Zoezi la Benki Kuu kutaka mabenki ya Update taarifa za wateja halihojiwi?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Nilikuwa nazungumza na rafiki yangu mmoja juu ya suala hili na mara moja tukawa na matatizo kadhaa; kwanza, linakusanya taarifa nyingi sana za mtu kiasi cha kutishia privacy ya mtu. Hizi taarifa zinasaidia vipi kuzuia money laundering? Hivi ni launderers wanaoutumia benki na kujanza taarifa zao zote muhimu? Vipi wanaotumia simu kulaunder money? Je makampuni ya simu yanayofanya shughuli za kibenki yanahitajiwa kufanya zoezi hili au ni mabenki tu?
Tatizo la pili ni kuwa inaonekana inatafutwa njia ya kuzidi kuwakamua na kuwabana law abiding citizens kwa ajili ya kodi na mapato kwa sababu serikali imegundua kuwa tax base yake haikui kwa kiasi kikubwa.

Jamaa yangu huyo alinidokeza (sijaweza kuthibitisha) kuwa VAT registered tax payers hawafiki 20,000 na wale wenye TIN hawazidi milioni moja. Sasa, hawa ndio ambao wanataka kuzidi kukamuliwa na TRA badala ya kufikiria namna ya kuexpand tax base yao na kuhakikisha kodi inalipwa ipasavyo na kwa wakati. Kwa mfano, mtu anayelipa kodi tayari taarifa zake nyingi zipo tayari kwanini benki nayo ijue hadi mtu anafanya kazi wapi? na hata kuhoji "estimated gross annual income"! Well, kama mtu akiandika EAGI halafu ikaonekana anapata fedha nyingi zaidi na akawa target ya TRA si itakuwa mtu kujichongea na badala yake watu wanaweza waka underpresent wanachokipata...

Hili zoezi hasa lina lengo gani kwa mwananchi anayetumia benki katika mazingira ya kawaida? Maana, wapo watu - kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali - wanaobadilisha kiasi kikubwa sana cha fedha nje ya mfumo wa mabenki na hawa hawaguswi!
 
Huwa nahisi wanatafuta acc ambazo zinahela hata laki mbili na hazijawa updated kwa muda mrefu, afu wao waka-assume pengine wamiliki wa acc hizo walishakufa kwa maajali ya tz, ili wajinufaishe.

Kwa kawaida watu wengi wana-acc nyingi na pengine familia zao hawazifahamu kabisa.
 
Hili ni very interesting concept... au wanajua kuna watu hawatojaza hizo forms au kuprovide hizo taarifa zote? Hivi mtu akikataa kujaza au kuwapatia hizo taarifa what happens to his moneys?
 
Kwa kweli hili ni sual zitto na linagusa nyanja nyingi katika maisha ya watu.nadhani wewe mwanakijiji anza mchakato wa kuhoji haya kupitia taaluma yako ya Law kama ulivyofanya kwa mafisadi wa Elimu!
 
Tatizo la pili ni kuwa inaonekana inatafutwa njia ya kuzidi kuwakamua na kuwabana law abiding citizens kwa ajili ya kodi na mapato kwa sababu serikali imegundua kuwa tax base yake haikui kwa kiasi kikubwa.

Jamaa yangu huyo alinidokeza (sijaweza kuthibitisha) kuwa VAT registered tax payers hawafiki 20,000 na wale wenye TIN hawazidi milioni moja. Sasa, hawa ndio ambao wanataka kuzidi kukamuliwa na TRA badala ya kufikiria namna ya kuexpand tax base yao na kuhakikisha kodi inalipwa ipasavyo na kwa wakati. Kwa mfano, mtu anayelipa kodi tayari taarifa zake nyingi zipo tayari kwanini benki nayo ijue hadi mtu anafanya kazi wapi? na hata kuhoji "estimated gross annual income"! Well, kama mtu akiandika EAGI halafu ikaonekana anapata fedha nyingi zaidi na akawa target ya TRA si itakuwa mtu kujichongea na badala yake watu wanaweza waka underpresent wanachokipata...

Hizo taarifa zitakuwa updated kila mwaka?

Kama haziwi updated walau kila mwaka, sidhani kama TRA wanaweza kutegemea kunufaika na zoezi hilo.
 
Moja ya vitu vinavyonikera sana ni namna ambavyo tunafanya kazi. Kila wakati tunafanya kazi after the fact. Kwanini wanahangaika na watu wasio fanya lolote kwenye money laundering.
Pengine kuna ukweli, hela imeota mbawa na kufilisika sio siri tena...wanajaribu kupanua wigo wa kukusanya kodi. Ila watakuwa wanafanya makosa na kukusanya kodi kwa watu wenye vipato vidogo....wahangaike na hao wanaopewa misahamaha bila kufuata taratibu
 
Hili zoezi zima kwa ujumla wake halieleweki. Benki Kuu haijaainisha ni taarifa gani muhimu zinazohitajika toka kwa wateja, matokeo yake kila benki ina mtindo wake tofauti...wakati benki nyingine unajaza fomu nusu kurasa benki nyingine fomu ndefu kurasa 2 hadi 4!
 
Hizo taarifa zitakuwa updated kila mwaka?

Kama haziwi updated walau kila mwaka, sidhani kama TRA wanaweza kutegemea kunufaika na zoezi hilo.

Ni kweli kabisa; maana wanataka hadi email; well kama ukiwapa ya kazi itakuwaje ukibadili kazi?
 
BOT haikutoa maelezo ya kutosha kwanini tunahitaji zoezi hili...anyway my take here MM ni kwamba zoezi hili linaweza kuwa na link na Patriotic Act ya 2001 ya kuingilia privacy za wananchi...maana tayari walishaanza kwenye mawasiliano sasa tunaingia kwenye finances zetu...
 
Mimi nilichokiona ni kwa ajili ya security wise kwani wanahitaji kujua nchi hii wanaotumia benki ni wangapi je income yao inatokana na nini je waajiriwa ni wangapi wafanyabi ashara wangapi je nikweli anafanya biashara gani?ana account ngapi?kwenye mabenk ya ndani je transaction zake huenda kwenye mitandao gani yanje je hulipa kodi kiasi gani kutokana na pesa zilizomo kwenye account na vitu kama hivyo!1
My take hii nchi haina uwezo wakumonitor hivi vitu kwani wafanyakazi wengi waserikali ni wavivu pili siyo competent!!
 
Ni kweli kabisa; maana wanataka hadi email; well kama ukiwapa ya kazi itakuwaje ukibadili kazi?

Kama suala ni kutakatisha pesa basi wanachotakiwa kufanya ni kuzuwia pesa kuingia kwenye account ya mtu, hadi mwenyewe awasiliane na benki iwapo zaidi ya kiwango fulani kitaingia kwenye account

Na hapo ndio namba za simu za wateja zinapohusika
 
nimepokea taarifa hizi toka wa mama...nikajiuliza lengo ni nini? na kwa nini wanataka taarifa nyingi kiasi hicho? kwa nini?...kama si kusumbua wananchi nini azma yao hao BoT?
 
Mimi nilichokiona ni kwa ajili ya security wise kwani wanahitaji kujua nchi hii wanaotumia benki ni wangapi je income yao inatokana na nini je waajiriwa ni wangapi wafanyabi ashara wangapi je nikweli anafanya biashara gani?ana account ngapi?kwenye mabenk ya ndani je transaction zake huenda kwenye mitandao gani yanje je hulipa kodi kiasi gani kutokana na pesa zilizomo kwenye account na vitu kama hivyo!1
My take hii nchi haina uwezo wakumonitor hivi vitu kwani wafanyakazi wengi waserikali ni wavivu pili siyo competent!!

hakuna cha security wala nini ni wapuuzi tu...nahili zoezi lao halitafanikiwa
 
Hizo taarifa zitakuwa updated kila mwaka?

Kama haziwi updated walau kila mwaka, sidhani kama TRA wanaweza kutegemea kunufaika na zoezi hilo.

Ni kweli kabisa; maana wanataka hadi email; well kama ukiwapa ya kazi itakuwaje ukibadili kazi?
Mkuu, hili zoezi ni hewa na usumbufu mkubwa! Halina tija kwa watumiaji, mabenki na hata TRA.

Watu wanafungua accounts kwa majina feki, wanatoa taarifa feki, barua feki za waajiri, hakuna wa kuthibitisha!!
Watamkamata nani?

Nikisema gross income yangu ni 200Mil tsh wakati ni 25Mil tsh, watathibitisha vipi sio au vise versa??

Hii nchi ya maigizo maigizo tu!!!
Watu kama mamvi wanatoa mabulungutu ya hela cash kama misaada wao wanazipata wapi? Umeshawahi kumuona mamvi ajitoa check?

Ina maana hela yake yeye inakaa kwrnye Sim Tank chumbani kwake sio!!!!
 
BOT wameona hakuna cha maana wanachofanya as far as economy is concerned,ili waonekane nao wapo active wamekurupuka na zoezi ambalo details zote wanazozihitaji benki wanazo na zaidi ya hizo kwenye kompyuta zao,..na kuna uwezekano watu wanatafuta sehemu ya kupigia posho kwa activity zisizokuwa na mantiki kama hizi..poor tanzania!!!
 
Huwa nahisi wanatafuta acc ambazo zinahela hata laki mbili na hazijawa updated kwa muda mrefu, afu wao waka-assume pengine wamiliki wa acc hizo walishakufa kwa maajali ya tz, ili wajinufaishe.

Kwa kawaida watu wengi wana-acc nyingi na pengine familia zao hawazifahamu kabisa.

KakaJambazi, nashukuru umenikumbusha jambo lingine la muhimu kuhusiana na hili zoezi, nilikuwa nikijiuliza nini haswa lengo lake-nahisi hili ulisemalo linaweza kuwa ni lengo kuu. Ziko acct. nyingi ambazo wenyewe washajiondokea na ambazo zina kiasi cha kutosha cha pesa nadhani inawezekana ikawa ndio target.
 
namna ya kupangiana kazi maalum ili wale allowance tu,
na zoezi lenyewe wamechemka limeongezwa mwaka mzima mbele.
 
Mimi nilichokiona ni kwa ajili ya security wise kwani wanahitaji kujua nchi hii wanaotumia benki ni wangapi je income yao inatokana na nini je waajiriwa ni wangapi wafanyabi ashara wangapi je nikweli anafanya biashara gani?ana account ngapi?kwenye mabenk ya ndani je transaction zake huenda kwenye mitandao gani yanje je hulipa kodi kiasi gani kutokana na pesa zilizomo kwenye account na vitu kama hivyo!1
My take hii nchi haina uwezo wakumonitor hivi vitu kwani wafanyakazi wengi waserikali ni wavivu pili siyo competent!!
Hitimisho lako limenishtua aisee!
Kama hawana uwezo, kwanini wanasumbua watu bure?
Pili, wasiotumia mabenki inakuwaje kama taarifa ndio izo zinahitajika? Je zile offshore accounts? Ina maana wazalendo wa kweli ndio wataandamwa na hili jinamizi? Wezi, mafisadi etc watakwepa hili zoezi muhimu lol.Nachoka kwelikweli.
Hili zoezi kama ni kweli lipo, basi BOT waje hapa watueleweshe nini madhumuni ya kukusanya taarifa za wateja.
BTW mambo ya account si ni siri au??
 
Maandalizi ya FREEMASONS kukamata uchumi wa dunia na kuitawala kirahisi.
 
Back
Top Bottom