JamiiSMS
  Show/Hide This
  Report Post
  Page 42 of 42 FirstFirst ... 32404142
  Results 821 to 835 of 835
  1. #1
   Kubota's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st October 2012
   Posts : 494
   Rep Power : 103864161
   Likes Received
   700
   Likes Given
   627

   Default Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Wana Jf,

   Kuna maandiko mengi JF ya ufugaji Kuku wa Kienyeji! Nawasilisha kwenu wadau wa JF mbinu ambazo kwa mikono yangu nimezitumia kutatua changamoto za kuku wa kienyeji! Nimeandika kuwalenga wajasiliamali ambao hawana nguvu kifedha kujenga mabanda kisasa, mashine kutotolesha vifaranga, kutibu magonjwa wala kujenga wigo (fence) n,k. Naomba mzijue mbinu hizi nisije kufa nazo, huu ni mchango wangu kwenu watanzania wenzangu wale ambao mtakuwa hamjawahi kuzisikia mbinu hizi. Mbinu hizi baadhi nilisoma vitabuni nikazijaribu na kuziboresha kwa mazingira yangu duni! Mbinu zingine niliziona kwa wakulima duni kama mimi nikazitumia na kuleta mafanikio makubwa, mbinu zingine nilizigundua mwenyewe na nikafanikiwa sana. Hizi mbinu hazijafanyiwa utafiti rasmi lakini nimeweza kufanikiwa kuwa na kundi kubwa la kuku kwa haraka sana kupitia ujanja huu!!

   Mdau wa JF nakualika utembelee uzi huu mara kwa mara kila upatapo fursa ili uweze kufuatilia simulizi yangu maana itakwenda kwa vipande vipande. Mnakaribishwa kuchangia uzoefu wenu ili tuboreke zaidi.

   Mbinu hizi zitagusia zaidi: Utotoreshaji vifaranga vingi kwa mara moja bila kutumia mashine! Ukuzaji wa vifaranga vingi kwa njia rahisi na kwa haraka zaidi, ulinzi wa kuku dhidi ya wanyama maadui, kudhibiti kuku wasizurule, magonjwa niliyofanikiwa kuyadhibiti, ujenzi wa vibanda wenye kukidhi mahitaji mbali mbali. Ni utaalamu nilioupata kwa gharama kubwa na mahangaiko ya muda mrefu, nauleta kwenu ili sote tuendelee kukua pamoja kiujasilia mali.

   Stay tuned and keep on visiting this thread!!


   ===============
   UPDATE
   ===============


   Quote By Kubota View Post
   Safari yangu ilianza baada ya kukutana na mhamasishaji aliyenitia chachu kwamba 10 x10 x 10 you become a millionea! Kwamba ukianza na kuku 10 kila mmoja akazaa 10 na hao watoto na mama zao wakazaa kila mmoja 10 unakuwa millionea! Wakubwa kuongea ni rahisi utekelezaji ukawa mgumu sana! Changamoto kuu aipatayo mfugaji wa kuku wa kienyeji ni kuzalisha vifaranga wengi na kuweza kuwakuza! Bila hivyo kundi haliwezi kukua na kukupa kipato cha uhakika!

   Safari ya ufugaji niliianza kwa kununua mitetea 30 na jogoo watatu! Ilibidi nisubiri muda hadi kuku waanze kutaga! Muda ukafika kuku wakaanza kutaga kwa fujo sana! Nilikuwa na banda moja tu ambamo kuku wote walikuwa wakilala humo. Nilitengeneza viota vingi kwa ajili ya kuku kutagia. Asubuhi nilikuwa nawafungulia! Changamoto nilizoanza kupambana nazo kwanza kama mjuavyo kuku tofauti walikuwa wanataga kwenye kiota kimoja! Ilipofika wakati wa kuatamia ikawa kila kwenye kiota kimoja kuna kuku kadhaa wamebanana wanaatamia! Hali hii haipaswi kutokea kwani kuku mmoja anaweza kuwa amejilundikia mayai mengi ambayo hawezi kuyapajoto la kutosha na kuku mwingine anakuwa amekaa kando tu hana hata yai moja. Hii ilibadilika ikawa kero kubwa! Nilijua utotoaji unaweza kuathirika sana!

