JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Kilimo cha Maembe: Ushauri na masoko yake

  Report Post
  Page 2 of 5 FirstFirst 1234 ... LastLast
  Results 21 to 40 of 94
  1. Chief's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th June 2006
   Posts : 1,228
   Rep Power : 1033
   Likes Received
   190
   Likes Given
   365

   Default Kilimo cha Maembe: Ushauri na masoko yake

   Msaaada tafadhali wajemeni. Nina shamba mahala ambapo nataka kupanda miembe. Ushauri? Wapi ntapata miche ya miembe?

   Nipo Dar
   Quote By Kichakoro View Post
   Mkuu salam u nyingi na karibu kwenye kilimo

   Wauza miche ni wengi sana Dar es Salaam na kwingineko lakini wauzaji miche bora ni wachahche sana.
   Hivyo ni vema ukafahamu mahali pa kupata miche bora( ya kiisasa ama ya kienyeji iliyoboreshawa)

   Kwanza kabisa Tambua mbegu bora: Kuna aina kama 17 ya mbegu bora za embe kwa ajili ya matumizi na masoko
   tofauti. Hivyo tambua kwanza soko lako linataka nini kisha chagua mbegu iendanayo na soko/matumizi yako.

   Kuna mbegu kama sita ivi kwanza BOLIBO (ya kienyeji lakini iliyoboreshwa), Kuna alfonso, Keit, Kent, Apple ambazo
   ni tamu hazina nyuzi nyuzi nyingi, zina zaa sana kati ya tunda 400 - 3000, ukubwa wake ni 0.25kg - 1.3kg nk.

   Hivyo kabla hujaenda kununua hizo embe ni vyema ukatambua sifa ya kila mojawapo (hata ukigoogle utapata).

   Wauzaji kama nilivyosema wapo wengi ila kuna association of Mango growers (AMAGRO) wapo mtaa wa Mkurumah karibu petrol station wale wanawajua wadau wenye vitalu vyenye mbegu za uhakika nchi nzima.

   Mimi nafahamu wachache
   1. Dr. Diwani anacho kitalu Kinondoni karibu na makaburini na ni Mkulima mkubwa sana wa embe wilayani Mkuranga hivyo yeye anazo mbegu za Uhakika.

   2. Kuna kitalu Rufiji - Kibiti kinamilikiwa na kikundi cha wakulima (Rufiji Environmental Group) ambao walipata tuzo mwaka jana Nanenane ukifika kibiti karibu na kituo cha polis utaona bango lao

   3. Chambezi Research Sub station kipo bagamoyo 5km kabla hujafika bagamoyo kuna kibao chao on the left hand side uningia ndani about 3km wana aina karibu zote 17 za embe za kisasa

   4. SUA wanazo hizo mbegu pia unaweza ukazipata ingawa zitakua ghali kidogo

   5. Mkuranga Research substation nao wana mbegu bora za miche ya miembe wapo few km (3-5) kutoka njia ya kwenda halmashauri ya wilaya ya mkuranga.

   Angalizo: Wapo wajasiriamali wengi wanauza micha ya embe wengine kweli ni nzuri na za uhakika lakini wengine wameiga tu na kuingia kwenye hiyo fani.

   Mfano: ukiotesha kokwa la embe yeyote linalozaa sana halafu ukaweka kikonyo cha embe bora halafu ikatokea chipukizi chini ya sehemu iliyoungwa(grafting) kama lisipokatwa na kuachwa na ikitokea kikonyo kilichoungwa kimekauka mche utaendelea kuwa wa kienyeji na sio wa kisasa.
   Imeboreshwa zaidi:   Maembe hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Tabora, Pwani, Mtwara, Tanga, Mwanza, Morogoro na Mbeya. Uzalishaji wake ni wastani wa tani 159,472 kwa mwaka. Maembe ni zao muhimu la biashara na chakula.

   MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI
   Ili kupata mazao bora ni muhimu kuzingatia kanuni bora za kilimo cha maembe hasa kanuni
   zifuatazo:
   Kuchagua aina bora ya kupanda kulingana na mahitaji ya soko.

   DHIBITI MAGONJWA, WADUDU, NA MAGUGU

   • Fanya ukaguzi wa shamba mara kwa mara ili uweze kudhibiti wadudu na magonjwa ya matunda kabla madhara hayajawa makubwa

   UGONJWA WA KUTU KWENYE MAJANI   • Ni muhimu kudhibiti wadudu, magonjwa na magugu ili kupata mazao bora ambayo yatapata soko zuri na kuweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
   • Hakikisha shamba ni safi wakati wote ili kupata matunda bora na kurahisisha uvunaji.

   MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA

   Kusafisha shamba pamoja na barabara za shamba
   • Safisha shamba ili kurahisisha uvunaji na usafirishaji shambani.
   Kukagua shamba kuona maembe kama yamekomaa Maembe hukomaa katika kipindi cha miezi 4 hadi-6 tangu kutoa maua kutegemea hali ya hewa na aina.

   DALILI ZA MAEMBE YALIYOKOMAA

   • Maembe hung’ara
   • Kwa aina nyingine rangi ya kijani hufifia na kuanza kubadilika kuwa ya manjano.

   ANDAA VIFAA VYA KUBEBEA, SEHEMU YA KUFUNGASHIA NA USAFIRI.

   VIFAA VYA KUBEBEA
   • Ngazi
   • Vikapu
   • Mifuko
   • Ndoo
   • Vichumio

   VIFAA VYA KUFUNGASHIA
   • Makasha ya mbao/plastiki na ya makaratasi magumu na matenga

   VYOMBO VYA KUSAFIRISHIA
   • Matoroli
   • Magari
   • Baiskeli
   • Matela ya matrekta

   KUVUNA
   Njia bora ya kuvuna maembe ni Kuchuma kwa mkono
   • Kwa miembe mifupi chuma maembe pamoja na kikonyo chake
   • Kwa miembe mirefu chuma kwa kutumia kichumio maalumu

   KICHUMIO MAALUM

   • Acha kikonyo chenye urefu wa sentimita tatu hadi nne ili kuzuia madoa ya utomvu. Utomvu huchafua matunda na hushusha ubora. Pia embe lililovunwa bila kikonyo chake huingiliwa na vimelea vya ugonjwa kwa urahisi.
   • Vuna wakati wa asubuhi au jioni ili kuepuka jua kali linaloweza kubabua matunda.
   • Wakati wa kuvuna hakikisha maembe hayadondoshwi chini, ili kuepuka kuchubuka kwa matunda ama kupondeka hasa yale yaliyoiva barabara. Aidha beba matunda kwa vikapu au mifuko na kusanya kwenye kivuli.   KUCHAMBUA MAEMBE
   Kuchambua ni kutenga matunda yaliyooza, kupasuka, yenye dalili za magonjwa au kubonyea, ili kupata matunda yenye ubora kwa ajili ya matumizi, kusindika au kuuza.
   • Matunda yaliyooza na yenye wadudu ni vyema yafukiwe ili kuzuia kuenea kwa wadudu waharibifu na vimelea vya magonjwa.
   • Matunda yaliyopasuka, kubonyea , kuchubuka kidogo wakati wa kuvuna au kuiva sana yatumike haraka kwa chakula.
   • Matunda mazuri ambayo hayajapata madhara yoyote yatunzwe kwa ajili ya kusindikwa, kutumika au kuuzwa.

   KUSAFISHA MAEMBE
   • Baada ya kuchambua, safisha matunda kwa maji safi ili kuondoa uchafu na mabaki ya madawa.
   • Maembe yanayokusudiwa kuuzwa nje ya nchi hunyunyiziwa nta ili kuzuia kunyauka na kudumisha ubora.
   • Baada ya kusafisha tumbukiza maembe kwenye maji yenye nyuzi joto zipatazo 52 za Sentigredi kwa muda wa dakika tano. Maji haya pia yanaweza kuchanganywa na madawa ya klorini asilimia 1 ili kuzuia magonjwa ya ukungu.

   KUPANGA MADARAJA
   Madaraja hupangwa kwa lengo la kurahisisha ufungashaji, usafirishaji na uuzaji. Madaraja hupangwa kulingana na ubora, ukubwa , aina rangi na uivaji.

   KUFUNGASHA MAEMBE

   Ufungashaji hufanyika katika sehemu safi na yenye kivuli. Ufungashaji wa kujaza kupita kiasi husababisha upotevu wa maembe. Aidha ubora hushuka kutokana na kuminyana na kubonyea kwa matunda wakati wa kusafirisha

   TENGA LA KUFUNGASHIA MAEMBE   Inashauriwa kufungasha kwenye makasha ya mbao/ plastiki , makaratasi magumu au tenga kwa sababu zifuatazo:
   • Matunda yanaweza kupangwa na kusafirishwa bila kuchubuka, kubonyea au kupasuka.
   • Huweza kupakiwa na kupakuliwa kwenye chombo cha usafiri kwa urahisi.

   Wakati wa ufungashaji ni muhimu kuzingatia yafuatayo:
   • Kasha moja lisizidi uzito wa kilo 20 ili kurahisisha ubebaji.
   • Makasha yawe imara na yenye matundu ya kutosha ili kuruhusu mzunguko wa hewa.
   • Ni muhimu kutanguliza vitu vilivyo safi ndani ya vifungashio ili kuzuia michubuko na mipasuko ya matunda wakati wa kusafirisha.
   • Maembe yapangwe kwa kubananisha na kwa kuhakikisha kuwa vikonyo havitoboi matunda na kusababisha majeraha wakati wa kusafirisha. Kubananisha matunda husaidia kuzuia mgongano unaoweza kusababisha matunda kusambaratika na hivyo kubonyea au kupasuka wakati wa kusafirisha.

   KUSAFIRISHA

   Ili kuepuka upotevu na uharibifu wakati wa kusafirisha, ni muhimu maembe yapangwe kwenye vyombo vya kufungashia na kusafirisha kwa uangalifu, ndani ya matela, mikokoteni na magari. Epuka kutupa matunda wakati wa kupakia na kupakua. Wakati wa kupanga mazao katika vyombo vya usafiri yasirundikwe ovyo na yasijazwe kupita kiasi ili yasimwagike. Vilevile yafunikwe ili yasipigwe na jua. Jua huongeza kasi ya kuoza. Matunda yakipigwa na jua kwa muda wa saa mbili mfululizo husababisha kuoza kwa asilimia 100.

   KUHIFADHI

   • Maembe huweza kuhifadhiwa kwenye chumba chenye hali ya hewa yenye joto la nyuzi 8 hadi 10 za Sentigredi na unyevu wa asilimia 85 hadi 90. Katika hali hiyo, maembe yanaweza kuhifadhiwa bila kuharibika kwa mwezi mmoja.
   • Kagua mara kwa mara ili kugundua uharibifu unaoweza kutokea  2. ngoshas's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th January 2011
   Posts : 696
   Rep Power : 685
   Likes Received
   168
   Likes Given
   173

   Default re: Kilimo cha Maembe: Ushauri na masoko yake

   One point five kilometa sio mbali, tafuta mkokoteni wa kuchukua kiasi cha lita 200 kwa safari moja. Kama hukai shambani jenga kibanda weka mtu ambaye utakuwa unamlipa kiasi utakachoelewana nae, kazi yk inakuwa kunyweshea miti yk na kutunza shamba kwa ujumla. It works mi natumia hy kwa shamba la mananasi

  3. ngoshas's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th January 2011
   Posts : 696
   Rep Power : 685
   Likes Received
   168
   Likes Given
   173

   Default re: Kilimo cha Maembe: Ushauri na masoko yake

   Kuna shamba la miche la serikali pale visiga karibu na mlandizi, 2500 kwa mche, aina zote zipo

  4. elmagnifico's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th July 2011
   Location : Brussels
   Posts : 3,094
   Rep Power : 2900
   Likes Received
   1153
   Likes Given
   222

   Default re: Kilimo cha Maembe: Ushauri na masoko yake

   hivi miche ya maembe inachukua muda gani mpaka ianze kutoa matunda

  5. elmagnifico's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th July 2011
   Location : Brussels
   Posts : 3,094
   Rep Power : 2900
   Likes Received
   1153
   Likes Given
   222

   Default re: Kilimo cha Maembe: Ushauri na masoko yake

   hivi hectre 1 ya miche ya maembe inachukua maji kiasi gani na unamwagilia kwa muda gani nikiwa nina maana mfano miaka 2 au mingap

  6. sexologist's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th December 2010
   Location : ITONGOITALE - SHINYANGA
   Posts : 2,300
   Rep Power : 129084
   Likes Received
   908
   Likes Given
   707

   Default Soko la maembe

   Wakuu nawaheshimu sana.. salaam!!!

   ninaomba msaada wa kimawazo kwa anayefahamu channel/soko la maembe hapa nchini..

  7. GOOGLE's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th October 2012
   Location : MIREMBE HOSPITAL
   Posts : 1,467
   Rep Power : 747
   Likes Received
   291
   Likes Given
   21

   Default Re: Soko la maembe

   Uko wap mkuu.??

  8. sexologist's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th December 2010
   Location : ITONGOITALE - SHINYANGA
   Posts : 2,300
   Rep Power : 129084
   Likes Received
   908
   Likes Given
   707

   Default

   Quote By GOOGLE View Post
   Uko wap mkuu.??
   nipo Kahama kiongozi... tuna maembe mengi sana!!

  9. Lukolo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd December 2009
   Location : Iringa
   Posts : 5,117
   Rep Power : 86242787
   Likes Received
   3034
   Likes Given
   2058

   Default Natafuta miche ya miembe na michungwa

   Mwenzenu nimeamua kujaribu kilimo maeneo ya Mkuranga na nimepanga kupanda miembe huko. Sasa natafuta mahali ambapo ninaweza kupata miembe na michungwa bora ya muda mfupi ambayo haijachakachuliwa. Nimeshaambiwa na baadhi ya watu kwamba niende Morogoro, lakini nafikiri huko ni mbali sana. Naomba kujua kama ninaweza kupata hii miche hapa maeneo ya Dar es salaam.
   Mama Joe likes this.
   Kama mtu alikuwa waziri au hata mkuu wa mkoa katika serikali ya Kikwete, hafai kuwa Rais wa Tanzania. Kimsingi mtu huyo ni sehemu ya uongozi mbovu na wa hovyo ulioliingiza taifa letu katika umaskini mkubwa na mdororo wa uchumi tulionao sasa. Kama mtu huyu alijua namna ya kuiokoa nchi na hakufanya hivyo, ina maana alitusaliti watanzania na hafai kuwa Rais wa nchi. Kama hakujua ni nini cha kumshauri Kikwete ili Mambo yaende sawa, ina maana hana analolijua. Je anataka awe Rais ili afanye nini ilihali hakuna alijualo?

  10. commited's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th February 2012
   Posts : 1,519
   Rep Power : 63388957
   Likes Received
   745
   Likes Given
   137

   Default Re: Natafuta miche ya miembe na michungwa

   ungekuwa mitaa ya moshi au arusha ningekusaidia mkuu, kwa zone hiyo sina mtu,, pole mkuu, wadau wanakuja watakusaidia... hongera kwa ujasiria mali maana ajira zimekuwa wizi mtupu,,,,
   Lukolo likes this.
   KUENDELEA KUICHAGUA SISIEMU NI KUCHAGUA UMASKINI NA MAJANGA. TUSHIRIKIANE KUITOKOMEZA.

  11. Lukolo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd December 2009
   Location : Iringa
   Posts : 5,117
   Rep Power : 86242787
   Likes Received
   3034
   Likes Given
   2058

   Default Re: Natafuta miche ya miembe na michungwa

   Quote By commited View Post
   ungekuwa mitaa ya moshi au arusha ningekusaidia mkuu, kwa zone hiyo sina mtu,, pole mkuu, wadau wanakuja watakusaidia... hongera kwa ujasiria mali maana ajira zimekuwa wizi mtupu,,,,
   Nashukuru sana mkuu kwa utayari wako kunisaidia. Ngoja niendelee kungoja labda atajitokeza mmojawapo anayejua.
   Kama mtu alikuwa waziri au hata mkuu wa mkoa katika serikali ya Kikwete, hafai kuwa Rais wa Tanzania. Kimsingi mtu huyo ni sehemu ya uongozi mbovu na wa hovyo ulioliingiza taifa letu katika umaskini mkubwa na mdororo wa uchumi tulionao sasa. Kama mtu huyu alijua namna ya kuiokoa nchi na hakufanya hivyo, ina maana alitusaliti watanzania na hafai kuwa Rais wa nchi. Kama hakujua ni nini cha kumshauri Kikwete ili Mambo yaende sawa, ina maana hana analolijua. Je anataka awe Rais ili afanye nini ilihali hakuna alijualo?

  12. matumbo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th July 2011
   Posts : 6,660
   Rep Power : 0
   Likes Received
   3401
   Likes Given
   1540

   Default Re: Soko la maembe

   Soko la maembe ni kubwa mbona kila sehemu..Dsm maembe buguruni na kariakoo pale soko la kutosha njoo ufanye utafiti kabla hayajaozea shambani.
   Mkeshahoi likes this.

  13. matumbo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th July 2011
   Posts : 6,660
   Rep Power : 0
   Likes Received
   3401
   Likes Given
   1540

   Default

   Quote By Lukolo View Post
   Nashukuru sana mkuu kwa utayari wako kunisaidia. Ngoja niendelee kungoja labda atajitokeza mmojawapo anayejua.
   kama ni miembe ya muda mfupi na michungwa hauna ujanja nenda SUA,pale kwanza ni uhakika na utapewa maelekezo ya ziada namna ya kuyahudumia miche kitaalamu..nimepanda mimi iyo miche ina maembe matamu sana,na wanakufundisha kupandishia mche mmoja unaweza toa aina tofauti za matunda tena mengi hadi mche unazidiwa.
   Lukolo likes this.

  14. Triple G's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th August 2011
   Posts : 586
   Rep Power : 1359
   Likes Received
   137
   Likes Given
   235

   Default Re: Natafuta miche ya miembe na michungwa

   Nenda Mombo pale,tanga iseeh kuna miche ya maembe ambayo after 2yrs unakula embe,alafu mazuri sana ile miembe..
   Lukolo likes this.

  15. Paterne's Avatar
   Member Array
   Join Date : 27th May 2012
   Posts : 85
   Rep Power : 493
   Likes Received
   14
   Likes Given
   19

   Default Re: Natafuta miche ya miembe na michungwa

   Embu ncheck kwa 0718182032
   Lukolo likes this.

  16. King Kong III's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th October 2010
   Location : Enaboishu-Umenyeni
   Posts : 23,566
   Rep Power : 168829816
   Likes Received
   8990
   Likes Given
   3536

   Default Re: Natafuta miche ya miembe na michungwa

   Nenda SUA kuna miche mingi na bei yake haizidi sh 100 kwa mche huku bongo wanauza sh 500 mali asili,kama vp ikifika 77 nenda pale utoe order yako!
   Lukolo likes this.

  17. Lukolo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd December 2009
   Location : Iringa
   Posts : 5,117
   Rep Power : 86242787
   Likes Received
   3034
   Likes Given
   2058

   Default Re: Natafuta miche ya miembe na michungwa

   Quote By King Kong III View Post
   Nenda SUA kuna miche mingi na bei yake haizidi sh 100 kwa mche huku bongo wanauza sh 500 mali asili,kama vp ikifika 77 nenda pale utoe order yako!
   Aaah, kumbe pale maliasili huwa wanaweza kuwa nayo? Panaweza kunirahisishia! Thanks mkuu.
   Maundumula likes this.
   Kama mtu alikuwa waziri au hata mkuu wa mkoa katika serikali ya Kikwete, hafai kuwa Rais wa Tanzania. Kimsingi mtu huyo ni sehemu ya uongozi mbovu na wa hovyo ulioliingiza taifa letu katika umaskini mkubwa na mdororo wa uchumi tulionao sasa. Kama mtu huyu alijua namna ya kuiokoa nchi na hakufanya hivyo, ina maana alitusaliti watanzania na hafai kuwa Rais wa nchi. Kama hakujua ni nini cha kumshauri Kikwete ili Mambo yaende sawa, ina maana hana analolijua. Je anataka awe Rais ili afanye nini ilihali hakuna alijualo?

  18. Lukolo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd December 2009
   Location : Iringa
   Posts : 5,117
   Rep Power : 86242787
   Likes Received
   3034
   Likes Given
   2058

   Default Re: Natafuta miche ya miembe na michungwa

   Quote By Paterne View Post
   Embu ncheck kwa 0718182032
   Thanks mkuu, unayo mwenyewe au wewe ni dalali? Sitaki middle man, kama unaifahamu ilipo nielekeze tu niifuate!
   Maundumula likes this.
   Kama mtu alikuwa waziri au hata mkuu wa mkoa katika serikali ya Kikwete, hafai kuwa Rais wa Tanzania. Kimsingi mtu huyo ni sehemu ya uongozi mbovu na wa hovyo ulioliingiza taifa letu katika umaskini mkubwa na mdororo wa uchumi tulionao sasa. Kama mtu huyu alijua namna ya kuiokoa nchi na hakufanya hivyo, ina maana alitusaliti watanzania na hafai kuwa Rais wa nchi. Kama hakujua ni nini cha kumshauri Kikwete ili Mambo yaende sawa, ina maana hana analolijua. Je anataka awe Rais ili afanye nini ilihali hakuna alijualo?

  19. Lukolo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd December 2009
   Location : Iringa
   Posts : 5,117
   Rep Power : 86242787
   Likes Received
   3034
   Likes Given
   2058

   Default Re: Natafuta miche ya miembe na michungwa

   Quote By matumbo View Post
   kama ni miembe ya muda mfupi na michungwa hauna ujanja nenda SUA,pale kwanza ni uhakika na utapewa maelekezo ya ziada namna ya kuyahudumia miche kitaalamu..nimepanda mimi iyo miche ina maembe matamu sana,na wanakufundisha kupandishia mche mmoja unaweza toa aina tofauti za matunda tena mengi hadi mche unazidiwa.
   Wengi wamenambia miche bora inapatikana SUA. Lakini naona King Kong anasema hata pale maliasilia naweza kupata. Labda nijaribu kwanza hapo. Hope hawachakachui.
   Kama mtu alikuwa waziri au hata mkuu wa mkoa katika serikali ya Kikwete, hafai kuwa Rais wa Tanzania. Kimsingi mtu huyo ni sehemu ya uongozi mbovu na wa hovyo ulioliingiza taifa letu katika umaskini mkubwa na mdororo wa uchumi tulionao sasa. Kama mtu huyu alijua namna ya kuiokoa nchi na hakufanya hivyo, ina maana alitusaliti watanzania na hafai kuwa Rais wa nchi. Kama hakujua ni nini cha kumshauri Kikwete ili Mambo yaende sawa, ina maana hana analolijua. Je anataka awe Rais ili afanye nini ilihali hakuna alijualo?

  20. Kichakoro's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th September 2008
   Location : EMDRUP
   Posts : 725
   Rep Power : 17181567
   Likes Received
   258
   Likes Given
   190

   Default Re: Natafuta miche ya miembe na michungwa

   Mkuu salama<

   Mkuranga ipo miche bora mingi sana. Nenda Mkuranga agriculture Research Sub station ipo about 4 kilometer kutoka Mkuranga main stand.

   Ukikosa hapo mkuranga kata ya Tambani kijiji cha Kibamba kuna Bustani kubwa ya miche ya embe na Machungwa utapata

   ukikosa hapo Nenda Kibiti kuna kikundi cha wakulima bora (QDS certified) wanaitwa Rufiji Environmental group (REG) wana miche zaidi ya 30,000 na wanavarieties zaidi ya 10.
   Mama Joe and Lukolo like this.

  21. #40
   Evarm's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2010
   Location : totoroni
   Posts : 1,259
   Rep Power : 909
   Likes Received
   379
   Likes Given
   187

   Default Re: Soko la maembe

   Nasikia hata bakheressa naye huwa anachukua maembe kwa wingi kwa ajili ya usindikaji na kutengeneza juisi za azam, ila sijui procedure ya kupata maelezo kamili juu ya hili. Nakushauri jaribu kutembelea kampuni yake dar kwa maelezo zaidi
   Everything in your life is a reflection of a choice you have made. If you want a different result, make a different choice.

  Page 2 of 5 FirstFirst 1234 ... LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...