JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Kilimo cha zao la Ufuta - Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

  Report Post
  Page 1 of 24 123 11 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 465
  1. Safari_ni_Safari's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th October 2007
   Location : Kibaruani
   Posts : 17,806
   Rep Power : 3277024
   Likes Received
   9581
   Likes Given
   3670

   Default Kilimo cha zao la Ufuta - Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

   KILIMO BORA CHA UFUTA


   Ufuta (sesamum indicum)ni zao linalolimwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani, Morogoro, Dodoma, Tanga na ukanda wa chini katika mikoa ya Rukwa na Mbeya. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. Mbegu za zao hili huwa na wastani wa mafuta kiasi cha asilimia 45.


   MAMBO YA KUZINGATIA WA KATI WA KUZALISHA MBEGU
   • Chagua aina ya mbegu inayotoa mazao mengi na bora, inayovumilia mashambulizi ya magonjwa na wadudu, inayokomaa mapema na kutoa mafuta mengi.
   • Chagua mbegu inayokomaa kwa pamoja ili kurahisisha uvunaji na pia kuepuka upotevu wa zao shambani.
   • Aina nyeupe ya mbegu ya ufuta hupendelewa zaidi kuliko aina nyeusi.


   MBOLEA
   Ufuta unahitaji rutuba ya kutosha ili kutoa mazao bora. Katika kudumisha rutuba ya udongo, tumia kilimo cha mzunguko wa mazao au weka mbolea za asili pale inapobidi.


   PALIZI
   Dhibiti magugu kwa kupalilia ili kuruhusu ufuta kutumia vizuri unyevu na virutubishi. Magugu mengine huwa ni maficho ya wadudu waharibifu wa zao la ufuta.


   MAGONJWA NA WADUDU
   Ufuta hushambuliwa na magonjwa na wadudu mbalimbali ambao huweza kusababisha upungufu na ubora wa mazao. Hivyo kagua shamba mara kwa mara hasa kwenye maua na mapodo ili kuona dalili za mashambulizi. Endapo kuna dalili zamashambulizi, chukua tahadhari mapema kabla ya uharibifu mkubwa haujatokea.


   MAANDALIZI KABLA YA KUVUNAKAGUA SHAMBA
   • Kagua shamba kuona kama ufuta umekomaa.
   • Ufuta hukomaa, kati ya miezi mitatu na minne tangu kupanda kutegemea aina.
   • Aina ya ufuta usiokuwa na matawi hukomaa mapema kuliko ile yenye matawi.
   • Ni muhimu kuwahi kuvuna ili kuepuka ufuta kupukutikia shambani.


   DALILI ZA KUKOMAA UFUTA SHAMBANI
   • Kwa kawaida majani hubadilika rangi kutoka kijani na kuwa ya manjano na hatimaye kudondoka.
   • Mashina hubadilika rangi kutoka kijani na kuwa ya kahawia.


   VIFAA VYA KUVUNIA
   • Kamba
   • Siko
   • Panga


   VIFAA VYA KUKAUSHIA
   • Sehemu ya kukaushia yenye Sakafu ya saruji
   • Maturubai
   • Sakafu safi
   USAFIRI
   • Mikokoteni
   • Matela ya matrekta
   • Magari


   KUVUNA
   • Vuna ufuta mapema kabla mapodo kukomaa sana na kuanza kupasuka na kuachia punje.Mapodo ya ufuta yaliyokomaa sana yakiguswa au kutikiswa na upepo hupasuka na kuachia mbegu, hali inayosababisha upotevu mkubwa.
   • Mbegu za ufuta ni ndogo na zikidondoka chini ni vigumu kuziokota. Vilevile mbegu zilizodondoka ni vigumu kuzitenganisha na uchafu.
   • Uvunaji wa ufuta huhusisha ukataji wa mimea yenye mapodo kwa kutumia vyombo vya mkono kama panga kwa kukata mashina.
   • Kwa aina za ufuta zenye mapodo yanayopasuka, uvunaji ufanyike wakati mimea bado ni kijani ili kuepuka upotevu wa mbegu.
   • Aidha uvunaji ufanyike wakati hakuna upepo wala jua kali.
   • Baada ya kukata mashina yafunge katika mizigo midogo na kuweka katika vyombo vya kusafirisha kama vile mikokoteni, matela au magari hadi sehemu ya kukaushia.
   • Panga mizigo midogo kwa kusimamisha katika malundo madogo yasiyozidi mizigo minane kwenye sehemu safi za kukaushia.


   KUKAUSHA
   Mapodo ya ufuta hukaushwa yakiwa yamefungwa katika vitita. Vitita huwekwa kwa kuegeshwa kwenye fremu ya kukaushia kwa muda wa wiki mbili hadi tatu kutegemea hali ya hewa. Fremu hii huwekwa juu ya turubai au sakafu ili kuzuia upotevu wa punje kutokana na kupasuka kwa mapodo.


   KUPURA
   Upuraji hufanyika kwenye turubai, mkeka au kwenye sakafu safi.
   • Vitita hupigwa taratibu kwa kutumia mti au hutikiswa vikiwa vimegeuzwa vichwa chini ili kuruhusu punje za ufuta kudondoka kwenye sakafu safi au turubai.


   KUPEPETA NA KUPEMBUA
   Kupepeta na kupembua hufanywa ili kuondoa takataka kama vile mawe, vipande vya mapodo,vijiti na vumbi.Njia bora ya kupepeta na kupembua ni kwa kutumia mikono.
   • Ufuta huwekwa kwenye vyombo kama vile ungo kwa kiasi cha kilo mbili hadi tatu. Ufuta hurushwa hewani kwa kasi ndogo na takataka nyepesi huchukuliwa na upepo. Zile nzito huondolewa kwa mikono.


   KUFUNGASHA
   Mbegu za ufuta zilizo safi huwekwa kwenye vifungashio kama vile magunia madogo ya aina ya juti ya ujazo wa kilo 50.
   • Fungasha mbegu za ufuta kwenye magunia yenye uzito usiozidi kilo 50. Kabla ya kufungasha hakikisha mbegu zimekauka hadi kufikia unyevu wa asilimia 10.


   KUHIFADHI
   • Panga magunia ya ufuta juu ya chaga.
   • Panga kwa kupishanisha ili kuruhusu mzunguko wa hewa kati ya magunia.


   KUSINDIKA MBEGU ZA UFUTA
   Ufuta husindikwa kupata bidhaa ya mafuta ambayo hutumika katika mapishi mbalimbali. Mafuta hukamuliwa kwa kutumia njia za asili na kwa kutumia mashine. Njia za asili zina ufanisi mdogo ukilinganisha na zile za kukamua kwa mashine, hivyo ni vyema kutumia mashine. Kuna mashine za aina mbili zinazotumika kukamua mafuta; mashine za mkono na zile zinazoendeshwa kwa injini au mota ya umeme. Mashine za mikono zinazotumika zaidi hapa nchini ni za aina ya daraja (Bridge press) na Ram.


   KUKAMUA KWA MASHINE YA DARAJA
   Mashine ya daraja ni moja ya mashine za kisasa zinazoweza kukamua mafuta ya ufuta. Mashine hizi huendeshwa kwa mikono na zina uwezo wa kukamua mafuta kwa asilimia 68 hadi 72. Inaweza kukamua kilo 25 za ufuta kwa saa moja. Ili kupata ufanisi mzuri wa mashine hii, ni muhimu ufuta uwe na unyevu wa kati ya asilimia 11 na 13. Iwapo unyevu utakuwa chini ya kiwango hicho inashauriwa kunyunyizi maji kwenye ufuta kabla ya kukamua.
   VIFAA VYA KUKAMULIA MAFUTA
   • Mashine ya daraja
   • Sufuria • Vifungashio
   • Mifuko midogo ya nguo au viroba vyenye upana wa sentimita 20 na urefu wa sentimita 20.
   • Chombo cha kukinga mafuta.
   • Chujio safi
   • Lebo
   • Lakiri Malighafi
   • Mbegu za ufuta safi
   • Maji safi


   UKAMUAJI MAFUTA
   • Nyunyuzia maji kidogo kwenye ufuta ili kuongeza unyevu kufikia asilimia 11 hadi 13. Mafuta hutoka vizuri kwenye kiwango hicho cha unyevu.
   • Jaza ufuta kwenye vifuko vya nguo au viroba
   • Vipange vifuko hivyo kwenye silinda na kuanza kuzungusha mhimili hadi mafuta yaanze kutoka kupitia matundu ya silinda.
   • Acha kwa muda mafuta yaendelee kutoka kisha endelea kuzungusha mhimili hadi mafuta yaishe. Mhimili ukiacha kuzunguka ni dalili kuwa mafuta yamekwisha.
   • Kusanya mafuta, chuja na fungasha kwenye chupa safi zilizochemshwa. Hakikisha chupa ni kavu na zina mifuniko.
   • Weka lebo na lakiri
   • Hifadhi mahali pakavu na pasipo na mwanga mkali.


   MASHINE YA RAM
   Mashine ya Ram ina uwezo wa kusindika kilo 7 za mbegu za ufuta kwa ufanisi wa asilimia 57%.Aina ya Ram (BP-30) ina uwezo wa kukamua lita 20 za mafuta kwa siku.


   VIFAA
   • Ndoo
   • Mashine ya Ram
   • Kichujio au kitmbaa safi
   • Vifungashio safi


   UKAMUAJI
   • Anika mbegu za ufuta juani kwa kuzitandaza kwenye mabati ili zipate joto la kutosha.
   • Lengo la kuanika mbegu juani ni kurahisisha ukamuaji wa mafuta.
   • Jaza mbegu za ufuta kwenye mpare wa kulishia
   • Funga wenzozuia (HANDLE)ili mbegu za ufuta zisitoke.
   • Nyanyua wenzozuia mpaka juu ili kuruhusu mbegu za ufuta kuingia kwenye silinda.
   • Shusha wenzozuia chini ili kuruhusu pistoni kusukuma mbegu za ufuta ziingie ndani ya eneo la shindilio
   . • Nyanyua tena wenzozuia mpaka juu na kushusha na wakati huohuo ukiendelea kujaza mbegu za ufuta kwenye mpare wa kulishia. Wenzoinua ukiwa mzito ni dalili kuwa msukumo wa kutosha umejengeka. Msukumo huo utasababisha mafuta kutoka.
   • Mafuta yanapoanza kutoka legeza wenzozuia ili kuruhusu mashudu kutoka.
   • Chuja na hifadhi mafuta kwenye vyombo safi vyenye mifuniko vilivyochemshwa.


   MATUMIZI

   Mafuta ya ufuta hutumika katika mapishi mbalimbali ili kuongeza ladha. Pia husaidia kuleta nguvu na joto mwilini. Mbegu za ufuta huchanganywa na vyakula mbali mbali kama mikate, keki, mboga na kadhalika.

   Kwa hisani ya mdau MITIKI -KILIMO KWANZA: KILIMO BORA CHA UFUTA

   Quote By frankclemence View Post
   UFUTA

   Ni zao linalostahimili baridi na hulimwa maeneo yasiyozidi mita 1500 juu ya usawa wa bahari.Mvua ni Kati ya milimita 400-500 ambazo hutosha kabisa kutoa mavuno Mengi.

   AINA ZA MBEGU

   Ziada 94,inakomaa Kwa siku 120-130 na inastahimili magonjwa.Ina uwezo wa kutoa mavuno zaidi ya kilo 1000 Kwa heka.
   Nal 92,inakomaa Kwa siku 90-110 na inastahimili magonjwa hasa mabaka ya majani.Ina uwezo wa kutoa mavuno kiasi cha kilo 1200-1500 Kwa heka.

   MAGONJWA NA NAMNA YA KUYAZUIA

   Magonjwa makubwa ya UFUTA ni mabaka na ukungu kwenye majani.Magonjwa haya yasipozuiwa yatapukutisha majani na hivyo kusababisha Mazao kupungua.

   KIZUIA


   • Panda UFUTA mapema
   • Tumia mboga zinazostahimili magonjwa Kama-Nal 92
   • Ng'o mimea iliyoathirika
   • Tumia kilimo cha mzunguko


  2. Chasha Poultry Farm's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th June 2011
   Posts : 5,035
   Rep Power : 1790
   Likes Received
   2696
   Likes Given
   725

   Default

   Ya Ufuta si kwamba unalipa sana bali una bei kubwa sana, Make ukiona bei iko juu , tambua kwamba kuna ugumu katika hiyo kazi, so kilimo cha Ufuta mpka ufikishe Gunia moja umelima shamba la kutosha,

   Ukiona kitu kinauzwa bei ya juu si kwamba kina lipa no ni bei iko juu kulingana na supply kuwa ndogo, Mfano Huku Arusha kuna KAMPUNI MOJA YA MAUA na kuna aina fulani ya maua huwa ukilima unawauzia Kilo Moja Tsh 300,000/ Ila mziki wa kupata hizo kilo si mchezo unaweza lima ukaishia kupata nusu kilo tu,
   Everything you want is on the other side of fear - Jack Canfield

  3. STREET SMART's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th February 2010
   Location : DAR - NEWALA
   Posts : 523
   Rep Power : 705
   Likes Received
   212
   Likes Given
   219

   Default Ninavuna Ufuta: MSAADA

   Nimeanza kuvuna ufuta shambani kwangu, kwa sasa nafanya comparison ya bei na wanunuzi. JF ni jungu kuu naombeni member wenye kujua wanunuzi mbali mbali wanipe contacts zao ile nilinganishe bei nifanye right choice ktk kuuza mzigo.
   Thanks wadau wote.


   Mrejesho:

   • kati ya eka 30 nilizopanda ufuta ulistawi vzuri na kuvunwa eka 17..hii ilisababishwa na uangalizi mbovu wa aliyekuwa ananisimamia shamba.
   • kila eka nilivuna wastani wa kilo 350, kipindi hiki ( july 2011-2012) wanunuzi binafsi hawakuruhusiwa lindi kununua ufuta, so niliuza kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani @ 1200/= kwa kilo jumla nilipata kama milion 7 kwa msimu mmoja (gharama za kusafisha msitu wa eka 30, mbegu na malipo ya wafanyakazi zilikuwa ni 3.5 milion), sikuingia gharama ya kusafirisha kwa kuwa walinifata shambani.
   • Mwaka 2013 sikulima nilipumzisha shamba kwa kulisafisha eka zangu zote 50 na kutanua kidogo (hili shamba lilikuwa ni msitu wakati nalichukua)
   • mwaka huo wa 2013 ulikuwa ni mzuri sana kwa upande wa bei, chomachoma (wanunuzi binafsi) waliruhusiwa na ufuta ulipanda bei hadi kufikia 2500 kwa kilo na unalipwa cash hapo hapo. waliolima walipata pesa nzuri tu.
   • mwaka huu vijana wanamalizia kupanda shamba nimelima ekari 35, nilibadili team ya wafanyakazi wa shamba kwa kuwa wengi walinikwamisha kwa kuendekeza starehe badala ya kazi. natumaini wanunuzi binafsi wataruhusiwa.
   • watu wengi kutoka mikoa mbali mbali (wachaga kibao) wameanza kuvamia misitu na kuiuza au kulima so kwa sasa kumechangamka sana tofauti na 2011 wakati naanza.
   • expectations zangu mwaka huu ni ........35(eka) x 400(kg) x 2500(bei/kg)=35,000,000.
   • NB: 400kg kwa eka ni kiwango cha chini cha mavuno, wataalamu wa chuo cha naliendele waliniambia kwa mbegu zao za lindi 2002 na malada natakiwa nipate 1200kg kwa eka. Vijana wapo shamba wanachakarika na mi nipo mjini namtumikia mkoloni (ajira).   Thanks kwa wote:

   UKITAKA KUUJUA UTAMU WA NGOMA .......UINGIE UCHEZE.
   Last edited by STREET SMART; 15th February 2014 at 12:18.

  4. MIGNON's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd November 2009
   Posts : 1,498
   Rep Power : 974
   Likes Received
   541
   Likes Given
   439

   Default Re: Ninavuna Ufuta: MSAADA

   Inategemea uko upande gani wa Tanzania na unategemea mavuno kiasi gani.Kama ni eka cchache ni afadhali uuze hapo ulipo kuwa tempted kupeleka Dar ambapo unaweza kuambiwa bei ni kubwa but in actual fact ukiweka gharama za usafiri,malazi na risk nyingine inakuwa ni hasara

  5. Mkeshahoi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th January 2009
   Posts : 2,386
   Rep Power : 1141
   Likes Received
   235
   Likes Given
   1015

   Default Mawazo na msaada..(bishara ya Mbao na zao la Ufuta)

   Helo wanajamvi ... naamini mu wazima na sote twaendelea chakachua akili zetu kukaba fursa za kiuchumi japo nchi yetu inauzwa kila kukicha.

   Naomba msaaada wa mawazo na ushauri:
   - kutaka kujua hali ya soko na wanunuzi(si madalali) wazuri wa mbao za mninga, mvule na mkangazi hapo DSM.. kuna ndugu anataka kujitosa katika anga hii na kaniomba ushauri. Biashara ni pale mzigo unapokuwa umefika kwa mnunuzi.

   -nahitaji jua michakato yote katika kilimo cha ufuta kwa yeyote anayeelewa... kuna mwananchi kanidokeza ni kilmo kinacholipa.

   Pamoja tunaweza.

   Nawakilisha.
   Hela silaha... Kisu Mzigo


  6. Rich Dad's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th December 2010
   Posts : 744
   Rep Power : 707
   Likes Received
   103
   Likes Given
   12

   Default

   Quote By Mkeshahoi View Post
   Helo wanajamvi ... naamini mu wazima na sote twaendelea chakachua akili zetu kukaba fursa za kiuchumi japo nchi yetu inauzwa kila kukicha.Naomba msaaada wa mawazo na ushauri:- kutaka kujua hali ya soko na wanunuzi(si madalali) wazuri wa mbao za mninga, mvule na mkangazi hapo DSM.. kuna ndugu anataka kujitosa katika anga hii na kaniomba ushauri. Biashara ni pale mzigo unapokuwa umefika kwa mnunuzi.-nahitaji jua michakato yote katika kilimo cha ufuta kwa yeyote anayeelewa... kuna mwananchi kanidokeza ni kilmo kinacholipa.Pamoja tunaweza.Nawakilisha.
   Tuma bei na size ya mbao nione kama naweza kununua na kuuza maeneo ya kigamboni.

  7. Malila's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd December 2007
   Location : Makete mjini
   Posts : 3,993
   Rep Power : 35923095
   Likes Received
   2158
   Likes Given
   944

   Default Re: Mawazo na msaada..(bishara ya Mbao na zao la Ufuta)

   Quote By Mkeshahoi View Post
   Helo wanajamvi ... naamini mu wazima na sote twaendelea chakachua akili zetu kukaba fursa za kiuchumi japo nchi yetu inauzwa kila kukicha.

   Naomba msaaada wa mawazo na ushauri:
   - kutaka kujua hali ya soko na wanunuzi(si madalali) wazuri wa mbao za mninga, mvule na mkangazi hapo DSM.. kuna ndugu anataka kujitosa katika anga hii na kaniomba ushauri. Biashara ni pale mzigo unapokuwa umefika kwa mnunuzi.

   -nahitaji jua michakato yote katika kilimo cha ufuta kwa yeyote anayeelewa... kuna mwananchi kanidokeza ni kilmo kinacholipa.

   Pamoja tunaweza.

   Nawakilisha.
   Kwa habari ya mbao unazosema, ni vema uangalie size ambazo zina soko zuri kwa wanunuzi hata wa reja reja ili asilete mzigo wa kuganda. Pia kama unaweza m-MP tiger, yumo humu, juzi alikuwa kwa GUE BUSNESS ( yaani Msumbiji kusaka mbao ngumu) anaweza kukupa habari za hiyo kitu.

   Kilimo kwa ujumla si kibaya, tatizo ni masoko, kuna watu huwaambii kitu ktk nyanya au viazi vya chips, lakini wengine wameapa hawatakaa walime zao fulani kwa sababu ya kubamizwa msimu fulani. Ufuta unalipa, japokuwa mwaka huu pande za Babati huko wanalia,bei imeshuka vibaya.
   Mtu mwema huacha urithi kwa wana wa wanawe.

  8. Candid Scope's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th November 2010
   Posts : 11,856
   Rep Power : 366017343
   Likes Received
   6654
   Likes Given
   4629

   Default Re: Mawazo na msaada..(bishara ya Mbao na zao la Ufuta)

   Soko la mazao ya biashara ni zuri sana tu kama unakuwa mbunifu wa kuzindika mwenyewe badala ya kutegemea uwauzie wengine mazao yako. Kama una mpango wa zao la ufuta ni bora kama unaamua kuwa na kinu cha kukamua mafuta na katu hutakosa soko la mafuta.

   Binafsi nakushauri sana kulima zao la ufuta iwapo utakuwa na mipango ya kuzindika na kupata mafuta wewe mwenyewe na kisha uuze mafuta yake, hapo utakomba faida yote badala ya kudanganywa na wanunuzi wa middles ambao hula faida ya wa juu na wa chini.

  9. Mkeshahoi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th January 2009
   Posts : 2,386
   Rep Power : 1141
   Likes Received
   235
   Likes Given
   1015

   Default Re: Mawazo na msaada..(bishara ya Mbao na zao la Ufuta)

   Quote By Malila View Post
   Kwa habari ya mbao unazosema, ni vema uangalie size ambazo zina soko zuri kwa wanunuzi hata wa reja reja ili asilete mzigo wa kuganda. Pia kama unaweza m-MP tiger, yumo humu, juzi alikuwa kwa GUE BUSNESS ( yaani Msumbiji kusaka mbao ngumu) anaweza kukupa habari za hiyo kitu.

   Kilimo kwa ujumla si kibaya, tatizo ni masoko, kuna watu huwaambii kitu ktk nyanya au viazi vya chips, lakini wengine wameapa hawatakaa walime zao fulani kwa sababu ya kubamizwa msimu fulani. Ufuta unalipa, japokuwa mwaka huu pande za Babati huko wanalia,bei imeshuka vibaya.
   Ahsante mkuu kwa ushauri wako, nitafikisha feedback kwa mhusika.
   Hela silaha... Kisu Mzigo

  10. mjasiria's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th January 2011
   Posts : 3,586
   Rep Power : 48540
   Likes Received
   1207
   Likes Given
   5531

   Default Kilimo cha ufuta

   Habari zenu wadau,
   Leo nimeona nije na mada ili kama kuna watu wenye information zinazoweza kusaidia basi na wachangie ili tuweze kupata faida. Kwa kifupi ni kuwa ninashawishika kujishughulisha na kilimo ili kuongeza kipato na nimeamua kujishughulisha na kilimo cha ufuta.

   Ufuta kama zao lingine lolote lina mahitaji yake muhimu. Ninaomba kama kuna yeyote anayeweza kutoa maelezo kuhusu zao hili kwenye vipengele vifuatavyo basi anisaidie.
   1. Je ni aina gani ya mbegu zinazopatikana na kustawi Tanzania, na katika hizo ipi ni bora zaidi.
   2. Kwa ekari moja, kama ukifuata ushauri wa kitaalamu unaweza kupata kiasi gani cha ufuta katika mavuno assuming normal conditions?
   3. Je ufuta unahitaji dawa za kuua wadudu, na kama ni ndivyo inahitajika kufanya zoezi hilo mara ngapi ili kupata mavuno mengi na bora? Pia gharama za kupiga dawa kwa ekari inaweza kufikia kiasi gani?
   4. Je zao hili ustawi katika mazingira gani? Hapa nina maana hali ya hewa, udongo n.k.
   5. Ni mbinu gani za kilimo naweza kutumia kuongeza wingi na ubora wa zao hili.

   Wakuu wenye hizi habari tunaomba mfunguke kwa faida ya wengi.
   Last edited by mjasiria; 10th August 2011 at 17:39.

  11. Dr wa ukweli's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th February 2011
   Posts : 883
   Rep Power : 724
   Likes Received
   178
   Likes Given
   68

   Default re: Kilimo cha zao la Ufuta - Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

   Quote By mjasiria View Post
   Habari zenu wadau,
   Leo nimeona nije na mada ili kama kuna watu wenye information zinazoweza kusaidia basi na wachangie ili tuweze kupata faida. Kwa kifupi ni kuwa ninashawishika kujishughulisha na kilimo ili kuongeza kipato na nimeamua kujishughulisha na kilimo cha ufuta.

   Ufuta kama zao lingine lolote lina mahitaji yake muhimu. Ninaomba kama kuna yeyote anayeweza kutoa maelezo kuhusu zao hili kwenye vipengele vifuatavyo basi anisaidie.
   1. Je ni aina gani ya mbegu zinazopatikana na kustawi Tanzania, na katika hizo ipi ni bora zaidi.
   2. Kwa ekari moja, kama ukifuata ushauri wa kitaalamu unaweza kupata kiasi gani cha ufuta katika mavuno assuming normal conditions?
   3. Je ufuta unahitaji dawa za kuua wadudu, na kama ni ndivyo inahitajika kufanya zoezi hilo mara ngapi ili kupata mavuno mengi na bora? Pia gharama za kupiga dawa kwa ekari inaweza kufikia kiasi gani?
   4. Je zao hili ustawi katika mazingira gani? Hapa nina maana hali ya hewa, udongo n.k.
   Wakuu wenye hizi habari tunaomba mfunguke kwa faida ya wengi.
   ukanda wa kati singida babati na dodoma nasikia ndio penyewe zamani nilikuwa nalima kifamilia zaidi maeneo ya kaskazini, tusubiri wataalam waje wakupe data za kibiashara zaidi
   Wanawake wanyimeni unyumba waume zenu kama watawaunga mkono wapinzani: Sofia Simba

  12. HAZOLE's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th February 2011
   Posts : 1,229
   Rep Power : 793
   Likes Received
   274
   Likes Given
   44

   Default re: Kilimo cha zao la Ufuta - Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

   Quote By mjasiria View Post
   Habari zenu wadau,
   Leo nimeona nije na mada ili kama kuna watu wenye information zinazoweza kusaidia basi na wachangie ili tuweze kupata faida. Kwa kifupi ni kuwa ninashawishika kujishughulisha na kilimo ili kuongeza kipato na nimeamua kujishughulisha na kilimo cha ufuta.
   WELL. ufuta ni biashara nzuri sana hapa tz. mnunuzi mkubwa wa hapa ndani ni mohamed enterprises hapa dsm.
   Ekari moja inakupa gunia 8@85-90 kgs so ni kama kilo 680 kwa ekari moja.
   nami nitafuatilia suala hili na mwakani ninampango wa kuanza na ekari 10 kwa mkoa wa lindi. kuhusu mbegu na wadudu nakushauri uende vyuo vya kilimo vilivyopo maeneo ambayo kilimo cha ufuta kinafanyika. kwa mimi nitaenda naliendele agricultural institute cha mtwara nadhani wananisaidia. kila la heri
   Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu chochote! Tumche Mungu wa Mbinguni siku zote! Amina

  13. mjasiria's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th January 2011
   Posts : 3,586
   Rep Power : 48540
   Likes Received
   1207
   Likes Given
   5531

   Default re: Kilimo cha zao la Ufuta - Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

   Quote By HAZOLE View Post
   WELL. ufuta ni biashara nzuri sana hapa tz. mnunuzi mkubwa wa hapa ndani ni mohamed enterprises hapa dsm.
   Ekari moja inakupa gunia 8@85-90 kgs so ni kama kilo 680 kwa ekari moja.
   nami nitafuatilia suala hili na mwakani ninampango wa kuanza na ekari 10 kwa mkoa wa lindi. kuhusu mbegu na wadudu nakushauri uende vyuo vya kilimo vilivyopo maeneo ambayo kilimo cha ufuta kinafanyika. kwa mimi nitaenda naliendele agricultural institute cha mtwara nadhani wananisaidia. kila la heri
   Mkuu kama ukipata details zaidi itakuwa vizuri ukishea nasi. Maana kwa uzoefu mdogo nilionao watu wanapata gunia kama 10 tu kwa ekari 5, lakini kwa mujibu wa maelezo yako kuna uwezekano mkubwa sana wa kutengeneza angalau gunia hata 30 kwa ekari 5.

   Pamoja sana mkuu.

  14. elf miaka's Avatar
   Member Array
   Join Date : 5th August 2011
   Posts : 18
   Rep Power : 528
   Likes Received
   2
   Likes Given
   0

   Default re: Kilimo cha zao la Ufuta - Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

   wizara ya kilimo ingekupa the right answers au wakulima wenye experience au ajiri afisa ugani

  15. #15
   Bhbm's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st October 2009
   Posts : 714
   Rep Power : 759
   Likes Received
   173
   Likes Given
   2

   Default Soko la ufuta Tanzania

   Wakuu wana JF wenzangu, naomba kujuzwa kwa wale wazoefu, ni wapi kuna soko zuri la ufuta?
   Fungukeni wapendwa bila uchoyo ili tuweze kusaidiana kuinua uchumi wa nchi yetu.

  16. HAZOLE's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th February 2011
   Posts : 1,229
   Rep Power : 793
   Likes Received
   274
   Likes Given
   44

   Default re: Soko la ufuta Tanzania

   Quote By Bhbm View Post
   Nimeanza harakati za kulima pamoja na kununua toka kwa wakulima mkuu.
   mkuu ishu ya soko ipo hivi;
   1. kuna wanunuzi hasa wahindi huja mashambani wakati wa mavuno(lindi and mtwara are my case study)
   2. unaweza funga mzigo wako ukauleta dsm kwa mohamed entreprises ni mnunuzi mkubwa na ukisafirisha utapata faida zaidi
   3. waweza tafuta mzigo mkubwa wa kutosha kontena kuanzia 3, 4, nk na ukauza nje ya nchi na nchi inayonunua sana ni india.
   mimi nilikuwa na mpango wa kulima next yr but ntaanza na mazoa jamii ya choroko na mbaazi. hivi naandaa shamba.
   Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu chochote! Tumche Mungu wa Mbinguni siku zote! Amina

  17. #17
   Bhbm's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st October 2009
   Posts : 714
   Rep Power : 759
   Likes Received
   173
   Likes Given
   2

   Default

   Quote By HAZOLE View Post
   mkuu ishu ya soko ipo hivi;
   1. kuna wanunuzi hasa wahindi huja mashambani wakati wa mavuno(lindi and mtwara are my case study)
   2. unaweza funga mzigo wako ukauleta dsm kwa mohamed entreprises ni mnunuzi mkubwa na ukisafirisha utapata faida zaidi
   3. waweza tafuta mzigo mkubwa wa kutosha kontena kuanzia 3, 4, nk na ukauza nje ya nchi na nchi inayonunua sana ni india.
   mimi nilikuwa na mpango wa kulima next yr but ntaanza na mazoa jamii ya choroko na mbaazi. hivi naandaa shamba.
   Mkuu mimu nakushukuru sana kwa msaada wako mubwa wa ushauri.

  18. M-pesa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th September 2011
   Posts : 605
   Rep Power : 654
   Likes Received
   127
   Likes Given
   20

   Default Re: Kilimo cha ufuta, pilipili

   Mambo ya JF hayachuji! Ni vizuri kupitia thread za zamani pia.

  19. Shadya's Avatar
   Member Array
   Join Date : 14th September 2011
   Posts : 88
   Rep Power : 537
   Likes Received
   15
   Likes Given
   0

   Default Mbegu za ufuta mweupe zinapatikana wapi?

   Habarini wana JF, kama kuna mdau anafahamu wapi mbegu za ufuta mweupe zinapatikana anijuze tafadhali.

  20. Sniper's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th March 2008
   Posts : 1,942
   Rep Power : 1095
   Likes Received
   495
   Likes Given
   565

   Default Re: Kilimo cha ufuta, pilipili

   Wadau kuhusu ufuta, je ni sehemu gani za Tanzania zinafaa kwa kilimo cha Ufuta? mi nipo Dodoma, je Dodoma kunafaa? Kama hakufai je maeneo yake ya karibu je?Morogoro au Singida?


   Il Gambino.
   Real sign of intelligence isn't knoweldge, it's imagination


  Page 1 of 24 12311 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Replies: 850
   Last Post: 23rd November 2015, 18:23
  2. Replies: 393
   Last Post: 10th November 2015, 14:27
  3. USHAURI: Kilimo cha Mananasi na masoko yake Tanzania
   By kanyagio in forum Ujasiriamali
   Replies: 55
   Last Post: 8th September 2015, 10:05
  4. Kilimo cha Maembe: Ushauri na masoko yake
   By Chief in forum Ujasiriamali
   Replies: 93
   Last Post: 9th July 2015, 17:20
  5. Kilimo cha ufuta, pilipili
   By mja in forum Ujasiriamali
   Replies: 16
   Last Post: 1st December 2011, 23:29

  Tags for this Topic

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...