Wajameni, habari za mishe mishe. Najitokeza humu jamvini nikijua humu ni darasa murua la kuelimishana hususani ktk ujasiriamali. Naomba msaada wenu, natarajia kuanza ufugaji kuku wa kienyeji kibiashara na ningependa kujua kama kuwa na mashine yangu ya kutotoa mayai (incubator) ni njia mwafaka. Mahali ninapoishi umeme haujafika, hivyo nikiwa na mashine itabidi kununua mafuta ya taa au dizeli.
1. Kuna thread niliwahi kuisoma jamvini humu kuwa kuna watu wanatotolesha kwa malipo. Je, ni njia ipi yaweza kuwa gharama nafuu kati ya kuwa na mashine mwenyewe (kununua mafuta) na kutotolesha kwa watu?
2. Kama kuendesha incubator ni nafuu kuliko kutototlesha kwa watu, Je, naweza kuipata mashine hiyo sehemu gani au kwa nani na kwa gharama kiasi gani? Kulingana na mtaji wangu, tuseme nahitaji yenye uwezo kuanzia mayai 100 na kuendelea.
Nawasilisha kwa maelekezo yenu

Reply With Quote
Follow Us Here