Zuhura, Zohali, Mwezi, Mstari Mmoja

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
279
202
Tena leo na kesho, sayari za Zuhura na Zohali zimeunganika na Mwezi mwandamo kutoa mandhari nzuri ya kupendeza sana angani jioni kuanzia kiasi saa moja jioni hadi saa mbili na nusu (7pm-8:30pm) upande wa magharibi karibu nyuzi 20 juu ya upeo wa macho.

Kwa leo Jumanne 1, Novemba, Mwezi mwandamo upo chini ya sayari mbili hizo, Zuhura iking'aa na kuwaka ajabu juu na Zohali inafuata chini kwa kung'aa kwa upole.

Hasa kesho Jumatano tarehe 2, Novemba, Zuhura, Zohali na Mwezi zitakuwa mstari mmoja.

Angalia hali itakavyokuwa hapo kesho:
zuhura-zohali-mwezi-mstari-mmoja-1

Zuhura, Zohali, Mwezi, Mstari Mmoja 2 Novemba
Zuhura, Zohali, Mwezi, Mstari Mmoja - Astronomy in Tanzania
 
Ok,hii inafaida gani na hasara gani kidunia,,,,au inaashiria nini,,,,kuna mtu aliniambiaga ikiwa ivyo kuna Kiongozi mkubwa atakufa au kupindulia katika nchi mojawapo
 
.....tutamkumbuka sheikh YAHAYA.....angelikuwepo angetupa kitakachojiri....siasa kidogo....dini kidogo..sayansi na uongo na ukweli kidogoo...siku inapita......SIKU HIZI SINA MUDA KABISA WA KUTAZAMA CHANNEL 10...
 
Ok,hii inafaida gani na hasara gani kidunia,,,,au inaashiria nini,,,,kuna mtu aliniambiaga ikiwa ivyo kuna Kiongozi mkubwa atakufa au kupindulia katika nchi mojawapo
Faida ni kufurahia mandhari ya kuvuta macho, pamoja na kuona jinsi vitu vya angani vinavyopishana na kuchangamsha bongo kufikiria kwa nini zifanye hivyo na hatimaye kuelewa maumbile ya ulimwengu wetu. Ukiwa na darubini kunautamu wake pekee pia kuona maumbo ya sayari hizi, hasa Zohali ni ya kipekee kabisa.
 
Ok,hii inafaida gani na hasara gani kidunia,,,,au inaashiria nini,,,,kuna mtu aliniambiaga ikiwa ivyo kuna Kiongozi mkubwa atakufa au kupindulia katika nchi mojawapo
Mambo ya kuathiri maisha yetu au kutufaidi kihali hayana msingi katika mipangilio ya sayari.
 
Back
Top Bottom