JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2015

  Report Post
  Page 2 of 122 FirstFirst 1234 12 102 ... LastLast
  Results 21 to 40 of 2421
  1. saggy's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 12th November 2008
   Posts : 151
   Rep Power : 698
   Likes Received
   68
   Likes Given
   3

   Thumbs down Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2015

   Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake kwa mujibu wa mawzo yake kwakuwa ana utashi wake binafsi so naomba nitoa mtizamo wangu na sitatoa maoni ili kumfurahisha mtu humu ndani ya Forum ni maoni yangu na nina haki ya kuwa tofauti au sawa kimawazo na mtu yoyote.EL anaifaa Tanzania kwa sababu zifuatazo:-

   Ni Kiongozi huyu shupavu,jasiri na mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama na serikali kwa upande wa serikali hili linadhihirika aliposhika nyazfa mbali mbali kama:-

   a.Kusimamia Sekta ya Elimu ambayo ndiyo Uti wa mgongo wa maendeleo ya Taifa lolote hapa Duniani.Alisimamia kwa ukakamavu kutekeleza mpango wa kupanua Elimu ya Sekondari na alihimiza kwa nguvu zake zote ujenzi wa Shule za Kata Nchi nzima ili kuwapa Fursa Mamilioni ya Watanzania wenzetu waishio Vijijini kupata Fursa ya Elimu.

   Zoezi hili lilihitaji uwekezaji mkubwa sana na Tukumbuke kwamba Taifa letu ni Maskini sana,changamoto zilizo ikabili Sekta ya Elimu kama Ukosefu wa vifaa vya maabara,Nyumba za Walimu,Madarasa ya Kutosha na upungufu wa Vitabu si kosa la mtu Fulani bali umaskini wa Taifa letu ndio maana WB na IMF hutoa misaada kwa nchi maskini kusaidia maendeleo ya Elimu kwakuwa ni Sekta inayohitaji uwekezaji mkubwa kifedha na Rasilimali zingine.

   EL ni mtu anayeamini katika Elimu ndi maana motto wake ni tofauti kidogo na Motto wa Chama chake na anasema ’’ ELIMU KABLA,KILIMO KWANZA’’ Ni kweli kabisa kwamba hakuna linaloweza kufanikiwa bila Elimu,Unaweza kuwaambia watu wasio na Elimu ya kutosha Walime Kilimo cha Kisasa?Me I agree kwamba Elimu KABLA na Kilimo Kwanza.

   Mataifa Makubwa yaliondelea leo Duniani yalifanya uwekezaji Mkubwa kwanza katika Elimu,hasa Elimu ya Msingi(Kwa mfano China,Brazil na USA) na Baadaye kufanya Mapinduzi Makubwa ya Kilimo,baadaye Viwanda Vidogo na baadaye Viwanda vikubwa ambavyo vilichochea kukua kwa kasi kwa Sekta za Huduma na kupelekea mfumuko wa nafasi kibao za ajira kwa Vijana!!!

   b.Kuwafukuza bila woga hadi kuwasindikiza Airport wawekezaji wababaishaji wa Kampuni ya City Water hadi kuwapandisha ndege uwanja wa
   Taifa:

   Akiwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo ,EL alitekeleza wajibu wake kwa umahili mkubwa na bila uwoga na moja ya mambo ambayo yatakumbukwa ni kufukuzwa kwa wawekezaji wababaishaji wa Kampuni ya Kitapeli ya City Water ambao walishindwa kutekeleza wajibu wao,aliwatimua na kuwasindikiza hadi Airport!EL ni Kiongozi Shupavu sana na asiyeogopa mtu!

   c.Kiongozi Mwajibikaji na asiyeogopa kufanya maamuzi magumu hata kama yatamuuza

   Kujiuzulu kwake kutoka katika Wadhfa wake wa Uwaziri Mkuu kufuatia Kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond inachukuliwa na wengi kama kuhusika kwake katika Saga hilo.Napenda kuwakumbusha Watanzania wenzangu kwamba Waziri Mkuu ndiye mtendaii Mkuu wa Shughuli za Serikali na mtekelezaji wa Maagizo ya Baraza la Mawaziri ambacho kimsingi ndicho chombo kikubwa cha Utendaji wa serikali (Govt. Machine) na hivyo kama kuna Kosa linafanyika basi Linatosha kuiangusha Serikali nzima so katika SAGA ile ilibidi Serikali Nzima akiwa ni Pamoja na Rais wajiuzuru lakini EL akubali mwenyewe kwa ajili ya kulinda heshima ya Chama chake na Serikali, huu ni mfano mzuri wa kuigwa kwa Waafrika wote.

   Siku zote tatizo letu waafrika ni kukosa kuwajibika pale inapobainika uzembe umefanyika,ukweli umebaki kuwa wazi mpake leo hii NCHI IPO GIZANI migao ya Umeme inaendele kama kawaida na dada wa Richmond ambaye ni Dowans Mitambo yake inawashwa na tumerudi pale pale!! Mimi nasema kwa kosa la Richmond,Serikali nzima ilikuwa imeanguka.

   d.Mfuatiliaji na asiyechoka kufuatilia kero za na hakai ofisini kungoja taarifa
   Wakati wa janga la Njaa lilisababishwa na ukame kwa msimu wa mwaka 2007/08 ni huyu EL alikuwa akishirikiana na Wakuu wa Wilaya zote zenye njaa na wakati mwingine alishiriki yeye mwenyewe kupita nyumba kwa nyumba kusimamia zoezi la ugawaji wa chakula kwenye Familia zenye njaa ili kuhakikisha kwamba azma ya serikali ya kwamba hakuna mwananchi atakayekufa kwa njaa inatimizwa ni huyu huyu EL.


   Mtu hawezi kukosa mapungufu hata siku moja,nakubali ana mapungufu yake lakini EL ni embe dodo lililoiva tayari kuvunwa na Watanzania Mwaka ukifika 2015.


   Nawaleteeni EL


  2. emmanuel1976's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th June 2011
   Location : Mwitongo
   Posts : 301
   Rep Power : 593
   Likes Received
   78
   Likes Given
   48

   Default Re: Kwa nini Lowassa anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   Unajua shida yetu wa TZ kubwa ni tabia ya kukubali kuaminishwa, Lowasa ana matatizo kidogo sana ukilinganisha bidii na umahiri wake katika siasa, hatujasema kuwa hakuna wengine ila tujenga hoja kuwa yeye alichafuliwa na anaziidi kuchafuliwa na kwa kuwa ukweli uko wazi si busara kuendelea kumchafua Lowasa. Si katoka madarakani mika 4 iliyopita mbona shida ndo kwanza zinazaliwa na nchi imewashinda, shule alizojenga Lowasa sasa ni mapagara tu yanayoongeza mzigo kwa taifa. Ukweli ni kwamba Lowasa kaonewa na wanazidi kumdharirisha sana, hii haikubaliki hapa. AListuambia kwa ufupi tu kwamba kilichokwa kinatafutwa wakati akiwa waziri mkuu ni uwaziri mkuu wake na tuliona ukichukuliwa machoni pake. Alipigwa shavu akanyamaza mbona wanaendelea kumfuata? Wanataka kumuua? Watanzania tumejua ukweli hatumtupi Lowasa sasa kwani atatusaidia kutuonyesha mlango wa kutokea kwa vyovyote vile

  3. emmanuel1976's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th June 2011
   Location : Mwitongo
   Posts : 301
   Rep Power : 593
   Likes Received
   78
   Likes Given
   48

   Default Re: Kwanini LOWASSA anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   Lowasa tunaambiwa tunakufagilia ingawa hatukujui ana kwa ana. Hebu njoo mbele utusadie kuwaambia watanzania madudu ya wakubwa zako ili usiwe na deni TZ, wa TZ wanakukumbuka sana, si umeona kuwa nia yao CCM na wakubwa zako ni kukumaliza wewe tu, kwa nini unawafichia siri? Mie nakukubali sana na wenzangu si umeona? toka mbele uwaambie watanzania ukweli ili uwe safi. Ni hilo tu

  4. Kakalende's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st December 2006
   Posts : 3,575
   Rep Power : 1493
   Likes Received
   659
   Likes Given
   628

   Default Re: Kwa nini Lowassa anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   Hii marathon ilianza 2008 sijui kufikia 2015 watakuwa wamebaki wangapi?
   Attached Thumbnails Attached Thumbnails Click image for larger version. 

