Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,581
18,124
Safari inaendelea. Vitisho. Haya ndiyo maisha yetu ya Kila siku. Mengine tumetoa Ripoti Polisi huko

Kuna watu hawa miongoni mwa wengi. Yeye anaandika "Ben Saanane unachokitafuta ndani ya Serikali hii utakipata. Kwa elimu na uwezo wako hatukutarajia ungefikia hatua ya ajabu kwa namna uliyofikia.

Hujiulizi kwanini upo huru hadi muda huu You are too young to die. Tunajua utaandika na hili. Andika lakini the next post hutaandika ukiwa na uhuru wa kutosha. Andika but your days are numbered. Unajua kuna rafiki yako alipuuza na hutaki kuandika kuhusu yeye labda kwa kuwa alitangulia. Andika Ben. Andika sana, ongea. Sema lakini utajikuta mwenyewe na chatu"

He's such a coward. Muoga. Muaji anayejitangaza nae ana hofu tupu

Nimemshukuru lakini nimemjibu kwa namba yake hii 0768797982 ambayo ipo polisi.

Haya tunasonga mbele Watanzania. Kama ni Uchochezi sidhani kama upo uchochezi mkubwa zaidi ya huu.

As long as tupo hai, Sauti zetu hazitakoma. Tutaandika, Tutasema, Tutahutubia na tutafanya vitendo

Kitu kimoja tu cha hakika ni kuwa Damu ikimwagika hasa damu ya kimapinduzi hutoa mvuke utakaonyesha na kutiririsha mafuriko katikati ya mito na vijito vya haki. Kama itanyesha mvua ya Radi basi itaambatana na mwanga na cheche zitakazowamulika walaghai, watesaji, wakandamizaji wa hakiWatetezi wa haki watapata mwanga katikati ya giza tororo la Unyanyasaji, unafiki na ubakaji wa taaluma na dhamiri zao kitaaluma na kiimani.

Yesu Kristu aliishi miaka 33 tu duniania. Nina Mwaka Mmoja bado. He fought the right cause. Alikuja Duniani kimungu. Kila mtu anaishi kutokana na makusudi ya Mungu. Mwenyezi Mungu huruhusu kila jambo kwa makusudi yake. Sisi ni akina nani tukatae makusudi yake? Hatukujileta Duniani na hatutaishi milele.

Wasichojua watu hawa ni kuwa nilizaliwa na kubatizwa hatari siku hiyohiyo kama Mkatoliki. Ubatizo wa kifo(Hatari) 13 Desemba miaka hiyo, nikapona kwa fadhila zake Muumba. Nimepata fadhila sana Machoni pa Mwenyezi Mungu hadi muda huu. Wanajisumbua! Nimeishi beyond that favour

Oh nakupenda mpenzi wangu Tanzania. I love you more than words can wield the matter, dearer than eyesight, space and Liberty. Oh I love you Tanzania. My Pride, My fountain of inspiration."

Mlale salama marafiki zangu wapendwa.

Mapambano na Yaendelee, Ushindi U Dhahiiri (Aluta Continua, Victory Ascerta)

Pumzika kwa amani Rafiki yangu kipenzi Alphonce Mawazo. Hukukopa, Ulijiandaa kulipa gharama. Ukalipa Deni. Tunasonga Mbele! Nitalitaka Jeshi la Polisi liunganishe ujumbe uliotumwa na kifo chako katika hatua za uchunguzi.

Ben Saanane
 
mh....hivi hii kitu ni kweli?

it just sounds too real to be true!
Kutishia maisha ya mwanadamu mwenzako kwa siasa, sio tabia zetu Tanzania. If there is any iota of truthness in this posting of Ben , than ni lazima tusimame nae pamoja na kuitaka serekali ichukue hatua kuhakikisha jambo hili linafuatiliwa na haki inatendeka.

We have the rest right to disagree, japokuwa me n Ben do not have the same political visions, siungi mkono vitisho anavyo fanyiwa period.
 
Kutishia maisha ya mwanadamu mwenzako kwa siasa, sio tabia zetu Tanzania. If there is any iota of truthness in this posting of Ben , than ni lazima tusimame nae pamoja na kuitaka serekali ichukue hatua kuhakikisha jambo hili linafuatiliwa na haki inatendeka.
We have the rest right to disagree, japokuwa me n Ben do not have the same political visions, siungi mkono vitisho anavyo fanyiwa period.
correct....
 
Back
Top Bottom