Zomea zomea yamwangukia Mwakyembe

haya sasa kazi anayo namuona kila mara kazi yake ni kwenda pale kariakoo maeneo ya mkunguni street kwa yule muhindi anaye wauzia suti za kuvaa mafisadi hao eti suti moja milioni moja nusu wakati jimboni kwake anashindwa hata kuwalipia karo baadhi ya watoto ambao hata wazazi wao walishakufa waige mfano wa mbunge wa musoma muda mfupi kafanya mambo makubwa sana
 
Rais , fukuza huyu kazi kwnio kuwa na waziri kwenye cabinet ambaye anazomewa na wananchi wake ni tatizo kubwa anaweza kukusababisha hata wewe kuzomewa kwa kumteua mtu mbovu kama huyu, Mbona Chenge na Mramba walipokuwa miundombinu hatukusikia wakizomewa tena kwenye majimbo yao?
 
Hafadhari yeye kazomewa bosi wake alipopolewa na mawe akaweka historia
 
naona wananchi watakuwa wamechoka na sound zake sasa wanataka vitendo na sio sound, inabidi afanye kweli na sio kupiga sound tu.
 
a Nifahamisheni fasta ili nianze mpango mzima wa uharakati wa kuongoza operation 'popoa mawe na kisha zomea' wabunge wote ambao hawawakilishi mawazo ya wana nchi!
Dah! Hahahaha hili litakuwa bonge la operesheni
 
:israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel:
 
Safi sanaa, amepata alichokitaka. Alisaliti wananchi kwa kutomtaja jk kwenye richmond. Jk yumo, ila kyembe akabana akapewa unaibu.
 
Mwakyembe ni FISADI kuliko hao anaowataja, sema yeye ni mwanasheria, hatumii jina lake, lakini fisadi mkubwa asitudanganye chochote

Umepata sehemu ya kupumulia kuonyesha hasira zako, unaweza kutupatia ushahidi walau kidogo
 
Yamekuwa haya tena, eti nayeye ni fisadi! Wa Tz bwana kumbe ukiwa mwanasheria unakuwa fisadi pasipo kufahamika sasa sijui ya chenge tusemeje tena yeye harvard
 
Yuko wapi bingwa wa thread hapa GINIASBRAIN mbona si msikii au bundle imekwisha? Ngoja mzee wa kaya naye akosee badala ya kutembelea mikoa ya ugaibuni aje hii ya kwetu naye aonje joto ya jiwe naamini kina GB watahama jf
 
Tatizo la kuzomewa kwa Mwakyembe ni ahadi zake alizoahidi. Inasemekana aliunda kikundi cha vijana wahuni mjini na kukiita Task Force na kuwaahidi mambo mengi. Hao vijana kweli walimsaidia lakini baada ya kupata wamejikuta hata simu zao tu hapokei.

Vijana hao hao ndio wamefunga standa siku tatu na wanasema bila kutengenezwa barabara haifunguliwi. Pia ziara za kwenye kata zimekwama maana sehemu nyingi wananchi wanamzomea kwasababu ya ahadi zake. Sasa kaamua kukutana na wana ccm peke yao. Lakini nao wanaenda wachache na pia wanamkumbushia ahadi zake.

Vijana hao jana walikuwa na mkutano na halmashauri, mwakyembe hakutokea. Mwenyekiti wa halmashauri alijikanyaga sana na akaendelea kutoa ahadi zingine.

Mchana mwakyembe alikutana na ccm kyela mjini na kuwaambia vijana wa chadema wamevamia ccm. wajumbe wakamwambia hao ni vijana uliowaingiza mwenyewe ccm wakusaidie kushinda ubunge, nenda kawatulize kwa kutimiza ahadi.

Ratiba inaonyesha Mbowe na Mnyika watakuwa kyela leo. kwa hapa mjini watavuna wanachama wengi sana hasa vijana.
 
Teh! teh! teh! hili picha ni kali ile kinoma na Stelingi mwenyewe bullcheka hao watendaji je? ,ikifika 2015 badala ya kubaki mlima kitabaki kichuguu teh teh!
 
Wakuu siku ya jana, mh Mwakyembe, amezuiliwa na wakazi wa Kyela kuingia stendi ya Kyela na kuzomewa na wakazi wa hapa wakidai aliwaahidi lami na hajatekeleza, toka juzi hakuna gari linaloingia stendi, natamani sana kuwatumia picha lakini nipo via mobile

nani asiyejua siasa za Kyela? Acha kuleta porojo za uongo hapa.
 
Leo nimejua kirefu cha UVCCM,Kuna bango limeandikwa kirefu chake ni Umoja Wa Virusi Chanzo Chake Mafisadi,hapa huku kijijini kweli Ccm chali,
 
mdau kaandika haya kwenye facebook kuhusu sakata la Kyela na kufungwa stand:

kiukweli ni kwamba CCM kwa hapa mjini wafanye kazi ya ziada saana kuwashawishi vijana waikubali jana ilikuwa ni aibu tupu diwani anatukanwa matusi ya nguoni ,mkurugenzi na wengineo kasoro DC ndio aliyekuwa anasikilizwa na Mbunge ndio hawataki hata kumsikia wlishamfukuza mara mbili na akipita anazomewa na alienda Ikolo(kijijijni kwao)walimzomea na kugoma kumsikiliza kutokana na ahadi ya maji aliyowa ahid ikabidi atoe 250,000 lakini wakadai wanachotaka ni maji,boda na ngana napo hakupata mapokezi mazuriKwakifupi Chama tawala wajipange upya vinginevyo CHADEMA wanachukua jimbo,Viongozi waliofika jana jioni ni Mbunge wa Mbeya mjini J.Mbilinyi(Mr 2,Sugu) Mbunge wa Hai Freeman Mboye na Dr Slaa na viongozi wengine wanawasili leo,Ila walipokelewa na wananchi wengi saana na wananchi waliwalazimisha watembee kwa miguu waone ubovu wa barabara na stand!Mengi mtayapata jion baada ya mkutano!!
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Karibu CHADEMA mzee uchukue jimbo .....
 
Karibu CHADEMA mzee uchukue jimbo .....

Masanilo,

Njoo ugombee Kyela tutakupa kura, hatuna ukabila.

Waliopewa makadi ya bandia ili wazitumie kusaidia mgombea, sasa kadi hizo hizo zinatumika kuwamaliza.

Kazi kweli hata mwaka haujaisha tayari yamekuwa haya.
 
kwa siasa za tz vilivyo hivi sasa, hakuna mtawala aliye salama. watu wamechoka na hali ngumu za maisha zinawapandisha hasira haraka sana. bora kila kiongozi achukue tahadhari. ikiwezekana achukue chake mapema akatatue shida za familia yake huku wenye nchi wakichukua nchi yao! hali ni mbaya sana kwa watawala na hakuna aliye salama
 
Back
Top Bottom