   Ili utotoreshe vifaranga vingi kwa wakati mmoja badala ya kutumia incubator, tumia hao hao kuku. Wakianza kutaga kila siku okota mayai na kuyahifadhi mahali salama ili kuku wasiyatie joto! Kuku wengi wanapotaga kwa pamoja hufikia wakati mayai huishatumboni unakuta wamelala kwenye viota wakiwa wameatamia mayai yaliyopo au udongo tu! Kuku anaekuwa amefikia kuatamia utamjua kwani ukimshitua haondoki kwenye kiota. Kuku anaetaga ukimshitua hukimbia! Kwa hiyo kama nimepanga kutotolesha vifaranga 100 kwa mara moja nikishagundua kuwa kuna kuku 8 wameanza kuonesha dalili ya kuatamia hapo husubiri usiku ninawawekea mayai amabayo nilikuwa nimeyahifadhi. Ambapo mimi huwekea kila kuku mayai 15. Kwa hiyo kuku 8 hufanya jumla ya mayai 120. Kwa kuwa banda langu ni hilo moja tu kuku wengine wanaoendelea kutaga walikuwa wanaendelea kutagia kwenye viota ambavyo kuku wengine walikuwa wanaatamia! Hali hii ilikuwa inaleta tabu sana kwani ilikuwa si rahisi kutambua mayai mapya na yenye siku nyingi. Kuondoa shida hii nilinunua MARKER PEN (rangi yoyote) na siku ya kuwawekea mayai kuku ili waatamie niliyachora mduara kuzunguka yai ili iwe rahisi kuyatambua mayai mapya. Huo mchoro hauwatishi kuku na hakuna dosari yoyote. Kwa hiyo kila siku jioni ninapokuja kuokota mayai yaliyotagwa nilikuwa pia nakagua kila kiota cha kuku walioatamia na kuondoa mayai mapya. Kumnyenyua kuku anaeatamia na kuondoa yai haileti shida yoyote!

   Kuku akifikia wakati wa kuatamia ukamnyima mayai hawa wanatabia kuendelea kung'ang'ania kuatamia, hapo ilibidi kutengeneza JELA! Watu wengine wanambinu tofauti kumwachisha kuku asiatamie! Mbinu ya kumtia kuku stress inafanya kazi nzuri sana! Jela inaweza kuwa ni Tega, au Box kubwa au chumba kidogo kilichopo. Ukimfungia kuku JELA bila maji wala chakula kwa kutwa mbili siku ukimfungulia akili yake huwa ni kutafuta chakula tu hakumbuki kurudi kwenye kiota! Njia hii ilifanikiwa sana na ilifanya kuendesha shughuri zangu bila bughudha! Kuna wakati JELA ilikuwa na kuku kibao hivyo unapaswa kutengeneza kibanda cha JELA. Hawa kuku wakitoka JELA hutaga mapema sana amabapo bila hivyo wangekuwa wanaatamia. Pia kuku wakishaatamia kwa muda wa siku 10 nilikuwa nayapima mayai ili kubaini kama kuna mayai yasiyoweza kuanguliwa! Ni rahisi sana kama una Tochi! Ukimulika yai Kwa kulizungushia vidole kiganjani kama ni yai zima linakuwa na giza kama ni yai bovu linapitisha mwanga kama yai lililotagwa siku hiyo! Jinsi ya kuzungushia vidole yai, tengeneza duara kwa vidole vyako na dole gumba kisha pachika yai katikati ya duara ili mwanga wa tochi upenye kwenye yai! Kwahiyo unaweka tochi inayowaka chini ya yai na hii ifanyike gizani au ndani ya chumba chenye mwaga mdogo. Kadri ya yai linavyokaribia kutotolewa ukilimulika huwa na giza zaidi! Ukimulika mayai toa mayai yasiyoweza kutotolewa maana hayo hutumia joto la Mama bure!

   Ndugu zangu wana JF naendelea kuelezea utotoleshaji bado sijamaliza hebu niwarushie hii kwanza maana nimeona nimechelewesha kuwakilisha na nimewaudhi, poleni, mwenzenu nilikuwa nahangaika kufukia tanuru la mkaa nimekuta limefunguka! Si mnajua maisha jamani!
   Invisible, Nyamgluu, RR and 100 others like this.


  2. naxon's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th December 2014
   Posts : 311
   Rep Power : 383
   Likes Received
   87
   Likes Given
   2521

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Mhh hili bonge la somo.
   MILCAH28 likes this.

  3. MANI's Avatar
   JF Tanzanite Member Array
   Join Date : 22nd February 2010
   Location : CHINI YA MBUYU
   Posts : 4,395
   Rep Power : 429497879
   Likes Received
   2024
   Likes Given
   3642

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Hii shule nzuri sana na mimi natamani nianze hii shughuli
   MILCAH28 likes this.
   " TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA"

  4. MILCAH28's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th July 2014
   Location : KILIMANJARO
   Posts : 735
   Rep Power : 489
   Likes Received
   107
   Likes Given
   405

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Nilianza na Kuku wawili mwaka Jana may now napapasa Kuku 200 wa kienyeji hadi June...nitakuwa muuzaji mkubwaaa wa mayai ya kienyeji....
   Mpangamji likes this.
   Baba milcah

  5. Ibra6's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd June 2013
   Posts : 287
   Rep Power : 457
   Likes Received
   51
   Likes Given
   0

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Kubota pitia mala kwa mala hapa kijiweni,nina imani mpaka sasa ulisha boresha mradi wako wa mkaa, siku hizi unatengeza mkaa wa kisasa sio ule wa kuharibu mazingira

  6. chamilitary's Avatar
   Member Array
   Join Date : 30th January 2015
   Posts : 18
   Rep Power : 316
   Likes Received
   4
   Likes Given
   1

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Habari yenu jf nimekuwa nikifuatilia tangu mwanzo na nimefurahishwa sana na kazi nzuri za Kubota na member wengine kwenye hii thread ila sasa nimeona nijitambulishe kwenu kama mtaalamu wa maswala ya mifugo hasa ufugaji wa ndege wafugwa na kuku.
   lengo langu sio kukusanya mapato kwasasa ila kujaibu kuinua Tanzania yangu kwa uwezo wangu mdogo nilionao..nimeshangazwa sana na tarehe ya mwisho ya post hii ilikuwa 2013 ila natumai bado mtakuwepo.
   tuendelee kuwasiliana.


  7. Kaundime2's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 24th February 2015
   Posts : 246
   Rep Power : 358
   Likes Received
   79
   Likes Given
   319

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Kubota yuko vizuri

  8. malamsha shao's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 23rd September 2012
   Location : Arusha & rombo
   Posts : 153
   Rep Power : 466
   Likes Received
   21
   Likes Given
   13

   Default

   Quote By chamilitary View Post
   Habari yenu jf nimekuwa nikifuatilia tangu mwanzo na nimefurahishwa sana na kazi nzuri za Kubota na member wengine kwenye hii thread ila sasa nimeona nijitambulishe kwenu kama mtaalamu wa maswala ya mifugo hasa ufugaji wa ndege wafugwa na kuku.
   lengo langu sio kukusanya mapato kwasasa ila kujaibu kuinua Tanzania yangu kwa uwezo wangu mdogo nilionao..nimeshangazwa sana na tarehe ya mwisho ya post hii ilikuwa 2013 ila natumai bado mtakuwepo.
   tuendelee kuwasiliana.
   kama mtaalam wa ndege wafugwao 2pia maujanja

  9. BabaG.com's Avatar
   Member Array
   Join Date : 5th March 2015
   Posts : 12
   Rep Power : 310
   Likes Received
   2
   Likes Given
   3

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Mkuu kubota natumai bado unapita huku,,.naomba fanya study tour hapo shamban kwako moro..!!namba yangu 0764396335..thnx..!
   Kubota likes this.

  10. TODAYS's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th April 2014
   Posts : 497
   Rep Power : 37552236
   Likes Received
   171
   Likes Given
   310

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Kubota likes this.

  11. TODAYS's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th April 2014
   Posts : 497
   Rep Power : 37552236
   Likes Received
   171
   Likes Given
   310

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Sasa ndugu hiki kinyesi cha tumboni si inabidi ukae karibu na machinjio ya ngombe ili ukipate?
   Vingnevo kwa siye wa mjini imekula kwetu !.

   Quote By rashid seif View Post
   mama timmy mimi si mgeni sana hapa jf.Huwa si comment chochote nachukuwa tu maujuzi.Ila nimeona nitoe mchango wangu kwa hili.Tafuta kinyesi cha ng'ombe cha tumboni (inabidi upate aliyechinjwa) jaza kinyesi kwenye mfuko wa rambo,funga mfuko vizuri,chimba shimo,fukia na uache kwa muda wa week 1 then fukua utakuta funza wakubwa sana. n.b. Nimeelekezwa sijajaribu.

  12. Pdidy's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd November 2007
   Posts : 20,321
   Rep Power : 316823603
   Likes Received
   3265
   Likes Given
   3390

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Kubota the best
   mkuu kibota hongera sana ingawa watu wanaalalamika tunajazana wote mmu wakati uko mtaalamu humu embu rudi basi kama jamaa alivyosema ameshtuka kuona sikuyamwisho ya hii thread ...usimwambie mtu

   hope to s ee u soon ..kama vipi anzisha tuition kabisa tukusanye mema ya nchi mpwa via emails vs

   mpesa .tigopesa.airtelmny
   Kubota likes this.

  13. Pdidy's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd November 2007
   Posts : 20,321
   Rep Power : 316823603
   Likes Received
   3265
   Likes Given
   3390

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Bible ikowazi jamani alaaniwe apokeae bure msihisi zaka na sadaka ni maneno ya watu yale ni maandiko
   so kabuta kwakuwa umekaa kimyaa sikunyingi naona unaweza anzisha tuition tukaangalia na wewe tunakuwezeshaje uongeze idadi ya kuku wa wako na account yako mpwa ya simbanking
   Kubota likes this.

  14. BabaG.com's Avatar
   Member Array
   Join Date : 5th March 2015
   Posts : 12
   Rep Power : 310
   Likes Received
   2
   Likes Given
   3

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Hv wadau,mkuu kubota amepotelea wapi?au ndio yuko porin anachoma mkaa...
   Kubota likes this.

  15. chamilitary's Avatar
   Member Array
   Join Date : 30th January 2015
   Posts : 18
   Rep Power : 316
   Likes Received
   4
   Likes Given
   1

  16. Hikma's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th April 2012
   Location : Pwani
   Posts : 352
   Rep Power : 22843910
   Likes Received
   229
   Likes Given
   168

   Default Re: Zijue Mbinu zangu: Ufugaji Kuku wa Kienyeji

   Wakuu habari zenu,

   Baada ya kupata uhamasishaji wa kutosha hapa niliamua kurudi tena katika ufugaji wa kuku.
   Nimeanza na kuku wa kienyeji. Nina makoo watano, jogoo kinda moja na jogoo kongwe moja.

   kesi niliyonayo ni kuwa makoo yote yalianza kutetea na kutaga kipindi kimoja.
   nilipoona hali hiyo niliamua kununua mfuko wa layers finisher na kuwapa.
   wameporomosha mayai ya kutosha na sasa watatu wanalalia na wawili wanaendelea kutaga.
   hofu yangu ni kuwa je mayai haya yatakuwa na ubora wa kuangulisha vifaranga?

   Naombeni uzoefu wenu magwiji.
   Kubota likes this.
   "Penda wapate watu kile upendacho ipate nafsi yako"(Mtume Muhammad (S.A.W)


  Page 42 of 42 FirstFirst ... 32404142

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...