Zitto umewadhalilisha Wabunge wa Viti Maalum CDM; Waombe Radhi

Mkuu,

I have great respect for Hon. Zitto lakini kwa hili kuita wanachama wapya wa CDM wa kuja sitamuunga mkono. Never. Nakubali sawa ya moto ni moto na sometimes inabidi utumie force lakini kuna repercussion zake. Mh Zitto, wewe, Gainjin na mimi tunaweza kuwa level moja hapa JF, lakini Mh Zitto ni public figure. As a public figure one would expect some form of behaviors hasa pale anapokuwa kwenye public domain.

Kweli kama binadamu wengine Mh Zitto ana mapungufu yake lakini does this excuse him kuita wanachama wapya wa Chadema wa kuja? Kama anamjua si angeenda kumwambia tuu in private? Unakumbuka yaliyomkuta Gordon Brown baada ya kumwita mwanachama mwanamke wa chama chke a "bigot"? Tena alisema hili in private lakini huenda ndio iliyomcost kwenye uchaguzi. I am sure kama tungekuwa na tabloid media hapa Bongo, front pages zingekuwa na headings "Zitto amwita mwanachama wa Chadema wa kuja".

Imagine kama kulikuwa na mtu analiyetaka kujiunga na Chadema because of being impressed na Mh Zitto bungeni apitie hapa, amkute huyo huyo Zitto anaita wanachama wapya wa kuja. Atajiunga na Chadema kweli? Inawezekana kabisa kuwa alichokuwa anaonyesha Zitto ni matabaka ya wanachama ndani ya Chadema wakati chama kinatambuka kama chama cha wanachama.

Juzi juzi tuu hapa watu walikuwa wanamuunga mkono Mh Mbowe kwa kutokwenda mahakani japokuwa alikuwa amefanya kosa. Leo hii Mh Zitto ana brand wanachama wapya wa kuja na tunataka kuumunga mkono on the ground kuwa ana mapungufu yake, nk. Mkuu hapana. Hata siku moja wrong plus wrong haiwezi kuwa right na haitakuwa.

Mkuu binasfi sidhani kama kuna mtu anaweza kuogopa kushindwa kujiunga ga CDM kwa kauli ya ziito kumuitwa mbunge wakuja. Kwangu threat kubwa kwa CDM sio makosa ya syntax ya mtu moja mmoja kuelezea kitu sahihi. bali threat ni tabia kama za huyu mleta mada. tena wengine ni wabunge. Tena wengine wanatumia screen name za kike. What if ni wanaume..... anyway niisiende huko nikajikuta nasema yale ya msekwa "tabia za kike" gaijin na wenzake wakanishambulia . teh teh teh

Ninaweza kupata hoja za msingi kwenye sentensi ya ziito japo z ina makosa ya lugha ya kukubalika lakini Hao wanaomlaumu hupati substance yeyote ya maana . ebu jaribu kungalia big picture ya CDM mkuu. Sometime mtu analeta mda inahusu zittto unajiuliza anajaribu kuachieve nini iwe ni kwa manufaa ya chama au nchi no maater lafudhi nzuri na sarufi atayotumia.

But kama CDM will be clean stable na hatutasikia mipshasho without ziito basi wamfukuze. kwenye footbal tunasema No single player is better than a team. tunachotaka watanzania ni mabadiliko.

Thanks i like politics but am not a politician
 
Kwa hiyo mtu akijiunga na CDM kwa mara ya kwanza ni sawa kumwita wa kuja? Unaona ni sawa kwa Naibu Katibu wa Chama Kukuu cha upinzani kuwaita wanachama wake wapya ni wa kuja? Ingekuwaje hapa kama Pius Msekwa amewaita wanachama wapya wa CCM wa kuja. I am sure hii thread ingekuwa na pages 30 by now. Nilidhani Chadema ni wanachama bila kubaguana. Kumbe chama kilikuwa kina recruit wanachama wa kuja huko mikoani. Kwa hiyo wanachama wa siku nyingi wanakuwa treated tofauti na wanachama wa kuja? Huku sio kubaguana na kujenga matabaka ya wanachama? Wanachama wa zamani na wale wa kuja? Kwa vile umesema Mh Zitto hajamung'unya maneno, ina mana aliyosema ni kweli sio. Siungi mkono kuwepo kwa wabunge sijui wa viti maalumu, lakini the way Mh Zitto alivyoiandika hili suala, well I will better keep my mouth shut.
Labda hujanisoma vizuri. Nimesema wa kuja halina ubishi kwani hata yeye Zitto anaweza kuitwa wakuja na wenyeji wake ktk mazungumzo yanayohusu ujio wake..Hiki ni kiswahili tunachokitumia siku zote na wala sii tusi unless wewe mwenyewe ndio unajihisi Ugeni ni tusi.

Swala ni mtu uliyechini yako na mgeni anaanza kutoa maneno ambayo kiaina yanakosa adabu na zaidi ya hapo mtu huyo hajui undani wakile anachokizungumza zaidi ya kushabikia. Mzee Pius Msekwa anaweza kabisa kuwaita wabunge wa CCM wa kuja kama hao wabunge watamkosea adabu na wataanza kumzungumzia yeye na sii kazi walokabidhiwa. Tena basi huyo mzee wetu pius Msekwa anaweza kutukana matusi ya nguoni acha hii habari ya kuitwa watu wa kuja. Kawaita upinzani wanafiki atashindwa kumwita mtu wa kuja?

Huyu mbunge alozungumza simjui ila Zitto anamfahamu vizuri na kuja kwake hapa JF akipinga matumizi ya lugha ya Zitto kwa kiongozi wake ktk FB hali yeye mwenyewe anarudia uozo ule ule hapa JF, inabidi apigwe kibao cha kerbu na ndio hayo majibu ya Zitto. Kifupi kule tulikotoka Zitto mwenyewe kakubali makosa ktk kusherehesha malalamiko yake, hata huyu mbunge wetu inabidi ajifunze kutumia lugha nzuri unapowakilisha hoja. Kama kuna malalamiko yoyote zipo njia mbadala za kufikisha malalamiko hayo na sii kuvuana nguo hapa JF kama vile Zitto ni baradhuli asiyejiweza..
 
  • Thanks
Reactions: EMT
CHADEMA is not a political party, it is rather a clique of lawbreakers organised by gangster leaders. Its ways and ideologies virtually resemble those of TALIBAN. The sole difference between the two is, while Taliban lives on drug trafficking and double dealing, CHADEMA's survival relies on VANDALISM.

Mwita,

I dont get your point,i mean what is the correlation?

Uko obsessed na chadema?nitaanza kuamini hivyo.....................
 
Acha wivu wewe,vaa sketi nawewe ili uzawadiwe Ubunge kama ubunge unazawadiwa.Wacha Vitimaalum viwepo ili nasisi tunaotaka kuingia tuupate.Abarkiwe aliyeleta wazo la vitimaalum.Mtapiga kelele habari ndio hiyo.Hilo ni takwa la SADC.Wivu tu..


Unaweza kutumbia. Assume uko bungeni leo hii unatoa speech kuchangia hotuba ya bajeti . Chagua wiziara yeyote unayopenda kuilenga.
  • tupe tathmini mambo gani unezungumza mjengoni?
 
Nimefuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea hapa JF uliokuwa ukijadili kuhusu Zitto,JK VS gazeti la tanzania daima na mmiliki wa gazeti hilo amabye ni Mbowe. Kuna mengi yamesemwa lakini lililoniku na hili la huyu Naibu Katibu Mkuu wa CDM Zitto Kabwe.Katika kujitetea na kuhamishia lawama kwa wenzake kiongozi huyu ninayemuamini miaka yote tangu nimemfahamu amewadhalilisha na kuwadharau wanachama wapya wa CDM.Naomba ninukuhuu maneno yake hapa chini wakati akimjibu mchangiaji mmoja kwenye ile thread.

[Ha ha ha ha ha ha. Kwi kwi kwi! Unanifanya nicheke kijuha juha na maneno yako.Chadema ni chama cha kidemokrasia na kitabaki hivyo. Sisi tulio ndani ya chama hiki toka kianze ndio tunajua utamaduni wa chadema. Wewe kwa kuwa ni wa kuja na ukazawadiwa ba Ubunge lazima useme hayo unayosema.Napenda nirudie kusema sina umri wa kugombea Urais kwa sasa. Nitamwunga mkono mgombea Urais wa CHADEMA atakayepitishwa ba vikao vya chama wakati utakapofika. Kwa sasa hakuna mgombea Urais CHADEMA na mie wala sioti kuwa mgombea. Kama uropokaji huu unatokana na Urais, mie simo. Kwamba sitaweza kuwa kama ningekuwa nina vigezo, unajidanganya tu na unajua unajidanganya. Chadema ni wanachama. Bring a free and fair election uone! ]

maneno haya ni ya dhihaka kubwa na hayakupaswa kuongelewa na kiongozi kama yeye tegemeo la taifa kwasababu zifuatazo
1. Zitto unaposema kuwa yeye ni mwananchama wa siku nyingi na wenzake ni wakuja ni dharau kubwa kwa wanachama wapya.Anamaanisha kuwa wanachama wazamani ndio wanajua zaidi utamaduni wa chama kuliko wapya na hawastahili kuhoji ukiukwaji wa tamaduni hizo zinapofanywa na wanachama wa zamani.Zitto unapaswa kuwaomba radhi wanachama hawa wapya.

2. Zitto unaposema kwa huyo aliyekujibu kuwa ni wakuja na amezawadiwa Ubunge ndio maana akaksema livyosema unamaanisha kuwa Wabunge wa CDM wamezawadiwa viti maalum-kauli hii ikitoka kwa kiongozi kama wewe maana yake ni kuwa vitimaalum CDM ni zawadi na hivyo waliopata wamepewa zawadi.Unatumaanisha nini sisi tuliogombea nahatukabahtaika kupata nafasi hizo?kuwa kumbe wenzetu walipewa zawadi?nilikuwa mgombea kwenye mchakato ule na baadaye tulitangaziwa vigezo kuwekwa ili watu wapite kwa vigezo ili kuepusha rushwa iliyotaka kufanyika aabayo iliasisiwa na wewe ndani ya chama,ulitumia pesa nyingi sana ili watu wako washinde. Zitto acha kupotosha umma,usikiharibu chama chako unapaswa kukijenga.Maneno kama hayo hayapawsi kusemwa na mtu kama wewe,ulishiriki kwenye mchakato wa kuwapata,unajua vigezo,mama yako alikuwepo kwenye kamati,rafiki yako Dk Kitilla alikuwa Mwenyekiti wa Kamati.Tueleze hawa wabunge walizawadiwaje?je ni mama yako,ni wewe,ni Kitilla,ni Dk Slaa,ni Mbowe tuambieni na sisi ambao hatkupata ili mwaka 2015 tujipange vizuri.

Zitto unapaswa kuomba radhi wabunge hawa waliopita kihalali kwa vigezo.

Nawasilisha.

Safi sana kwa hili hata mimi asubuhi nilitangaza azma ya kulipeleka hili kamati kuu kwa kudhalilisha wabunge wa viti maalumu kwenye mitandao.hii ni dharau iliyopitiliza.nilishasema hawa wanawachukia kwa sababu walitaka kuchomeka watu wao.kinachoshangaza zaidi kuna tetesi kuwa wana mahawara zao huko huko.Mwone huyu hapa chini nae amejaribu sana kujiweka mbali na hii kashfa lakini amejenga hoja zenye muelekeo wa kufuta viti maalumu.Dharau zao ziko waziwazi.Hebu watuache wasituharbie chama mbelekeni mawazo yenu huko nccr hakuna anayewazuia bwana


Ukipiga hesabu ya wabunge wanaoteuliwa na wengine kupita kupingwa utashangaa aian ya democracy tuliyo nayo.Ndiyo maana kuna post moja nilikuwa nimetoa suggestion kwamba kama tukiwa na federal system basi Bicameral parliament haitaepukika na pengine hapo tunaweza kuunda structure nzuri ya uwakilishi na ya demokrasia ya kweli kama INDIA,US,Switzerland etc.

Najaribu kutafakari aina hii ya Demokrasia ambayo Executive kama mhimili wa Dola unapata mwanya mkubwa wa kuingilia bunge kwa teuzi holela tu za wabunge,unategemea nini kutoka kwenye mhimili wa mmoja kuuwajibisha mwingine na kuusimamia?Kwa hiyo sisi kama Taifa huu mjadla unaweza kuwa mpana zaidi

Hilo fungu la wabunge wengi wa viti maalumu ambao hata kazi yao haipo consistent na dhumuni la kuwa na bunge au dhana nzima ya parliamentary system ni bora lingetumika vizuri kwa kupanua wigo wa uwakilishi kwa kuunda Rotating pyrammid like structure of representative kwa kusogeza uwakilishi zaidi kwa councillors/madiwani ili tuwe na Demokrasia ya pekee,vinginevyo tutaishia kuwa na udikteta wa mhimili(pillar dictatorship or totalitarian).Wale disadvateged group wataweza kuwakilishwa vizuri zaidi na kujenga uwakilishi uliokusudiwa kwa haki ya walipa kodi na katika utekelezaji wa dhamira ya kweli ya uhuru wa mawazo na uwakilishi uliotukuka kwa wananchi wake. nPengine tungeweza kuwa mfano wa kuandiaka theory mpya ya uwakilishi

 
Labda hujanisoma vizuri. Nimesema wa kuja halina ubishi kwani hata yeye Zitto anaweza kuitwa wakuja na wenyeji wake ktk mazungumzo yanayohusu ujio wake..Hiki ni kiswahili tunachokitumia siku zote na wala sii tusi unless wewe mwenyewe ndio unajihisi Ugeni ni tusi.Swala ni mtu uliyechini yako na mgeni anaanza kutoa maneno ambayo kiaina yanakosa adabu na zaidi ya hapo mtu huyo hajui undani wakile anachokizungumza zaidi ya kushabikia. Mzee Pius Msekwa anaweza kabisa kuwaita wabunge wa CCM wa kuja kama hao wabunge watamkosea adabu na wataanza kumzungumzia yeye na sii kazi walokabidhiwa. Tena basi huyo mzee wetu pius Msekwa anaweza kutukana matusi ya nguoni acha hii habari ya kuitwa watu wa kuja. Kawaita upinzani wanafiki atashindwa kumwita mtu wa kuja?Huyu mbunge alozungumza simjui ila Zitto anamfahamu vizuri na kuja kwake hapa JF akipinga matumizi ya lugha ya Zitto kwa kiongozi wake ktk FB hali yeye mwenyewe anarudia uozo ule ule hapa JF, inabidi apigwe kibao cha kerbu na ndio hayo majibu ya Zitto. Kifupi kule tulikotoka Zitto mwenyewe kakubali makosa ktk kusherehesha malalamiko yake, hata huyu mbunge wetu inabidi ajifunze kutumia lugha nzuri unapowakilisha hoja. Kama kuna malalamiko yoyote zipo njia mbadala za kufikisha malalamiko hayo na sii kuvuana nguo hapa JF kama vile Zitto ni baradhuli asiyejiweza..
THANKS! For being fair .
 
Safi sana kwa hili hata mimi asubuhi nilitangaza azma ya kulipeleka hili kamati kuu kwa kudhalilisha wabunge wa viti maalumu kwenye mitandao.hii ni dharau iliyopitiliza.nilishasema hawa wanawachukia kwa sababu walitaka kuchomeka watu wao.kinachoshangaza zaidi kuna tetesi kuwa wana mahawara zao huko huko.Mwone huyu hapa chini nae amejaribu sana kujiweka mbali na hii kashfa lakini amejenga hoja zenye muelekeo wa kufuta viti maalumu.Dharau zao ziko waziwazi.Hebu watuache wasituharbie chama mbelekeni mawazo yenu huko nccr hakuna anayewazuia bwana
Utakapopeleka hoja ya kudhalilishwa viti maalum usisahau na hoja ya kiti maalum mmoja kutamka wazi Zitto kamwe hawezi kugombea urais CDM, ili tupate uhakika kama hoja hyo ilishajadiliwa tupewe na vigezo.
 
Mh inaelekea Chadema ndani yake kuna makundi kama ilivyo CCM. Chadema wasipo angalia wataanza kugeuka replica ya CCM kabla hata ya kushika madaraka. Ubaya wa wao kuwa kama CCM ina maanisha chama kitakua kimeenda kinyume kabisa na ujumbe wao wa kuwa chama mbadala na CCM watahakikisha wananchi wanajua na wananchi hawato sahau.
 
Labda hujanisoma vizuri. Nimesema wa kuja halina ubishi kwani hata yeye Zitto anaweza kuitwa wakuja na wenyeji wake ktk mazungumzo yanayohusu ujio wake..Hiki ni kiswahili tunachokitumia siku zote na wala sii tusi unless wewe mwenyewe ndio unajihisi Ugeni ni tusi.

Swala ni mtu uliyechini yako na mgeni anaanza kutoa maneno ambayo kiaina yanakosa adabu na zaidi ya hapo mtu huyo hajui undani wakile anachokizungumza zaidi ya kushabikia. Mzee Pius Msekwa anaweza kabisa kuwaita wabunge wa CCM wa kuja kama hao wabunge watamkosea adabu na wataanza kumzungumzia yeye na sii kazi walokabidhiwa. Tena basi huyo mzee wetu pius Msekwa anaweza kutukana matusi ya nguoni acha hii habari ya kuitwa watu wa kuja. Kawaita upinzani wanafiki atashindwa kumwita mtu wa kuja?

Huyu mbunge alozungumza simjui ila Zitto anamfahamu vizuri na kuja kwake hapa JF akipinga matumizi ya lugha ya Zitto kwa kiongozi wake ktk FB hali yeye mwenyewe anarudia uozo ule ule hapa JF, inabidi apigwe kibao cha kerbu na ndio hayo majibu ya Zitto. Kifupi kule tulikotoka Zitto mwenyewe kakubali makosa ktk kusherehesha malalamiko yake, hata huyu mbunge wetu inabidi ajifunze kutumia lugha nzuri unapowakilisha hoja. Kama kuna malalamiko yoyote zipo njia mbadala za kufikisha malalamiko hayo na sii kuvuana nguo hapa JF kama vile Zitto ni baradhuli asiyejiweza..

Mfundishe kwanza Zitto halafu uje kwangu,mwisho malizia na kwako.
 
Safi sana kwa hili hata mimi asubuhi nilitangaza azma ya kulipeleka hili kamati kuu kwa kudhalilisha wabunge wa viti maalumu kwenye mitandao.hii ni dharau iliyopitiliza.nilishasema hawa wanawachukia kwa sababu walitaka kuchomeka watu wao.kinachoshangaza zaidi kuna tetesi kuwa wana mahawara zao huko huko.Mwone huyu hapa chini nae amejaribu sana kujiweka mbali na hii kashfa lakini amejenga hoja zenye muelekeo wa kufuta viti maalumu.Dharau zao ziko waziwazi.Hebu watuache wasituharbie chama mbelekeni mawazo yenu huko nccr hakuna anayewazuia bwana


Hatutaki viti maalum/kuteuliwa....It's nonsense and undemocratic!!,let alone cost effectiveness of the whole dumb idea.
 
Hata mimi sioni ubaya wa maneno ya Zitto..
Watanzania tuna ustaarabu wetu wa lugha na matumizi yake. Majibu yalikuwa safi kabisa kwa mhusika kwani aloanza maneno haya sii Zitto. Nachopenda na kufurahia ni uwezo wa viongozi wa Chadema kuwa mbele ktk kujibu maswali na unapoleta uhuni unapewa dawa! Na nampenda Zitto kwaq kutomung'unya maneno. Ujasiri na kiburi chake kinahitajika sana na hakika tunamuhitaji mtu kama yeye ktk nafasi muhimu.

Mbunge wa viti maalum ni kuzawadiwa hilo halina ubishi tena kama umejiunga hivi karibuni ndio kabisa inatakiwa ukae kimyaa maanake hujui! na kutojua sii tusi bali ni usia mzuri kwa viongozi wageni wapate kujifunza kuheshimu viongozi wao. Zitto ni naibu katibu wa chama, na lugha inayotumiwa na baadhi ya vijana wa Chadema hapa JF nadhani inavuka mpaka wa heshima wakati wao wamemkabidhi mamlaka hayo..


MKANDARA,
Nami napenda nikuunge mkono bila uficho katika maneno yako yenye ukweli mtupu.
Ila natofautiana na wewe katika kipegele kimoja, hawa wanaojibu matusi na mashabiki wanaojivika gwanda la chadema kwa kujifanya wanajua sana na eti wanauchungu na chama ni watu wenye milengo butu isiyo na maono hai.
Hawa ni wale waishio kwa upepo uvumao kusi-kaskaz, tena ukiwawataka wajadili kitu kwa uhalisia hutapata majibu na ukitaka ukoshe waombe wajadili ushibiki wenye wingi wa porojo utaona mandiko yenye ufundi wa kijuha kabisa.
Nayasema haya bila gubi lolote kwani nimewashauri mara kadhaa wawe wenye kujadili hoja na sio kushambulia kwa matusi, lakini hawashiki mpambanuo huo.
Nami nakazia...UBUNGE VITI MAALUM NI ZAWADI NA HATA WAO WANAJUA WAMEZAWADIWA...NA WANAJUA KABISA NI BAHATI NA SIO KWA VIGEZO VYA UWEZO BINAFSI.
 
Naomba mtu mmoja aweke link ya hiyo thread nimejaribu kuitafuta siioni, nataka na mimi niweke mawazo yangu baada ya kuwa nimeshasoma hayo majibizano.
 
Mwenye majina ya wabunge wote wa viti maalum kupitia chadema/picha zao,namuomba ayaweke hapa
 
THANKS! For being fair .

He's always fair.....

Sio shabiki ndiyo maana utaona baadae watu wataanza kumshambulia ati mbona jana ulikuwa una-oppose mbona leo una-support.Watu wanashindwa kuelewa tofauti kati ya Analysis by intellectual reasoning na political fanatiscism cum personal vendatta.Sio kila mtu JF ni shabiki
 
good!!!!!thanks.

Nyakarungu/Jikedume

Unaatamani na wewe kama ungekuwa mwanamke vile ili upate ubunge wa vitimaalum uache kurandaranda.Hivi kwenye Uongozi wa BAVICHA hakuna vitimaalum ili uteuliwe na wewe?maana ulifanya kazi nzuri sana ya washa taa mchana.hivi mfadhili wako bado yupo?
 
I agree, two wrongs dont make it right, but tuangalie pia kwanini Zitto ametoa comment hyo? Maneno ya Marytina yalistahili kusemwa? Hayakuwa 7bu ya zito kureact hivyo? Alimaanisha nini kusema Zitto hawezi kuwa Rais akiwa CDM, labda CCM au NCCR? Kwa mtazamo wangu alimaanisha Zitto despite mchango wake kuikuza CDM hawamuhitaji. Lets b fair to both of them kwa kuwaeleza wote walipokosea.

Kama Mh. Zitto hakufurahishwa na aliyosema Marytina, taratibu za JF zinasemaje? Mods hawakuona aliyosema Marytina? I don't know whether or Marytina is also an MP, but if she is then I don't condone what she said either hata kama anajificha kwa ID feki. Similarly, I don't condone Hon. Zitto's response. Angetumia busara zaidi. Otherwise, anaweza kuwekwa kundi moja na Martyana. Kuna njia nyingi za busara za ku address issue kama hii. Badala yake ame-respond in way that tries to justify demarcations of members within the party.

Hon Zitto should have been wise to give thought to Marytina's remarks before responding. If it were you responding to Marytina's remark, as a person holding a public office, you would want to put a little thought into what you are about to post in a forum like this. If people post comments that are critical or even insulting you, you would always maintain an even demeanor. Hon Zitto should not have over reacted in a way which he might come to regret later or which will cast him in a negative light in the same way as Marytina. Condoning Hon Zitto's response is condoning Marytina's remarks and vice versa.
 
si condone maneno ya kiburi aliyoyatoa zitto na wala sikubaliani na mkandara kupongeza kiburi cha viongozi.

Lakini ukweli unasimama kuwa viti maalum ni zawadi za chama kwa wapenzi wao. Na kama ni mfuatiliaji mzuri suala la vigezo lilikwisha jadiliwa hapa sana. Kuwa model iliyotumiwa na kitila, kulikuwa na uwezekano wa kutizama wanaotakiwa "kuzawadiwa" kwanza, kisha akaweka vigezo, ili kuhakikisha hao wanaotakiwa kuzawadiwa wanafanikiwa kwenye hilo. Kwa hiyo uliposhindwa vigezo inaweza kumaanisha kuwa hukuwa na vigezo stahili kuzawadiwa.

Lakini firstlady unanishangaza kumpinga zitto kwa kuhujumu chama lakini wewe kufanya kile kile. Hapo kwenye maelezo ya zitto alitoa rushwa unadhani upo katika kukijenga chama? Kuwa zitto alitoa rushwa ili watu wake wapite na ikajuulikana wazi mpaka mfumo kubadilishwa lakini bado anaendelea kuwa nafasi ya juu kwenye chama, hii inakipa chama credibility ya aina gani?

hakika kweli huyu ni wa kuja, sio wakuja cdm tu, bali katika siasa huyu ni wa kuja.
Anaamini siasa ni kupigana majungu tu, anaamini hana uwezo wa nguvu za ushawishi bali anatumia njia za aina hii kuwaharibu wenye hoja.
Ninamuomba aende kwa wananchi afanye kazi ya kujenga chama tuone uwezo wake.
Na watu wa aina hii ni hatari sana, kwani watagombania jimbo la viti maalum na mwisho wa siku watawagawa wananchi na hali hii imemponza dada mmoja ni viti maalum sasa.

Kuna mambo yakufanya ili jamii ikuamini na ikupende sio kupiga majungu kila wakati mama.
 
heee makubwa haya kumbe ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni ni kweli. Nijuavyo mimi CDM ni chama chenye watu makini na nilimtegemea Zitto ni mmoja wao lakini kwa hili amesikitisha na kuonesha his true colours! Zitto ndio alikuwa msimamizi mkuu wa Uchaguzi huo kabla haujavurugika na yeye anajua kwa nini hali ilifika pale. Lakini hata baadaye alikuwa kwenye kamati ya kuteua waheshimiwa hao sasa leo inakuwaje aseme haya! Kama si unafiki dhahiri nini? Atueleze ni wapi aliwapa na wale waliokosa waende wapi?
Hii inatuonesha kwamba vigezo vilivyoelezwa na Dr Kitila ni vya uongo?? Tunaomba viongozi wakuu mumfunde huyu maana atakiingiza chama pabaya
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom