Zitto umewadhalilisha Wabunge wa Viti Maalum CDM; Waombe Radhi


..wanawake ni zaidi ya asilimia 50% ya raia wote wa Tanzania. lakini ukiangalia uwakilishi wao ktk maeneo mbalimbali mfano elimu, biashara kubwa, nafasi za uongozi,umiliki wa ardhi, uwakilishi bungeni, etc etc unaona kuwa wanaume ndiyo wamejaza nafasi nyingi. suala ni kujiuliza ni kwamba, tutaweza vipi kuwainua mama zetu,dada zetu, binti zetu, ili nao waweze kupata mafanikio[have an equal share of the national cake] kama yale waliyonayo wanaume?​
Mkuu equal share haiwezi kufumbuliwa kwa kuongeza hesabu kubwa ya wabunge wanawake...
Mkutano wa Beijin, haukuwa na maudhui haya ila wanawake wamekuwa WAKINYIMWA nafasi za uongozi na zipo nchji nyingi duniani hata kusimama kugombea hawaruhusiwi. Kuwezeshwa kulikozungumziwa ni kuondokana na mila za mfumo dume ambao umewadhalilisha wanawake kwa karne nyingi zilizopita na message ya msingi ilotoka ni kwamba wanawake wana uwezo mkubwa au sawa na wanaume ktk utekelezaji wa kazi na haki yao kupokea mishahara sawa na wanaume.

Nadhani hadi sasa hivi Canada na nchi za Nordic ndizo haziweki tofauti ya mishahara kati ya wanaume na wanawake ktk kazi moja na nasema bila kumung'unya maneno Tanzania pia ni moja ya nchi za kiafrika ambayo haina migogoro ya utoaji ajira na mishahara. Hivyo kuhudhuria kwetu mkutano wa Beijin hautupi nafasi ya kutafuta sababu nyingine nje ya kile kilichokusudiwa.

Aidha mkutano huo uliwaamsha wanawake kudai haki hizi na kujitokeza kugombania nafasi ktk uongozi, ajira na maswala mengine ambayo walidhalilishwa kwa sababu ya uke wao. Kwa nini wanawake hawapo wengi bungeni kwetu?.. jiulize ni wangapi hujitokeza kama sii kwamba bado wamefunikwa na utumwa wa kimila kumtumikia mwanaume.... Mkoa wa Tabora sidhani kama una mbunge au Diwani hata mmoja na mwanamke, na sii kwamba wananchi wanashindwa kuwachagua isipokuwa hawajitokezi kutokana na utumwa wa mila zetu. Sheria inawaruhusu lakini bado wao wanataka kuiwezeshwa kwa kupitia viti maalum. na kikubwa zaidi ubunge nchini unahitaji uwe na mtaji mkubwa wa kifedha, hili lingeangaliwa na kupatiwa ufumbuzi.

Elimu ya uraia kwa wanawake inatakiwa kuongezwa hivyo vyanzo kama Taasisi ya kuwawezesha wanawake ndio ziundwe na zipate uwakilishi bungeni. Tuna Umoja wa Wanawake (UWT) badala ya kudeal na wanawake WOTE NCHINI ina deal na maMbo ya chama CCM, kuhamasisha wanawake wajiunge na CCM...tena inaelekeza nguvu zake zote ktk uwekezaji kwa wanachama wa CCM ambao hawafiki hata asilimia 1 ya wanwake nchini, hao waliobakia nje watafute pa kutokea.

Sasa kama tuna nia njema tuvunje Umoja wa wanawake na iundwe taasisi ambayo itawakilisha wanwake wote nchini na hata wapewe wabunge 10 wa kuteuliwa na wanawake wenyewe ktk taasisi zao ni bora zaidi kuliko huu mfumo dume ambao pamoja na kuwepo hivi viti maalum bado ni wanaume wanaochagua kina nani wapewe nafasi hizo..
Mfumo dume ni - Nguvu ya mamlaka alopewa mwanaume kufanya maamuzi ambayo yanamhusu hata mwanamke!​
 
Mkuu hata mimi hili nakubalina nalo lakini je unaweza kutaja ni marekebisho gani hayo kwa mtazamo wako.

Mfano mm kw amtazamo wangu napenda nione kuna percent ya wakulima amabao watateuliwa kutokana na uzalishaji wao. tena kwa hili kundi ningesema term yao iwe mwaka mmoja mmoja. au miwili.

I mean viti maalum vinatakiwa kuwalenga disadavantaged group amabao hawana uwakilishi kabisa.( eg wakulima watu wa vijijini na wilayani)

Sasa mwanamama msomi anaacha kazi UDSM, SUA , etc anaenda kuomba viti maalum. Tayari tuna wasomi wengi tena wote makazi yao ni mjini. na. Ni wawakilishi wachache ambao residence zao ziko wilayani achilia mbali vijijini.

Huo ndio mtazamo wangu kama hivi viti ni vya muhimu

Hoja nzuri lakini sidhani kama itasolve tatizo linalotukabili linapokuja suala zima la uwakilishi bungeni. Wabunge wa kuchaguliwa tayari wanayo majukumu ya kuwatetea watu wote including disadvantaged groups kama wakulima wilayani na vijijini. Sasa tukiwa na wabunge wa kuteuliwa kuwakilisha wakulima, hao wabunge waliochaguliwa watakuwa wanawawakilisha akina nani? Wilayani kwangu ni full kulima. Tumemchagua mbunge wetu ili atetee interests zetu za kilimo. Hapo sidhani kama tutahitaji tena mbunge mwingine wa kuteuliwa kututetea. We don't need double representation. Itatu cost.

Hata hivyo, intention ya viti maalumu ilikuwa nzuri tuu lakini siku hizi imekuwa very abused kiasi cha kusema kuwa they are not fit for purpose. Huwezi kumpa mtu mwenye Ph.D kiti maalumu cha ubunge kwa madhumuni ya kumkomboa. Sijui Chadema walikuwa na lengo gani kugawa points nyingi kwa wale waliokuwa na Ph.D. Lakini kitu ambacho kilinifanya nilione viti maalumu ni completely useless ni pale yule mbunge wa zamani wa kuchaguliwa wa jimbo la Kawe (nimemsahau jina), alipoacha kugombea tena kwenye hilo jimbo na kwenda kuwa mbunge wa viti maalumu. Hii inamaanisha nini?

Lakini kama ulivyosema zipo disadvantaged groups kwenye jamii ambazo tunafikiri zanahitaji special representation bungeni. Watu kwenye hizi groups wanayo haki ya kupiga kura na kuwakilishwa bungeni na wabunge waliowachagua. Tatizo hapa ni kwamba hawa wabunge wakishachaguliwa wanawasahau kabisa watu kama walemavu n.k. Tukiangalia role ya mbunge kama ku represent all people across the society regardless of their gender, religion, race, etc, then hakuna haja ya kuwa na viti maalumu. Unfortunately, this is not the case in our country. Je, solution ni these disadvantaged groups kuwa na special representatiion bungeni? If so, hao wabunge watakuwa wana tofauti yoyote na wale wa kuchaguliwa ambao wameshindwa kuwatetea hata watu waliowapigia kura?
 
Zitto is right, ni msimamo wake ktk swala la viti maalum na hakujificha kumwambia huyu binti ambaye kaja na lugha ya kihuni akaambiwa anajivuna leo kwa kuzawadiwa Ubunge!

Hivi Zitto aliyasema haya kama Zitto, kama kiongozi wa chama kikuu cha upinzani au kama mbunge na nyanyifa zake bungeni?
 
EMT Yule mbunge wa Kawe ni Rita Mlaki, kaona njia rahisi ni viti maalumu kwasababu huko ana masilahi. Anyway!

Mkandara, viti maalumu vilikuwa na maana lakini vime kuwa abused kiasi cha kupoteza ile maana halisi na iliyokusudiwa. Angalia chama kama CCM chenye wabunge wengi wa vitimaalumu, 70% ni vitimaalaumu 'kwa sababu!!' Haiwezekani vitimaalumu viwe sehemu za kuwatunukia zawadi tutegemea watetee wanawake.

Angalia wasomi wameacha kazi zao na badala ya kugombea ili kukabiliana na mfumo dume ili wawe mfano kwa wanawake wenzao, wanakimbilia viti maalumu kwa maana ya kwamba pamoja elimu zao za PhD,master n.k bado wanajisikia dhalili, hawa wanawezaje kwenda bungeni kumtetea mwanamke wa kijijini ikiwa wao wenye silaha muhimu ya elimu hawawezi kuitumia. Utagundua kuwa kinachowapeleka si utetezi ni uroho na njia za mkato za maisha tu.

Rsearch nyingi zimeonyesha kitu kinachoitwa positive affirmative action hakimsaidii mwanadamu. Nimewahi kutoa mifano ya makabila na kanda zilizowahi kupewa positive affirmative action na hakuna hata moja iliyokuwa na matokeo mazuri.

Ukiniuliza tufanye nini kuwainua akina mama, nina jibu moja, futa vitimaalumu chukua hizo pesa invest kwa mtoto wa kike miaka 5-10 utapata wabunge wa wanawake wanaokaa na kufanya kazi na wanawake huko waliko na si wabunge wa kushangilia hovyo hovyo Dodoma hata kama hoja ni ya kumuumiza mwanamke kule kijijini.Kwao posho kwanza mwanamke baadae, tunahitaji watu wa aina hii kweli!!!
Wekeza katika elimu utapata wanawake watakaojitambua na watakaojiuliza mfumo dume hadi lini? Ipo siku wataingia mtaani. Wanajitambua!!

Ukiangalia katika jamii za kitanzania sehemu ambazo mwanamke amepewa elimu zinamaendeleo na ndiyo imekuwa chanzo cha viti maalumu iwe CCM, CUF, Chadema. Ukombozi wa mwanamke utokane na yeye kujitambua, na kutambua mfumo uliopo na yeye mwenyewe kupanga mbinu za kukabiliana na mfumo. Silaha kubwa ni kumpa ellimu ili ajitambue kwanza.
 
Viti maalum vipo Tanzania kwa muongozo wa SADC na wameambizana kuwa ifikie asilimia 50.

Linapokuja suala hili, ni dhahiri kuwa ni kuzawadiana tu na wala vyama haviweki dhumuni la viti hivyo kwenye ajenda yake wakati wa kuteuwa.

Kwa CCM ni dhahiri kuwa wanagawana kulipana fadhila japo kuwa wanavika jokho la demokrasia. CHADEMA wao ndio wamechemka zaidi kwenye hilo. Mwanamke mwenye PHD na ambae amefanya kazi kwenye taasisi zinazojuulikana anapewa points kubwa zaidi kuliko mwanamke mwengine. Licha ya kupuuza dhumuni la viti maalum, pia wanapuuza sera ya chama inayotaka kubadili mfumo wa upataji elimu kwa kuwa sasa hakuna usawa wala haki badala yake wakaamua kumpunish yule mwenye elimu ndogo. Hapa ndipo lilipoibuka suala iwapo vigezo viliwekwa baada ya kuwatazama wanaotaka kuzawadiwa au la.

CCM wana kesi ya Rita Mlaki lakini na CHADEMA wana kesi ya RACHEL (jina lake silijui) ambae demokrasia ilimpitisha agombee lakini viongozi wa chama 'wakamshauri' amuachie Mpendazoe na yeye kuahidiwa viti maalum (haikusemwa wazi peupeni). Kwa mara nyengine tena, demokrasia ilipindishwa na mfumodume kutawala. Hapa mwanamke hakujengwa, amerudishwa nyuma na viti maalum kutumika kujaza makombo ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na wale waliokataliwa majimboni.

