EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Hata mimi sioni ubaya wa maneno ya Zitto..
Watanzania tuna ustaarabu wetu wa lugha na matumizi yake. Majibu yalikuwa safi kabisa kwa mhusika kwani aloanza maneno haya sii Zitto. Nachopenda na kufurahia ni uwezo wa viongozi wa Chadema kuwa mbele ktk kujibu maswali na unapoleta uhuni unapewa dawa! Na nampenda Zitto kwaq kutomung'unya maneno. Ujasiri na kiburi chake kinahitajika sana na hakika tunamuhitaji mtu kama yeye ktk nafasi muhimu.
Mbunge wa viti maalum ni kuzawadiwa hilo halina ubishi tena kama umejiunga hivi karibuni ndio kabisa inatakiwa ukae kimyaa maanake hujui! na kutojua sii tusi bali ni usia mzuri kwa viongozi wageni wapate kujifunza kuheshimu viongozi wao. Zitto ni naibu katibu wa chama, na lugha inayotumiwa na baadhi ya vijana wa Chadema hapa JF nadhani inavuka mpaka wa heshima wakati wao wamemkabidhi mamlaka hayo..
Kwa hiyo mtu akijiunga na CDM kwa mara ya kwanza ni sawa kumwita wa kuja? Unaona ni sawa kwa Naibu Katibu wa Chama Kukuu cha upinzani kuwaita wanachama wake wapya ni wa kuja? Ingekuwaje hapa kama Pius Msekwa amewaita wanachama wapya wa CCM wa kuja. I am sure hii thread ingekuwa na pages 30 by now. Nilidhani Chadema ni wanachama bila kubaguana. Kumbe chama kilikuwa kina recruit wanachama wa kuja huko mikoani. Kwa hiyo wanachama wa siku nyingi wanakuwa treated tofauti na wanachama wa kuja? Huku sio kubaguana na kujenga matabaka ya wanachama? Wanachama wa zamani na wale wa kuja? Kwa vile umesema Mh Zitto hajamung'unya maneno, ina mana aliyosema ni kweli sio. Siungi mkono kuwepo kwa wabunge sijui wa viti maalumu, lakini the way Mh Zitto alivyoiandika hili suala, well I will better keep my mouth shut.