JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

  Report Post
  Page 44 of 44 FirstFirst ... 34424344
  Results 861 to 872 of 872
  1. #1
   Kubota's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st October 2012
   Posts : 499
   Rep Power : 103864185
   Likes Received
   771
   Likes Given
   634

   Default Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Wana Jf,

   Kuna maandiko mengi JF ya ufugaji Kuku wa Kienyeji! Nawasilisha kwenu wadau wa JF mbinu ambazo kwa mikono yangu nimezitumia kutatua changamoto za kuku wa kienyeji! Nimeandika kuwalenga wajasiliamali ambao hawana nguvu kifedha kujenga mabanda kisasa, mashine kutotolesha vifaranga, kutibu magonjwa wala kujenga wigo (fence) n,k. Naomba mzijue mbinu hizi nisije kufa nazo, huu ni mchango wangu kwenu watanzania wenzangu wale ambao mtakuwa hamjawahi kuzisikia mbinu hizi. Mbinu hizi baadhi nilisoma vitabuni nikazijaribu na kuziboresha kwa mazingira yangu duni! Mbinu zingine niliziona kwa wakulima duni kama mimi nikazitumia na kuleta mafanikio makubwa, mbinu zingine nilizigundua mwenyewe na nikafanikiwa sana. Hizi mbinu hazijafanyiwa utafiti rasmi lakini nimeweza kufanikiwa kuwa na kundi kubwa la kuku kwa haraka sana kupitia ujanja huu!!

   Mdau wa JF nakualika utembelee uzi huu mara kwa mara kila upatapo fursa ili uweze kufuatilia simulizi yangu maana itakwenda kwa vipande vipande. Mnakaribishwa kuchangia uzoefu wenu ili tuboreke zaidi.

   Mbinu hizi zitagusia zaidi: Utotoreshaji vifaranga vingi kwa mara moja bila kutumia mashine! Ukuzaji wa vifaranga vingi kwa njia rahisi na kwa haraka zaidi, ulinzi wa kuku dhidi ya wanyama maadui, kudhibiti kuku wasizurule, magonjwa niliyofanikiwa kuyadhibiti, ujenzi wa vibanda wenye kukidhi mahitaji mbali mbali. Ni utaalamu nilioupata kwa gharama kubwa na mahangaiko ya muda mrefu, nauleta kwenu ili sote tuendelee kukua pamoja kiujasilia mali.

   Stay tuned and keep on visiting this thread!!


   ===============
   UPDATE
   ===============


   Quote By Kubota View Post
   Safari yangu ilianza baada ya kukutana na mhamasishaji aliyenitia chachu kwamba 10 x10 x 10 you become a millionea! Kwamba ukianza na kuku 10 kila mmoja akazaa 10 na hao watoto na mama zao wakazaa kila mmoja 10 unakuwa millionea! Wakubwa kuongea ni rahisi utekelezaji ukawa mgumu sana! Changamoto kuu aipatayo mfugaji wa kuku wa kienyeji ni kuzalisha vifaranga wengi na kuweza kuwakuza! Bila hivyo kundi haliwezi kukua na kukupa kipato cha uhakika!

   Safari ya ufugaji niliianza kwa kununua mitetea 30 na jogoo watatu! Ilibidi nisubiri muda hadi kuku waanze kutaga! Muda ukafika kuku wakaanza kutaga kwa fujo sana! Nilikuwa na banda moja tu ambamo kuku wote walikuwa wakilala humo. Nilitengeneza viota vingi kwa ajili ya kuku kutagia. Asubuhi nilikuwa nawafungulia! Changamoto nilizoanza kupambana nazo kwanza kama mjuavyo kuku tofauti walikuwa wanataga kwenye kiota kimoja! Ilipofika wakati wa kuatamia ikawa kila kwenye kiota kimoja kuna kuku kadhaa wamebanana wanaatamia! Hali hii haipaswi kutokea kwani kuku mmoja anaweza kuwa amejilundikia mayai mengi ambayo hawezi kuyapajoto la kutosha na kuku mwingine anakuwa amekaa kando tu hana hata yai moja. Hii ilibadilika ikawa kero kubwa! Nilijua utotoaji unaweza kuathirika sana!

   Ili utotoreshe vifaranga vingi kwa wakati mmoja badala ya kutumia incubator, tumia hao hao kuku. Wakianza kutaga kila siku okota mayai na kuyahifadhi mahali salama ili kuku wasiyatie joto! Kuku wengi wanapotaga kwa pamoja hufikia wakati mayai huishatumboni unakuta wamelala kwenye viota wakiwa wameatamia mayai yaliyopo au udongo tu! Kuku anaekuwa amefikia kuatamia utamjua kwani ukimshitua haondoki kwenye kiota. Kuku anaetaga ukimshitua hukimbia! Kwa hiyo kama nimepanga kutotolesha vifaranga 100 kwa mara moja nikishagundua kuwa kuna kuku 8 wameanza kuonesha dalili ya kuatamia hapo husubiri usiku ninawawekea mayai amabayo nilikuwa nimeyahifadhi. Ambapo mimi huwekea kila kuku mayai 15. Kwa hiyo kuku 8 hufanya jumla ya mayai 120. Kwa kuwa banda langu ni hilo moja tu kuku wengine wanaoendelea kutaga walikuwa wanaendelea kutagia kwenye viota ambavyo kuku wengine walikuwa wanaatamia! Hali hii ilikuwa inaleta tabu sana kwani ilikuwa si rahisi kutambua mayai mapya na yenye siku nyingi. Kuondoa shida hii nilinunua MARKER PEN (rangi yoyote) na siku ya kuwawekea mayai kuku ili waatamie niliyachora mduara kuzunguka yai ili iwe rahisi kuyatambua mayai mapya. Huo mchoro hauwatishi kuku na hakuna dosari yoyote. Kwa hiyo kila siku jioni ninapokuja kuokota mayai yaliyotagwa nilikuwa pia nakagua kila kiota cha kuku walioatamia na kuondoa mayai mapya. Kumnyenyua kuku anaeatamia na kuondoa yai haileti shida yoyote!

   Kuku akifikia wakati wa kuatamia ukamnyima mayai hawa wanatabia kuendelea kung'ang'ania kuatamia, hapo ilibidi kutengeneza JELA! Watu wengine wanambinu tofauti kumwachisha kuku asiatamie! Mbinu ya kumtia kuku stress inafanya kazi nzuri sana! Jela inaweza kuwa ni Tega, au Box kubwa au chumba kidogo kilichopo. Ukimfungia kuku JELA bila maji wala chakula kwa kutwa mbili siku ukimfungulia akili yake huwa ni kutafuta chakula tu hakumbuki kurudi kwenye kiota! Njia hii ilifanikiwa sana na ilifanya kuendesha shughuri zangu bila bughudha! Kuna wakati JELA ilikuwa na kuku kibao hivyo unapaswa kutengeneza kibanda cha JELA. Hawa kuku wakitoka JELA hutaga mapema sana amabapo bila hivyo wangekuwa wanaatamia. Pia kuku wakishaatamia kwa muda wa siku 10 nilikuwa nayapima mayai ili kubaini kama kuna mayai yasiyoweza kuanguliwa! Ni rahisi sana kama una Tochi! Ukimulika yai Kwa kulizungushia vidole kiganjani kama ni yai zima linakuwa na giza kama ni yai bovu linapitisha mwanga kama yai lililotagwa siku hiyo! Jinsi ya kuzungushia vidole yai, tengeneza duara kwa vidole vyako na dole gumba kisha pachika yai katikati ya duara ili mwanga wa tochi upenye kwenye yai! Kwahiyo unaweka tochi inayowaka chini ya yai na hii ifanyike gizani au ndani ya chumba chenye mwaga mdogo. Kadri ya yai linavyokaribia kutotolewa ukilimulika huwa na giza zaidi! Ukimulika mayai toa mayai yasiyoweza kutotolewa maana hayo hutumia joto la Mama bure!

   Ndugu zangu wana JF naendelea kuelezea utotoleshaji bado sijamaliza hebu niwarushie hii kwanza maana nimeona nimechelewesha kuwakilisha na nimewaudhi, poleni, mwenzenu nilikuwa nahangaika kufukia tanuru la mkaa nimekuta limefunguka! Si mnajua maisha jamani!
   ========

   Mayai viza! Mayai yasiyototolewa kwangu ni hazina kubwa kwani huyatumia kuwawekea kuku ili wasubiriane! Yaani inaweza kutokea kuku wameanza kuonyesha dalili ya kuatamia ili aishituke akaahirisha kuatamia huwa namlundikia hayo mayai yasiyoweza kutotoleshwa! Hufanya hivi hadi idadi ya kuku ninaotaka waatamie ikitimia, siku hiyo huondoa mayai feki na kuwawekea siku moja kuku wote mayai halisi ya kuatamia! Hakika nilikuwa ninasisimka sana inapofikia siku ya siku kuku wote wanamwaga vifaranga kwa siku moja!!

   Ufugaji huu wa kuharakisha kuwa na idadi kubwa ya kuku huendana na kutenganisha vifaraga na mama zao. Watu wa mjini hufanikisha kirahisi sana kwa kutumia taa za umeme kuwapatia joto vifaranga! Wengine wanaweza kutumia majiko ya mkaa! Ni wazi kwamba ukiwanyang'anya mapema vifaranga Mama zao ndani ya siku 10 huwa wanaanza kutaga mayai tena, ambapo bila hiyo angeendelea kulea vifaranga wake hadi miezi 3. Kwa kumnyang'anya vifaranga kuku hutotoa vifaranga wengi kwa mwaka! Sasa kazi ndiyo ipo hapa! Ukinyang'anya vifaranga mama zao halafu ukawarundika vifaranga wenye umri tofauti sehemu moja hapo ni balaa! Vifaranga wenye umri mkubwa huhakikisha vifaranga wadogo hawali! Vifo vingi vinavyosababishwa na lishe duni hutokea kwa vifaranga kutokana na ubabe unaotokea kwamba wale wenye umri mdogo hawashibi! Kwa hiyo ni muhimu kutotolesha vifaranga wote siku moja ili uwakuze pamoja!

   Kwa mazingira yasiyokuwa na umeme nilifanikiwa kukuza vifaranga kwa kutumia mama zao! Kwenye kuatamisha kila kuku nilimpa aatamie mayai 15 baada ya kutotoa nilikuwa kila kuku mmoja ninamkabidhi vifaranga 30! Kuku alikuwa anatandaza mabawa yake na kuwafunika wote! Nitawaingizia PICHA mshuhudie! Vifaranga wakirundikana ndani ya mabawa ya mama yao wanazalisha joto la kutosha na wala si kwamba wanategemea joto la Mama yao tu! Kwa kufanya hivi vifaranga waliototolewa na kuku 8 walilelewa na kuku watatu au wanne tu! Kwa hiyo wale kuku wengine 4 au 5 walipelekwa JELA ili kuondoa usumbufu na baada ya kutoka JELA baada ya siku 10 wanaanza kutaga mayai!
   ======

   Nashukuru Kamuzu kwa kuonyesha uwepo wako nilifikiri niko mwenyewe tu peke yangu hapa jukwaani maana wakubwa wamekasirika wameondoka kwa kuwa nimechelewa kuwasilisha, jamani tuvumiliane!

   Nilivyoendelea kufuga baada ya kuona kuwa kuku wanaoatamia wanapata usumbufu sana kutoka kwa kuku wanaoendelea kutaga, Banda langu la kuku nililigawa kukawa chumba na sebule! Nitaeleza wakati ukifika nilivyojenga mabanda yangu. Kwa hiyo chumbani niliweka viota na ndiko ambako nilikuwa nawaweka kuku wanaoatamia ili wasibughudhiwe kabisa na kuku wenzao, mlango wa kuingia chumbani nilitengeneza geti la mianzi iliyopigiliwa karibu karibu kuzuia kuku kupenya. Hapo sebuleni ndiko kuku wote watagao na wasiotaga walikuwa wanalala, kwa hiyo kulikuwa na viota vingi ambavyo juu yake nilikuwa naviwekea kizuizi kwa kutumia Mabanzi ya mbao ili usiku kuku wengine wanaposimama juu yake wasichafue kwa kinyesi chao kwenye viota. Viota hivi nilikuwa navitengeneza kwa kuweka partitions (yaani vijivyumba) kwa kutumia tofari za tope, zenye saizi kama ya matofali ya kuchoma. Kwa hiyo kwa kuambaa ukuta nilikuwa nalaza tofari nne chini kwenda juu, nilifanya hivyo kila baada ya upana wa futi moja, juu ya hizo tofali ndiyo niliweka Banzi! Ndani ya hivyo vijivyumba nilitifua umbo kama kijibeseni na kuweka Majani laini ili mayai yatulie yasisambae. Huko chumbani wakati wote kulikuwa na chombo chenye chakula na chenye maji! Hakuna kuku kutoka na hakuna kuku wa kuwaingilia! Ilikuwa ni incubator TOSHA! Nilikuwa nawaona kuku kama wananishukuru kwa kuwatengenezea mazingira safi maana walikuwa hawabughudhiwi na walikuwa wanashiba chakula vizuri tu! Nitaeleza siku nyingine juu ya harakati zangu za kutengeneza chakula na changamoto nilizokutana nazo! Huko chumbani nilikuwa nimetandaza carpet la nyasi; kando kando ya kuta zote kulikuwa na viota ambavyo nilivizamisha ndani ya hilo kapeti la nyasi nadhani mtanielewa! Ninaposema carpet la nyasi, ni nyasi tu nilizisambaza kwa unene wa kama sm 15 au nchi sita! Kwa hiyo kipindi hawa kuku wanapokuwa wanaatamia nilikuwa nazuia wengine wasiatamie hadi hawa watakapototoa! Kwa hiyo mayai yanayopatikana wakati hawa wengine wanaatamia nilikuwa ninakula na mengine kuuza maana mpango wangu ilikuwa kutotolesha mara moja tu kuku mia kwa mwezi! Hii ndiyo Incubator yangu ambayo nilikuwa ninatotolesha vifaranga 100 kwa siku moja!! Kwa kuwa nilikuwa ninajukumu pia la kulea kuku utotoleshaji nilikuwa ninaudhibiti uendane na miundombinu yangu ya kulea kuku na vifaranga.
   ========


  2. JEKI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th August 2013
   Posts : 1,652
   Rep Power : 89249469
   Likes Received
   549
   Likes Given
   539

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   mkuu Kubota Mungu akubariki.

  3. Tutor B's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th June 2011
   Location : Mwanza City Tanzania
   Posts : 3,735
   Rep Power : 117956
   Likes Received
   1282
   Likes Given
   458

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Quote By chama2chawa View Post
   Amani iwe nanyi!Nikitambo sijachangia uzi huu sio kwa sababu sikuwa na interest nao la hasha!Kwa kipindi kile uzi huu ulikuwa kama functionless kwangu kutokana na mazingira yangu hayakunuruhusu kabisa kufuga kibiashara ingawa nilikuwa natamani kufuga.Nikaona ni busara niweke uzi huu mkuu kama hazina hivyo kuamua kujiweka bize kutafuta njia za kujikwamua na mazingira yale,katika njia za kufanikisha hilo nimejukuta kwa miaka miwili iliyo pita nimepitia katika wakati mgumu na maisha yakukatisha tama sana ndugu wana jf hatahivyo,namshukuru MWENYEZI MUNGU kwa sasa ninavyo andika hii post nipo mahali ambapo naweza kufuga na kuwekeza katika miradi mingine,na nimeanza kufanya hivyo kwani hivi sasa nina kuku wakubwa kumi na nne na vifaranga kumi na tatu napia natarajia mnamo tarehere mbili mwezi huu kuwa na vifaranga wengine 25-30 kwani kuna kuku watatu wamelalia mayai thelathini.Nafikiri huu ndio umekuwa wakati wangu muafaka wa kutafuta hazina yangu ambayo ni hii thread,nashukuru kwa sasa uzi una michango mingi tofauti na hapo awali nilipo ishia ulikuwa na pages 13 ila kwa sasa una pages 43 naomba niwapongeze kwa hilo na naomba msikate tamaa kutuelimisha.Nimesomo pages zote na sasa nitaendelea kutoa mrejesho wa maendeleo ya ufugaji wangu ingawa ni mvivu kidogo kuandika ila nitajitahidi kadri ya uwezo kwa hili kuhakikisha nami natoa nilichokipata kwa manufaa ya wenzangu.MUNGU akubariki Kubota MUNGU awabariki Mama Joe,Chasha, Liverpoolfc,MamaTimmy,Guta,Fid el80,Aza,Asigwa,Chamilitary,An koeli,Poutry Sayuni na wengine wote ambao nimewasahau.
   Umefanya kilicho chema mkuu
   Kubota likes this.
   "Ebya nyenkya bibyalwa mbwenu" = Mavuno ya kesho hupandwa leo.

  4. bab-D's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd May 2015
   Posts : 922
   Rep Power : 507
   Likes Received
   136
   Likes Given
   3

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   We hapo umeshatobozea, jitahidi dawa tu, mimi niliwahi kufuga kuku wakafika 57, nikajisahau kuendeleza dawa, kilicho nikuta kila siku nikawa nakula kuku tatu hadi nne nanyingine kutupa, toka hapo hadi leo sijajipanga kufuga ingawa moyo ninao,pia kama una alovela wapatie uwezavyo ila isichukue zaidi ya siku nne mwaga na weka tena, pia otc ya unga inasaidia, pia dawa ya viroboto hakikisha viroboto haviwapati, safisha banda kila siku, hapo watasema unadawa, pamoja mkuu

  5. chama2chawa's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 5th October 2012
   Posts : 200
   Rep Power : 498
   Likes Received
   44
   Likes Given
   37

   Default

   Quote By bab-D View Post
   We hapo umeshatobozea, jitahidi dawa tu, mimi niliwahi kufuga kuku wakafika 57, nikajisahau kuendeleza dawa, kilicho nikuta kila siku nikawa nakula kuku tatu hadi nne nanyingine kutupa, toka hapo hadi leo sijajipanga kufuga ingawa moyo ninao,pia kama una alovela wapatie uwezavyo ila isichukue zaidi ya siku nne mwaga na weka tena, pia otc ya unga inasaidia, pia dawa ya viroboto hakikisha viroboto haviwapati, safisha banda kila siku, hapo watasema unadawa, pamoja mkuu
   Asante sana mkuu kwa kunitia moyo na ushauri wako nitaufanyia kazi.

  6. Mr Econ's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th March 2014
   Posts : 443
   Rep Power : 468
   Likes Received
   90
   Likes Given
   3

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   elimu ya kuku wa kienyeji naihitaji sana jamani.


  7. KakaJambazi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th June 2009
   Posts : 10,843
   Rep Power : 119107379
   Likes Received
   3625
   Likes Given
   3075

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Quote By Zanzibar Spices View Post
   Aisee hembu niambine mwenzenu mbumbumbu.
   Hivi Kuku wa Kienyeji kwa Kiingereza wanaitwaje?
   Na hawa Juju wengine(maana hata jina lao sijui niwekeje)wanaitwaje?

   Sasa akili yangu inaniambia
   -Kuku wa Kienyeji wanaitwa LOCAL CHICKEN
   -Sasa hawa wengine(tumezoea kuita wakizungu)inakuwaje,maana FOREIGN CHICKEN mhhh,hapa huwa nacheka mwenyewe

   Hembu mtujuze wataalam
   Usituletee mambo ya jukwa la mapenzi na facebook huku tafadhali. huku ni serious brains tu.
   Tutor B likes this.

