Zitto Vs Spika

Pundit,
Maneno yako kweli na yanaleta maana zaidi hasa tukizingatia kuwa Zitto anachukua hatua nyingine kukosha jina lake for the record. Mimi kidogo nashikwa na utata napolitazama swala hili kuwa amekubali kutumikia kifungo cha kijeshi kwa kutii Bunge ambalo leo anataka kuliondoa credibility yake.. Again for the record sawa kabisa but he should have done that wakati akitembelea mikoa kuwataarifu wananchi kilichotokea, hivyo sakata la Buzwagi lisingewapa usingizi hata kidogo.
Na ndio maana baada ya Karamagi kuona Zitto kanywea nje ya Bunge Kisheria alikuwa na ubavu hata wa kusimama mbele ya waandishi wetu na kutoa baadhi ya taarifa zenye utata zaidi lakini tulishindwa ku question kwani maamuzi ya Bunge yalionekana halali KISHERIA hali kulikuwepo na hitilafu. Kutembelea mikoa na kadhalika ilikuwa kazi nje ya sheria na tuliweza kuipongeza sana tu na hata wananchi waliingia mitaani kulaani kitendo cha Bunge, yet tulishindwa kuendeleza vagi lile kisheria.
Binafsi sidhani kama ni jambo zuri kukiri mahakamani kama wewe ni guilty hali ukijua wazi kuwa huna hatia kisha baada ya kutumikia kifungo ndio unasimama na kuweka madai yako kisheria. Aluta Continua huwa haisimami hata kidogo, tunapowapa pumzi CCM na kujikusanya upya inakuwa inaondoa munkar wa harakati zetu ktk kutafuta demokrasia ya kweli.
 
Ni wangapi kati yenu wanajua kucheza Chess?

Zitto, bravo on your move, hapa unamsarandia King kwenye Chess Board, umepiga Check, ni aidha mfalme aaunguke au ule malkia bure!

La msingi ni kufuata kanuni za bunge kwa kutumia demokrasia na si nguvu ya chama. ukiangalia kipengele cha sita cha barua ya Zitto, inatamka wazi kusitishwa kwa Bunge kuacha shughuli na taratibu zake na kugeuka kuwa kamati za vyama.

Nakumbuka mbinu hii imetumika sana na CCM hata wakati ule wa chama kimoja. Mbunge akiondoa shilingi, kamati kuu hukusanyika na mbunge huyo kufinywa makende na kupewa vitisho vya kichama (muulizeni Mzindakaya wa asili)!

This is great move kwa wapenda dmokrasia. Alichofanya Zitto ni kucheza mchezo mchafu kama wao CCM. Katumikia kifungo (alikuwa na uwezo wa kupinga hukumu mapema), ukweli wa hoja yake umekuwa wa wazi na kuleta tafurani (udhaifu wa CCM kulijua hili) maana mkataba tumeuona, Raisi kaunda kamati kuchunguza kiini cha hoja ya Zitto na mwisho, Zitto ana support ya Wananchi.

Kitakacho kuwa kigumu kwa CCM (Bunge) ni kukataa kupitia hii barua yake! Kama kawaida na kama Mzee ES alivyotuambia, tayari wameshaanza(CCM na Sitta) kuropoka hovyo. This is political suicide for Sitta and those who will oppose this motion.

Hii ni Uchiteme, Uchimumunye, Usimeze! Whatever the outcome, tayari Zitto kaonyesha mapungufu ya Bunge kufuata kwa makini kanuni zake. Na zaidi, hili analoliomba ni kinga ya baadaye kwake na wabunge wengine ambao watatoa hoja na kudhalilishwa kichama (including CCM members).

Zitto kafanya la busara kufuata mkondo, kaanzia kwa bosi wake Spika, kama Spika na Waziri Mkuu watalitupilia mbali hili shauri(kumbuka ote ni watuhumiwa wa kutumia vibaya madaraka na kanuni za Bunge), hatua ya pili ni Mahakamani kwa Ramadhani na Mahakama ya panya Jangwani na Mwembe Yanga.

Bunge wamepigwa bao, wakikataa hii hoja, wanajiunguza, wakiikubali wanajiunguza!

Kunkoma Nyani Giladi!
 
I like the chess analogy, but nadhani upande mwingine ni kama 'poker' sasa sijui kama Spika ana kadi ambazo hatuzijui bado...
 
Rev,

If it comes to Ramadhani vs Sitta si itakuwa political stalemate kama siyo constitutional crisis?

Hivi yule Judge Ramadhani ana integrity gani ya kuwa impartial katika swala divisive kama hili? je Mahakama Kuu kama chombo cha kutafsiri sheria iliyotungwa na bunge linaweza kulifunga bunge kwa kutumia kanuni za bunge? Mi nilifikiri kanuni za bunge ni arena ya Spika.
 
I like the chess analogy, but nadhani upande mwingine ni kama 'poker' sasa sijui kama Spika ana kadi ambazo hatuzijui bado...

au kwa mfano mwingine
kwa mabingwa wa drafti, anakupa kete unakula tu unaona raha, baadae bingwa akiweka mambo sawa anakutwanga force king halafu anakomba kete zako zilizosalia moja baada ya nyingine. hii ndiyo move ya mh Zuberi Zitto. walipomfungia waliona raha kumbe hawajui watu wantaka kuingia king kw mtindo wa tutusa!
 
I like the chess analogy, but nadhani upande mwingine ni kama 'poker' sasa sijui kama Spika ana kadi ambazo hatuzijui bado...

Yes, he has the cardsand he may call a bluff! Katamka rasmi yey ndio kwanza kayasikia haya kwenye vyombo vya habari na hajapata barua (does it sound like Balali's case?) Je ni kanuni gani Zitto kavunja kwa kuvujisha Barua yke kwa Spika kwenye vyombo vya habari kabla ya Spika kuipata?

Hii kama ni ishu, basi ni mkorogano wa kufahamu vizuri protokali na mambo ya kisasa. Kwa siye wakaaji Unyamwezini na kwa Malkia, si jambo la ajabu barua kuwa ni public kabla ya mlengwa kuamua atafanya nini.

Lakini kwa kuwa sisi bado mambo ni kama PP(People'a Party of China) ni ki-CCM (vikao va kamati za Chama kujadili malalamiko) it is very possible for Sitta kung'aka namna hiyo (rejea malalamishi ya Butiku)!

CCM inapenda sana usiri katika mambo ambayo ni bayana nani wazi, no wonder hata miktaba ni siri kuu badala ya kuwa ni haki kwa wananchi kuipitia na kujua tumetumbukizwa shimoni kwa kiasi gani!

What works for Sitta (CCM) may not always be the right way and work for everybody!
 
Rev,

If it comes to Ramadhani vs Sitta si itakuwa political stalemate kama siyo constitutional crisis?

Hivi yule Judge Ramadhani ana integrity gani ya kuwa impartial katika swala divisive kama hili? je Mahakama Kuu kama chombo cha kutafsiri sheria iliyotungwa na bunge linaweza kulifunga bunge kwa kutumia kanuni za bunge? Mi nilifikiri kanuni za bunge ni arena ya Spika.

Honestly sijui ni vipi suala hili litatatulika. Mfano ni Ushindi wa Mtikila kuhusu hoja ya Wagombea Huru. Je Mahakama kusema Wagombea huru ni Halali sasa ni Sheria au ni mpaka Waziri wa Sheria na Mwanasheia Mkuu wawakilishe Serikalini halafu Bungeni ili mswaada wa kubadilisha sheria za uchaguzi zifanyike?

Our systems are a bit complex (purposely) hivyo hata ushind wa Mtikila waonekana ni Batili kwa maana naamini maamuzi ya Mahakama kwa Tanzania katika kipengele cha Sheria au Katiba si Sheria!

Nilichosema ni kuwa ikiwa Bunge (Spika) litakataa kufuatilia hii hoja, ndipo Zitto anaweza kwenda mahakamani kutaka usuluhishi.

Kuna mtu kadai eti aandike barua kwa JK, JK hana mamlaka juu ya Bunge kiutendaji zaidi ya kulivunja!
 
Rev. Kishoka,
Kuna mtu kadai eti aandike barua kwa JK, JK hana mamlaka juu ya Bunge kiutendaji zaidi ya kulivunja!

Sawa mkuu lakini hawezi kulivunja hivi hivi tu bila kuwepo sababu, sasa hiyo sababu ataweza kuipata vipi ikiwa yeye hana mamlaka ya ku question utendaji kazi wa bunge hilo.
Binafsi nadhani swala la Zitto sasa hivi linatokana na kutodhirika kwake na utendaji kazi wa Bunge...who would you call?..Gost buster! - na sio ghost mwenyewe.
At the same time ni kauli ya rais kuhusu kusimamishwa kwa mikataba ndiyo iliyokuwa ushahidi bungeni, unless kama sababu kubwa ya barua hii ya Zitto ni kuweka record sawa.... nadhani kuna utata hapa.
Huu ni mtazamo wangu ktk swala hili.
 
Way to go Zitto.

Kwa mtaji huu nina uhakika kabisa kwamba ifikapo mwisho wa 2010 majimbo mengi likiwemo la Mzee Sita yatakuwa wazi.
Vijana noeni vichwa vyenu mkae tayari kujimwaga kwenye kinyang'nyiro cha Ubunge.

Uzuri wa hoja hii ni kwamba Wazee wazima wanalazimika kuijadiri na kujikanyakaga wapende wasipende, hapo hamna kukaa kimya.
Kwa desturi yao wakianza kuongea siku zote ni lazima wapishane maneno kama Piston kwenye injini, moja ikipanda nyingine inashuka.

Safi sana,safi saaaana!
 
Hakuna cha kushangaa hapa. Zitto ana haki ya kuomba jina lake kusafishwa kwa sababu aliitwa mwongo ndani ya Bunge la Tanzania. Pamoja na kuwa hakupewa nafasi ya kujitetea, Bunge lilifikia uamuzi wa kumpa adhabu ya kutohudhuria Bunge kwa kusema uwongo.

Yale aliyosema kuhusiana na mkataba wa Buzwagi yalikuja kubainika kwamba yalikuwa ni kweli tupu, nyie mliomuita mwongo ndio mliokosea. Zitto ana haki ya kuombwa samahani na wote waliomkosea. Usijifanye kushangaa shangaa kama huelewi nini kilichotokea.


Spika amshangaa Zitto

Hii article sikuiweka yote hapa, mniwie radhi.

na Tamali Vullu
Tanzania Daima

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta, ameeleza kushangazwa kwake na kitendo cha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kumuandikia barua akimtaka aiagize Kamati ya Kanuni ya Bunge kupitia upya adhabu aliyopewa.
Zitto alisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge Agosti 14, mwaka huu, kwa madai ya kusema uongo wakati akiwasilisha hoja binafsi akitaka Bunge liunde kamati kuchunguza, pamoja na mambo mengine, kusainiwa kwa mkataba wa mradi wa mgodi wa Buzwagi nje ya nchi.

Mkataba huo ulisainiwa na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi mapema mwaka huu katika hoteli moja jijini London, Uingereza.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Sitta, alisema ingawa bado hajapata barua hiyo, lakini amezisoma habari kuhusu hatua ya Zitto katika vyombo vya habari.

Alisema kuwa baada ya kusoma, hakutegemea barua ya aina hiyo inaweza kuandikwa na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Bado sijapata barua, ndiyo kwanza narejea kutoka India, lakini sikutegemea mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuandika barua ya aina hiyo, ingawa kila mtu ana uhuru wa kuzungumza.

"Barua hiyo nimeisikia kwenye vyombo ya habari, ina maneno ya ajabu, nasubiri nipate barua hiyo ndiyo nitajua la kufanya," alisema Spika.
 
Asanteni, barua nimeiona. Ndugu Zitto hongera sana, hapo umewashika patamu, na USIACHIE. Hata kama wataamua kukukatia kipande cha shati ubaki nacho, tunza, itakuwa kumbukumbu yako na yetu kwa vizazi vijavyo kwamba kuna mtu aliwahi kupambana na mafisadi hadi hatua hii, nayo itawatia moyo wengine kupambana na mafisadi. Huo mfano wa kipande cha shati ni hivi: Unakamata mwizi nyumbani kwako, unamshika shati wakati unaendelea kupiga yowe la kuomba msaada. Mwizi anakuzidi nguvu, anakimbia nawe unabaki na kipande cha shati lake ulilokuwa umemshikilia. Si haba, ni hatua, kitatumika baadae kumtambua na kumtia hatiani.

Usijali hata kama mwishowe watatumia dhuluma hiyohiyo na abuse of majority kutamka kuwa adhabu ilikuwa halali wakati haikuwa hivyo. Hata wayahudi walitumia abuse of majority katika mashtaka yao dhidi ya Yesu, wakamsulubu, lakini matokeo yake akawa maarufu kuliko wakati wa mashtaka. Hata Kanisa Katoliki walitumia abuse of majority's belief kumhukumu Galileo Galilei (1664-1642) alipoandika kanuni isemayo dunia huzunguka jua, wakamuadhibu kuwa amesema uongo, kwani ati wao walijua jua ndilo huzunguka dunia! Baadae waliaibika sana, na kuomba radhi (though very late by Pope John Paul II), lakini mchango wake huu umechangia maendeleo makubwa katika sayansi ya anga za juu (astronomy). Na mifano mingine lukuki ipo. Jambo la kutia moyo kuhusu hili suala lako ni kwamba halitachukua karne na karne kama mifano niliyotaja. Uko kwenye nafasi nzuri tayari, na inaelekea umepanga vizuri karata zako.

Ushauri ni kwamba panga vizuri na timu yako pia, ili itakapofikia wakati watu wameamua dhahiri wanataka timu mbadala, muweze kuwepo kupokea nafasi na changamoto hiyo. Maana kinachoweza kutengenezwa hapo kikawa kibaya kwa demokrasia ni kujenga hisia kwamba upinzani ni "brain group" fulani ndogo tu ambayo mtu akiiondoa (kwa njia zozote, including kuwanunua), basi upinzani umekwisha! Jengeni mazingira ya kujenga upinzani wa kimfumo na kitaasisi, badala ya upinzani unaotegemea bidii za mtu mmoja au watu wachache (wajua "one-man show" ni rahisi sana kuisambaratisha, kama ndondi ukiumia kwenye mechi ndo kwa heri, wanasema ni TKO mechi imeisha, lakini kwenye mpira wa miguu mchezaji mmoja akiumia kocha anambadilisha mechi inaendelea!) Tunahitaji mapambano ya mfumo dhidi ya mfumo, taasisi dhidi ya taasisi (na si individual dhidi ya mfumo "Zitto vs CCM" itakuwa kama "me against the world" ambayo ni rahisi kushindwa), timu dhidi ya timu. Kumbe licha ya bidii zako zote ambazo nazipongeza sana, nakushauri pia mjenge timu, muwe na kina Zitto wengi, hata wakim-kabwe mmoja wengine wanaendelea na mapambano. Hapo kitaeleweka.
 
Yaapu Masatu.
Tu pamoja.Hatuwezi kila wakati tukawa tunasikiliza Bunge likijadili masuala ya Kabwe na huku vikao vingi vyenye kugharimu fedha vikifanyika.
Aende mahakamani ambako mahakimu wanalipwa kwa kazi hiyo.Kama nilivyotangulia kusema hapo juu mbona hoja yenyewe imechelewa kwani mmwisho wa adhabu umefika.
Au kuna nini ktk hili.Tuangalie sana tusije kuwa twamsupport mtu kumbe anamaslahi yake zaidi na si kwa Taifa kama tufikiriavyo.Fuatilieni historia ya huyu Kabwe baada ya kuupata Ukatibu wa DARUSO pale Mlimani ni nini alifanya.Tofauti kabisa na kipenzi cha watu Gelvas Mkilli ambaye mimi namuita mwanamapinduzi wa kweli asiyetaka Ummaarufu.Aliweza kuwashawishi ata Walimu wa St Mary kugoma kwa kuwa walikuwa wananyonywa lakini hatulijui hili na yuko kimya.
Aache umaarufu na afanye kazi.Adai haki ni kile tulichomtuma sisis kama wananchi kama alivyofanya kwa Bwana Karamagi na ubovu wa suala la madini.
Umaslahi ukizidi ndipo chama kitapoteza legitimacy kwa watu.
 
Yaapu Masatu.
Tu pamoja.Hatuwezi kila wakati tukawa tunasikiliza Bunge likijadili masuala ya Kabwe na huku vikao vingi vyenye kugharimu fedha vikifanyika.
Aende mahakamani ambako mahakimu wanalipwa kwa kazi hiyo.Kama nilivyotangulia kusema hapo juu mbona hoja yenyewe imechelewa kwani mmwisho wa adhabu umefika.
Au kuna nini ktk hili.Tuangalie sana tusije kuwa twamsupport mtu kumbe anamaslahi yake zaidi na si kwa Taifa kama tufikiriavyo.Fuatilieni historia ya huyu Kabwe baada ya kuupata Ukatibu wa DARUSO pale Mlimani ni nini alifanya.Tofauti kabisa na kipenzi cha watu Gelvas Mkilli ambaye mimi namuita mwanamapinduzi wa kweli asiyetaka Ummaarufu.Aliweza kuwashawishi ata Walimu wa St Mary kugoma kwa kuwa walikuwa wananyonywa lakini hatulijui hili na yuko kimya.
Aache umaarufu na afanye kazi.Adai haki ni kile tulichomtuma sisis kama wananchi kama alivyofanya kwa Bwana Karamagi na ubovu wa suala la madini.
Umaslahi ukizidi ndipo chama kitapoteza legitimacy kwa watu.

Mkuu HAM vipi???

We huoni kwamba kupitia issue yake hii itasaidia kuweka misingi ya demokrasia bungeni ambayo wote tuna ililia?? ambayo kukosekana kwake ndo kumetufikisha hapa tulipo??

Hili ndo tatizo letu walio wengi na ndo maana tumeburuzwa na mafisadi muda wote huu, hii tabia ya kuona hilo limepita tuliache tuangalie ya mbele, hii tabia ya tumuache huyu ni mwenzetu muache apumzike, hii tabia ya kuona kila anaye simama kutetea misingi ya haki na kweli kumtazama kwa jicho la kibinafsi na kuona kwamba anatafuta maslahi binafsi badala ya kumsupport ili kubadili mfumo mzima ulio oza,

Hebu jiulize, Hivi kweli alivo simamishwa bungeni, umma usingekuwa nyuma yake na kushiriki kumpokea na kuwazomea hili joto la mageuzi tunalo liona lingekuwepo?? Hata hii kamati ya mazingaombwe aliyo iunda JK ingekuwepo?? japo najua haitakuwa na maana sana. lakini nafurahi kwamba kwa kumshirikisha, atapata uelewa mkubwa zaidi wa madudu yaliyo jificha kwenye mikataba mibovu, na kama alivyo kwisha sema, makombora mengi zaidi yatakuwa yamepatikana kumalizia kazi.

Ebu watanzania tujifunze kuwaunga mkono mashujaa wachache wanao jitolea kutetea maslahi ya wengi badala ya kuwabeza na kuwatazama kwa jicho la kwamba hawawezi ama kwamba wanatafuta sifa!
 
Spika kitanzini

na Charles Mullinda
Tanzania Daima

NGUVU za Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sasa zinaelekea kuporomoka baada ya kambi yake kuu kuanza kumgeuka.
Sitta, ambaye mara kadhaa tangu aliposhika wadhifa wa Uspika amekuwa akijikuta katika migongano ya hapa na pale na wabunge na wananchi, amekuwa akiitegemea zaidi kambi ya wabunge vijana kumkingia kifua, wakiwemo wale wa kambi ya upinzani.

Kambi hiyo ya wabunge vijana, sasa imemgeuka Spika baada ya matukio ya hivi karibuni kuhusu uamuazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, ‘kukata rufaa’ akilitaka Bunge lipitie upya adhabu ya kusimamishwa aliyopewa mwezi Agosti.

Baada ya kupokea barua ya mbunge huyo kuhusu suala hilo, Spika alikaririwa akimbeza Zitto na kusema kuwa anamuonea huruma kutokana na kuonyesha kwake (Zitto) kutokomaa kisiasa.

Zitto ni mmoja wa wabunge mahiri katika kambi ya wabunge vijana, ambao mara kadhaa wamelitikisa Bunge kutokana na hoja zao na pia, ingawa ni mbunge wa upinzani, amekuwa moja ya nguzo muhimu za Spika hasa kwa mahasimu wake wa kisiasa wa ndani ya chama chake.

Habari zilizolifikia Tanzania Daima Jumapili, zilieleza kuwa Zitto, amemuweka Spika Sitta katika wakati mgumu baada ya kuendelea na msimamo wake wa kutaka adhabu yake ipitiwe, licha ya kauli ya Sitta.

Ingawa jana katika mahojiano yake na gazeti hili alisema hataki kulumbana na Spika Sitta katika suala hilo kwa sababu anamuheshimu sana, Zitto aliendelea kusisitiza kwamba anachotaka ni haki itendeke kwa sababu anaamini adhabu iliyotolewa na Bunge dhidi yake haikuwa sahihi.

“Ninamuheshimu sana Spika, sipendi kabisa kubishana naye, ninachokiomba ni haki itendeke kwa sababu ninaamini sikutendewa haki kwa kupewa adhabu ile, sijaridhika. Lakini kamati ikiketi na kupitia adhabu hiyo nitaridhika na maamuzi yake,” alisema Zitto.

Aidha, akizungumzia madai kwamba alisambaza barua yake hiyo kwa vyombo vya habari na katika mtandao wa ‘internet’, jambo ambalo Spika amekaririwa akieleza kuwa ni kinyume cha taratibu za Bunge, Zitto alisema hilo si kweli kwa sababu alitoa nakala kwa kiongozi wa upinzani bungeni na kwa katibu wa Bunge tu.

Huku akiongea kwa kuchagua maneno, Zitto alisema kamwe hana nia ya kutumia nafasi hiyo kutafuta umaarufu. “Sikutumia nafasi kujitafutia umaarufu kama inavyoelezwa, ningetaka hivyo ningezungumzia jukwaani, kwa sababu wakati naadhibiwa watu wengi walikuwa hawampendi Spika, hapo ndipo ningemchafua.

“Ninasema kweli, ningetaka umaarufu ningekwenda mahakamani, nina orodha ndefu ya wanasheria wazuri wanaotaka suala hili nilipeleke mahakamani na wao watalisimamia ili haki ipatikane, lakini mimi nasema hapana, na tangu nilipoadhibiwa nilikuwa kimya, nimetumikia kifungo kimya, hiyo yote ni kwa sababu ya kumuheshimu tu Spika, ni unyenyekevu wa hali juu,” alisema Zitto.

Inadaiwa kuwa msimamo huu wa Zitto na kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na Spika dhidi ya barua iliyoandikiwa na mbunge huyo, unaashiria kuwa Spika ana wasiwasi kuwa iwapo Kamati ya Kanuni za Bunge itaipitia upya adhabu hiyo, Bunge linaweza kujikuta matatani kwa kukiuka kanuni au desturi zake.

Wataalamu wa wafuatiliaji wa masuala ya Bunge waliozungumza na gazeti hili walieleza kuwa, Bunge linaendeshwa kwa kanuni na desturi ambazo huliongoza kufikia maamuzi yake, lakini katika kesi ya Zitto, vyote hivyo havikufuatwa.

Ukweli huu unathibitishwa na adhabu kadhaa zilizokwishatolewa na Bunge kwa wabunge ikiwemo aliyopewa aliyewahi kuwa Mbunge wa Temeke, Augustino Mrema baada ya kutamka bungeni kuwa serikali imepanga kumuua yeye (Mrema) na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharrif Hamad.

Mrema aliliambia Bunge kuwa habari hizo alipewa na aliyewahi kuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa Imran Kombe. Bunge lilimpa Mrema siku tano za kuthibitisha maelezo yake, lakini alishindwa kufanya hivyo na kujikuta akiadhibiwa kusimama kufanya shughuli za Bunge kwa muda wa siku 40.

Baadhi ya wabunge walioadhibiwa kwa utaratibu wa kupewa siku za kuthibitisha kauli zao ni pamoja na Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa aliyetiwa hatiani kwa kuchezea taarifa za Bunge kuhusu sakata la fedha za matibabu zilizotumiwa na Hassy Kitine.

Mwingine ni Philemon Ndesamburo ambaye aliadhibiwa na Bunge baada ya kushindwa kuthibitisha kauli yake kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, aliwaambia wafanyabiashara wakitaka mambo yao yawanyookee, wajiunge na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kwa kuzingatia mlolongo huu wa matukio ya adhabu zilizokwishawahi kutolewa bungeni, kambi ya wabunge vijana imepanga kumshinikiza Spika kuiamuru Kamati ya Kanuni za Bunge kuipitia upya adhabu hiyo na kwamba matokeo yake yatachambuliwa ili kuona kama kamati hiyo inafanya kazi kwa kufuata haki.

Mmoja wa wabunge vijana kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee, alilieleza gazeti hili kuwa kambi ya wabunge vijana haikubaliani na msimamo wa Spika na inataka adhabu ya Zitto ipitiwe mpya kwa sababu hata Rais Jakaya Kikwete ameonyesha kwa vitendo kutokubaliana na adhabu hiyo.

“Adhabu aliyopewa Zitto ilitokana na hoja yake ya kutaka mkataba wa Buzwagi uchunguzwe, wabunge wa CCM waliungana kumpinga kwa sababu wanazozijua na ambazo sasa Watanzania wengi wanazijua, wakamsimamisha.

“Lakini ninaamini walimsimamisha kwa sababu za kiitikadi, ingawa mimi sikuwepo, hawa wamemsimamisha, rais kaunda kamati ya kupitia upya mikataba ya migodi ya madini ukiwemo huo wa Buzwagi, haijalishi hata kama kaunda kisiasa au kwa dhamira ya dhati, kinachoonekana hapo ni kwamba rais amekubaliana na hoja ya Zitto.

“Na kama rais amekubaliana na hoja ya Zitto, maana yake ni kwamba adhabu aliyopewa na Bunge haikuwa sahihi, sasa Bunge linapaswa lijitizame upya, vinginevyo kulishitaki ni sawa tu.

“Kwa Spika, kumuita mbunge mtoto ni jambo la ajabu sana kwa mtu tunayemuheshimu kama yeye, utoto wa mtu haupimwi kwa umri bali hoja zake, wanaomsikiliza Zitto akitoa hoja wanajua kama ni mtoto au la… katika hili atauona utoto wetu,” alisema Halima kwa kujiamini.

Pamoja na hayo yoye, kivuli cha Rais Kikwete nacho, ambacho kimekuwa kikiyaandama maamuzi ya Spika, kinaonyesha kumuweka katika hali ngumu zaidi kwa vile kimekuwa kikipingana naye kila mara.

Kwa uchache, Rais Kikwete alionekana kutofautiana na Spika pamoja na wabunge mapema mwaka jana, pale walipokosoa madai yao ya nyongeza ya mishahara na marupurupu wakati taifa likiwa katika hali ngumu ya chakula na ukosefu wa umeme.

Kikwete pia ameonekana kutofautiana na Spika na wabunge wa CCM baada ya kuunda kamati ya kupitia upya mikataba ya madini, jambo ambalo lilikuwa likidaiwa na Zitto kabla ya kusimamishwa na wabunge wa CCM.

Wafuatiliaji wa masuala ya Bunge wanaeleza kuwa iwapo Spika Sitta hatatumia busara zaidi katika kutatua mgogoro huu na kambi ya wabunge vijana, na hivyo kusababisha kufarakana nao, atakuwa amebakia peke yake jambo ambalo ni hatari zaidi kwa siasa za hapa nyumbani.

Wengi wamemtaka akumbuke kazi kubwa iliyofanywa na wabunge hao, wakati wa sakata lake na Mbunge Malima, ambapo baadhi ya vigogo ndani ya chama chake waliamua kumshughulikia huku wakiwa na dhamira ya dhati ya kumuengua katika Uspika.

Sitta aliokolewa na kambi ya wabunge vijana, baada ya Mdee kuwasilisha hoja bungeni, akilitaka Bunge kumuadhibu Malima kwa kumdhalilisha mbunge na kiti cha Uspika, hoja ambayo iliua nguvu za wapinzani wa Spika na kumpa mwanya wa kukwepa mashambulizi yaliyokuwa yakielekezwa kwake.




 
Zitto alituwekea barua yake hapa ukumbini. Kwenye barua hiyo sikuona chochote kilichoonyesha Zitto katumia lugha ya ubabe au ufedhuli. Huyu Mzee naona sasa anaanza kuchanganyikiwa kwa kupotosha ukweli wa mambo.

Sitta sasa ‘amshtaki' Zitto
Maulid Ahmed
HabariLeo; Sunday,December 30, 2007 @20:02

BAADA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kulitaka Bunge kupitia upya adhabu ya kumsimamisha, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, amelikataa ombi hilo kwa mujibu wa kanuni, lakini ameahidi kuifikisha barua hiyo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Amesema maneno yaliyotumiwa na mbunge huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika barua hiyo, yamejaa ufedhuli na ubabe dhidi ya Bunge kama Taasisi na dhidi ya viongozi wa Bunge na Spika.

Desemba 24, mwaka huu, Zitto alimwandikia barua Spika, akitaka kuipitia upya adhabu ya kumsimamisha kutokana na kwamba imesababisha adhalilike na kushushiwa hadhi ndani na nje ya nchi. Sambamba na hilo, anataka spika na mawaziri wengine kadhaa wachukuliwe hatua, kwa madai walinukuliwa na vyombo vya habari wakisema yeye ni mwongo bila madai hayo kuthibitishwa.

Katika taarifa ya majibu ya Spika iliyotolewa na Katibu wake, Daniel Eliufoo kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilisema barua ya Zitto itapelekwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kupata ushauri wake. Hata hivyo, hakusema lini ataipeleka barua hiyo zaidi ya kueleza ni utakapofika wakati mwafaka.

"Kwa kuzingatia, maneno yaliyojaa ufedhuli na ubabe dhidi ya Bunge kama Taasisi na dhidi ya Viongozi wa Bunge, Spika wa Bunge, kwa wakati mwafaka ataifikisha barua hiyo ya Mhe. Zitto kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kupata ushauri wake. "Aidha, ni muhimu kwa Bunge siku za usoni kuweka utaratibu na mipaka kuhusu haki ya Mbunge aliyemo Bungeni kulishambulia Bunge na viongozi wake nje ya Bunge," alisema Spika.

Spika alisema mbunge huyo kijana ana hiari ya kwenda mahakamani ikiwa anadhani hatua hiyo itamsaidia kupata haki yake aliyonyimwa na Bunge. Sitta, ambaye anatambulika kama Spika wa Viwango na Kasi, alisema barua ya Zitto ya rufaa si ya mbunge, bali ni waraka wa propaganda binafsi za kisiasa. "Hali hiyo inadhihirisha wazi pale ambapo msisitizo wa Zitto umekuwa siyo kuifikisha barua kwa spika ishughulikiwe kwa utaratibu wa kibunge unaoeleweka, bali ni kuisambaza dunia nzima ili kujipamba taswira ya yeye kuwa ni mpigania haki mashuhuri," alisema Sitta.

Taarifa ya majibu ya Spika, ilisema kuwa barua ya mbunge huyo imepotosha kwa makusudi dhana ya hoja ndani ya hoja katika mijadala bungeni. Alisema maamuzi dhidi ya Zitto yalifuata utaratibu wa kuhoji usahihi anayoyasema mbunge, hutolewa bila taarifa wakati wowote bungeni kwa mbunge kuthibitisha usahihi wa anayoyasema ama hufuta usemi au kuomba muda wa kupeleka uthibitisho.

"Kanuni 4(3) ya Kanuni za Bunge (2004) anayoinukuu Zitto katika barua yake inahusu rufaa dhidi ya maamuzi ya Spika, Naibu Spika au Mwenyekiti wakati uamuzi anaoulalamikia siyo wa Spika, bali ni wa Bunge. Maamuzi ya Bunge kupitia kura ni maamuzi ya taasisi nzima na hayawezi kuhesabika kuwa ya mbunge fulani au spika…

"Ikiwa Zitto anataka Bunge zima limuombe radhi au lijutie uamuzi wake na kuahidi kutorudia tena, itabidi apeleke hoja binafsi bungeni na siyo kumtaka Spika kuitisha kikao cha Kamati ya Kanuni kuipitia upya adhabu dhidi yake. Spika na Naibu Spika ambao huongoza Kamati ya Kanuni, wao pia kwa mtazamo wa Zitto ni watuhumiwa," alifafanua Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki.

Majibu hayo ya Spika, yametokana na barua aliyoandika Zitto ambaye alidai adhabu aliyopewa haikuwa halali kutokana na kutofuata Kanuni za Bunge na kutopewa nafasi ya kujitetea. Zitto alisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge Agosti 14, mwaka huu, kwa madai ya kusema uwongo dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi kuhusiana na mkataba wa madini wa mgodi wa Buzwagi uliosainiwa nje ya nchi. Adhabu hiyo imekwisha na anatarajiwa kuhudhuria vikao vya Bunge vinavyokuja.

Copyright @TSN 2006 All Rights Reserved
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom