ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
Swali ni je, Zitto amewasiliana na Spika officially kumwambia haya kimaandishi? Isije kuwa umaarufu search kwenye facebook tu...
Bunge linatunga sheria lenyewe kisha lenyewe linazikiuka. Makinda ana masuali ya kujibu kwa wananchi, yeye yupo juu ya sheria?
Swali ni je, Zitto amewasiliana na Spika officially kumwambia haya kimaandishi? Isije kuwa umaarufu search kwenye facebook tu...
Swali ni je, Zitto amewasiliana na Spika officially kumwambia haya kimaandishi? Isije kuwa umaarufu search kwenye facebook tu...
Zitto anasema from facebook
" Spika wa Bunge anajua kwamba posho zote hulipwa Baada ya Rais kuidhinisha. Posho anazotangaza hazijaidhinishwa kwani uthibitsho wa kuidhinisha ni Masharti Mapya ya Kazi kwa Wabunge ambayo hayajatolewa na Ofisi ya Rais. Hivyo kitendo cha kuanza kulipa posho mpya bila Masharti Mapya ya kazi za Wabunge ni kukiuka sheria ya utawala wa Bunge kifungu cha 19.
Tume ya Bunge inapaswa kuwajibika kwa kutumia vibaya mamlaka yake, posho mpya zifutwe na zilizolipwa zirejeshwe mara moja kwani zimelipwa kinyume na sheria.
Spika anapaswa kuheshimu sheria ambazo Bunge limepitisha na kwenda kinyume na sheria kwa makusudi ni kosa la kuvuliwa Uspika.
Wabunge wasifanye mchezo na suala la posho. Wananchi wamekasirishwa sana na kwa kweli hatuwaelewi. Wakati Bunge la Tisa lilisifika kwa kupambana na ufisadi, Bunge la kumi litabatizwa Bunge la Posho. Ni lazima tukatae kuonekana tunajijali badala ya kujali wananchi.
Namsihi Spika aachane kabisa na suala hili la posho. Tukazane kukuza uchumi wa nchi ili wananchi wapate ajira, kodi iwe nyingi na tuongeze mishahara kwa wafanyakazi wote. Hoja ya ugumu wa maisha ni kwa wananchi wote sio wabunge peke yao.
Jambo la kuzingatia kwa sasa ni kwamba, iwapo posho hizi zitalipwa kwa wabunge, nini kitazuia posho Kama hizo kulipwa kwa wabunge wa Bunge Maalumu la katiba? Huo mzigo serikali itaubeba namna gani na Hali hii ya uchumi?
Wabunge tujielekeze katika kukuza uchumi, kuongeza uzalishaji viwandani, mashambani na kwenye shughuli nyingine za huduma za kiuchumi. Tuachane na fikra za posho."