JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Ufugaji wa samaki

  Report Post
  Page 1 of 5 123 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 81
  1. Nteko Vano's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th February 2012
   Location : Dar es salaam
   Posts : 437
   Rep Power : 500
   Likes Received
   107
   Likes Given
   27

   Default Ufugaji wa samaki

   Wana JF

   Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vya maji ya asili ikiwemo mito, mabwawa, maziwa, bahari, chemchem nk. Kutokana na vyanzo hivi tunapata samaki wa aina mbalimbali wakiwemo perege/sato, kambale, kambamiti (prawns), vibua, changu, kaa n.k.

   Samaki ni chanzo cha lishe, kipato na ajira, tunaweza tukatengeneza vito kutokana na lulu wa chaza. Nimejaribu kuzungukia katika soko letu la fery pale nikagundua akina mama na wadau wengi wanafaidika sana na biashara ya samaki nadhani tunawaona mitaani kwetu lakini wanalalamika bei imekuwa juu na upatikanaji wake ni wa shida sana kulingana na msimu.

   Nilijaribu kufuatilia kwa undani suala hili kwa wizara husika nikaelezwa ni kweli bei ya samaki iko juu na upatikanaji wake ni mgumu kutokana na samaki wamepungua kwa kiasi kikubwa na wanapungua kwa kasi ya ajabu...Hali hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, nguvu kubwa ya uvuvi iliyopo kwa mfano samaki sangara kutoka ziwa victoria wamepungua sana na wanaopatikana kwa sasa ni wadogo. Pia wizara ililazimika kufunga uvuvi wa prawns kwa meli kubwa kubwa kutokana na hali kuwa mbaya. Hata perege wanaopatikana ni wadogo na kwa uchache.

   Ili kuokoa suala hili, njia pekee ni kuhamasisha UFUGAJI WA SAMAKI kwa ajili ya kipato, ajira na chakula. Nimevutiwa na suala hili nikaona niwashirikishe wana JF. Nchi za asia china, ufilipino, japan, indonesia fani hii imekuwa sana na wananchi wanajikwamua kiuchumi kutokana na ufugaji wa samaki.

   Bado ninafanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu suala hili la ufugaji samaki na jinsi tunavyoweza kufaidika nalo. Ninaamini tunaweza kufuga na kupata faida kubwa pia tukatunza mazingira yetu ya asili.

   Wakati naendelea kufuatilia suala hili naomba mwenye taarifa basi tushirikiane hapa JF. Nitarudi tena kwa maada hii mara nitakapokusanya taarifa ndani ya siku chache.

   Nawasilisha kwa michango yenu.

   Nteko Vano Maputo

   Penye nia pana njia

   Paloma, Slave, sioni and 3 others like this.


  2. Chipukizi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th March 2009
   Location : Manzese
   Posts : 1,301
   Rep Power : 827
   Likes Received
   344
   Likes Given
   97

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Nenda pale chuo cha uvuvi Mbegani ,bagamoyo utapata maelekezo na pia vifaranga vya samaki.vifaranga vya sato kimoja ni Tsh 50. Na baada ya miezi 3 unaweza anza kuwauza kama kitoweo

  3. newmzalendo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd March 2009
   Location : tanganyika
   Posts : 1,104
   Rep Power : 786
   Likes Received
   219
   Likes Given
   85

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   kingolwira wanauza na kukuchimbia bwawa bei ni laki tano tu,
   Pro bono publico - For the public good

  4. Sita Sita's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th August 2008
   Location : Jamii Forums
   Posts : 1,052
   Rep Power : 806
   Likes Received
   133
   Likes Given
   349

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Samahani kwani nikiwa na bwawa la maji chumvi litafaa kufugia samaki?
   Slave and Dr.zero like this.
   If You Get Them by Their Balls,
   Their Minds and Hearts will Follow


  5. Timtim's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th February 2008
   Posts : 431
   Rep Power : 710
   Likes Received
   50
   Likes Given
   93

   Default

   Quote By newmzalendo View Post
   kingolwira wanauza na kukuchimbia bwawa bei ni laki tano tu,
   Kingolwira ndio nani? Jee ni kampuni au sehemu? Contact yao mkuu na wapo wapi?
   Slave, sioni and Dr.zero like this.

  6. JF SMS Swahili

  7. Malila's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd December 2007
   Location : Makete mjini
   Posts : 3,211
   Rep Power : 11140
   Likes Received
   1437
   Likes Given
   661

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Quote By Timtim View Post
   Kingolwira ndio nani? Jee ni kampuni au sehemu? Contact yao mkuu na wapo wapi?
   Ni kituo cha mafunzo ya wakulima juu ya ufugaji wa samaki, kipo Morogoro kabla hujafika Morogoro jr seminary kama watokea Dsm upande wa kulia. Ukishamaliza mashamba ya mkonge, kunja kulia kama 1km basi utawaona jamaa pale wamejaa tele.

   Si warasimu, wala hawana njoo kesho. Ili kuondoa longo longo piga 0757891761 moja kwa moja ili upate majibu ya maswali yako yote.
   Timtim, Slave, asigwa and 2 others like this.
   Mtu mwema huacha urithi kwa wana wa wanawe.

  8. TIQO's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th January 2011
   Posts : 12,644
   Rep Power : 8509
   Likes Received
   1673
   Likes Given
   220

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Quote By Timtim View Post
   Kingolwira ndio nani? Jee ni kampuni au sehemu? Contact yao mkuu na wapo wapi?
   Mkuu kabla hujafika Moro kwenye mikatani pale
   Slave and Dr.zero like this.
   Mwisho wa Ubaya Aibu.

  9. Timtim's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th February 2008
   Posts : 431
   Rep Power : 710
   Likes Received
   50
   Likes Given
   93

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Asante Mkuu kwa maelezo yako.

  10. Nteko Vano's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th February 2012
   Location : Dar es salaam
   Posts : 437
   Rep Power : 500
   Likes Received
   107
   Likes Given
   27

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Quote By Sita Sita View Post
   Samahani kwani nikiwa na bwawa la maji chumvi litafaa kufugia samaki?
   Unaweza kufuga samaki. Kuna samaki wa maji chumvi ambao wanafugwa kama vile kambamiti (prawns), koazi (milkfish), perege wa maji chumvi. Hawa ndio kwa sasa wanafuga hapa nchini. Ila nimefuatilia nchi nyingine wana teknolojia ya kufuga zaidi ya hao kama vile samaki chewa, tuna. Kwa ushauri zaidi nenda wizara ya mifugo na uvuvi kuna idara ya ufugaji samaki.
   Slave, sioni and Dr.zero like this.

  11. Nteko Vano's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th February 2012
   Location : Dar es salaam
   Posts : 437
   Rep Power : 500
   Likes Received
   107
   Likes Given
   27

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Quote By Chipukizi View Post
   Nenda pale chuo cha uvuvi Mbegani ,bagamoyo utapata maelekezo na pia vifaranga vya samaki.vifaranga vya sato kimoja ni Tsh 50. Na baada ya miezi 3 unaweza anza kuwauza kama kitoweo
   Ahsante mkuu

   Nimejaribu kupitia thread za miaka ya nyuma mulikuwa na mjadala mpana wa suala hili la ufugaji wa samaki, je kwa uzoefu wako na katika mawasiliano na wadau ambao walikuwa wanaonesha nia ya kuanzisha ufugaji huu, ni wangapi walifanikiwa na takwimu zao zikoje? Tunaweza tukapata uhalisia wa jinsi walivyofanikiwa?
   mrere and Dr.zero like this.

  12. BYONA's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 8th May 2012
   Posts : 8
   Rep Power : 404
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Kambale nao wanafugwa?

  13. Chiwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th April 2008
   Posts : 613
   Rep Power : 736
   Likes Received
   176
   Likes Given
   632

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   do! naipenda sana familia yetu ya jf wapo tayari kukusaidia kwa kiasi kikubwa mno
   Slave and sioni like this.

  14. ntamaholo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2011
   Location : Mwilavya
   Posts : 4,564
   Rep Power : 1524
   Likes Received
   1021
   Likes Given
   434

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Quote By Chipukizi View Post
   Nenda pale chuo cha uvuvi Mbegani ,bagamoyo utapata maelekezo na pia vifaranga vya samaki.vifaranga vya sato kimoja ni Tsh 50. Na baada ya miezi 3 unaweza anza kuwauza kama kitoweo
   kuna mradi wa usalama wa chakula kibondo nao wanafuga samaki. nenda watafute redeso wakupe mbinu. halafu yule aliyeshindwa ubunge na mkosa mali ndiye anayelisha samaki pale kibondo
   Slave and Dr.zero like this.
   UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE

  15. zomba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th November 2007
   Posts : 17,177
   Rep Power : 11212
   Likes Received
   3497
   Likes Given
   2562

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Hizi ndio mada za kusaidia na kukwamua jamii. Hongera mleta mada.

   Nawapigia hao Kingurwila sasa hivi. Nna eka moja Kibaha si inatosha sana kwa hii kazi?

  16. ILA's Avatar
   Member Array
   Join Date : 18th March 2012
   Posts : 14
   Rep Power : 412
   Likes Received
   17
   Likes Given
   50

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Quote By BYONA View Post
   Kambale nao wanafugwa?
   Mkuu kambale wanafugwa, japo changamoto ya kambale ni kuwa ukishawafuga hawawezi kuzaliana kwa njia ya kawaida (natural breeding), hivyo unatakiwa uwazalishe (artificial breeding). Teknolojia yake ni rahisi mno wala haiitaji uwe mtaalamu kinachotakiwa ni mafunzo tu kidogo. Ukiweza watembelee wataalam wa Kingolwira utajifunza mengi hata kwa vitendo.
   Maundumula, sioni and Dr.zero like this.

  17. ILA's Avatar
   Member Array
   Join Date : 18th March 2012
   Posts : 14
   Rep Power : 412
   Likes Received
   17
   Likes Given
   50

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Changamoto kubwa inayoikabili hii sekta hapa Tanzania ni ukosefu wa sehemu za kuzalishia vifaranga (hatcheries) na chakula (feeds). Tuna jamii nyingi za samaki wanaoweza kufugwa kama Chewa (grouper), mwatiko (milkfish), Kambamti (shrimps), Kaa (crabs), Kambale, perege n.k. Kufuga samaki hakuhitaji utaalam sana tena kwa jamii ya wavuvi ambao wanamjua samaki na maji kuliko mtu yeyote inaweza kuwa rahisi sana kwao. Teknolojia pia ni rahisi mfano mabwawa (ponds), vizimba (cages), matanki n.k. Kwa sasa perege ndio anafugwa sana kwa sababu ya urahisi wa upatikanaji wa vifaranga na chakula. Lakini bado tuna potential kubwa hasa baharini ukizingatia maji ya bahari hayana competition katika matumizi yake.

  18. ILA's Avatar
   Member Array
   Join Date : 18th March 2012
   Posts : 14
   Rep Power : 412
   Likes Received
   17
   Likes Given
   50

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Quote By Ribosome View Post
   Hizi ndio mada za kusaidia na kukwamua jamii. Hongera mleta mada.

   Nawapigia hao Kingurwila sasa hivi. Nna eka moja Kibaha si inatosha sana kwa hii kazi?

   Inatosha mkuu, waone tu wataalam kwa msaada zaidi
   Maundumula, Slave and Dr.zero like this.

  19. Slave's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th December 2010
   Location : jamiiforums area
   Posts : 4,226
   Rep Power : 60059
   Likes Received
   1718
   Likes Given
   1795

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Asanteni sana wadau, mie pia nina bwawa langu la mita kumi kwa kumi,bwawa hiili nilipandikiza vifaranga 200 miezi sita iliyopita bahati mpaya hao samaki mpaka sasa hawajakuwa wakubwa kufikia saizi kubwa,nilikwenda kwa wataalam wa nyegezi walinipa maelekezo mazuri na sasa mambo yanasonga mbele. Mpaka sasa hawa samaki wametotoa watoto wengi sana kiasi cha kutishia udogo wa bwawa hata hivyo nipo mwishoni namalizia uchimbaji wa bwawa kubwa la mita 35 kwa 30 nadhani mwezi ujao nitapandikiza hao fingerings. Kwa hivi sasa ninacho hitaji ni vitabu vitakavyo nisaidia kuielewa zaidi hii kazi maana mie sijasomea,kama kuna mtu anajua wapi naweza kupata vitabu basi anielekeze au kama kuna mtandao wowote ambapo naweza ku downlod hasa vya kiswahili.
   Stoudemire and Dr.zero like this.

  20. Malila's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd December 2007
   Location : Makete mjini
   Posts : 3,211
   Rep Power : 11140
   Likes Received
   1437
   Likes Given
   661

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Quote By Slave View Post
   Asanteni sana wadau, mie pia nina bwawa langu la mita kumi kwa kumi,bwawa hiili nilipandikiza vifaranga 200 miezi sita iliyopita bahati mpaya hao samaki mpaka sasa hawajakuwa wakubwa kufikia saizi kubwa,nilikwenda kwa wataalam wa nyegezi walinipa maelekezo mazuri na sasa mambo yanasonga mbele. Mpaka sasa hawa samaki wametotoa watoto wengi sana kiasi cha kutishia udogo wa bwawa hata hivyo nipo mwishoni namalizia uchimbaji wa bwawa kubwa la mita 35 kwa 30 nadhani mwezi ujao nitapandikiza hao fingerings. Kwa hivi sasa ninacho hitaji ni vitabu vitakavyo nisaidia kuielewa zaidi hii kazi maana mie sijasomea,kama kuna mtu anajua wapi naweza kupata vitabu basi anielekeze au kama kuna mtandao wowote ambapo naweza ku downlod hasa vya kiswahili.
   Toa mail address yako nikusukumie manual za jamaa wa Kenya na Uganda ambao wanafuga.

   Kambale kwa mazingira ya kisasa ( yaani ukitengeneza bwawa kisasa mara nyingi hawazai, ni sawa na Kanga), wanataka mazingira asili zaidi.

   Nimepata kambale ( Wild african cat fish ) kama 470 hivi, 20 july nimewapata 230 na 22july nimewapata 240 wakiwa wakubwa size ya kidole gumba,nimewaweka ktk ponds mbili tofauti, hakuna aliyekufa mpaka mchana huu. Nitawalisha vizuri kwa miezi sita nione ukuaji wake. Naanda pond ya tatu ili nifikie kambale 700 kwa kuanzia.

   Nitayafanya (ponds) mabwawa haya yapate uasili kidogo hata kwa kuchelewa ili niweze kuzalisha fingerlings za mbegu pia. Hawa kambale nimewapata ktk mazingira asilia kabisa kwa kukausha vidimbwi kando ya mto Mduzi huko Shungubweni. Mpango ni kuhamisha kambale wote ktk vidimbwi vile kila baada ya msimu wa mafuriko/mvua unapopita. Kwa kufanya hivi nitaokoa gharama za kwenda Mbegani,kinguluira kuwanunua.

   Naamini wengi watapata mbegu toka kwangu ya kambale asilia.
   Mtu mwema huacha urithi kwa wana wa wanawe.

  21. Malila's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd December 2007
   Location : Makete mjini
   Posts : 3,211
   Rep Power : 11140
   Likes Received
   1437
   Likes Given
   661

   Default Re: Ufugaji wa samaki

   Quote By ILA View Post
   Mkuu kambale wanafugwa, japo changamoto ya kambale ni kuwa ukishawafuga hawawezi kuzaliana kwa njia ya kawaida (natural breeding), hivyo unatakiwa uwazalishe (artificial breeding). Teknolojia yake ni rahisi mno wala haiitaji uwe mtaalamu kinachotakiwa ni mafunzo tu kidogo. Ukiweza watembelee wataalam wa Kingolwira utajifunza mengi hata kwa vitendo.
   Uzuri wa kambale ni rough rider, nilifika Kinguluira na kupata maelezo haya ya kuzalisha hawa samaki.
   Slave and sioni like this.
   Mtu mwema huacha urithi kwa wana wa wanawe.

  22. JF SMS Swahili

  Page 1 of 5 123 ... LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...