Zuma anusurika kupigiwa kura

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,261
Viongozi wa Zimbabwe na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, wamekubalia kuchukuliwa kwa hatua kadhaa, kwa ajili ya kuzuia kuvunjika kwa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Zimbabwe, ambayo inalegalega.
Rais Jacob Zuma alikuwa nchini Zimbabwe kufanya mazungumzo ya kuimarisha serikali ya umoja wa kitaifa, na kuondoa tofauti kati ya Rais Robert Mugabe, na Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai.
Katika ziara hiyo, Rais Zumaamesema mazungumo hayo yalikuwa na mafanikio, na kuwa viongozi hao wamekubaliana kutekeleza hatua kadhaa, zitakazosaidia kuondoa tofauti zilizopo.
Wakati huo huo Rais Jacob Zuma, amenusurika kupigiwa kura na bunge la nchi hiyo ya kutokuwa na imani naye iliyoitishwa na vyama vya upinzani, kufuatia hatua ya rais huyo kutangaza kuwa na mtoto nje ya ndoa.
Kura hizo ambazo ni za kwanza kufanywa na bunge tangu chama Tawala cha ANC kuingia madarakani mwaka 1994, kura 241 zilipinga hatua hiyo na kura 84 ziliunga mkono.

Source;
http://www.tbc.go.tz/technology/395-zuma-anusurika-kupigiwa-kura.html
 
hii mi bunge nayao badala ya ku deal na mambo ya maana ina kazi ya kuhangaika na maisha binafsi ya watu
 
Back
Top Bottom