Zitto tena kachafua hali ya hewa bungeni

Ilikuwa ni utani tu kwa Mbunge mwenzangu tena jirani yangu na rafiki yangu. Mbunge wa chama changu. Narudia. It was a joke

Hapa sawa umejibu vyema ingawaje toka mwanzo mimi nilikuwa sijaamini kama kweli ulikuwa serious na maneno yako!.....ila plz Mh bado tunakuhitaji sisi kama vijana wenzio hebu acha kutuchanganya kila kukicha.........unatuvunja moyo.....tunahisi labda kuna kundi fulani linakutumia kwa manufaa yao ila bado pia sitaki kuamini kama kweli Zitto unaweza kununuliwa na yeyote hata kama wanasema pesa ni mwanaharamu!.......turudishie Zitto wa zamani tafadhali!
 
Last edited by a moderator:
Wakati mwingine mnajiabisha kwa kuwa obsessed na maisha ya watu wengine. Hivi mnaujua uhusiano kati ya Zitto na Tundu na aina mbalimbali ya jokes kati yao. Unaweza kukuta wenzenu wanakumbushana story fulani iliyotokea chako ni chako nyinyi huku mnatoa nyongo tumboni. Vidonda vingine vya tumbo ni vya kujitakia!
Let Tundu be the one to complain. Tundu is smiling wewe huku unatokwa povu!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Bunge sio lao, ni letu sisi. Kama ni mambo ya chako ni chetu au Changu ni changu, yasihusishe bunge. Wasijaze hansad na mambo ya utani wao. Tunachokisoma kwenye hansadi yetu ni Tundu ana poorest hand writting ever. Sijui waalimu wake walimpaje maksi
 
Ule ulikuwa utani wa kibunge tuu,kwanza muda wake ulikuwa umekwisha na pia alitaka watu wajue kuwa kuna kawaida ya kupeana mawazo mtu anapochangia. Hakuna baya hapo.
Hapo kwenye red ndio nini hicho? Kama huna hoja si ukae kimya?
 
Aaaah jamni sio kila kitu cha kukichukulia serious, ule ulikuwa utani tu baada ya zitto kusema vile kwa pa1 yy na Lissu walicheka sana huku wakigonganisha mikono yao.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kwa mawazo na michango hii, kumbe bado vyama vingine havijafikia muda wa kuunda serikali. Nyinyiemu itaendelea kukaa madarakani hadi kitakapotokea chama mbadala chenye nguvu na usikivu mpana, na sio katika hivi vilivyopo sasa. Wazo tu la kuchukua fomu, laweza kubabaisha watu hadi kuchukiana kiasi hiki???? Kwa mantiki hii, Raisi wa awamu ijayo, tutaomba atoke Tarime!!!!!
 
Ha ha haaaa.....hasira za watu!

Tujiulize kwanza,Je kuna uhusiano kati ya akili na Mwandiko mbaya?

Wengine hatujali miandiko hata tulipokuwa tunawaandikia ma-girlfriend zetu walikuwa wakituchukulia hivyo hivyo na miandiko yetu mibaya,wasahihishaji wa mitihani walikuwa wanazingatia majibu sahihi ingawa ni vizuri kuimarisha mwandiko wako

Je,kuna uhusiano kuwa kiongozi mzuri/makini na aina ya uandishi wako? jibui ni hapana...kiongozi mzuri ni mtazamo

Matamshi kama haya Zitto ni matamshi ya kawaida tu na tuyachukulie simple.Mwandiko wa Lissu kama ni mbaya tuuchukulie simple tu kwa kuwa ni kiongozi makini.

Zitto tumchukulie simple tu,kwa kuwa kateleza kashindwa kuwa insensitive katika matamshi.Ili kuwa kiongozi makini ni lazima uwe sensitive anahitaji kujiimarisha hapa....

Lakini katika yote hayo kuhusu Lissu Zitto kadai ilikuwa utani tu.watu wana hasira kweli kweli.Sio mapovu.Lol
 
Bora umekuja kuclarify....watu walikuwa wameshaanza kutokwa na mapovu!!

Hajajibu hoja zetu. Povu halitoki, ukweli utasemwa daima. Hatuangalii ni magamba au magwanda, ngunguri au ngangali katika ukweli. Zitto ajirekebishe. Ina maana yote nayoyatolea povu bungeni huwa ni utani?
 
Mimi napenda kushabikia juhudi binafsi za mtu..kutokana na utendaji wake..na wala sifuati siasa za vyama na ushabiki. Lakini kwa sasa siasa ya Tanzania inaelekea pabaya. Hasa kwa kijana wetu tuliyemwamini Zito..amelewa sifa za kijinga amejenga dharau na kujiona yeye ni wa tufauti sana. Kama kweli hujatumwa kuharibia wenzake basi ana matatizo makubwa ambayo yanahitaji washauri wazuri wamsaidie ili abadilike otherwise 2015 hataweza kusimama jukwaani watu wamsikilize tena..ataishia tu kwenye jimbo lako na akicheza hata jimbo lake CCM itachukua kiulaini!!
 
kama hayo maneno Zitto kayaongea Bungeni inaonyesha kabisa hekima yake ni ndogo sana

Historia inaonyesha kuwa hekima ya Zito si ndogo sana kama unavyosema bwana Manyanza. Yawezekana hekima na busara zake katika suala hili zimetumika upande wa pili,Upande wa kuharibu. Sasa cha muhimu hapa ni kujua malengo yake katika kauli ile kwani anajua kabisa kwamba chochote atakachoongea pale kitarushwa 'Live' nchi nzima. Kikubwa hapa ni kuangalia mahusiano yake na Chama chake na wanachama wenzake katika wakati ambapo amezongwa na mambo mengi.
Kichaa akikurushia jiwe hata kama ni kubwa sana jitahidi kulikwepa tu na kuendelea na shughuli zako. Lakini mtu mzima unayemjua kwamba anaakili timamu na busara tele akikurushia hata punje ya mchanga, lazima utafakari mara nyingi sababu ya kufanya hivyo.
Kwa hiyo suala la Zito halipo katika hekima yake, bali makusudi na malengo yake.
 
Nashukuru kuona na wewe umesikia hivyo ndugu. Maana kuna uzi nilianzisha watu wakanitukana kweli kweli na kuomba nipigwe ban. Mpaka nikahisi nilikuwa nasikiza mzimu au!!. na uzi ukafutwa!. Sijui kama na huu utakuwa na muda mrefu. Sidhani kama hapa kuna suala la Ugamba au Ugwanda. ndivyo alivyosema. Kama mtu utapigwa ban kwa kuandika ukweli humu JF basi sina haja ya kuwa member tena hapa JF.

Wasiomjua Zitto ndo watamtetea sie tunaomjua tunamfahamu nia yake, kazi aliyotumwa hajaimaliza. He is soo busy selling himself for the Presidency! He thinks he has soo many people behind him but he better think twice, He is nothing kama sio Chadema, if he thinks he is popular aache Chadema aanzishe chama chake aone kama atamanage! Anatakiwa kujibu shutuma dhidi yake, atueleze kama baada ya kujua kiasi cha 3 Bilioni kilichookolewa na Maswi kwenye mafuta bado anaendelea na msimamo wake kumtetea Mhando??? kwamba utaratibu haukufuatwa??
 
Ilikuwa ni utani tu kwa Mbunge mwenzangu tena jirani yangu na rafiki yangu. Mbunge wa chama changu. Narudia. It was a joke
Binafsi niliamini hivyo toka awali. Mie pia nilicheka sana. Unajua kwa kawaida mtu ambaye huna uhusiano naye wa karibu au urafiki huwezi kumtania. Umetudhibitishia TL ni rafiki na kamanda mwenzio katika mpambano huu.
 
Ha ha haaaa.....hasira za watu!

Tujiulize kwanza,Je kuna uhusiano kati ya akili na Mwandiko mbaya?

Wengine hatujali miandiko hata tulipokuwa tunawaandikia ma-girlfriend zetu walikuwa wakituchukulia hivyo hivyo na miandiko yetu mibaya,wasahihishaji wa mitihani walikuwa wanazingatia majibu sahihi ingawa ni vizuri kuimarisha mwandiko wako

Je,kuna uhusiano kuwa kiongozi mzuri/makini na aina ya uandishi wako? jibui ni hapana...kiongozi mzuri ni mtazamo

Matamshi kama haya Zitto ni matamshi ya kawaida tu na tuyachukulie simple.Mwandiko wa Lissu kama ni mbaya tuuchukulie simple tu kwa kuwa ni kiongozi makini.

Zitto tumchukulie simple tu,kwa kuwa kateleza kashindwa kuwa insensitive katika matamshi.Ili kuwa kiongozi makini ni lazima uwe sensitive anahitaji kujiimarisha hapa....

Lakini katika yote hayo kuhusu Lissu Zitto kadai ilikuwa utani tu.watu wana hasira kweli kweli.Sio mapovu.Lol

Mwandiko wa Lissu ni Mbaya au Msomaji wa mwandiko (Zito) ni Mbaya?
 
Back
Top Bottom