Name:	Bounce+back+by+Jacob+Zuma.jpg 
Views:	3653 
Size:	35.1 KB 
ID:	32156  

  5. mkali wa leo's Avatar
   Member Array
   Join Date : 27th May 2011
   Posts : 84
   Rep Power : 552
   Likes Received
   3
   Likes Given
   7

   Default Re: Kwa nini Lowassa anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   lowasa anafaa kuwa rais ni vizuri ccm wakatambua hilo coz hata anayempinga lowasa ni mnafiki.hao mwanahalisi wamembeza baba wa watu lowasa lakini watz bado tunamkubali tena me naamini hata dr slaa hafikii mziki wa lowasa.

  6. MONTESQUIEU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th November 2010
   Posts : 846
   Rep Power : 738
   Likes Received
   79
   Likes Given
   63

   Default Re: Kwa nini Lowassa anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   Kwasababu amewaomba mumpigie campaign


  7. Mpangamji's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th May 2010
   Posts : 524
   Rep Power : 694
   Likes Received
   123
   Likes Given
   100

   Default Re: Kwa nini Lowassa anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   saggy

   e. Alisimamia utekelezaji wa kuchukua maji kutoka ziwa victoria hadi Shinyanga na Kahama, mradi pekee ulioendeshwa kwa fedha za serikali.
   The truth speaks for itself, it is always in 3-D

  8. kanta's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th January 2011
   Posts : 326
   Rep Power : 618
   Likes Received
   58
   Likes Given
   21

   Default Re: Kwa nini Lowassa anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   Kachafuka kama shilingi iliyotumbukia chOoni, ananuka,kaoza,kafulia yeye pamoja na wewe unayemwosha kwa maji ya kisoda.

  9. mbogo31's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th November 2008
   Posts : 646
   Rep Power : 795
   Likes Received
   138
   Likes Given
   137

   Default Re: Kwanini LOWASSA anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   Quote By saggy View Post
   Unasema Ukweli Mkuu,mimi jamani nimesema haya kwa mujibu wa ufahamu wangu mdogo ninaofahamumengine siyafahamu,kama kuna anayemfichia siri aseme sasa na Watanzania watamwelewa,nani asiyejua kwamba Waziri Mkuu anatengeneza maagizo ya Baraza la Mawaziri,kwanini Mzigo huo akatatwikwa EL peke yake?Je Bunge ambacho ni Chombo cha Wananchi katika kuihoji serikali ilikuwa wapi na Je Bunge ni chombo cha kungoja kungoja Kufanya Uchunguzi wa Matatizo ambayo tayari yameishatokea?Kwanini halisadii kuishauri Serikali kuepuka matatizo hayo?
   Hapo kwenye nyekundu

   na pia kule kwenye story yako ulisema yupo kwenye chama na system mbovu.

   Tunataka kubadili chama na hiyo system mbovu, na kwa kuwa humfahamu vizuri ni bora usimsemee, Chama mbadala kipo na kimeonyesha kinaweza kubadili hii system, kama majirani zetu karibu wote wameweza sisi tushindwe tuna nini?

   Mabadiliko ndio muhimu kwa nchi yetu.

  10. Rocket's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 11th April 2011
   Posts : 134
   Rep Power : 569
   Likes Received
   7
   Likes Given
   8

   Default Re: Kwa nini Lowassa anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   Hata mm namkubali sna EL but autangazie umma kilicho moyoni mwake kuhusu hizi tuhuma!!!!maanake naye akikaa kimya sna itakuwa vigumu watu kumwamini....

  11. almasy revo's Avatar
   Member Array
   Join Date : 10th June 2011
   Posts : 14
   Rep Power : 536
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By emmanuel1976 View Post
   unajua shida yetu wa tz kubwa ni tabia ya kukubali kuaminishwa, lowasa ana matatizo kidogo sana ukilinganisha bidii na umahiri wake katika siasa, hatujasema kuwa hakuna wengine ila tujenga hoja kuwa yeye alichafuliwa na anaziidi kuchafuliwa na kwa kuwa ukweli uko wazi si busara kuendelea kumchafua lowasa. Si katoka madarakani mika 4 iliyopita mbona shida ndo kwanza zinazaliwa na nchi imewashinda, shule alizojenga lowasa sasa ni mapagara tu yanayoongeza mzigo kwa taifa. Ukweli ni kwamba lowasa kaonewa na wanazidi kumdharirisha sana, hii haikubaliki hapa. Alistuambia kwa ufupi tu kwamba kilichokwa kinatafutwa wakati akiwa waziri mkuu ni uwaziri mkuu wake na tuliona ukichukuliwa machoni pake. Alipigwa shavu akanyamaza mbona wanaendelea kumfuata? Wanataka kumuua? Watanzania tumejua ukweli hatumtupi lowasa sasa kwani atatusaidia kutuonyesha mlango wa kutokea kwa vyovyote vile
   ccm wote ndo wameleta matatzo yote hayo. Hatuwataki. Awe rais wa kaya yako tu

  12. MAKALA's Avatar
   Member Array
   Join Date : 31st March 2009
   Posts : 42
   Rep Power : 656
   Likes Received
   9
   Likes Given
   0

   Default Re: Kwa nini Lowassa anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   Mimi simfahamu lowasa na sijawahi kukutana nae, but kutokana na record yake ya kazi nazani anaweza kua raisi mzuri, huyu ameshatubu mazambi yake, anafahamu wapi arekebishe tumpe nafasi 2015.
   LOWASA OYEEEEEEEEEEE

  13. Fredrick Sanga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th January 2011
   Location : Kijitonyama
   Posts : 3,126
   Rep Power : 2750
   Likes Received
   678
   Likes Given
   802

   Default Re: Kwanini LOWASSA anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   meonewa sana, amedhililishwa sana, tatizo lilikuwa uwaziri mkuu, Lakini huyo ndie kipenzi che CCM 2015.

  14. Mkiliman's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th June 2011
   Posts : 908
   Rep Power : 719
   Likes Received
   217
   Likes Given
   54

   Default Re: Kwa nini Lowassa anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   What can i say on EL's move...,lkn sisi wengi tunajadili paraproofs coz hatuna indepth play ya hao majuha wanaotaka kuwa predisents esp. the name under discussion! i thnk sifa za kiongozi kwa jamii yenye ustaarabu hatakiwi kuwa na mapungufu ambayo EL anakumbana nayo hata kama ni kusingziwa,bad attitudes dhidi yake ni obvious, hakuna sababu ya kuhold kuwa anafaa kuwa RAIS! he's dirty,morally unspeakable, thence with due respect i recommend him and his aliens to 4get such dream!

  15. Mzee Dogo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th November 2010
   Location : Kwetonge
   Posts : 295
   Rep Power : 623
   Likes Received
   55
   Likes Given
   33

   Default Re: Kwa nini Lowassa anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   lowasa ni mzuri tu kwa kumlinganisha na chekibobu lakini hafai kuwa kiongozi wa serikali bado, ni mwizi bwana unataka nini ili uamini?

  16. Feedback's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th March 2011
   Posts : 7,816
   Rep Power : 7592
   Likes Received
   4023
   Likes Given
   1523

   Default Re: Kwanini LOWASSA anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   Quote By Balantanda View Post
   Teh teh.....................

   Hoja ipi unataka,ukweli mbona uko dhahiri kwamba hata umuingize kwenye washing machine ama umsugue kwa steel wire kama sio dodoki huyo mtu hasafishiki........Ni mchafu sugu.......Period.

   Hata aende Nigeria sijui kwa nabii Joshua et al.......Kamwambie hafai kuishi Magogoni...

   Sababu za uchafu wake zinajulikana,sina haja ya kuziweka hapa,nitajaza bandwith bureeee.....

   Bala.....
   Hujajenga hoja kusema uchafu wake unajulikana haina maana yeyote ni sawa na wanafunzi kuandika kwenye pepa kuwa majibu yanajulikana sina haja ya kujibu swali.

  17. solution's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th April 2009
   Posts : 418
   Rep Power : 731
   Likes Received
   86
   Likes Given
   63

   Default Re: Kwa nini Lowassa anafaa kuwa Raisi wa Tanzania?

   Lowasa hasafishiki

  18. Sooth's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th April 2009
   Posts : 1,281
   Rep Power : 3463047
   Likes Received
   585
   Likes Given
   286

   Default Re: Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania?

   Kama unamwangalia EL wa kashfa ya Richmond, basi unaweza ukaokoteza maneno ya kumsafisha na kufanikiwa. Tatizo ni kwamba tuhuma kwa EL hazijaanza na Richmond, wakati wa uchaguzi 1995, huyu ndugu alisemekana ni bepari-ana mali nyingi ambazo haziwezi kupatikana kihalali kwa mfanyakazi wa umma. Kama EL ni safi, tuanzie huko, hata kabla ya kashfa ya richmond. Atueleze mali anazomiliki na ili tumwamini, aeleze hata mali za watoto wake ambao ijapokuwa ni vijana wadogo tu, wana ukwasi kama wamerithi toka enzi na enzi.
   "Iko siku haki itashinda na hiyo ndio siku utakapojua tofauti ya kuvua chupi na kuvua samaki."-Mohammed Ali-KTN.

  19. Dickson Mpemba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st January 2010
   Posts : 278
   Rep Power : 489
   Likes Received
   58
   Likes Given
   227

   Default Re: Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania?

   Lowassa ndiyo mtu pekee anayeweza kulitoa taifa hili la tanzania kwenye umaskini huu wa kipato na fikra pia ikubukwe kwamba ndiye aliye engineer mchakato wote wa ujenzi wa chuo kikuu cha dodoma ingawa credit wanapewa watu wasiostahili kabisa , kwa kifupu tanzania kwa sasa. "WE NEED DEVELOPMENT NOT DEMOCRACY"

  20. boma2000's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th October 2009
   Location : nyumbani
   Posts : 2,900
   Rep Power : 1200
   Likes Received
   135
   Likes Given
   110

   Default Re: Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania?

   Umelipwa shilingi ngapi? au wewe ndo yule uliyeoa mtoto wa dada yake halafu akakusogeza BOT
   Tanzania Itajengwa na Watanzania Wazalendo wa Ukweli

  21. Dickson Mpemba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st January 2010
   Posts : 278
   Rep Power : 489
   Likes Received
   58
   Likes Given
   227

   Default Re: Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania?

   Lowassa ndiyo mtu pekee anayeweza kulitoa taifa hili la tanzania kwenye umaskini huu wa kipato na fikra pia ikubukwe kwamba ndiye aliye engineer mchakato wote wa ujenzi wa chuo kikuu cha dodoma ingawa credit wanapewa watu wasiostahili kabisa , kwa kifupu tanzania kwa sasa. "WE NEED DEVELOPMENT NOT DEMOCRACY"


  Page 2 of 122 FirstFirst 1234 12 102 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Lowassa au Mwandosya kuwa Rais wa Tanzania 2015?
   By Mchambuzi in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 1623
   Last Post: 31st May 2015, 20:05
  2. Slaa na Zitto nani anafaa kuwa mgombea chadema 2015,
   By janja pwani in forum Uchaguzi Tanzania
   Replies: 10
   Last Post: 3rd September 2011, 14:57
  3. Replies: 16
   Last Post: 13th July 2011, 14:50
  4. Kagame anafaa kuwa rais wa tanzania
   By tunduma in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 0
   Last Post: 24th March 2011, 16:59

  Tags for this Topic

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...