Zongh Tong ni wawekezaji au dealers

Mapinduzi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
2,422
91
Kampuni ya Zongh Tong imechukua eneo la iliyokuwa TAMCO (nadhani Tanzania Motors Company). Hii kampuni ya Zongh Tong wanatengeneza mabasi ya abiria na kuuza. Nadhani wengi mtakuwa mmeona matangazo yao kwenye television.

Nisichokijua ni kuwa hii kampuni imejiandikisha hapa nchini kama mwekezaji au kama car dealer?

Kama walijiandikisha kama wawekezaji, je wanatengeneza magari hapa nchini au wanatengeneza mabasi huko nchini kwao na kuyaleta Tanzania kuuza?

Kama wanatengeneza nchi kwao na kuuza hapa nchini, ina maana TAMCO imebadilika kutoka kuaasemble magari hadi kuwa yard/dealership?

Kama wanatengeneza magari huko kwao na kuja kuyauza Tanzania kwa mgongo wa uwekezaji, ina maana ajira nchini kwao itakuwa imeongezeka, export nchini kwao itakuwa imeongezeka, na uchumi wa nchi yao utakuwa umeimarika zaidi wakati uchumi wetu unazidi kudidimia, na tatizo la ajira linazidi kuongezeka, n.k.
 
nchi hii kila kitu ni possible ilimradi mtu apewe tu go ahead! agtafanya atakacho hata kufuga kuku!
 
Bongo ni shamba la bibi kwa mtu yeyote asiyekuwa mtanzania. Ukiwa mtanzania utapigwa mkwara wa nguvu, ukiwa ukiwa raia wa kutoka nchi yoyote ya nje (hata ile jirani tu kama Kenya, Uganda, Somalia n.k.) utaachwa ufanye unalotaka bila hata kuulizwa lolote.
 
Nafikiri hii inaitwa 'Doing Business in the ever changing environment' , lakini sisi hatuangalii kwa kina kama tunafaidika au tunapata hasara kiuchumi. Uingereza waliamua kufunga viwanda vyao vya nguo na kuwapa Bangladesh, Vietnam kufanya kazi hiyo baada ya kupiga mahesabu kuwa ni bora kuwalipa mishahara midogo wa-Asia lakini wao wakamiliki 'brand' ya vitu hivyo kwa faida kubwa, kwa Tanzania bado sijajua.
 
Back
Top Bottom