Zomea zomea ya Mramba huko Rombo

Msisahau mabandiko yenu baada ya kura kupigwa manake wananchi wanajua wanataka nini hata mkiwasemea namna gani. Rombo si kuna Kiliwater sasa kama wao nao wanatatizo la maji basi watu wa Kibakwe - Dodoma huko wasemaje?

Sikubaliani na wote wanaona raisi/mbunge au diwani ni suruhisho la matatizo kwa wananchi kwa 100%. Wananchi wenyewe wanayo nafasi kubwa ya kujiletea maendeleo wao wenyewe hata kama hakuna mbunge kutoka chama chochote kwa zaidi ya 40%.

Ubunge ni uwakilishi zaidi kuliko kutatua matatizo ya wananchi, wananchi wenyewe watajiletea maendeleo kama mtaacha kuwatukuza wanasiasa na uchaguzi.
 
Asante Mkuu kwa kuliona hili. Ni kweli Mramba amefanya makubwa Rombo na Laiti Selelii asingemkalia kooni ungekuta barabara ya Marangu mpaka kamanga ingekuwa mkeka. Huwezi kumlinga nisha na kina Chenge na Kawambwa.

Warombo wameweka standard za juu sana kumpata mbunge. Hili ni jambo jema sana. Inabidi hata kumpata rais au kiongozi yeyote tumwekee standard za juu na kwenye kumjaji performance tumhukumu kwa aliyoshindwa.

Nawaombea Mungu wananchi wa Rombo wafanye mabadiliko ili yeyote atakayeahidi aweze kutimiza yote aloahidi.

Mradi wa maji Rombo si alipewa Salakana (Kiliwater) ili arudi CCM? Mwenye uhakika wa hili atujuze

Mkuu I berg to differ with you.

Nakubaliana na hayo mafanikio yake. Lakini hata kama hajui au ni feki stories or any blah blah iliyoko juu yake. Ukweli ni kwamba amesontwa kwenye kashfa ya amtumizi mabaya ya ofisi ambayo ni dhamana ya wananchi. Ni vizuri asubiri jina lake lisafishwe ndo arudi huko. Yeye kwa sasa hafai hadi hapo kesi yake itakapokwisha!

Haya mambo ya double standards ndani ya CCM ndo ubabaishaji wenyewe. Yeye aende bana aache wengine hadi hapo atakapokuwa msafi bana!!!
 
bar za rombo watu wanakunywa bure bili kwa mramba
wanasema tutalewa na kura tutampigia selasini
 
..tatizo ni kwamba ame-deliver!!

..kati ya shule 10 bora mkoani Kilimanjaro 5 zinatoka jimbo la Rombo.

..Mramba ufisadi wake anafanya kwenye manunuzi ya ndege ya raisi, na alex stuwart. hafanyi ufisadi kwenye miradi inayohusisha jimbo lake la uchaguzi.

..mtofautishe na Kikwete na Dr.Kawambwa wanaofanya ufisadi kwenye miradi ya ujenzi wa barabara bagamoyo.
alaa kumbe ni fisadi eeeh?!!! haya nielezee uzuri wa ufisadi baba ili utushawishi tusimfunge huyu bazazi
 
Msanii,

..there is no where nimesema ufisadi ni mzuri.

..lakini mafisadi, kama wahalifu wengine, wana madaraja.

..mwizi wa kutumia silaha, ni tofauti na mwizi mchomoaji mifukoni.
 
Back
Top Bottom