  8. Tutor B's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th June 2011
   Location : Mwanza City Tanzania
   Posts : 3,735
   Rep Power : 117956
   Likes Received
   1282
   Likes Given
   458

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Quote By KakaJambazi View Post
   Usituletee mambo ya jukwa la mapenzi na facebook huku tafadhali. huku ni serious brains tu.
   Ndo maana watoto huwa hawaruhusiwi kuchangia mijadara ya wakubwa. Umefanya jambo la maana kumpa ukweli wake.
   "Ebya nyenkya bibyalwa mbwenu" = Mavuno ya kesho hupandwa leo.

  9. emmanepoultryfarm's Avatar
   Member Array
   Join Date : 8th August 2015
   Posts : 17
   Rep Power : 312
   Likes Received
   2
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By muonamambo View Post
   Kaka Kibanga Ampiga Mkoloni... Nilidhani kila kuku anabidi kuwa na mpenzi wake!!!!
   Mkuu umenifurahisha sana,halafu hapo uliposema kuku huwa hawatotoi wakt wa baridi nadhani ulimaanisha kutaga,ni kweli kutaga huathiriwa na hali ya hewa lkn unaweza kuwasaidia kwa kuwakinga na baridi.

  10. emmanepoultryfarm's Avatar
   Member Array
   Join Date : 8th August 2015
   Posts : 17
   Rep Power : 312
   Likes Received
   2
   Likes Given
   0

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Jmn hii bei ya chakula inanitesa kwakweli,hivi nikichanganya pumba na virutubisho km dcp kuku wangu watakua vizuri?hapa nazungumzia kuku wakubwa wa miezi 5 hadi 6.

  11. emmanepoultryfarm's Avatar
   Member Array
   Join Date : 8th August 2015
   Posts : 17
   Rep Power : 312
   Likes Received
   2
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By Muangila View Post
   Msaada wakuu nimenunua kuku wa kienyeji watatu kwa ajili ya kuanza ufugaji na nina jogoo mmoja tatizo langu hawa kuku wanataga mfululizo hawalalii mayai nimekusanya mayai zaidi ya 60 naengine ninakula lakini hawaonueshi kulalia nifanyeje ili haya mayai nipate vifaranga?
   Inawezekana hao kuku ni chotara na sio kienyeji pure,kienyeji lazima alalie mayai,ni ngumu kutofautisha kati ya kienyeji pure na chotara,tafuta kienyeji Kazi yake iwe kuatamia au tafuta Incubator.

  12. tired's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 25th February 2014
   Location : Canada
   Posts : 101
   Rep Power : 405
   Likes Received
   21
   Likes Given
   21

   Default

   Quote By Kubota View Post
   Mkuu Msuruhishi, tunashukuru sana kwa kututia moyo tutashukuru sana iwapo utatimiza lengo lako maana hapo ndipo lengo na manufaa ya JF yatakapodhihirika! Tutashukuru sana kama mara moja moja ukipita na kuchangia chochote utakachokutana nacho huko kuweza kujazia mawazo, ukikutana na changamoto zozote tushirikishane, na usiache kutoa mwendelezo wa harakati zako huko! Hongera kwa kutengeneza Encyclopedia ninaamini Volume two itakuwa ni ushuhuda wa wachangiaji!!
   Vifaranga wa wiki 2 ninaweza kuwapa MLONGE au Muarobaini kwa ajilia ya kinga

  13. ferre.g's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd March 2013
   Location : MWANZA
   Posts : 2,191
   Rep Power : 1013
   Likes Received
   301
   Likes Given
   159

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Mods.. Huu Uzi uwekeni juu uwe sticky thread..... Unahamahama sana na ukizingatia una points za uhakika. Tupeni msaada huo


  Page 44 of 44 FirstFirst ... 34424344

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...