JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Mashine za kutotolesha mayai (Incubators): Upatikanaji wake, aina zake, matumizi na ushauri

  Report Post
  Page 3 of 32 FirstFirst 12345 13 ... LastLast
  Results 41 to 60 of 622
  1. day 24's Avatar
   Member Array
   Join Date : 21st December 2010
   Posts : 13
   Rep Power : 552
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Mashine za kutotolesha mayai (Incubators): Upatikanaji wake, aina zake, matumizi na ushauri

   Habari zenu wanajamvini,

   Mimi ni mfugaji mdogo wa kuku, sasa kidogo biashara yangu imepanuka, nahitaji mashine ndogo ya kutotoleshea vifaranga.

   Naomba mnisaidie bei na mahali zinapopatikana, nitashukuru kwa msaada wenu.


   --------------------

   Quote By Doltyne View Post
   Kuna jamaa yangu alinunua magomeni, incubator na inayoweza kuhatch mayai elfu tisa (9,000) hapo magomeni, cost ilikuwa arround milioni 20 za kitz, inafanya kazi mpaka leo. Yeye biashara yake ni kutotolesha vifaranga tu, unaenda na mayai yako anakucharge 300 kwa kila yai. Yakitoka yasitoke that's the cost.

   Nikavutiwa na biashara nikatafuta vendor china nikapata kwa dola 2900 kila kitu, hiyo iliikuwa ni hatcher ya mayai 5000 na incubator ya mayai 6000, bei ya hatcher ilikuwa dola 700, na incubator 1100, na hizo 1100 zilikuwa ni contena la futi ishirini kuja tz. Sasa hizi habari ni za mwaka 2010 mwanzoni, sijui sasa zikoje.pia kumbuka kuna tra na customs mzigo ukishafika, fanya utafiti wa gharama za kutoa mzigo.

   Kama uko interested ingia alibaba.com, jiridhishe mwenyewe na wauzaji kwa kusearch kama unavyofanya google. Halaf malizana nao. Ila kuwa makini, matapeli wengi. Ingekuwa vema ukawatumia watz wanaoenda kununua bidhaa zao huko japo wakachungulie kama jamaa wana kiwanda na wahakikishe usalama wa pesa zako kwa kuthibitisha mzigo unapakiwa melini.

   Nb: hata hao watz usiwaamini sana, sanaa zimezidi nchini hapa.
   Quote By Chasha Poultry Farm View Post
   Na kama nilivyo sema hapo mwanzo unapo taka kuchagua Incubators zingatia mambo makuu kama Matatu hivi

   1. Automatic au Manual- Mashine ambazo ni automatic ni nzuri sana kwa sababau zinakurahisishia kazi kuliko ambazo ni manual turining

   2. Forced Air Incubators

   Hii huwa nafeni kwa ndani na hiyo feni husaidia kutawanya joto kwenye mayai, na uzuri wa Forced Air incubators ni kwamba hata Joto ikizidi haitaharibu mayai kwa sababu feni inasaidia kupunguza hilo joto,

   Na hii ndo Bora zaidi kwa sababu feni husaidia sambaza joto na humidity ndani ya mashine

   3. Still- Air Incubators

   Hii haina feni, na inategemea Contro za Nje, so kwa hii aina ni lazima mtu awe karibu na mashine 24 hour ili kucheki, lakini kwa ile aina ya kwanza ukiwa na uhakika na umeme na ukawa umeongeza maji ya kutosha kwenye mashine unakuwa hauna haja ya kuwepo muda wote


   Hizi ndo aina kuu za Incubators na unapo enda kununua incubator hakikisha unajua hili, make mara nyingi katika ununuzi wa Incubators unatakiwa kutambua hiyo.

   Na kwa ishu ya Power nyingi za hizi kubwa kutoka China zina sehemu ya kutumia Gesi kama altenative energy ila unapo tumia gesi maana yake hata kama Incubators ilikuwa ni Automatic itabidi ubadilishe mayai kwa mkono au manual kwa sababu gesi inakuwa haifui umeme bali inasaidia katika kutoa joto kwa incubators
   Quote By Chasha Poultry Farm View Post
   KUHUSU INCUBATORS
   Incubators ni Mashine zinazo tumika kutotoreshea viuombe mbali mabali hasa Ndege,

   AINA ZA INCUBATORS
   1. Forced Air Incubator
   2. Still Air Incubators


   FORCED AIR INCUBATOR
   - Forced Air Incubators ni mashine yenye Feni kwa ajili ya kutawanya joto ndani ya incubators

   STILL AIR INCUBATORS
   - Hii ni mashine siyo kuwa na fane

   IPI NZURI?
   - Inashauriwa kutumia/kununua Forced Air Incubators ndo bora kabisa na haiatakusmbua na hatahivyo kwa incubator kubwa karibia zote ni Fored air, na mara nyingi ndogo ndo still air

   3. AINZA INCUBATOR KWENYE OPERATION
   - Manual
   - Automatic

   MANUAL INCUBATORS
   - Hizi hutumia mikono katika kugeuuza mayai na katika maswala mengine kama kucontro joto na kazalika

   AUTOMATIC INCUBATORS
   - Hizi hujiendesha kama Computer, kila kitu hufanywa automatically so kazi za manual hupunguza sana
   - Ukiwa na Incubnator Automatic na ikawa na sehemu ambayo inajiongeza maji automatically basi inaweza hata kata wiki bila kuchungulia mashine yako na ikawa inapiga kazi bila tatizo.
   -

   NI IPI NZURI?
   -Kwa kweli kwa maisha ya sasa inahitajika Automati Incubators ambayo haitahitaji wewe kuwepo mara kwa mara katika ku contro mashine, Ingawa kuna wakati Manual inahitajika kuliko Automatic na kuna wakati Automatic inahitajika kuliko manual
   NB: Automatic nyingi zina manual, yaani kuna sehemu ya kushft kwenda manual, ila manual karibia zote hazina sehemu ya kushift kwenda automatic

   ILA ZOTE ZINAFANYA KAZI KWA UFANISI SAWA, TOFAUTI MOJA NI AUTOMATIC NA NYINGINE NI MANUAL
   MAMBO MUHIMU SANA KWENYE INCUBATORS
   - Aina ya incubators
   - Model of operation
   - Manufacture
   - Nguvu inazo tumia
   - Altenative source of power

   4. MANUFACTURE
   Incubator nyingi za nje ni nzuri sana, Kuna za Italy, Denmark, Uk, China, USA, India, South Africa Trukey na kazalika na bei zinatofautiana. Na utaona kwamba Incubator kama za Uk, South, USA, Italy ni very expensive compare na za kutoka China au India.
   Ila bei kutofautiana sana sio ishu na kama mnavyo jua China wao wna Policy yao kuhusu Internatinal Trade that is why.

   Mashine nza Ndani ya Nchi nazo zipo nzuri na zipo zingine ni vimeo ila watengenezaji wanatakiwa kuwekeza zaidi kwenye Utafiti na si kujikita kwenye mauzo, inatakiwa kuboreshwa zaidi na zaidi ili ziwe na viwango vizuri

   5. SOURCE OF ENERGY
   Incubators karibia zote zinatumia Umeme kama source namba one na jua, makaa yam awe au gas kama source namba mbili, ingawa zipo za mafuta ya taa pia kama source No 1

   6. ALTENATIVE SOURCE OF ENERGY
   Kila aina ya mtengenezaji ana source yake ya altenative energy, zipo za Gas, zipo za umeme jua na zipo za mvuke wa maji na zipo za mafuta ya taa, na zipo za makaa yam awe.

   7. ALTENATIVE SOURCE NZURI
   - Kwangu mimi Incubators ambazo altenative source of energy ni Mvuke wa maji nimetokea kuzipenda sana
   - Hapa umeme ukikatika unaunga pipe kwenye Mashine na unakuwa na birika special na unaiweka jikoni maji yanachemka na mvuke unapita hadi kwenye incubators, ni source nzuri sana,
   - Hata jua nayo ni source poa

   ILA BADO SOURCE YA JUA AU GAS INAKUWA NI ALTENATIVE NZURI SANA.


   MATATIZO YA INCUBATORS
   Incubators nyingi zina shida moja kubwa sana, Incubators inaweza ikaharibika na wewe usiwe na habari kabisa na mpaka uje kushutuka ilisha haribu mayai yote na hilo ni tatizo kubwa sana,

   MFANO:
   -Heating tube zinaweza kufa na wewe usijue kabisa, na ukija shitikia ilisha haribu kila kitu
   -Humidity Tube inaweza kufa na wewe usijue na ukija shitukia ni balaa
   -Eggs turning inaweza kufa na usitambue hata siku mbili
   - Humidity sensor na temperature sonsor zinaweza kufa na wewe usijue chochote
   Na mara nyingi kinaweza kufeli kifaa kimoja za vingine viakendelea na kazi bila shida ila ikawa ndo kama hivyo, Mfano Mashine inaweza kuwa imekufa Humidity tube, na hapo inaweza endelea kufanya kazi na some time ni vigumu sana kugundua.
   - Na tofauti na mitambo kama gari, Incunator inapo haribika huku ukiwa umeweka mayai ni balaa tupu, kama huna mashine nyingine ndo inakuwa imeharibu mayai yote.

   KUKATIKA KWA UMEME- Endapo umeme utakatika na ukatumia Gas, au mafuta ya taa au makaa yam awe kama source nyingine ni lazima ugeuze mayai kwa mkono, na hapa tatizo liko kwamba ile mashine haiwezi kukubali kugeka ni lazima ubonyeze sehemu ya kubadilisha kutoka automatic kwenda manual. HAPA NDO HUWA KUNA KAZI PEVU

   Na Mwisho ni kuhusu uendeshaji wa Incubators, Mara nyingi uendeshaji nao ni tatizo kubwa nasa hasa kwenye seting joto na humidity, make seting lazima zitofautiane kulingana na maeneo au vipindi Fulani, Joto na wakati wa Baridi kari

   Quote By Chasha Poultry Farm View Post
   Wakuu kama una mashine za kuangulia mayai unaweza pata kutoka kwangu.

   1. Spare parts zote za incubators


   2. Trays za kuwekea mayai kwenye mashine
   3. Tray za kutotoleshea


   4. Kufanya repair za mashine mbovu/iliyo haribika
   Quote By pozzyfaza View Post
   Natengeneza Incubator Temberea Uzi umeandikwa natengeneza Incubator
   Hizi ni incubator Ninazo tengeneza Attachment 164925Attachment 164926Attachment 164927Attachment 164928Attachment 164930hii imeisha kula mzigo tayari Attachment 164931

  2. Wazo Langu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st March 2011
   Location : Tanzania
   Posts : 632
   Rep Power : 1196785
   Likes Received
   240
   Likes Given
   22

   Default Re: Gharama ya kutotoa vifaranga: Ninunue mashine (Incubator) yangu au nipeleke mayai kwa watotolesh

   Mi sijapata jibu wapendwa,
   kipi nafuu,kupeleka kwa watotoleshaji au kuwa na incubator yangu?
   Nami nipo kwenye hatua za ufugaji kuku wa kienyeji na wa mayai.

  3. ntamaholo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th August 2011
   Location : Mwilavya
   Posts : 6,255
   Rep Power : 2071
   Likes Received
   1481
   Likes Given
   504

   Default Re: Gharama ya kutotoa vifaranga: Ninunue mashine (Incubator) yangu au nipeleke mayai kwa watotolesh

   For future benefits, ni bora ukawa full equiped, yaani nunua incu yako
   UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE

  4. HP1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th February 2012
   Posts : 3,233
   Rep Power : 1138
   Likes Received
   708
   Likes Given
   27

   Default Re: Gharama ya kutotoa vifaranga: Ninunue mashine (Incubator) yangu au nipeleke mayai kwa watotolesh

