Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,299
- 33,079
Friday, October 09, 2009 4:36 PM
ALIYEKUWA Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe ameandika barua ya kuacha kazi katika jeshi hilo baada ya Serikali kukata Rufaa dhidi yake.
Jeshi la Polisi limethibitisha kupokea barua ya Zombe inayoeleza kutotaka tena kuendelea na ajira ya jeshi hilo.
Maamuzi ya Zombe yamekuja kwa kudai kuwa baada ya kuona amefikia hatua hiyo ya hofu ya kwa kutengenezewa kesi nyingine na kulazimika kuandika barua ya kuomba kuacha kazi.
Kamishna wa utawala na rasilimali watu wa Jeshi la Polisi, CP Clodwig Mtweve, amesema barua hiyo imepokelewa na imekabidhiwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ambaye kiutaratibu ndiye mwajiri wa Zombe.
Mtwere alisema kuwa katibu huyo ndiye mwenye mamlaka ya kujibu barua hiyo ya kuacha kazi ama kuendelea nay eye ndiye atakayekuwa na mamlaka juu ya maombi hayo.
Hatua ya Zombe imekuja baada Juzi Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) alikata rufani dhidi ya Zombe na wenzake wanaotuhumiwa kwa mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, Morogoro, na dereva teksi mmoja.
Rufani hiyo ina sababu 11 zinazopinga kuachiwa huru kwa washitakiwa hao wanaodaiwa kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara hao.
Sababu hizo zilizowasilishwa na DPP ni pamoja na Jaji Salum Massati, ambaye ndiye alikuwa akisikiliza kesi hiyo na kutoa hukumu ya kuwaachia huru washitakiwa hao, kufanya makosa katika kujielekeza, kujenga na kutoa tafsiri katika kanuni za kosa.
Rufani hiyo inadai kuwa Jaji Massati alifanya makosa katika kumwachia huru mshitakiwa wa kwanza, ambaye ni Zombe, pamoja na kuwapo ushahidi wa kutosha wa kimazingira ambao ungeweza kumtia hatiani.
Rufani hiyo pia inadai kuwa Jaji alishindwa kutoa sababu za washitakiwa wa WP Jane na D.2300 D/CPL Sarro kwa kuathirika kwao kimazingira kama alivyoeleza kwenye hukumu yake.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3296882&&Cat=1