Zitto Vs Mkulo, Nani Mwongo? IMF yaikalia kooni serikali

Zitto anajua anachokisema, na amesema wazi kuwa baadhi ya madai ya wah wabunge hayajalipwa. Akatolea mfano wa pesa ya mafuta ya magari yao kwa ajili ya safari majimboni nk. Hajasema kuwa wabunge wote hawajalipwa mishahara yao. Ndo maana kama Tasso alifuatilia kauli ya Katibu wa bunge Kashillila alipokuwa Iringa kwenye msiba alisema "kama kuna mbunge hajalipwa stahili yake yoyote apeleke /wapeleke majina ofsini kwake.

Hii ina maana Kashillila hana uhakika kama wabunge wote wamelipwa "Full pay" kulingana na madai au stahili zao. Halafu kumbuka Zitto ni waziri kivuli wa wizara ya fedha, usitegemee mtu makini kama Zitto aongee kitu bila kuwa na evedence, sote tunajua hili.

Subirini mwezi June muone Mkullo atakavyo kaangwa, amezoea ubabe kwa sababu ya kibri ya pesa. Na alishasema kwenye bajeti hii kwamba "Kila mtu atakula kwa jasho" hivyo na yeye ajitayarishe kula kwa jasho lake.

MH Zitto: Usilegeze uzi mkuu huyu Mkullo mpaka kieleweke, wapambe wao wanapenda sana kuwazomea mjengoni, safari hii zamu yake.
 
Unajuaje......pengine wamelipwa wachache(wa CCM hasa)
Unajuaje, pengine wamelipwa wote, wa upinzani kwa kuanzia, ili wasipige kelele.

...yaani Zitto alipwe halafu aseme hajalipwa yeye hajui gharama ya kaulki yake?
...yaani Zitto asilipwe halafu Waziri aseme kalipwa, Waziri hajui gharama ya kauli yake?

Waziri katoa tarehe ya siku Zitto alipopokea hela, Zitto hajabisha, Zitto kaongopa.
 
Zitto usibadili mada, ulisema Wabunge hawajalipwa.

Waziri kasema wamelipwa na tarehe katoa.

Sasa unakuja na michongo ya makusanyo ya kodi 15% imepungua blah blah blah

Zitto ulibwatuka uzushi, kwa watu makini credibility yako ina suffer!

Ndugu Taso, mada haikuwa mishahara ya wabunge. Mada ni hali mbaya ya fedha serikalini. Mishahara ya wafanyakazi kuchelewa ikiwemo Wabunge ilikuwa ni mfano tu.
Mkulo kaongopa na anajua kaongopa. Mimi mpaka tarehe 7 Mei sikuwa nimepata mshahara. Serukamba nilikuwa naye Kigoma kwenye vikao vya mkoa tarehe 6 Mei hakuwa amepata mshahara. Wabunge wengi hawakupata mshahara on time pia wafanyakazi wa serikali.
Hata hivyo huo ulikuwa ni mfano tu!

Mada ni hali mbaya ya fedha serikalini. Mada ni kushindwa kukusanya kodi. Kutolipa mishahara kwa wakati ni matokeo tu!

Tuendelee na mada. Mkulo hafai kuwa Waziri wa Fedha kwa uchumi kama huu wetu.
 
Cha kushangaza zaidi hadi lile deni la ndani Serikali nayo imekula yaani hapa sielewi kabisa
 
Zitto usibadili mada, ulisema Wabunge hawajalipwa.

Waziri kasema wamelipwa na tarehe katoa.

Sasa unakuja na michongo ya makusanyo ya kodi 15% imepungua blah blah blah

Zitto ulibwatuka uzushi, kwa watu makini credibility yako ina suffer!

Unajuaje, pengine wamelipwa wote, wa upinzani kwa kuanzia, ili wasipige kelele.

...yaani Zitto asilipwe halafu Waziri aseme kalipwa, Waziri hajui gharama ya kauli yake?

Waziri katoa tarehe ya siku Zitto alipopokea hela, Zitto hajabisha, Zitto kaongopa.

Mh. Zitto, maneno ya fedheha yanayotolewa authoritatively kama haya usiyatilie maanani. Yananenwa makusudi ili kukutelezesha.
 
Ndugu Taso, mada haikuwa mishahara ya wabunge. Mada ni hali mbaya ya fedha serikalini. Mishahara ya wafanyakazi kuchelewa ikiwemo Wabunge ilikuwa ni mfano tu.
Mkulo kaongopa na anajua kaongopa. Mimi mpaka tarehe 7 Mei sikuwa nimepata mshahara. Serukamba nilikuwa naye Kigoma kwenye vikao vya mkoa tarehe 6 Mei hakuwa amepata mshahara. Wabunge wengi hawakupata mshahara on time pia wafanyakazi wa serikali.
Hata hivyo huo ulikuwa ni mfano tu!

Mada ni hali mbaya ya fedha serikalini. Mada ni kushindwa kukusanya kodi. Kutolipa mishahara kwa wakati ni matokeo tu!

Tuendelee na mada. Mkulo hafai kuwa Waziri wa Fedha kwa uchumi kama huu wetu.
Kuwaasa viongozi wa ngazi za juu kama mawaziri kumepitwa na wakati, hauwezi kuwateua watu wa level hiyo halafu kila siku ni kupelekena kwenye semina elekezi zisizokuwa na msingi wa tija eti kuwakemea hawafanyi hili wala lile. Dunia ya sasa ni kumpa mtu targets na timeline halafu mnakutana kwenye taarifa ya utekelezaji. Halafu wananchi wanasikia umechukua hatua gani kwa wale ambao hawakufikia targets....politics baada ya uchaguzi haisaidii kitu chochote kwenye hii nchi
 
Nimesema kwa mfano dhahiri, mpaka tarehe 7 Mei sikuwa nimelipwa. Hata Mbunge wa CCM Serukamba hakuwa amelipwa na wajumbe wote wa kamati ya Bunge ninayoongoza hawakuwa wamelipwa. Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma hawakuwa wamelipwa. Ruzuku za vyama ambazo huwa zinalipwa tarehe 25 kila mwezi hazikuwa zimelipwa mpaka tarehe 5 Mei.

Hii ni mifano tu. Hoja ni kwamba Serikali imefilisika. Haina uwezo wa kukusanya mapato ya kutosha japo kulipia matumizi ya kawaida. Imekwenda kukopa benki. Tutamwajibisha Mkulo Bungeni.
 
Ingekuwa busara kwa mkulo kukili kuwa serikari ina hali mbaya kifedha kutokana na kutokuwa na ubunifu wa vyanzo mbadala vya fedha na mapato,

Tunajua kuyumba huku kwa mapato ya serikari ni kutokana na kuwa tegemezi wa wafadhili na nchi wahisani kwani mwaka jana walipunguza misaada kwa takribani USD300 BILLION na serikari ilibidi wakope kwenye commercial bank kuziba gap,na hiyo inaathiri sana uchumi wa nchi kwani small business na wananchi watashindwa kupata mikopo kwenye bank kwa urahisi kwa kuwa serikari imekomba pesa kibao kutoka kwenye bank za kibiashara.

Hata hivyo serikari ilitakiwa kufanya spend cut kwenye reccurent expenditure ilikuwa na budget yenye uwiano sawa nakubuni vyavyombadala vya mapato kutoka kwenye makampuni ya madini, na hivyo kutoa tax cut kwa bidhaa zinazoathiri wananchi wengi ili kukabiliana na mfumuko wa bei.

Mkulo amekiri kuwa serikari ilikopa kwenye commercial bank, hilo sio jambo la kawaida kiuchumi hivyo inakuwaje anashindwa kukiri kuwa serikari imefilisika mpaka kufikia hatuo ya kukomba pesa kwenye bank za ndani za biashara?

Zitto yupo sahihi kabisa na mkullo kadanganya umma na amekiri kuwa walikopa pesa kwenye bank za ndani na hiyo ni dalili mbaya ya kufilisika kwa serikari, hivyo inabidi awe mkweli moja kwa moja,mbona serikari ya ugiriki imefilisika wamekiri wazi wazi na kuomba msaada jumuia ya ulaya? kwa nini serikari yetu wanakuwa waongo waongo sana kiasi hicho?

Mkulo, mficha ugonjwa kifo kitamuumbua!
 
Nimesema kwa mfano dhahiri, mpaka tarehe 7 Mei sikuwa nimelipwa. Hata Mbunge wa CCM Serukamba hakuwa amelipwa na wajumbe wote wa kamati ya Bunge ninayoongoza hawakuwa wamelipwa. Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma hawakuwa wamelipwa. Ruzuku za vyama ambazo huwa zinalipwa tarehe 25 kila mwezi hazikuwa zimelipwa mpaka tarehe 5 Mei.

Hii ni mifano tu. Hoja ni kwamba Serikali imefilisika. Haina uwezo wa kukusanya mapato ya kutosha japo kulipia matumizi ya kawaida. Imekwenda kukopa benki. Tutamwajibisha Mkulo Bungeni.
Si ajabu Serikali itakuwa imekopa hadi hela kwa ajili ya mkutano wa semina elekezi kwa ajili ya mawaziri
 
tatizo Zitto alitoa kauli yake wakati mawaziri wa mr. kikwete wametoka kwenye semina elekezi walikoagizwa kujibu chochote ambacho kinasemwa kuhusu serekali badala ya kukaa kimya.

kwa hiyo bwana mkulo alikuwa anatekeleza agizo la mkuu wake. suala kama alichosema (mkulo) ni uwongo au ukweli, siyo ishu...ishu ni kujibu mapigo kama alivyoagizwa na mkuu wake.

mkuu unataka kusema kuwa inawezekana mkulu kashampigia mkullo kumpa pongezi kwa kuwa mtu wa kwanza kuwajibu mapigo wapinzani?! Teeh teeh teeh! Akili za kuambia si alisema wawe wanachanganya na zao?! Ona sasa mkullo kajibu utumbo!!
 
My Take:
  1. Yaliyosema na Zitto kuhusu ukata Serikalini ni kweli tupu.
  2. Kelele za CHADEMA kuhusu serikali kuongeza mapato, hasa kwenye madini na kuangalia vyanzo vingine ni kweli tupu.
  3. Kelele za wafanyakazi kuhusu wigo finyu wa mapato serikalini ni hakika na kweli tupu
  4. Mkulo ni mwongo na ni hatari kwa nchi hiii
Hii ni kali, kama kungekuwa vichwa kama hivi, mambo supa:israel:
 
IMF sounds alarm over Tanzania economy

The international Monetary Fund (IMF) is concerned about Tanzania's increasing borrowing for recurrent spending. Presenting a report titled Regional Economic Outlook:Sub-Saharan African yesterday in Dar es salaam, IMF senior resident representative John Wakeman-Linn urged the government to immediately review its fiscal policy to curb high debt levels taking into consideration the fact that food and fuel prices are rising and are likely to harm the economy.

The government budget for 2010/2011 was Sh11.1 trillion. Of the amount Sh6 trillion was to be raised from domestic revenue and the rest from domestic loans and external grants and credit. Meanwhile the IMF has lowered Tanzania's economy growth forecast by one per cent this year to six percent due to rising food and fuel prices. The IMF forecast growth in 2011 and 2012 to be 7.2 percent and 7.5 percent respectively

SOURCE: THE CITIZEN, THURSDAY 5TH MAY
 
Ni hKhatari kubwa Serikali kukopa kwenye mabenki ya ndani tena ya kibiashara kwa kulipana mishahara.

Huo ni mwanzo wa mwanguko wa uchumi na mwelekeo mbaya sana wa uchumi wa nchi.
 
Nimesema kwa mfano dhahiri, mpaka tarehe 7 Mei sikuwa nimelipwa. Hata Mbunge wa CCM Serukamba hakuwa amelipwa na wajumbe wote wa kamati ya Bunge ninayoongoza hawakuwa wamelipwa. Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma hawakuwa wamelipwa. Ruzuku za vyama ambazo huwa zinalipwa tarehe 25 kila mwezi hazikuwa zimelipwa mpaka tarehe 5 Mei.

Hii ni mifano tu. Hoja ni kwamba Serikali imefilisika. Haina uwezo wa kukusanya mapato ya kutosha japo kulipia matumizi ya kawaida. Imekwenda kukopa benki. Tutamwajibisha Mkulo Bungeni.

Shukrani kwako Mkuu nadhani kuna watu wanapenda kubisha na kukwepa mada !
 
Nimesema kwa mfano dhahiri, mpaka tarehe 7 Mei sikuwa nimelipwa. Hata Mbunge wa CCM Serukamba hakuwa amelipwa na wajumbe wote wa kamati ya Bunge ninayoongoza hawakuwa wamelipwa. Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma hawakuwa wamelipwa. Ruzuku za vyama ambazo huwa zinalipwa tarehe 25 kila mwezi hazikuwa zimelipwa mpaka tarehe 5 Mei.

Hii ni mifano tu. Hoja ni kwamba Serikali imefilisika. Haina uwezo wa kukusanya mapato ya kutosha japo kulipia matumizi ya kawaida. Imekwenda kukopa benki. Tutamwajibisha Mkulo Bungeni.

Mkuu Zitto, Thanx for your repply!
Hata mimi nimepata mshahara tarehe 7 tofauti na mazoea yangu ya kupata mshahara tarehe 25 kila mwezi. Harafu Mkulo anakataa katakata! Lol, he must resign the post.
 
Kwa mwendo huu je Tanzania tutafika kule tunata kufika?Nna wasiwasi sana na viongozi hawa wa ccm (wa magamba)kama wanafahamu kile wanachotakiwa kukifanya(wanawaza wizi tu)
 
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema atamthibitishia bungeni, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo kuwa Serikali imefilisika.Zitto alisema jana mjini Sumbawanga kuwa wataweka hadharani jinsi Serikali ilivyokopa fedha benki ili Waziri Mkulo aweze kuwajibika kutokana na kauli yake aliyoiita ya kukataa kusema ukweli.

Alisisitiza kwamba serikali haina fedha na kudokeza kuwa taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya mapitio ya uchumi ya mwezi Machi mwaka huu, inaonyesha kuwa imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15.

"Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali katika makusanyo ya kodi zote imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15 isipokuwa ushuru wa forodha. Hivyo haikufikia malengo ya ukusanyaji wa kodi," alisema Zitto.

Kwa mujibu wa Zitto, Machi, mwaka huu Serikali ilikopa fedha katika Benki ya Exim na benki zote za biashara nchini na ilikuwa ikihangaika ili iweze kuwalipa wafanyakazi.

"Mkulo atueleze ni serikali gani duniani inakopa kwenye benki za biashara kwa kuwa kitendo hicho ni hatari sana kwa nchi," alisema na kuongeza:"Bajeti ya mwaka uliopita ilikuwa ni Sh11 trilioni ambayo Serikali ilishindwa kufikia malengo ya Sh 1.6 trilioni kutokana na kushindwa kukusanya kodi kwa asilimia hiyo 15 isipokuwa ushuru wa forodha."
Alimtaka Mkulo kuacha kuwaona wanaosema kwamba serikali haina fedha si wazalendo kwa kuwa wawekezaji hawatakuja nchini, bali atambue kuwa kukosekana kwa fedha si suala la uzalendo.

"Serikali ni kweli haina fedha na hakuna suala la uzalendo katika hili. Tatizo la uwekezaji ambalo analizungumzia, linatokana na sera mbovu za CCM kwa kuwa tangu mwaka 2007, hakuna uwekezaji wowote wa maana uliofanyika hapa nchini," alisema Zitto.

Akiwahutubia wanachama wa Chadema na wananchi wa mji wa Vwawa, Mbozi, mkoani Mbeya hivi karibuni, Zitto alisema Serikali ina hali mbaya kifedha kwa sasa kiasi cha kukopa ili kulipa mishahara ya wafanyakazi.
Alidai kuwa hali hiyo mbaya kifedha kwa serikali imesababisha watumishi wake pamoja na wabunge kutolipwa mishahara hadi Mei 7, 2011.

Alisema Serikali sasa inatafuta fedha za kuwalipa watumishi wake mishahara ya mwezi Aprili.
"Hata sehemu ya posho za wabunge mkutano uliopita, zikiwemo za kugharimia mafuta ya safari za wabunge majimboni bado hazijalipwa kutokana na Serikali kukosa fedha," alidai Zitto.

Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali imekwenda kukopa Sh540 bilioni kutoka benki za ndani ili watu wasijue kuwa inakabiliwa na ukata."Serikali haikopi fedha ili ijenge bandari, viwanda au kugharimia miradi ya maendeleo, bali inakopa ili ilipe mishahara ya wafanyakazi," alisema Zitto.
source; mwananchi
Mkulo anaficha ficha nini wameunda liserikali kubwa la mawaziri na maofisa wasio na tija lukuki sasa wameshindwa hata kulipa mishahara. CCM hawana sera tena ni mufilisi, wamekwisha wasubiri kuporomoka tuu!!!!!!!!
 
Naungana na Ng'wanangwa, Mkulo alichofanya ni kukurupuka na kushambulia mtu na si hoja, alichopaswa kujibu hakukijibu akaanza kumsema mtoa hoja kitu ambacho ni upungufu wa akili.
Watu wanakopa kwa ajili ya vitu vya maendeleo, serikali inakusanya kodi na kuila muda huo huo yaani kama funza kula na kunya wkati huo huo. Semina elekezi ya dodoma ulikuwa ni mwendelezo mwingine wa kula pesa zetu:bange:
 
Kuwaasa viongozi wa ngazi za juu kama mawaziri kumepitwa na wakati, hauwezi kuwateua watu wa level hiyo halafu kila siku ni kupelekena kwenye semina elekezi zisizokuwa na msingi wa tija eti kuwakemea hawafanyi hili wala lile. Dunia ya sasa ni kumpa mtu targets na timeline halafu mnakutana kwenye taarifa ya utekelezaji. Halafu wananchi wanasikia umechukua hatua gani kwa wale ambao hawakufikia targets....politics baada ya uchaguzi haisaidii kitu chochote kwenye hii nchi
The Finest hizo semina elekezi ni njia ya kula fedha za umma vilevile, yote hayo ni kufilisi nchi yetu. Wewe uchague mawaziri incompetent na wafanya kazi wa ngazi za juu mafisadi type ya Mkulo unategemea nini, the whole managerial system ya hii serikali ni lotten. Bado tutaona mengi tuu!!!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom