Wana Jamii,
Habarini ya mapumziko?
Naomba msaada wenu kupata maelekezo juu ya Biashara ya Chumvi.
Nataka kuwekeza kwenye usagaji na upakiaji wa chumvi ya baharini kwa matumizi ya binadamu na mifugo. Shughuli yangu itakuwa kununua chumvi toka kwa wamiliki wa mabirika ya chumvi halafu nitasaga, niweke Iodine na kupakia katika vifuko vya ujazo mbalimbali, kisha nitasambaza kwa wauzaji wa Jumla. Soko langu tarajiwa ni Kanda ya Ziwa
Naomba msaada wa uzoefu toka kwa yeyote aliyewahi kufanya Biashara katika sekta hii. Na mambo ambayo sina ufahamu nayo ni pamoja na:
- Nahitaji machine (mfano grinder) za aina gani, nitazipata wapi na vigezo gani nitumie kuzichagua?
- Nahitaji leseni na vibali vya aina gani kufanya hii Biashara rasmi?
- Mambo gani ni muhimu kuzingatia toka awali ili kuepuka hasara?
Natanguliza shukrani kwa wale woote watakao nipa mwangaza.
Maruk Vanilla Farming and Processing (MVFP) Ltd,
P.O Box 1361, Bukoba
Mob: 0717972957/0786972958
E-mail: [email protected]


Reply With Quote


Follow Us Here