Zomea zomea imetawala mkutano wa rc laurent gama na walimu kilimanjaro

Sir R

JF-Expert Member
Oct 23, 2009
2,175
298
Leo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro aliamua kukutana na walimu wa Sekondari manispaa ya Moshi katika ukumbi wa shule ya sekondari Majengo kwa ajili ya kusikiliza kero za walimu.
Mkutano uliaanza kwa mkurugenzi kutambulisha meza kuu. Baada ya utambulisho aliamkaribisha mkuu wa wilaya Ibrahimu Msengi kusema machache na kumkaribisha Rc Gama.

Mkuu huyo aliaanza kwa kuwasifu walimu kwa kusema walimu wanafanya kazi nzuri mfano walimu wengi walishiriki katika zoezi la uandikishaji wa sensa, hatua hiyo ilikumbana na kelele za kuzomea, kwani walimu wengi walikosa nafasi ya kushiriki katika zoezi hilo kwa kuwa walishiriki katika mgomo wa walimu. DC aliamua kumkaribisha mkuu wa Mkoa.

Wakati wa utambulisho watumisho wote wa halmashauri wakupigiwa makofi isipokuwa viongozi wa CWT waliokuwa meza kuu.

Mkuu wa mkoa aliongea kwa ufupi kuwa alikuja kusikiliza kero za walimu halafu akawakaibisha walimu kutaja kero zao. Baada ya kero kutajwa, Rc aliwakaribisha wakuu wa idara mbalimbali kujibu na kutoa ufafanuzi wa hoja za walimu.
Idara iliyokumbwa na zomea zomea ni idara ya utumishi. Walimu walikuwa wakali mno.

Bwana Gama alijitahidi sana kuwatuliza walimu na kwa kiasi kikubwa alifanikiwa. Mkurugenzi na watumishi wake walikuwa kimya muda wote.

Rc alisema kuwa itakuwa ni utaratibu wake wa kukutana na walimu ili kuboresha sekta ya elimu mkoa wa Kilimanjaro.

Mkutano ulianza saa 4:15 asbuhi na kumalizika saa 10 jioni.
 
Sasa ukimzomea RC ndo madiwani wako wataruhusiwa kwenda kutumbua pesa za wavuja jasho kwa safari za kisanii?? Hii mada mpelekee nanii wako. Nisawa na wale waliowadanganya wahandishi kwenda kufungua mashina wakati wa sensa sasa anawadanganya eti wafanye maandamano nchi nzima. wao wanaishi kwa stori wakiota vigimbi na pesa ndo noo
 
Hii Jamii Forum inabidi iheshimiwe. Kuna maba zisizo natija zinakaa sana humu lakini kuna zingine zikimgusa tuu CHADEMA haraka sana zinatolewa sasa hatujui ni administrators wanazitoa au kuna mtu ana hike na kuhujumu huu mtandao. Heshimuni mawazo ya watu wote. Msije kmashangaa mkishindwa kwenye uchaguzi mkuu kwa sababu mliruhusu genge la watu wanaofanana kuwaaminisha vitu ambavyo wa Tanzania wengine hawamo kabisa kwenye fikra zenu za kislaa slaa ki Movement Change ambazo hazieleweki una change kwenda mbele au kuiga tunayoyaona Somalia na Congo???
 
Almasiomary,
Soma vizuri taarifa niliyokupa.
CDM na slaa wanahusikaje hapo. RC hakuzomewa ila watumishi waliokuwa wakijaribu kupindisha ukweli.

Je wewe ni miongoni mwa hawa watumishi waongo?
Karibu
 
Vipi kuhusu hoja ya malimbikizo ya walimu??
Kasemaje kuhusu kuhusu hilo?
maana kusikiliza matatizo peke yake haitoshi.
iNATAKIWA YATATULIWE
 
Hivi vichwa vingine sijui visigino! Ilipaswa kuripoti hoja na sio mtu au ushabiki. Kwa mfano kero za walimu 1,2,3 na majibu yalikuwa hivi 1,2,3 na mwisho pande hazikuafikiana.......
 
Leo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro aliamua kukutana na walimu wa Sekondari manispaa ya Moshi katika ukumbi wa shule ya sekondari Majengo kwa ajili ya kusikiliza kero za walimu.
Mkutano uliaanza kwa mkurugenzi kutambulisha meza kuu. Baada ya utambulisho aliamkaribisha mkuu wa wilaya Ibrahimu Msengi kusema machache na kumkaribisha Rc Gama.

Mkuu huyo aliaanza kwa kuwasifu walimu kwa kusema walimu wanafanya kazi nzuri mfano walimu wengi walishiriki katika zoezi la uandikishaji wa sensa, hatua hiyo ilikumbana na kelele za kuzomea, kwani walimu wengi walikosa nafasi ya kushiriki katika zoezi hilo kwa kuwa walishiriki katika mgomo wa walimu. DC aliamua kumkaribisha mkuu wa Mkoa.

Wakati wa utambulisho watumisho wote wa halmashauri wakupigiwa makofi isipokuwa viongozi wa CWT waliokuwa meza kuu.

Mkuu wa mkoa aliongea kwa ufupi kuwa alikuja kusikiliza kero za walimu halafu akawakaibisha walimu kutaja kero zao. Baada ya kero kutajwa, Rc aliwakaribisha wakuu wa idara mbalimbali kujibu na kutoa ufafanuzi wa hoja za walimu.
Idara iliyokumbwa na zomea zomea ni idara ya utumishi. Walimu walikuwa wakali mno.

Bwana Gama alijitahidi sana kuwatuliza walimu na kwa kiasi kikubwa alifanikiwa. Mkurugenzi na watumishi wake walikuwa kimya muda wote.

Rc alisema kuwa itakuwa ni utaratibu wake wa kukutana na walimu ili kuboresha sekta ya elimu mkoa wa Kilimanjaro.

Mkutano ulianza saa 4:15 asbuhi na kumalizika saa 10 jioni.
Hapo kwenye Bold ni Idara iliyopo chini ya Halmashauri (Afisa Utumishi) au Idara ya Utumishi wa Walimu? Kwanini Idara hii imepigiwa kelele kwa mtazamo wako Mkuu Sir R?
 
Last edited by a moderator:
Hii Jamii Forum inabidi iheshimiwe. Kuna maba zisizo natija zinakaa sana humu lakini kuna zingine zikimgusa tuu CHADEMA haraka sana zinatolewa sasa hatujui ni administrators wanazitoa au kuna mtu ana hike na kuhujumu huu mtandao. Heshimuni mawazo ya watu wote. Msije kmashangaa mkishindwa kwenye uchaguzi mkuu kwa sababu mliruhusu genge la watu wanaofanana kuwaaminisha vitu ambavyo wa Tanzania wengine hawamo kabisa kwenye fikra zenu za kislaa slaa ki Movement Change ambazo hazieleweki una change kwenda mbele au kuiga tunayoyaona Somalia na Congo???

are you ok up there?
 
Vipi kuhusu hoja ya malimbikizo ya walimu??
Kasemaje kuhusu kuhusu hilo?
maana kusikiliza matatizo peke yake haitoshi.
iNATAKIWA YATATULIWE

Walidai baadhi ya madai ni ya tangu kwa katibu mkuu, zaidi walisema wataendelea kushughulikia na RC kawaomba walimu watulie kwani mambo yanaanza upya kwani atafuatilia kero hizo mpaka zitakapotatuliwa.
 
Hapo kwenye Bold ni Idara iliyopo chini ya Halmashauri (Afisa Utumishi) au Idara ya Utumishi wa Walimu? Kwanini Idara hii imepigiwa kelele kwa mtazamo wako Mkuu Sir R?

Ni afya utumishi. Sababu ya kuzomewa ni kuhusu maswala ya madaraja na scale za mishahara, hakuwa anatoa maelezo kwa kupindishapindisha. Mengine ni kuhusu posho ya uhamisho kwa kunukuu standing orders kifungu tofauti ambacho kinamnyima mwalimu haki zake za uhamisho.

Pia walimu walichangishwa michango ya mwenge na vitambulisho.

Mwishowe waliomba msamaha kuwa kulikuwa na makosa.
 
Sasa ukimzomea RC ndo madiwani wako wataruhusiwa kwenda kutumbua pesa za wavuja jasho kwa safari za kisanii?? Hii mada mpelekee nanii wako. Nisawa na wale waliowadanganya wahandishi kwenda kufungua mashina wakati wa sensa sasa anawadanganya eti wafanye maandamano nchi nzima. wao wanaishi kwa stori wakiota vigimbi na pesa ndo noo

Hivi unajua kweli kinachoongelewa hapa?
 
Back
Top Bottom