Juu ya hayo hakuna mantiki ya kuwa na viti maalum to begin with. Tumeshuhudia na kuona kuwa kujaa kwa wanawake kwenye bunge hakujasaidia kuondoa matatizo ya mwanamke nchini, tofauti na mabunge ya Marekani, Asia, na nchi za Ulaya ukiachia hizo za Nordic ambapo uwiano wa wanawake kwa wanaume ni ndogo mno bungeni , lakini maendeleo yamesambaa kwa wote. Hii inatokana na wabunge wawe wanawake au wanaume kulazimishwa kujua wajibu wao na kuwawakilisha kwa usawa wanajimbo wote.

Nitatofautiana na Mkandara kidogo unaposema

jiulize ni wangapi hujitokeza kama sii kwamba bado wamefunikwa na utumwa wa kimila kumtumikia mwanaume....

Kutokujitokeza kwa wanawake kugombea hakumaanishi kuwa wamefunikwa na utumwa wala wako katika kumtumikia mwanamme. Nafikiri suala la kwanza ni selft interest. Hivi mwanamke analazimika awe na interest na siasa na asipojitokeza kuwania basi amefunikwa na utamaduni wa kumtumia mwanamme? Tunasahau kuwa mwanamke huyu huyu hana interest na sayansi au engineering hata katika nchi zilizoendelea.

Kwa hiyo kwanza kama tunataka wanawake waingie kwenye siasa, tuanze kuchochea interests zao kwenye siasa (na sio kuwapa nafasi japo hana interest wala uwezo wala watu hawamtaki), kwa sababu Tanzania hii ya leo wanawake wenye uwezo wa kugombea majimboni na wakashinda wamejaa tele, lakini interest hawana, na wako radhi kuendelea na kazi zao huko walipo.

Lakini pia hakuna ulazima wa wanawake kuingia kwenye siasa ili shida na matatizo yao yaweze kutatuliwa. Si tumeona kwenye nchi zilizoendelea? Kinachotakiwa ni kuongeza uelewa kwa wanawake hasa kweny elimu ili kwanza aweze kupigia kura mgombea atakaewakilisha vyema interests zake, na pili aweze kumbana mbunge wake asiyetekeleza matakwa yake.
 
Gaijin;2229815]Viti maalum vipo Tanzania kwa muongozo wa SADC na wameambizana kuwa ifikie asilimia 50
Hapa tujiulize, endapo wingi wa akina mama ni maendeleo dhidi ya ujinga, maradhi na umasikini kwanini tusiwape 100%. Sijali hata kama bunge zima litachaguliwa na kuwa la akina mama ili mradi tu uwepo wao uwe wa kuchaguliwa(merits) na sio kuteuliwa(favor)
CCM wana kesi ya Rita Mlaki lakini na CHADEMA wana kesi ya RACHEL (jina lake silijui) ambae demokrasia ilimpitisha agombee lakini viongozi wa chama 'wakamshauri' amuachie Mpendazoe na yeye kuahidiwa viti maalum (haikusemwa wazi peupeni). Kwa mara nyengine tena, demokrasia ilipindishwa na mfumodume kutawala. Hapa mwanamke hakujengwa, amerudishwa nyuma na viti maalum kutumika kujaza makombo ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na wale waliokataliwa majimboni
Tungetegemea wanawake wote bila kujali itikadi zao wakemee mfumo dume kama wanavyosema, hakuna aliyethubutu. Sitegemei mwanamke aliyebeba ndoo ya maji km 10 kuelewa hili, lakini wale wasomi wa viti maalumu wanalielewa na wao wangesimama kidete hata kabla ya kuingia mjengoni. Kwanza ingeweza kuwasadia kupata wingi wa kupaza sauti zao. Hakuna aliyesema, tunawasikia wakitetea posho za madiwani na kuzomea ukumbini, halafu mtu aseme wanatetea wanawake!!
Juu ya hayo hakuna mantiki ya kuwa na viti maalum to begin with. Tumeshuhudia na kuona kuwa kujaa kwa wanawake kwenye bunge hakujasaidia kuondoa matatizo ya mwanamke nchini, tofauti na mabunge ya Marekani, Asia, na nchi za Ulaya ukiachia hizo za Nordic ambapo uwiano wa wanawake kwa wanaume ni ndogo mno bungeni , lakini maendeleo yamesambaa kwa wote. Hii inatokana na wabunge wawe wanawake au wanaume kulazimishwa kujua wajibu wao na kuwawakilisha kwa usawa wanajimbo wote
Ndiyo maana nimetolea mfano wa mama Ananilea Nkya(TAMWA), huwa napenda kusikia kauli zake kwasababu sauti yake ni sawa na sauti za vitimaalumu combine.Indira Gandhi ,Gloria Arroyo, Hang san su kyi, au Sharnawata(hivi majuzi) hawaongozi kwa jinsia bali uwezo wao. Silaha kubwa waliyo nayo dhidi ya mfumo dume ni ELIMU.
Kwa hiyo kwanza kama tunataka wanawake waingie kwenye siasa, tuanze kuchochea interests zao kwenye siasa Lakini pia hakuna ulazima wa wanawake kuingia kwenye siasa ili shida na matatizo yao yaweze kutatuliwa. Si tumeona kwenye nchi zilizoendelea? Kinachotakiwa ni kuongeza uelewa kwa wanawake hasa kweny elimu ili kwanza aweze kupigia kura mgombea atakaewakilisha vyema interests zake, na pili aweze kumbana mbunge wake asiyetekeleza matakwa yake
Anachomaanisha Gaijin ni kuwa tusiwape wanawake samaki, bali tuwafundishe mbinu za kuvua. Mbinu ni elimu tu! Mwaka wa pili mfululizo watoto wa kike wanaongoza mitihani ya taifa, maana yake ni nini! ni kuwa wakipewa mazingira mazuri hawana tofauti na wavulana. Badala ya kuwekeza katika kutafuta elimu ya watoto wa kike mamilioni, tunawekeza kwa kundi la watu 100 wanaosubiri samaki tukitegemea watawafundisha wengine kuvua! Not!

Lakini nina wasi wasi (I stand to be corrected), ukiangalia kwa undani hawa wa vitimaalumu wengi wao wamekulia katika mazingira mazuri, jambo jema kabisa, shida ni pale wasipojua nini maana ya kubeba ndoo ya maji km 5, kurudi shule na kwenda kukata kuni, kukoswa koswa kubakwa wakienda shule, halafu tuna invest (billions) tukijua wanajua uchungu na adha anayopata mwanamke!! I'm not sure!
 
Ndiyo maana nimetolea mfano wa mama Ananilea Nkya(TAMWA), huwa napenda kusikia kauli zake kwasababu sauti yake ni sawa na sauti za vitimaalumu combine.

Si huwa kuna mbunge wa viti maalumu akiwakilisha NGOs? Sidhani anaweza kutamka, aliyosema mama Nkya kwenye hii video. naomba tuu asirubuniwe kwenye viti maalumu. Abaki huko huko TAMWA. Huyu mama ni the most feminist in Tanzania. Amekuwa cited kwa zaidi ya lugha tano (Swedish, Dutch, German, English, Italian and Swahili). Huyu naweza kusema ndie the most woman Tanzania anaye advocate gender equality ambayo tulitegemea wabunge wa viti maalumu wangeitumia nafasi yao kufanya hivyo.



Mwaka jana alitunukiwa na Ubalozi wa Marekani "Tanzanian Woman of Courage award" kwa juhudi zake za ku promote equality, opportunity, and justice for Tanzanian women and girls. According to a statement from the American Embassy, Mama Nkya has been a leading advocate for women's advancement through awareness-raising and judicial reform for over 20 years.

Ananilea%2BTAMWA.JPG



Hii ni kazi ambayo ingetakiwa ifanywe na wabunge wa kuteuliwa kulishawishi bunge libadilishe sheria zinazowakandamiza wanawake. Huyu ni moja ya wanawake wachache waliwezesha kuundwa kwa sheria ya Sexual Offence Special Provision Act (SOSPA) 1998 which for the first time criminalized FGM and increased the punishment of rapists to 30 years in jail and life sentence for gang rape and raping minors. Lakini ukiangalia hii ni moja ya kazi ambazo zilitakuwa kufanywa na wabunge wa viti maalumu.

She holds MA in Journalism Cardiff, UK 1992, BA in Development Studies Kimmege, Ireland 2008 (First Class), Diploma in Journalism, Tanzania School of Journalism,1986. She is using her education and experience to empower and promote women equality across the country. Now compare her na mbunge mwenye kiti cha kuzawadiwa tokea miaka ya 1990s.
 
Last edited by a moderator:
EMT

Hakuna viti maalum vilivyowekwa kwa NGO kisheria. Wanachofanya CCM ni kugawa nafasi zao kwenye makundi yakiwemo vyama vya walemavu, wafanyakazi na wakulima (provided that they are CCM)
 
EMT au mwingine kuna mtu ana background ya kuanzia huko alikotoka, kielimu(shule za awali kabla ya nondo za juu) na kijamii.
Umeona anavyoongea kwa authority! ni mambo ya shule, hata kama hatutakubaliana na kila anachosema, tukubaliane kuwa anajua anachosema, ana uwezo wa kutetea anachokisema kwa hoja zenye mashiko na amesimama kidete kuwatetea akina mama.
 
Tungetegemea wanawake wote bila kujali itikadi zao wakemee mfumo dume kama wanavyosema, hakuna aliyethubutu. Sitegemei mwanamke aliyebeba ndoo ya maji km 10 kuelewa hili, lakini wale wasomi wa viti maalumu wanalielewa na wao wangesimama kidete hata kabla ya kuingia mjengoni. Kwanza ingeweza kuwasadia kupata wingi wa kupaza sauti zao. Hakuna aliyesema, tunawasikia wakitetea posho za madiwani na kuzomea ukumbini, halafu mtu aseme wanatetea wanawake!!

Tatizo la wanawake wengi wa Tanzania ni kwanzo wako too self concious kuwa wao ni wanawake na hilo ndilo linalowarudisha nyuma.

Mwanamke ameshindana jimboni ameshindwa/(anamini ameshinda) unamsikia anasema " nimemuendesha pute (nimemshinda) licha ya uanauke wangu", ambayo kwangu inamaanisha moja kwa moja kuwa anaamini kuwa mwanamke ni dhaifu kuliko mwanamme. With that mentality hatuwezi kupiga hatua ya kuondoa mfumodume. Kwa sababu yeye mwenyewe hajui mfumodume ni nini na huyu ndie tunaemtegemea kwenda kuwakilisha sauti za wanawake wenziwe kupitia viti maalum.

Mwanaamke anapokubali kuachia jimbo ampishe mwanamme kisha yeye apewe nafasi kwa viti maalum alitakiwa akatae kwa kuwa ni kujivunjia thamani yake. Wananchi wanajua na hata viongozi wa vyama wanajua (kama alivyofanya Zitto) kuwa thamani ya viti vya upendeleo na vya kuchagulia ni tofauti japo mshahara na mafao ni ule ule.

Na kama Nguruvi unavyosema, kuna wengine hadi hapo wanapofika hawajawahi kukabiliwa na changamoto ya mfumodume wala dhiki na adha wanazopata wanawake wengi hususan wa vijijini, atawakilisha vipi sauti zao?

Ni bora hata hiyo investment ingewekezwa kwenye elimu. Hata ujenzi wa Chuo Kikuu cha Wanawake nafikiri ungekuwa na faida bora zaidi ya huu mfumo uliopo sasa.
 
dawa ya moto ni moto..kamwe usiogope kumwambia mtu ukweli eti kwa kuogopa kwamba atajiskia hovyo kwa vile hataweza kujifunza. tuambiane ukweli. UKWELI UNAJENGA.
 
Hivi Zitto aliyasema haya kama Zitto, kama kiongozi wa chama kikuu cha upinzani au kama mbunge na nyanyifa zake bungeni?
Nilivyomsoma mimi - Kayasema haya maneno hapa JF kama Zitto kumjibu bibie ambaye kazungumza pia kama mwana JF na sii mbunge! Labda kosa la Zitto linaweza kuwa la ki JF kutoa ID ya mtu hadharani kwa sababu ya beef lao. Lakini kwa ukhakika binti ndiye alianza kuwa personal na Zitto alijibu mapigo, ambayo hata kisiasa inakubalika swala linapofikia personal mhusika anaruhusiwa kujibu mapigo maadam uwe na ukweli..Kinachonishanga mimi ni pale mnapoukubali ukweli lakini maneno haya yasingesemwa na Zitto hali sote tunakubaliana kutomung'unya maneno - Call spade a spade.
Nimewahi kusoma mengi ktk mashambulizi ya Field Marshal na baadhi ya wana JF na ilifika kubaya zaidi ya haya.

Gaijin,

Mkuu wangu swala la wanawake wetu kutawaliwa na utumwa wa kiasili kumtumikia bwana bado ni tatizo kubwa sana kwa pande zote mbili kuachana na utamaduni huu. Bado wanaume wengi hawapendi wake zao washiriki ktk maswala ya kisiasa ama hata kufanya kazi maofisini. Nina marafiki, ndugu na jamaa nawafahamu ambao wamelazimika kuwaachisha kazi wake zao ikiwa wanataka ndoa zao zidumu. Hii imetokana na utamaduni wa ajira ambao mwanamke hulazimika kujidhalilisha kwanza kwa mwajiri ili apate ajira au apande cheo. Swala la KUWEZESHWA limeingia hadi ktk relationship makazini na hakuna sheria ya kuwalinda wanawake kama isivyokuwepo sheria ya kupambana na Ufisadi. Na hakika mila na desturi za wanaume wa Kitanzania jinsi wanavyo wa treat wanawake inaogopesha! bado kabisa hatujajenga utamaduni wa mahusiano mazuri baina ya wanaume na wanawake isipokuwa kwa kutegemea mwanamme ktk imani ile ile ya Wadanganyika kwamba - Tanzania bila CCM haiwezekani!

Bado nitaendelea kutetea kuwepo viti maalum bungeni kwa kufuata dhamira yenye malengo ya kuwasilisha taasisi zinazowahusu wanawake ktk utendaji kazi kwani sisi sote tumelelewa na wanawake na kuwezeshwa kwa vyombo hivyo ndio ujenzi wa Taifa bora zaidi. Hawa ndio mama zetu ambao kwa muda mwingi wa maisha ya utoto na ujana wetu wamekuwa msingi wa makuaji yetu na hakuna ubishi ktk wezo wa mwanamke ktk malezi ukilinganisha na mwanamme. Na siku zote nimezungumzia swala la WATU na MAZINGIRA (rasilimali) kuwa kioo cha mikakati yetu wakati WATU ni pamoja na hekima ya Mwenyezi Mungu ktk maumbile yetu, wenye mila na desturi ( identity) zinazotuwezesha kujenga utamaduni wa kizazi kipya.

Kama tunataka kulijenga Taifa la kesho, nguvu na mamlaka ya mwanamke ktk kushiriki lazima ihusishwe na kupewa dhamana ya kuongoza sekta husika na sii kutunukiwa viti Bungeni ili mradi kujenga uuwiano wakichaguliwa na wanaume kwa faida ya wanaume (kuwa na vipapi bungeni). Kinachotakiwa ni kuwatunukia wanawake nguvu na mamlaka ya Ujenzi wa Taifa la kesho kwani sii wanawake wote wanaopenda kuolewa, kuzaa na kulea watoto ambao ni Taifa la kesho!. Katika hali hiyo hiyo ni wanawake wanaojua zaidi wanachokihitaji kama wanavyojua ktk malezi wa watoto wao ambao ndio kizaizi cha kesho!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom