Zitto: Serikali ya JK katika hali mbaya kifedha; Mkulo Akanusha!

Babu Lao

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
2,043
179
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alidai kuwa hali hiyo mbaya fedha kwa Serikali imesababisha watumishi wake pamoja na wabunge kutolipwa mishahara hadi jana Mei 7, 2011.

Akizungumza na wananchi Vwawa katika Jimboni Mbozi Mashariki katika viwanja ya ofisi ya Afisa Mtendaji, Zitto alisema Serikali sasa inatafuta fedha za kuwalipa watumishi wake mishahara ya mwezi Aprili.


"Hata sehemu ya posho za wabunge mkutano uliopita, zikiwemo za kugharamia mafuta ya safari za wabunge majimboni bado hazijalipwa kutokana na Serikali kukosa fedha," alidai Zitto.


Alisema kutokana na hali hiyo Serikali imekwenda kukopa
Sh540 bilioni kutoka benki za ndani ili watu wasijue kuwa inakabiliwa na ukata.

"Serikali haikopi fedha ili ijenge bandari, viwanda au kugharamia miradi ya maendeleo,
bali inakopa ili ilipe mishahara ya wafanyakazi," alisema Zitto.

Angalizo:
Kama ndio mwaka wa kwanza tu mambo yamekuwa hivi, ikifika 2014 itakuwaje? Na kama haina hata hela za kulipa mishahara tu je hiyo miradi itawezekana kweli?
 
Kama mishahara iliyopo inashindikana itawezaje kuongeza mishahara kwa wafanyakazi.
 
Tatizo hilo sio la leo, tangu wafadhiri wa utegemezi wapunguze bajeti yao kwa mkweli!

Inasikitisha sana, kama Salma anakwenda Amerika na kuwapiga longolongo na kupewa 45bl na mtoto wao Riz1 anachukua tenda ya kuuza magari ya kifahari kwa King Mswat, Omar Bongo, Kabila, na marais wingi wa Afrika halafu leo kuna mfanyakazi hajalipwa mshahara tangu Machi?
 
hata kauli ya waziri fedha mkulo katika gazeti la mwananchi jumapili si ya kauli fasaha ya kujibu madai ya zito bali ni ya kisiasa zaidi
 
Duh, hii ni hatari. Hivi ni kitu gani kilichotokea ambacho ni tofauti na enzi ya BWM katika ukusanyaji wa mapato?

Matumizi yamekuwa makubwa kuliko wakati ule? Mahitaji ya serikali yamebadilika na kuwa ya ghali zaidi? Usimamizi mbovu wa mapato? Majukumu mazito yanayohitaji maamuzi yenye maslahi kwa taifa yamo mikononi mwa vilaza?

Kwa nini tusidadisi awamu ya tatu walikuwa na mikakati gani ya ukusanyaji wa mapato ya taifa tofauti na sasa?
 
Kama mishahara iliyopo inashindikana itawezaje kuongeza mishahara kwa wafanyakazi.

Hapo ndio utata unapojitokeza kama hela za mishahara tu hakuna, je hiyo nyongeza itatoka wapi!!
 
kwani si tulishakanywa kuongozwa na CCM will be another disaster natabiri tena huu utawala hautafika mwisho bila ya vurugu

Kweli kabisa kwa huku tunakoenda ni wazi kuwa miaka mitano haitoisha bila kutwangana!!:A S cry:
 
Hayo ndiyo maisha bora kwa kila Mtanzania tuliyo ahidiwa.

Lakini sasa ndio tujifunze jinsi ya kuchanganua mbivu na mbichi, kama vile naiona miradi yote ya maendeleo itakavyokwama!!!
 
hata kauli ya waziri fedha mkulo katika gazeti la mwananchi jumapili si ya kauli fasaha ya kujibu madai ya zito bali ni ya kisiasa zaidi

Kweli serikali ya kisanii niya kisanii tu.. majibu ya Mkulo "Serikali haiwezi kujibu tuhuma za mitaani za Chadema ambao wana ajenda yao ya mitaani ambayo wataendelea nayo. Serikali inashughulika na masuala ya wananchi na itajibu maswali yao kuhusu matatizo yao na serikali kupitia bajeti ya mwaka huu."

Swali ni kwamba hayo masuala ya wananchi ni yapi kama uhakika wao na familia zao kuishi?
 
Ahaaaaaaa,...
kumbe ndo maana wanavyuo wana cheleweshewa hela kwa
ngonjera za system haifanyi kazi vizuri eh?

sijui week ijayo itakuaje vyuoni
 
Du! Hii ni hatari kweli, Tatizo viongozi wetu sisi sisiem wana tabia kama ya "baba" anayependa kuoenekana mwenyenazo wakati uwezo hana. Kila siku wanakesha angani ka popo, kutembelea magari ya kifahari wakati uwezo halisi ni bajaji.
 
Duh, hii ni hatari. Hivi ni kitu gani kilichotokea ambacho ni tofauti na enzi ya BWM katika ukusanyaji wa mapato?

Matumizi yamekuwa makubwa kuliko wakati ule? Mahitaji ya serikali yamebadilika na kuwa ya ghali zaidi? Usimamizi mbovu wa mapato? Majukumu mazito yanayohitaji maamuzi yenye maslahi kwa taifa yamo mikononi mwa vilaza?

Kwa nini tusidadisi awamu ya tatu walikuwa na mikakati gani ya ukusanyaji wa mapato ya taifa tofauti na sasa?

Kwa kuangalia tu walitoka watendaji sasa wameingia wezi na wasanii, mwizi siku zote atatumia kile kidogo alichokuta, anadanganya watu ili wasistuke, hakusanyi kodi na amekalia mambo ya anasa tu badala ya maendeleo!!!
 
Ahaaaaaaa,...
kumbe ndo maana wanavyuo wana cheleweshewa hela kwa
ngonjera za system haifanyi kazi vizuri eh?

sijui week ijayo itakuaje vyuoni
Na hayo mabenki yakistuka, wanafunzi ndo wasahau!!
 
Srikaili ya jk ilipoingia madarakani ilikuta fedha za kutosha hazina; tofauti na BWM alikuta hazina haina fedha na madeni kibao. Tatizo la jk na serikali yao waliendekeza sana kutumia bila kujali namna ya kuongeza kipato cha serikali (mapato).

Baada ya kuona jk huyooooooooooo majuu kila uchao, wajanja nao wakajua kujilimbikizia mali ni wakati huu (mi kwapuo/michoro). Sasa hawana fedha, sijui miradi kibao ya maendeleo itatekelezwaje iliyoahidiwa wakati wa kampeni za uchaguzi na usitawi wa wafanyakazi... basi tusubiri!!
 
Kwenye Mei Mos JK aliiweka kapuni hii inshu ya nyongeza za mishahara.... I think this is the secret behind!!

Mi hamu yangu kubwa ni kuona wafanyakazi wanagoma!!yaani ikitokea hili, maisha yatabadilika kwa kasi sana!!

I can't wait for this... nadhani mliona SA ilivyokuwa! Mgomo wa wafanyakzi ndio mpango nzima
 
Hapa ndipo utaona tofauti kati ya JMK na BWM, hotuba ya Mkapa tuzo za TASWA ilikuwa ni kuwakumbusha watz umuhimu wa kukusanya kwa ajili ya kufanya vitu vya maendeleo kwa umma.

Mkapa aliamua kutokopa katika mabenki ya ndani ili taasisi hizi ziwakopeshe watz, leo kikwete ameanza kukopa katika mabenki ya ndani na hivyo kubana mikopo kwa watanzania (benki zinapenda kufanya kazi na serikali kwa kuwa kuna uhakika wa kulipwa kwa faida kubwa).

Unaposhindwa kubuni mikakati ya kukuza uchumi mkubwa na unapoamua kukopa kwa ajili ya kazi zisizo za maendeleo ni hatari sana kwa uhai wa taifa kwani kila mtz anabandikwa deni ambalo hakulikopa.

JK badilika rais wangu jua linakuchwa
 
ZITTO ADAI INAKOPA HATA MISHAHARA YA KUWALIPA WAFANYAKAZI

Boniface Meena, Mbeya na Exuper Kachenje

VIONGOZI wakuu na wabunge wa Chadema jana waliushambulia mkoa wa Mbeya kona zote kwa mikutano ya hadhara iliyofanyika katika majimbo kadhaa ya uchaguzi ya mkoa huo.

Akiwahutubia wanachama wa Chadema na wananchi wa mjini Vwawa, Mbozi jana, Naibu Katibu Mkuu chama hicho, Zitto Kabwe, aliifyatuli kombora zito Serikali ya Rais Jakaya Kikwete akidai kuwa ina hali mbaya kifedha kwa sasa, hata mishahara ya kulipa wafanyakazi inakopa.


kwa habari zaidi...............

Source gazeti la mwananchi la tarehe 8/may/2011 .
 
Back
Top Bottom