “Send money”, selects a recipient from your contact list (or phone number input), inputs the amount, and it’s done!. Hii inaifanya Nala kuwa rahisi Sana kutumia, haraka na kufanya transaction mara moja. Spidi ya Nala katika kufanya transactions ni seven (7) times faster than mobile money

2. Historia ya miamala uliyofanya
Nala inarekodi transactions zote uliyofanya na kuziweka sehemu moja. zaidi hasa utaweza kuback up na kurestore pale itakapo tokea ume re-install App. Hivyo basi kwa kutumia Nala huna haja ya kuomba Taarifa fupi Wala kulipia chochote. Kwa kutumia Nala utaweza kutrace na kutrack transactions zote


f_CFO86Yd4kYFHj1msbgH83HyDyYLb7qcEOadu12MS_3mw6bHsjERtBsa4u5oAr93FyXXxcAnjnmnBD_pbPJ4bbGtLxHhCokHMEt49GSm8Das88KGE-6x2DRJHGHXw_dV3Hf3yvQ



3. Kuangalia Salio
Ukiwa na Nala huna haja ya kuongalia Salio lilobaki kwenye account yako. Kwa sababu Nala hunyesha Salio lilobaki katika account yako mara baada ya kufanya transaction ya mara ya mwisho.


4. Ulinzi was hadhi ya kibenki
Miamala yote utakayofanya kwenye Nala hulindwa na ulinzi wa Hali ya juu yaani bank grade security.


5. Huduma zote zimewekwa mahali pamoja
Nala acts as one-stop-service center ambapo Huduma zote hitajika kama vile kutuma pesa, kulipia bill na Huduma nyingine hupatika sehemu mmoja kwa urahisi na uharaka

9mB_MlsghQoLpPocbZEw2A2IfbrwAmLF3aPtUEJnrHUnJ5XRAwlU_aksqq-CNyslRNbrGJFQWcHc4q6ie6LtNwQOFSjhb0srnpFhARMzliLMq6rOzpsFGJgjlL20Ix1gS5k4ErQ2



6. NALA haihitaji kuunganishwa na internet ili iweze kufanya kazi
Nala inaifanya kazi offline hii inaifanya iwe tofauti Zaidi na apps kama vile mpesa, Tigopesa na nyingine.ambazo huhitaji internet connection ili zifanye kazi


Hizo ni baadhi ya faida za NALA. Kuona na kujua uzuri wake zaidi download NALA kwa playstore na uanze kutumia


Kumbuka App hii ipo katika hatua za mwanzo za matumizi hivyo team ya NALA inapokea maoni na ushauri kuhusu Huduma hii ili iweze kufanya iwe Bora na nzuri. Kizuri zaidi NALA is built for the community and by the community. Team ya Nala Ni sikivu na inapenda kusikia nini watumiaji wa Nala wanahitaji. Hili tumeliona kwa wale ambao walichaguliwa kwenye beta version. Hivyo basi download Kisha Anza kutumia na kutoa maoni yako Hapa

Email
WhatsApp +255 735 737 475
Facebook
 
Ok na vipi huduma za halopesa zimo ndani yake mkuu?
NALA inafanya kazi na line ya tIGO, Vodacom na Airtel. Kutuma pesa kwa watu.Kununua vifurushi. Kulipia bili (kwa sasa huduma hii inapatikana kwa Vodacom na tiGO tuu).
 
na je kama natumia line ya line ya halotel kwenye simu yangu kwa ajili ya internet then nikadownload hyo app kwa ajili ya kuitumia kwa ajili ya tigo pesa itafanya kazi?
 
je ni app inayoweza kukusaidia kuweka fedha(deposit)?
2,je nawezaje kuweka fedha zangu?
3,vipi gharama za kutuma na kupokea pesa?

1. Fedha zako unaweka Kama kawaida kwenye mtandao wako pendwa uwe Tigo, Vodacom ama Airtel. Kwani NALA inafanya kazi na mitandao tajwa hapo juu

2. Gharama za kutuma pesa na kufanya transaction zozote ni zile zile za mitandao husika. Nala haina service charge yeyote kwa Kila transaction unayofanya

Download hapa https://play.google.com/store/apps/details?id=money.nala.pay uanze kutumia Kama una maswali na maoni email au WhatsApp kwa namba za hapo juu
 
na je kama natumia line ya line ya halotel kwenye simu yangu kwa ajili ya internet then nikadownload hyo app kwa ajili ya kuitumia kwa ajili ya tigo pesa itafanya kazi?

Ndio
Kwanza kabisa tambua Nala inafanya kazi offline haihitaji kuunganishwa na internet ili iweze kufanya kazi. with NALA noINTERNET noPROBLEM. unachotakiwa ni kuhakikisha hiyo line ya Tigo ipo kwenye hiyo simu.


Download https://play.google.com/store/apps/details?id=money.nala.payhapa
 
Kwa hiyo mwana aligoma mshara wa nusu billion za kibongo aje kuanzisha hii app yake sio,

Hingera zake nampa shavu kwa kuidownload right now
Tutarajie mengi mazuri kutoka kwa Benjamin. Kama utakuwa umeangalia hii interview yake utaelewa kwanini ameamua kurudi nyumba.
Nala Ni mwanzo tusubiri mazuri kutoka kwake.

Vizuri Sana jimmyfoxxgongo download Kisha Anza kutumia Nala. Kumbuka maoni yako na ushauri Ni muhimu Sana katika kuboresha Nala
 
Mleta uzi mimi nashauri pia muweke option ya mikopo ili mvutie wateja maana sasa hivi ubunifu ndo kitu muhimu naamin mkiongea na banks na taasisi zingine za kifedha naamin mtafanikiwa
 
NALA is the simple, fun money app for sending cash quickly between friends, making payments, buying your favourite bundles and keeping track of your financial history. NALA is building the bank of the future, designed for the world we live in today. Join more than 40,000 people who have signed up for NALA during our waitlist and become part of the digital banking revolution!

[HASHTAG]#NALAFasta[/HASHTAG] has become the smartest way to make payments in Tanzania.

NALA is compatible with: TiGO Pesa, Vodacom M-Pesa and Airtel Money.

**QUICK & EASY**
Send money quickly to friends by simply clicking their name in your contact book. There’s no additional transaction fee for sending money with your mobile money. Use your mobile money balance for payments, or easily cash it out to your bank.

INSTANT TRANSACTIONS
Need to complete a payment? Don’t remember your LUKU or DAWASCO number? Don’t worry, NALA will store it for you so you can make those payments instantly.

NALA WORKS OFFLINE
No internet, No Problem. NALA allows you to make transactions offline without an internet connection.

BUY FROM YOUR FAVOURITE AIRTIME BUNDLES
Check out without your mobile money wallet. Use NALA to buy your favourite airtime bundle within seconds. Check your bundle balance with one click.

STAY ON TOP OF IT ALL
Easily track your finances with our budgeting tools and transaction history. Keep up with what you owe, what friends owe you, and what you’ve bought.

YOUR SECURITY IS OUR TOP PRIORITY
NALA makes money transfers easy and fun, and we take the protection of your NALA account very seriously by using security measures to help protect your account information.

WASILIANA NA SISI
Daima tunafurahi kusikia kutoka kwako! Kama una maoni, swali au wasiwasi wowote, tafadhali tumia barua pepe ifuatayo:

mamanala@nala.money

Tufuate kwenye Twitter: twitter.com/NALAMoney
Tufuate kwenye Facebook: facebook.com/NALAMoney
Tembelea tovuti yetu: nala.money
 
Mleta uzi mimi nashauri pia muweke option ya mikopo ili mvutie wateja maana sasa hivi ubunifu ndo kitu muhimu naamin mkiongea na banks na taasisi zingine za kifedha naamin mtafanikiwa
Tuma maoni yako na ushauri kwa email and WhatsApp number iliyotajwa hapo juu
 
Good job Benjamin & your team.My fellow Tanzanians,Let us support this innovation because it solves people's problem(s). I believe in the next 5 or ten years; almost everyone will be using or benefiting from this service.Good job!!
 
Back
Top Bottom