Zombe ni zaidi ya muuwaji-CHADEMA

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
[h=2]Chadema yang`ang`ania kumwanika Zombe katika mauaji[/h]

Na Thobias Mwanakatwe

14th August 2011

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

comment_bubble.png

Maoni

ZombeDullah(2).jpg

Abdallah Zombe

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoa wa Mbeya kimeanzisha mkakati wa kumwanika aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe kwa kuwaeleza wananchi katika mikutano ya hadhara jinsi anavyodaiwa kushiriki mauaji ya wafanyabiashara wa mkoa wa Morogoro kama hotuba ya kambi ya upinzani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ilivyotolewa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema hivi karibuni Dodoma bungeni.
Mkakati huo wa kumshambulia Zombe umeanza rasmi jana ambapo Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, John Mwambigija, aliwasomea mamia ya wananchi wa kata ya Ruanda jijini Mbeya walioshiriki mkutano wa hadhara wa chama hicho, hotuba ya kambi ya upinzani ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Akisoma hotuba hiyo kwa wananchi ambayo alidai imeletwa mkoani Mbeya ikitokea Dodoma, alisema Zombe hana sababu za kuanza kumshambulia Mbunge wa Arusha, Lema kuhusu yeye (Zombe) kushutumiwa kuhusika na mauaji ya wafanyabiashara wa Morogoro.
Mwambigija alisema Zombe anapaswa kutambua kuwa Lema alisoma hotuba hiyo siyo kwamba yalikuwa ni mawazo yake binafsi bali yalikuwa ni ya kambi ya upinzani ambapo yeye (Lema) aliiwasilisha kwa sababu ni Waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani.
Mwenyekiti huyo wa Chadema alidai yeye (Mwambigija) alishaishi Dar es Salaam na kwamba alimfahamu Zombe jinsi alivyokuwa na mtandao wa majambazi na kwamba kwa kuwa Zombe alikuwa mfanyakazi wa Jeshi la Polisi na alifahamu kuwa Godbless Lema alikuwa katika mtandao wa wezi wa magari je alichukua hatua gani.
Alisema Chadema inamheshimu sana na Watanzania wapenda amani wanampenda Mbunge wa Arusha, Lema na ndiyo maana alichaguliwa kwa kura nyingi na kushika nafasi ya pili kitaifa nyuma ya mbunge wa Ubungo, John Mnyika aliyeshika nafasi ya kwanza.
Mwambigija ambaye wakati akihutubia wananchi wa kata ya Ruanda huku akisoma nakala ya hotuba ya bajeti ya Kambi ya Upinzani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya mwaka 2011/2012, alisema katika mikutano yao yote watakayokuwa wakiifanya katika mkoa wa Mbeya watahakikisha wanamwelezea Zombe kuwafahamisha Watanzania jinsi anavyodaiwa kushiriki katika mauaji ya wafanyabiashara wa Morogoro hata kama ameshinda kesi.
Mapema Julai 31, mwaka huu Mkuu wa Upelelezi wa zamani wa Mkoa wa Dar es Salaam, Zombe ameibuka tena na kutoa kauli kwa kudai kuwa siku Chadema kikiingia madarakani yeye atajinyonga na kumshutumu Mbunge wa Arusha, Lema kwamba alikuwa kwenye mtandao wa wizi wa magari.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Ye zombe amejitenga na jamii..na anatumia umaarufu wa chadema kama ngazi ya kujirejesha kinyemela...atasema mengi kwani mfa maji haachi kutapatapa.
 
[h=2]Chadema yang`ang`ania kumwanika Zombe katika mauaji[/h]

Na Thobias Mwanakatwe

14th August 2011

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

comment_bubble.png

Maoni

ZombeDullah%282%29.jpg

Abdallah Zombe

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoa wa Mbeya kimeanzisha mkakati wa kumwanika aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe kwa kuwaeleza wananchi katika mikutano ya hadhara jinsi anavyodaiwa kushiriki mauaji ya wafanyabiashara wa mkoa wa Morogoro kama hotuba ya kambi ya upinzani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ilivyotolewa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema hivi karibuni Dodoma bungeni.
Mkakati huo wa kumshambulia Zombe umeanza rasmi jana ambapo Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, John Mwambigija, aliwasomea mamia ya wananchi wa kata ya Ruanda jijini Mbeya walioshiriki mkutano wa hadhara wa chama hicho, hotuba ya kambi ya upinzani ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Akisoma hotuba hiyo kwa wananchi ambayo alidai imeletwa mkoani Mbeya ikitokea Dodoma, alisema Zombe hana sababu za kuanza kumshambulia Mbunge wa Arusha, Lema kuhusu yeye (Zombe) kushutumiwa kuhusika na mauaji ya wafanyabiashara wa Morogoro.
Mwambigija alisema Zombe anapaswa kutambua kuwa Lema alisoma hotuba hiyo siyo kwamba yalikuwa ni mawazo yake binafsi bali yalikuwa ni ya kambi ya upinzani ambapo yeye (Lema) aliiwasilisha kwa sababu ni Waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani.
Mwenyekiti huyo wa Chadema alidai yeye (Mwambigija) alishaishi Dar es Salaam na kwamba alimfahamu Zombe jinsi alivyokuwa na mtandao wa majambazi na kwamba kwa kuwa Zombe alikuwa mfanyakazi wa Jeshi la Polisi na alifahamu kuwa Godbless Lema alikuwa katika mtandao wa wezi wa magari je alichukua hatua gani.
Alisema Chadema inamheshimu sana na Watanzania wapenda amani wanampenda Mbunge wa Arusha, Lema na ndiyo maana alichaguliwa kwa kura nyingi na kushika nafasi ya pili kitaifa nyuma ya mbunge wa Ubungo, John Mnyika aliyeshika nafasi ya kwanza.
Mwambigija ambaye wakati akihutubia wananchi wa kata ya Ruanda huku akisoma nakala ya hotuba ya bajeti ya Kambi ya Upinzani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya mwaka 2011/2012, alisema katika mikutano yao yote watakayokuwa wakiifanya katika mkoa wa Mbeya watahakikisha wanamwelezea Zombe kuwafahamisha Watanzania jinsi anavyodaiwa kushiriki katika mauaji ya wafanyabiashara wa Morogoro hata kama ameshinda kesi.
Mapema Julai 31, mwaka huu Mkuu wa Upelelezi wa zamani wa Mkoa wa Dar es Salaam, Zombe ameibuka tena na kutoa kauli kwa kudai kuwa siku Chadema kikiingia madarakani yeye atajinyonga na kumshutumu Mbunge wa Arusha, Lema kwamba alikuwa kwenye mtandao wa wizi wa magari.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

sioni sababu ya CHADEMA kuanza kuvutana na Zombe na kwa vile kasema ushaidi anao nazani kinachoitajika ni kumuomba aende mahakamani.
Pamoja na hayo binafsi naona bado tunasafari ndefu kama mtu aliyekuwa na dhamana ya kupeleleza na hatimaye kupeleka ushaidi mahakamani, leo hii anatuambia anaushaidi ambao amekaanao muda mrefu????
Binafsi sio mzuri kwenye mambo ya sheria ila nazani huyu alikua anapaswa kufunguliwa kesi ya kutotimiza wajibu, kwa kuwa ifahamike kuwa katika upelelezi huo fedha za umma zilitumika ambazo ni kodi za wananchi ambao walikuwa wanafanyiwa huo uharifu.
 
mbona ya zombe yana fahamika sana na hizo ni damu za watu zinakula naye sahani moja
 
huyu mzee aya mambo ya kusema atajinyoka anahitaji psychologist haraka, tunafanya utani ila inawezekana kaanza kuchanganyikiwa, genge la ujambazi enzi zake na mahita lilikuwa linajulikana, na polisi walikuwa ni sehemu ya genge hilo. Mzee piga kimya subiri adhabu kwa mungu kwa roho za watu mlizotoa kwa ulafi wenu
 
Waswahili husema.Damu nzito kuliko maji, so damu ya watu wasio na hatia inaanza kumrudi sasa Zombe ameanza kuweweseka!
 
Zombe aliposema Chadema wakiingia ikulu yeye atajinyonga alimaanisha nini? au kwakuwa anajua wazi kuwa alitenda makosa mengi ambayo hao jamaa kwakuwa anajua hawataki kuleana watayafufua na yeye ataozea jela ama kunyongwa hivyo ni bora ajiwahi?
 
Bosi wake Mahita alitafuta majambia na kuyaweka nembo ya CUF, aliyaonyesha kwa waandishi wa habari.
Aliapa CUF hawawezi kutawala, ni kweli?
 
Amini usiamini!DAMU ya mtu haiend bure.Siku si nyingi mtamsikia ikila kwake.
 
Back
Top Bottom