Zitto tena kachafua hali ya hewa bungeni

Rejao ni kweli anajua kazi yake afanyayo CDM.Ni mharibifu tu
 
Last edited by a moderator:
Anafikiri mwaandiko mbaya ni kigezo cha kuonyesha kuwa mtu ni incompetent. Inawezekana pia huo mchango ungempa Lissu ujiko kaona anaweza kufunikwa hivyo aka ukatilia mbali
 
jamani.... tujaribu bas kujikosoa: katika hali ya siasa za sasa, mbunge mpinzani akisema tu walau maneno mawili tofauti na ya mwenzake, watu wana tafsiri kwamba "kuna kitu". Sasa ili kuweka reccord sawa, asionekane kwamba "amedharau", wakati mwingine ni lazima awe accountable kwa watu....
Mimi mwenyewe nina muandiko mbaya...
Mweye muandiko mbaya mwenyewe, yuko fine, haja lalamika... sisi wengine sasa tunaopenda malumbano...!!
 
Wakuu,

I think we need to contibute with cool heads!,kwa hilo alilolisema Zitto kuna uwezekano wa mambo mawili,aidha kweli alimaanisha au alisema kwa utani kama ambavyo tumezoea wabunge kutaniana.The only person to tell is the one who was physically present and thanks he read his demenour!!
 
ZZK ni bomu hatari sana ktk taifa letu hili changa linalohitaji falsafa za kimapinduzi ili kuvuka hatua moja mbele ya kimaendeleo. Maana nia na upeo wake mdogo ewa mawazo umeshadhihilika wazi kwamba hana lolote ktk mapambano dhidi ya udhalimu na ukandamizi wa sirikali hii ya babamkwe wake JK.

Anakidhaifisha CDM kwa mtaji wa wapigakura wake wa kigoma na imani tuliyokuwanayo kwake before. Ila ukweli ni kwamba chama makini CDM kimeshamsoma na mbinu zake chafu. Kwa sasa Bro' huna lolote waachiye wapiganaji wengine wapambaniye ukombozi wa mali za taifa letu.
 
kama kaongea kweli basi amekosea ila nayeye ni binadamu tusimhukumu kikubwa ajirekebishe awe anaangalia anaongea wapi na kwa manufaa ya nani
 
Aiseeh ! hata mie nimeshaanga, mbona mnafanya maisha magumu hivyo ? yaani hamna hata jokes ? khaaa ! hata watengeneza nuclear kuna wakati wanaangalia cartoon network !

:biggrin1: waambie hao.. Kila wakati zitto akiongea kuna watu wanatekenyeka humu khaa!!!
 
kama hayo maneno Zitto kayaongea Bungeni inaonyesha kabisa hekima yake ni ndogo sana
 
Rejao unaheshimika sana hapa JF, lakini usitake kutuaminisha haya. Zitto ni mchumia tumbo. Kuliko na POSHO ndiko anakolalia. Huanzisha mijadala inayoonekana kuwa na mashiko lakini mashiko yakianza tu, keshapigwa LI-BUZWAGI lake kimyaaaa kama vile siyo yeye aliyelianzisha.

Fuatilia aliyoyaanzisha yameishia wapi! Haya ya akina Mkulo alikuwa anajijengea WAMHOFU ili hata akitamka dau apewe, japo amesema hana bei.

Zitto bado hajawa mzalendo kama anavyojionyesha kuwa.
Nisaidie kuhusu hiyo kauli yako hapo juu mkuu. Sidhani kama ina ukweli wowote maana nikiangalia hata posho za vikao vya bunge amezikataa. Sijui unamaanisha anapenda posho za aina gani.
 
kabla hatuja muhukumu mtoa mada na wengine mlio ona mtwambie,alipokuwa anasema hayo alikuwa kwenye mode ipi? alikuwa serious au utani wa bungeni? asije akawa alikuwa anatania sisi tunamchukulia serious...
 
this is what zitto had to respond to one of his tweet followers.

kama great thinkers hatuwezi kupoteza muda kujadili 'jokes Bungeni'

Mods kuweni serious bana. toa hii kitu, au peleka mahala pake

zitto-responds.jpg
 
Nisaidie kuhusu hiyo kauli yako hapo juu mkuu. Sidhani kama ina ukweli wowote maana nikiangalia hata posho za vikao vya bunge amezikataa. Sijui unamaanisha anapenda posho za aina gani.

POSHO za bungeni kuzikataa ni gia ya kuoneka muadilifu.

POSHO za Zitto ni NZITO sio vijisenti vya bungeni. Mengi tunayo, ila sio muda wake kuyamwaga hapa jamvini. Ila ieleweke kuwa sio mweredi.

1. Issue ya Buzwagi aliishia nayo wapio?
2. Issue ya PPF na mabilioni waliyochota wakurugenzi aliishia nayo wapi?
3............................. jazia
4. Hili la Tanesco, nalo litapita tu.
 
Wakati mwingine mnajiabisha kwa kuwa obsessed na maisha ya watu wengine. Hivi mnaujua uhusiano kati ya Zitto na Tundu na aina mbalimbali ya jokes kati yao. Unaweza kukuta wenzenu wanakumbushana story fulani iliyotokea chako ni chako nyinyi huku mnatoa nyongo tumboni. Vidonda vingine vya tumbo ni vya kujitakia!
Let Tundu be the one to complain. Tundu is smiling wewe huku unatokwa povu!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ule ulikuwa utani wa kibunge tuu,kwanza muda wake ulikuwa umekwisha na pia alitaka watu wajue kuwa kuna kawaida ya kupeana mawazo mtu anapochangia. Hakuna baya hapo.
lakini si hata kama muda wako ulikuwa umekishwa si ungekaa tu bila kutamka hayo? Wewe na Lissu pengine ni watani lakini mnataniana bungeni? Kaka nenda pole pole na wenzako mkuu
 
Haters are out..........mtajisema tu. It is a HATE that guide you

Kiukweli Zitto siku hizi wanaokuchukia wameongezeka sana.....hebu jaribu kujitizama upya uone wapi unakosea manake siku hadi siku vijana wanazidi kushuka kwenye meli yako.....tukiacha hili la Lissu kuwa na mwandiko mbaya umekuwa ni mtu usiyeeleweka .....huyu siyo yule Zitto wa zamani tunaemjua.... Zitto mtetezi wa wanyonge siku hizi anatuangusha wanyonge wake......imefika mahali tunakosa kabisa imani na wewe.......nini tatizo Mh?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom