Zitto Zuberi Kabwe soma huu waraka ukusaidie kutekeleza azimio lako la hoja binafsi

kiroba

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
324
114
Mh Zitto ni kweli kwa wazo lako wengi wa raia wema wa nchi yetu wanakuunga mkono. Hata hao wabunge wa CCM pia wanapenda iwe hivyo lakini ni woga tu ndio unawasumbua.

Sisi tumeamua kujitolea kuwashawisi wabunge wetu ili waweze kutia hizo sahihi ili upate kuwasilisha hoja binafsi. Ni kweli kama hutopata sahihi za wabunge wetu basi watakuwa wametusaliti kwa kiwango cha juu sana.

Hapo tunakuomba utusaidie ili na sisi kazi yetu iwe rahisi kuwatia adabu kwa usaliti wao. Baada ya kupata hizo sahihi tutakuomba utupe orodha ya wale walioweza kukupatia sahihi zao ili tuwajue wasaliti ni akina nani.

Unajua kwa jinsi wabunge walivyokuwa wakiongea kwa uchungu kiasi kile nitashangaa sana kama watashindwa kutumia nafasi hii kuiwajibisha serikali yao.

Haiwezekani kabisa eti uchangie kwa kupinga uozo wa serikali yako halafu unashindwa kuiwajibisha. Hapa Mh Zitto tunakuomba utuwekee orodha ya wote watakao saini.

Kushindwa kutupa hiyo orodha ni kutusaliti sisi wananchi wa Tanzania. Kwa kitendo hicho na wewe pia tutakuchukulia pia ni msaliti na mfitini wa taifa letu. Mimi naamini huwezi kutusaliti sisis watanzania wenzako.

Mungu akubariki na akulinde na wale wote wanaotaka kukufanyia ubaya!
 
Nashauri wananchi tuandamane Kama wabunge hawataweka saini tushinikize. Twende hadi Dodoma na sisi iwe km middle east. Wananchi tuungand.
 
Zitto ana wazo zuri ila kamwe hatapata sahihi za wabunge wa magamba. Hatafanikiwa
Mkuu Mnyisanzu hili suala lisipofanikiwa ni wazi wabunge wetu watakuwa wametuhadaa. Kwa hiyo hapa mh zitto atupe orodha ya waliosaini ili tuwajue waliotusaliti. Na tukishawajua basi inakuwa rahisi sana kuwaadhibu. Kwa hili tunatakiwa tuwe na msimamo wasituhadae tena.
 
Mkuu Kiroba, nakubaliana na wewe kwamba Mh. Zitto atupatie list ya wabunge waliotia sahihi ili itusaidie kuwa-evaluate wabunge wetu. Wabunge wa magamba ni wanafiki sana, wanasema wasichokisimamia!
 
Mh Zitto ni kweli kwa wazo lako wengi wa raia wema wa nchi yetu wanakuunga mkono. Hata hao wabunge wa CCM pia wanapenda iwe hivyo lakini ni woga tu ndio unawasumbua.
Sisi tumeamua kujitolea kuwashawisi wabunge wetu ili waweze kutia hizo sahihi ili upate kuwasilisha hoja binafsi. Ni kweli kama hutopata sahihi za wabunge wetu basi watakuwa wametusaliti kwa kiwango cha juu sana.
Hapo tunakuomba utusaidie ili na sisi kazi yetu iwe rahisi kuwatia adabu kwa usaliti wao. Baada ya kupata hizo sahihi tutakuomba utupe orodha ya wale walioweza kukupatia sahihi zao ili tuwajue wasaliti ni akina nani.
Unajua kwa jinsi wabunge walivyokuwa wakiongea kwa uchungu kiasi kile nitashangaa sana kama watashindwa kutumia nafasi hii kuiwajibisha serikali yao.
Haiwezekani kabisa eti uchangie kwa kupinga uozo wa serikali yako halafu unashindwa kuiwajibisha. Hapa Mh Zitto tunakuomba utuwekee orodha ya wote watakao saini.
Kushindwa kutupa hiyo orodha ni kutusaliti sisi wananchi wa Tanzania. Kwa kitendo hicho na wewe pia tutakuchukulia pia ni msaliti na mfitini wa taifa letu. Mimi naamini huwezi kutusaliti sisis watanzania wenzako.

Mungu akubariki na akulinde na wale wote wanaotaka kukufanyia ubaya!
Hamna kitu hapo,mimi nimekushtukia wewe.hii ni mbinu ya magamba ili kuwatisha wabunge wa ccm wenye nia ya kutia sahihi ili waogope na kubadili uamuzi kwa kuhofia kutambulika na kuchukuliwa hatua kichama.,
Najua kwamba anapotia sahihi tayari hakuna kificho ila hii ni kama kitisho ili waweze kubadili maamuzi au kusita na watakapoamua basi iwe ni too late.
 
Ndiyo mkuu PETITION Inakubalika ni just sahihi za idada fulani kubwa ya wananchi zinazopelekwa kule kuonesha wameunga mkono hoja fulani.
Basi kama petition inakubalika kisheria, Mh. Zitto hana budi kurudi kwa umma kama hili zoezi la kwanza likifeli.
 
Mkuu Kiroba, nakubaliana na wewe kwamba Mh. Zitto atupatie list ya wabunge waliotia sahihi ili itusaidie kuwa-evaluate wabunge wetu. Wabunge wa magamba ni wanafiki sana, wanasema wasichokisimamia!

Nasisitiza, nahitaji kuona sahihi ya Mwigulu nchemba, mbunge wa iramba magharibi. ikikosekana inatosha kuwa mtaji wa kumuondoa jimboni.
 
Hamna kitu hapo,mimi nimekushtukia wewe.hii ni mbinu ya magamba ili kuwatisha wabunge wa ccm wenye nia ya kutia sahihi ili waogope na kubadili uamuzi kwa kuhofia kutambulika na kuchukuliwa hatua kichama.,
Najua kwamba anapotia sahihi tayari hakuna kificho ila hii ni kama kitisho ili waweze kubadili maamuzi au kusita na watakapoamua basi iwe ni too late.
Fikra potofu hizo. Lakini ndio uhuru wa kutoa maoni. Kwangu mimi naona kama huna hoja ya kuchangia hili suala nyeti na lenye manufaa kwa taifa letu.
 
Nashauri wananchi tuandamane Kama wabunge hawataweka saini tushinikize. Twende hadi Dodoma na sisi iwe km middle east. Wananchi tuungand.
Hapa umenena, lazima tufight kuikomboa nchi yetu, tukikaa kimya hili likapita nasi tutakuwa wasaliti wa taifa letu. So kila mtu awajibike kivyake kuikomboa nchi toka kwa hii serikali dokozi.
 
Mkuu Kiroba, nakubaliana na wewe kwamba Mh. Zitto atupatie list ya wabunge waliotia sahihi ili itusaidie kuwa-evaluate wabunge wetu. Wabunge wa magamba ni wanafiki sana, wanasema wasichokisimamia!
Ni kweli mkuu Mnyisanzu, hawa wabunge huwa wanatuona sisi hatuna akili kabisa. Kwa hili ndio tutaona hivi ni kweli wabunge walikuwa wakiongea kwa kumaanisha au ni hadaa tu za kisiasa? Hivi Olesendeka kwa hili amesimama upande gani?
 
Hata mimi ninamtazamo kama wako. Ilaikitokea wabunge kama Lowasa na Chenge wakasaini, tutawapa credity? Ila kwa hawa ambao hawana kashfa basi tutawapongeza na kuwa-support hata kama watabaki CCM. Wengine wasitimize hasira zao kwa wakuu wao huku wakitegemea msamaha wetu. Ila nijuavyo mimi, ni vigumu sana kuipinga CCM ukiwa ndani. Nakushauri Mh. Filikunjombe uchomoke kwenye gamba humo uje huku kusafi tulitetee Taifa.
 
Back
Top Bottom