Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

Status
Not open for further replies.

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Zitto
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma ambayo imeunganishwa kwenye tuhuma hizo, Zitto Kabwe, alisema tuhuma hizo anazisikia, lakini anaziona kama siasa za majitaka kwa sababu zinarushwa bila ushahidi wowote.

"Hakuna hata mbunge mmoja aliyesimama kusema nani amehongwa nini. Mimi binafsi sijahongwa na mtu yeyote wala mimi sijamtetea mtu isipokuwa natetea taratibu kufuatwa," alisema.

Zitto alibainisha kuwa anaamini tuhuma hizo zimetokana na hasira za yeye kupinga posho za wabunge na sasa wameona hilo ndilo eneo la kumkomoa.

"Kwa kuwa ‘my conscious is clear', (dhamira yangu safi) sina mashaka, uzushi, uongo na siasa za majitaka hizi zitaumbuliwa na ukweli. Hata hivyo, kwa kuwa tuhuma hizo zinasemwa juu juu tu, tutataka vyombo vya dola vichunguze na ikithibitika hatua zichukuliwe," alisema na kuongeza:

"Kwangu mimi naona hizi ni siasa za urais na hasira za posho. Wenye kutaka urais wa vyama vyote na wapambe wao, wameungana kunichafulia heshima yangu. Wabunge wenye njaa ya posho, wameungana kunikomoa. Ukweli una tabia ya kutopenda kupuuzwa. Mwalimu Nyerere (Julius) alisema katika andiko lake la 'Tujisahihishe'."

Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini(Chadema) alishauri pia Spika wa Bunge kutumia Kamati ya Maadili kuchunguza tuhuma hizo kwa kuwa hazipaswi kuachwa zikapita hivihivi.


Source: Mwananchi Jumapili.
 
Zitto, kujitokeza hadharani kujiingiza kwenye mgogoro wa management ya Tanesco na body kunazua maswali mengi zaidi kuliko majibu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
:yawn: Zitto hamaki ya nini kama huhusiki? Nani kasema mambo ya urais hapa. Kwani Jairo alikuwa anagombea urais alipolipuliwa last year. Mama Lwakatare nae anagombea urais?

Tumekujua, una mikono michafu. Usicheze na sisi!
 
Zitto kama mwananchi imekunukuu sahihi basi umeshakwisha wewe ni mlafi wa madaraka na asilani usiye na shukrani na pia huna busara za kuwa rais haiwezekani ukatumia fallacy kubwa namna hiyo ya haste generalization eti wote wanaopinga wanaoutaka urais kutoka vyama vyote wewe kwa membe, prof lipumba, slaa, lowassa bado ni kinda kisiasa.

Hata jimbo lako linakushinda ndio useme kwamba wewe uko kwenye seat za mbele za urais acha utoto kuwa mtu mzima sasa. Ila kama mwananchi imekunukuu sahihi umekosa kura moja mwAndiga
 
Ktika hali isiyokuwa ya kawaida wachaga waliop chadema wameungana na wabunge wapenda posho wa ccm ili kumuadabisha Mh zuberi zitto, yote hayao yametokana na mambo makuu mawili;

1.Zitto kukataa posho na kuendelea kutozichukua mpka leo, wahafdhina ndani ya chadema wameona wanaaibika hasa baada ya mbungewa iramba mwigulu kuwachana ukweli, kma hiyo hitoshi wabunge wengi wa chadema ambao ni wa kaskazini waliingia kwenye chama na lengo lake likiwa ni kupata pesa , walitumia mbinu nyingi sana kumharibia zitto reputation yake ndani ya jamii na nje ya siasa ili aonekane yeye amehongwa au alikuwa na ubia na mhando wa tanesco.

2.Kitendo cha zitto kutangaza kugombea urais 2015 kiliwastua sana wachaga kiasi cha kutengengeneza mkakati wa kummaliza kwenye medani za siasa kwa kushirikiana na ccm, ikumbukwe kwenye maswala ya ukabila wachaga huweka nje itikadi zao, na hiyo kazi alipewa selasin amabaye uhusiano wake na wachaga wenzio haupo na alizungumza vitu vingi sana
Kama CHADEMA wataendelea na huu ujinga 2015 chma hakifiki na hata kikifika ccm wameshajuwa mahali pa kuwamamlizia ni juu ya urais na posho pekee yake.

Mnyika ambaye yeye daiama ni mnafiki huwa anazungumzia hilo chini ya meza na maelezo yake niliyoyapata kwa njia ya kiintelejensia nitayaweka very soon baada ya secretary wangu kumalaiza kuyatype. Kafulila alisema CHADEMA ni ya wachaga na wewe ukijifanya ni yako wako tayari kukuharibia kwa gharama yoyote ile
 
huu ndo upande wa pili wa zitto tuliokuwa hatuujui kila siku anazidi kupoteza point katika ulingo wa siasa
 
Zitto tulia acha papara. Kuongea sana hakuleti tija. Kila jambo linawakati wake. Hakuna aliyesema posho au urais. Acha kutuangusha.
 
Jamani tusimshambulie sana ZZK hayo ni yake ameyaonge sasa tusubiri uchunguzi utakapo fanyika tutajua na hapo tutatoa maneno yetu yote ya kumkashifu ZZK kama atakuwa amehusika, na mara nyingi kwenye ukweli uongo ujitenga tuvute subira
 
Zitto, kujitokeza hadharani kujiingiza kwenye mgogoro wa management ya Tanesco na body kunazua maswali mengi zaidi kuliko majibu.

Mwananchi na Zitto naona mnatengezeana habari!!mwisho wa unafiki na uroho wa kisiasa ni aibu na kufirisika kisiasa,watch out Mr. Zitto,kiongozi wa watu alazimishi kupendwa na watu au kua kiongozi!kiongozi wa watu ni yule anaependwa na watu kwa ridhaa ya watu na kuombwa kuwaongoza watu!!unakataa posho bungeni kumbe unapokea hela za kifisadi
 
Ktika hali isiyokuwa ya kawaida wachaga waliop chadema wameungana na wabunge wapenda posho wa ccm ili kumuadabisha Mh zuberi zitto, yote hayao yametokana na mambo makuu mawili
1.Zitto kukataa posho na kuendelea kutozichukua mpka leo, wahafdhina ndani ya chadema wameona wanaaibika hasa baada ya mbungewa iramba mwigulu kuwachana ukweli, kma hiyo hitoshi wabunge wengi wa chadema ambao ni wa kaskazini waliingia kwenye chama na lengo lake likiwa ni kupata pesa , walitumia mbinu nyingi sana kumharibia zitto reputation yake ndani ya jamii na nje ya siasa ili aonekane yeye amehongwa au alikuwa na ubia na mhando wa tanesco
2.Kitendo cha zitto kutangaza kugombea urais 2015 kiliwastua sana wachaga kiasi cha kutengengeneza mkakati wa kummaliza kwenye medani za siasa kwa kushirikiana na ccm, ikumbukwe kwenye maswala ya ukabila wachaga huweka nje itikadi zao, na hiyo kazi alipewa selasin amabaye uhusiano wake na wachaga wenzio haupo na alizungumza vitu vingi sana
Kama CHADEMA wataendelea na huu ujinga 2015 chma hakifiki na hata kikifika ccm wameshajuwa mahali pa kuwamamlizia ni juu ya urais na posho pekee yake
Mnyika amabye yeye daiama ni mnafiki huwa anazungumzia hilo chini ya meza na maelezo yake niliyoyapata kwa njia ya kiintelejensia nitayaweka very soon baada ya secretary wangu kumalaiza kuyatype
Kafulila alisema CHADEMA ni ya wachaga na wewe ukijifanya ni yako wako tayari kukuharibia kwa gharama yoyote ile

yaani umejiunga specific kujibu hoja hii ama?ukibaraka huo..Zitto hata iweje hawezi kuwa rais ...tna uzoefu na dini anayotoka zitto kuwa haitoi viongozi makini..so aendelee tu na ubunge au awe rais wa kikundi cha wasaniii wa kigoma-leka tutigite
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom