Zuzu amwandikia barua bill gate tar 1

Oct 2, 2012
18
8
Kwenda kwa: Bill Gates, Microsoft
Kutoka kwa: Zuzu, Tanzania
Tarehe: 1 Oktoba 2012
Yahusu: Matatizo kwenye kompyuta yetu mpya.

Ndugu Bill Gates,
Anko wangu amenunua kompyuta mpya kwa ajili ya kutumia nyumbani kwetu. Nilipoichunguza nimegundua ina matatizo kadhaa. Nimeamua kukuandikia barua hii ili uyafanyie kazi.

1. Kuna batani ya 'start' lakini hakuna batani ya 'stop' button. Tafadhali tazama kwa makini.
2. Nina mashaka kama umeweka 're-guta' maana nimeona umeweka tu 're-cycle', lakini nyumbani kwetu kuna guta na siyo baskeli.
3. Pia nimeona kuna sehemu ya 'Find' lakini wala haifanyi kazi. Anti yangu jana alipoteza funguo. Nimejaribu sana kubonyeza find ili itusaidie kutafuta funguo imeshindwa. Naripoti tatizo hili.
4. Nimeona tu kuna 'Microsoft word' sasa nataka kujifunza 'Microsoft sentence', sasa ni lini utatuwekea Microsoft Sentence?
5. Tumenunua CPU, mouse na keyboard, lakini kuna kipicha kimoja tu kinachoonyesha 'My Computer': lini utatuwekea vipicha kwa ajili ya hivyo vifaa vingine?
6. Nimeshangaa kuona kompyuta imeandika mahali 'MY Pictures' lakini sijaona picha yangu hata moja humo. Lini mtaziweka?
7. Pia mmeweka 'MICROSOFT OFFICE' inakuwaje kuhusu 'MICROSOFT HOME' kwa kuwa hii ni kompyuta tunayotumia nyumbani kwetu na wala siyo ofisini.
8. Pia umeweka 'My Recent Documents'. Vipi kuhusu 'My Past Documents'?
9. Pia umeweka 'My Network Places'. Tafadhali sana iondoe hiyo maana anko atakuwa anajua mahali nilipo, kuna siku huwa natoroka shule.

Jambo la mwisho. Wewe jina lako ni GATES sasa kwa nini umeamua kuuza WINDOWS?

Wasalaam,
Zuzu.
 
ahsante zuzu ndio maana kwenye Microsoft Office kuna Home Premium.
Hatujaweka widget ya Mouse kwa sababu kuna Cut (cat).
kuhusu jina langu hiyo ni simple.
You must first pay your Bills at the Gate before we open our Windows!
 
Tenk yu veri machi wakli kwa kumpresent zuzu b4 mwanaJF Mchanga wa safu hii na nyingine...dah nyie wakli
 
Back
Top Bottom