   Quote By gvyagusa View Post
   Mawenzi asante kwa ufahamisho, nimewasiliana na Dr Singa akanieleza kuwa anazo mashine hizo, nafanya mipangilio nimwendee. Shukrani mkuu
   Vipi maendeleo ya mradi wako? Kama unaendela Unatotolesha pia wa mayai?
   Use what you get to get what you want

  5. gvyagusa's Avatar
   Member Array
   Join Date : 25th August 2010
   Posts : 11
   Rep Power : 569
   Likes Received
   5
   Likes Given
   0

   Default Re: Gharama ya kutotoa vifaranga: Ninunue mashine (Incubator) yangu au nipeleke mayai kwa watotolesh

   Quote By HP1 View Post
   Vipi maendeleo ya mradi wako? Kama unaendela Unatotolesha pia wa mayai?
   Mkuu mie nitajihusisha na kutotoa kuku wa kienyeji tu na kwa sasa nitazalisha kuku wa kufuga mwenyewe hadi nitakapofikisha idadi ninayotaka ndipo niangalie kama naweza kutotoa vifaranga wa kuuza. Kuku wa mayai nao nitafuga lakini kwa kununua vifanga kutoka kwa wengine kama Interchick.

  6. gvyagusa's Avatar
   Member Array
   Join Date : 25th August 2010
   Posts : 11
   Rep Power : 569
   Likes Received
   5
   Likes Given
   0

   Default Re: Gharama ya kutotoa vifaranga: Ninunue mashine (Incubator) yangu au nipeleke mayai kwa watotolesh

   Quote By LiverpoolFC View Post
   NtakuPM muda wowote Kamanda kwa maongezi zaidi!

   Thankx!
   Kwa faida ya wengine ni kuwa nilimpigia simu jamaa huyo wa Mgana Incubator (Dr.Singa) akaniambia kuwa anatengeneza mashine za aina tatu (3).

   1. Zinazotumia mafuta pekee
   2. Zinazotumia mafuta na/au umeme - ikitokea umeme umekatika unawasha mafuta yako na kuatamia kunaendelea
   3. Zinazotumia umeme pekee

   Aidha alisema anatengeneza zenye uwezo wa kuatamia mayai 100, 150, 200 hadi 1000 na kwamba mashine ya mayai 200 inauzwa shilingi laki 7 (700,000) na ile ya mayai 150 inauzwa shilingi laki 6 (600,000). Ni vizuri tuachane na ufugaji wa kale na tufuge kibiashara zaidi kwa kutotoa mayai mengi kadri inavyowezekana.

   Kwa maelezo zaidi zaidi mtwangie mtengezaji mwenyewe kwa namba iliyoonyeshwa na MAWENZI hapo juu

   Nawasilisha kwa wanaotarajia kuwa wafugaji


  7. mabwana's Avatar
   Member Array
   Join Date : 15th February 2012
   Location : sweden
   Posts : 54
   Rep Power : 500
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Machine ya kusaga chakula cha kuku kwa bei ya kitanzania na incubator

   Last edited by mabwana; 15th July 2012 at 15:32. Reason: insert photo

  8. olng'ojine's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 2nd December 2010
   Posts : 119
   Rep Power : 576
   Likes Received
   9
   Likes Given
   18

   Default Re: Machine ya kusaga chakula cha kuku kwa bei ya kitanzania na incubator

   mkubwa tupe basi hiyo e mail address tuwasiliane

  9. HP1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th February 2012
   Posts : 3,233
   Rep Power : 1138
   Likes Received
   708
   Likes Given
   27

   Default Re: Machine ya kusaga chakula cha kuku kwa bei ya kitanzania na incubator

   Quote By mabwana View Post
   Tafadhali nieleweshe hapo kwenye red, ni mashine ya kuchanganyia chakula cha kuku au?
   Use what you get to get what you want

  10. bluetooth's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th January 2011
   Posts : 3,362
   Rep Power : 1375
   Likes Received
   677
   Likes Given
   200

   Default Re: Machine ya kusaga chakula cha kuku kwa bei ya kitanzania na incubator

   picha ya machine ya chakula cha kuku ipo wapi mkuu

   hii capacity ya 100kg ni per hour au per day?

  11. mabwana's Avatar
   Member Array
   Join Date : 15th February 2012
   Location : sweden
   Posts : 54
   Rep Power : 500
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Machine ya kusaga chakula cha kuku kwa bei ya kitanzania na incubator

   wajamii hiyo picha ni ya incubator

  12. mabwana's Avatar
   Member Array
   Join Date : 15th February 2012
   Location : sweden
   Posts : 54
   Rep Power : 500
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Machine ya kusaga chakula cha kuku kwa bei ya kitanzania na incubator

   kilo 100 kwa saa 1. picha nimejarribu kuweka lakin nimeshindwa
   tuma email nakurushia

  13. andishile's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st April 2012
   Location : Tanzania
   Posts : 1,360
   Rep Power : 756
   Likes Received
   446
   Likes Given
   588

   Default Re: Machine ya kusaga chakula cha kuku kwa bei ya kitanzania na incubator

   mpya hizo mashine au used?

  14. mabwana's Avatar
   Member Array
   Join Date : 15th February 2012
   Location : sweden
   Posts : 54
   Rep Power : 500
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Machine ya kusaga chakula cha kuku kwa bei ya kitanzania na incubator

   mashine mpya azijatumika

  15. malamsha shao's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 23rd September 2012
   Location : Arusha & rombo
   Posts : 153
   Rep Power : 489
   Likes Received
   23
   Likes Given
   13

   Default Incubators yaani mashine ya kuangulia vifaranga bei yake ikoje?

   Incubator ya kuangulia vifaranga 600 used na mpya bei yake vipi naomba mchango wenu wana jf kwa wenye uzoefu ktk hilo na efficiency yake.
   Mama Joe likes this.

  16. Chasha Poultry Farm's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th June 2011
   Posts : 5,000
   Rep Power : 1776
   Likes Received
   2683
   Likes Given
   725

   Default Re: Incubators yaani mashine ya kuangulia vifaranga bei yake ikoje?

   Mkuu kwa China zinapatikana kwa Bei nzuri kabisa, za hapa Bongo hazifai kabisa ni kujitakia Presha, Ila bei inategemeana google alibaba utapata kila kitu,
   Mama Joe likes this.
   Everything you want is on the other side of fear - Jack Canfield

  17. Kubota's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st October 2012
   Posts : 499
   Rep Power : 103864185
   Likes Received
   770
   Likes Given
   634

   Default Re: Incubators yaani mashine ya kuangulia vifaranga bei yake ikoje?

   Chasha mlishauri kuepukana na incubator za kerosine za watengenezaji wa bongo, hivi hizi za umeme kwa back up ya generator kaka garama yake italipa kweli! Maana umeme wa bongo sometimez ni kama hakuna kitu, mnafanyaje wakubwa? Kwa generator inalipa maana no way lazima uwe na back up power source! Labda option ya gesi inanipa matumaini kidogo!

  18. Mama Joe's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th March 2009
   Posts : 1,502
   Rep Power : 21030577
   Likes Received
   708
   Likes Given
   727

   Default Re: Incubators yaani mashine ya kuangulia vifaranga bei yake ikoje?

   Quote By Chasha View Post
   Mkuu kwa China zinapatikana kwa Bei nzuri kabisa, za hapa Bongo hazifai kabisa ni kujitakia Presha, Ila bei inategemeana google alibaba utapata kila kitu,
   Thanks Chasha Alibaba niliisha google siku nyingi nikapata suppliers kibao na wananikumbusha kila leo ila napata kigugumizi kuwaamini itanifikiaje hiyo mashine yao, umeishawai kufnay biashara nao. Mimi ninahitaji ingawa kuanzia sio kubwa hata ya mayai 200 kwa matumizi binafsi

  19. Chasha Poultry Farm's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th June 2011
   Posts : 5,000
   Rep Power : 1776
   Likes Received
   2683
   Likes Given
   725

   Default Re: Incubators yaani mashine ya kuangulia vifaranga bei yake ikoje?

   Quote By Kubota View Post
   Chasha mlishauri kuepukana na incubator za kerosine za watengenezaji wa bongo, hivi hizi za umeme kwa back up ya generator kaka garama yake italipa kweli! Maana umeme wa bongo sometimez ni kama hakuna kitu, mnafanyaje wakubwa? Kwa generator inalipa maana no way lazima uwe na back up power source! Labda option ya gesi inanipa matumaini kidogo!
   Mkuu incubators mfano za mayai mpaka 1500 unaweza tumia solar na ikaendesha vizuri tu na nyingi hutunza moto kwa masaa hadi matano, so baada ya hapo unaweza tumia solar au genereta vile vidogo, haiwezi kuwa ghalama kwa sababu si dhani kama umeme un akatika kila daily na labda ukatike siku nzima lakini kama ni masaa matutu manne haina shida kabisa
   Everything you want is on the other side of fear - Jack Canfield

  20. Sabayi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th December 2010
   Posts : 2,329
   Rep Power : 1018
   Likes Received
   866
   Likes Given
   1859

   Default Re: Incubators yaani mashine ya kuangulia vifaranga bei yake ikoje?

   Quote By Chasha View Post
   Mkuu kwa China zinapatikana kwa Bei nzuri kabisa, za hapa Bongo hazifai kabisa ni kujitakia Presha, Ila bei inategemeana google alibaba utapata kila kitu,
   Mkuu hivi hawa Alifather wanaaminika kweli? Sio Matapeli?
   NAIKATAA CCM NA MAMBO YAKE YOTE NA WATU WAKE WOTE EEE MWENYEZI MUNGU NISAIDIE!!!!!!!!

  21. Chasha Poultry Farm's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th June 2011
   Posts : 5,000
   Rep Power : 1776
   Likes Received
   2683
   Likes Given
   725

   Default Re: Incubators yaani mashine ya kuangulia vifaranga bei yake ikoje?

   Alibaba sio wauzaji wao ni waunganishaji, tu, ni kama livyo kwa jamii fulum leo hii huwezi tapeliwa na mtu humu janvini then ukaenda kuwalaumu wenye mtandao

   Alibaba wana condition wamezi weka ambazo mnunuzi unatakiwa kufuata na ukizifuata huwezi tapeliwa, hii ni panoja na kuklipia kupitia ESCROW, hawa ukisha walipa pesa hukaa nazo na mpaka supler atume mzigo kwako ndo wao wampatie Suplier pesa, Hawawezi mpatia pesa muuzaji bila kwanza wewe kudhibitisha kwamba mzigo umetumwa na ndo wenyewe
   SO WAKO FRESHI TU NA MIMI KUNA MZIGO NDO NAJIANDAA KUNUNUA KWA SUPLIER MMOJA MWEZI HUU,
   Mama Joe likes this.
   Everything you want is on the other side of fear - Jack Canfield


  Page 3 of 32 FirstFirst 12345 13 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Mashine za kutotolesha mayai(incubators).
   By ELIASANTE in forum Matangazo madogo
   Replies: 0
   Last Post: 20th June 2014, 03:26
  2. Mashine za kutotolesha mayai(incubators).
   By ELIASANTE in forum Matangazo madogo
   Replies: 0
   Last Post: 16th June 2014, 11:28
  3. mashine za kutotolesha mayai (Incubators)
   By Ndamwe in forum Matangazo madogo
   Replies: 1
   Last Post: 27th August 2013, 01:13
  4. Kuhusu Mashine ya Kuatamisha mayai(Incubators) Majibu ya TRA
   By Chasha Poultry Farm in forum Jukwaa La Biashara na Uchumi
   Replies: 15
   Last Post: 9th January 2013, 15:12

  Tags for this Topic

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...