Zitto: Nitagombea Ubunge 2010

Ni lipi la kifisadi aliloliibua Zitto ambalo wengi mnadhani ni wa muhimu kiasi hicho yeye kuwepo BUNGENI? Au ni ule ubishiubishi wake wa watu wa KIGOMA kama akina KADUGUDA wa Simba?

Michango yake inaeleweka. Kuibua hoja za ufisadi sio umihimu wa kuwepo bungeni.

Je atagombea ubunge tena? Wapi?
 
Kama kweli Kulikoni waliandika kuwa Zitto atagombea "Jimboni mwake" (wakimaanisha Kigoma Kaskazini) basi watakuwa wamekosea, si huko tena! Lakini, muda muafaka ukifika atakuja 'mwenyewe' ndani ya JF kuwafahamisha ni Jimbo gani atagombea na sababu hasa za maamuzi yake.
Very good, agombee tu hata hapa Dar, nadhani atasaidia kero nyingi za jiji hili, argh!
 
Ni lipi la kifisadi aliloliibua Zitto ambalo wengi mnadhani ni wa muhimu kiasi hicho yeye kuwepo BUNGENI? Au ni ule ubishiubishi wake wa watu wa KIGOMA kama akina KADUGUDA wa Simba?
Fuatilia ansadi za bunge utajua hayo unayoyauliza
 
Michango yake inaeleweka. Kuibua hoja za ufisadi sio umihimu wa kuwepo bungeni.

Je atagombea ubunge tena? Wapi?
Hana mchango wowote wa maana. Ubishi wake ule umemsaidia kuingia /kuteuliwa kwenye tume/kamati mbalimbali za ulaji. Nasikia atagombea kwenye jimbo mojawapo la Dar Es Salaam. Anawambia washikaji wake wa karibu kuwa majimbo ya Dar yamekaa kitaifa zaidi ambayo anadhani ndio hadhi yake. Yeye ni Mbunge wa Kitaifa zaidi. Haelewi kuwa mbunge wa kitaifa ni RAIS wa nchi peke yake.
 
Lakini Karamagi mwenywe yuko hoi ofisi aliiachia.
Na sasa anasubiri kuzikwa kwao Bukoba 2010:D
 
Ni lipi la kifisadi aliloliibua Zitto ambalo wengi mnadhani ni wa muhimu kiasi hicho yeye kuwepo BUNGENI? Au ni ule ubishiubishi wake wa watu wa KIGOMA kama akina KADUGUDA wa Simba?

My Goodness! Duu kazi kweli kweli.
 
Hivi kuna ukweli na haya 'Matamshi ya wakuu' ?
Rorya?

Ni kweli mimi binafsi nimezungumza naye Biharamulo na akanieleza kuwa atagombea, na kwamba msingi wa kauli ile ulikuwa wa dhati lakini baada ya kupatra ushauri kwa watu wengi ikiwemo michango ya wana JF ameamua kugombea tena na Jimbo lake ni lilelile wala siyo KAWE kama wanavyoeleza watu.
Nilimuomba pia atoe ukweli huo hapa JF na akaeleza angefanya hivyo.
 
Nothing new.... mshahara wa 10,000,000 sio mchezo.

Talk abt staki nna taka!

Sioni tatizo ukilipwa hela hizo na kuchangia hoja za maana. Sikitika kwa ajili ya wale wanaofika na kulala bungeni bila michango na wakichangia ni pumbaaaaa...................
 
Hawa wanasiasa bwana! Zitto aseme kwenye forum hii ili mamemba tumafagilie kikwelikweli.

Anyway, at his tender agee and demonstrated youthfullness it is, kwa baadhi ya watu, unthinkable that he will quit politcs just when he has only just begun.
 
Spika amesema Zitto hajakosea kusema mawaziri wanatoa majibu ya ovyo ovyo ila alikosea kukaidi maagizo ya "kiti" cha aliyekuw Mwenyekiti wa Bunge, Zubeir Ali Maulid
 
Hana mchango wowote wa maana. Ubishi wake ule umemsaidia kuingia /kuteuliwa kwenye tume/kamati mbalimbali za ulaji. Nasikia atagombea kwenye jimbo mojawapo la Dar Es Salaam. Anawambia washikaji wake wa karibu kuwa majimbo ya Dar yamekaa kitaifa zaidi ambayo anadhani ndio hadhi yake. Yeye ni Mbunge wa Kitaifa zaidi. Haelewi kuwa mbunge wa kitaifa ni RAIS wa nchi peke yake.

Ubishi wake ndio 'ulimbwende wake'... ni sifa!

Ubunge wa kitaifa? Si achaguliwe kiti maalum basi... kuna Utaifa hapo!

Mchango wake uheshimiwe.
 
Zitto Z Kabwe ni miongoni mwa wabunge wachache walikuwa wakinikosha roho kwa msimamo wake wa kupigania haki,usawa na maslahi ya taifa.Lazima niseme kweli baada ya lile sekeseke la Dowans Zitto amenitoka kabisa simwamini hata kidogo huyu mheshimiwa alivyoyumba katika jambo lililowazi kabisa ni ishara mbaya kwa watanzania kumwami katika siku za usoni.

Mheshimiwa Zitto alionywa sana hapa jamvi asikurupuke kusabikia Dowans lakini kwa jeuri na kiburi bado aliendelea kuwa mpiga debe wa Rostam Azziz na mitambo yake iliyopitwa na wakati.Kwa kuunga mkono ufisadi uliowazi kama wa Dowans kunanifanya nisimwamini tena kijana wetu Zitto.

Mheshimiwa Zitto kabwe kugombea ubunge Dar au Kigoma kwangu mimi nachukulia uamuzi wake kama mkakati wa kuendelea kuganga njaa kama ilivyo kwa wabunge wengi wa CCM.

Mheshimiwa Zitto hata baada ya kuchemsha bado alishindwa kuomba radhi watanzania waliomwamini sana.Huu ni udhaifu mkubwa ambao kama Mheshimiwa Zitto asipojirekebisha unaweza kumwondoa katika medani ya siasa.
 
Ni kweli mimi binafsi nimezungumza naye Biharamulo na akanieleza kuwa atagombea, na kwamba msingi wa kauli ile ulikuwa wa dhati lakini baada ya kupatra ushauri kwa watu wengi ikiwemo michango ya wana JF ameamua kugombea tena na Jimbo lake ni lilelile wala siyo KAWE kama wanavyoeleza watu.
Nilimuomba pia atoe ukweli huo hapa JF na akaeleza angefanya hivyo.

Kwahiyo bado ataendelea na 'Jimbo' lake Kigoma?
 
Kama kweli Kulikoni waliandika kuwa Zitto atagombea "Jimboni mwake" (wakimaanisha Kigoma Kaskazini) basi watakuwa wamekosea, si huko tena! Lakini, muda muafaka ukifika atakuja 'mwenyewe' ndani ya JF kuwafahamisha ni Jimbo gani atagombea na sababu hasa za maamuzi yake.

Kama ulivyosema, hata hao KULIKONI hawakusema atawania jimbo gani na wamemnukuu akisema kupitia mtandao wa Bidiiforum "Baada ya kutafakari sana na kuzingatria changamoto za nchi kuelekea uchaguzi wa 2010. Na Hasa hasa, narudia hasa hasa kipindi cha 2010 mpaka 2015, nimeamua kuwa NITAGOMBEA UBUNGE uchaguzi ujao! Inshaalah Mungu anipe uhai."
 
Kama kweli Kulikoni waliandika kuwa Zitto atagombea "Jimboni mwake" (wakimaanisha Kigoma Kaskazini) basi watakuwa wamekosea, si huko tena! Lakini, muda muafaka ukifika atakuja 'mwenyewe' ndani ya JF kuwafahamisha ni Jimbo gani atagombea na sababu hasa za maamuzi yake.

Mmh! kwa nini asigombee tena jimboni kwake? nadhani jibu ni kwamba ameshindwa kutatua shida za watu wa jimboni kwake.Mimi hawali nilipo sikia kuwa hatagombea tena niliona amefanya jambo la busara sana kwani kazi aliyopewa na wananchi wa jimbo lake imemshinda,hivyo ingekuwa vigumu sana kukubalika kwenye jimbo hilo tena...

Juzi baada ya kusikia hizi habari mpya kuwa atagombea tena nilipata wasi wasi kidogo kuwa atakuwa na wakati mgumu sana kulichukua hilo jimbo kwa mara ya pili.Kama ulivyo sema Invisible kuwa sio jimboni kwake tena,hapo amecheza.Unajua mh.Zitto na umerufu wake wote bungeni na nje ya bunge,ameshindwa kabisa kuwaletea mabadiliko yoyte watu wa jimboni kwake.Zitto siasa zake ni za jukwaani tu na si vinginevyo.
 
Hivi mnaosema hajafanya kitu jimboni kwake mna uhakika? Nadhani waulizeni watu vijiji vya Bitale, Mkongoro, Matyazo, Kalinzi n.k ndiyo wako kwenye position nzuri zaidi ya ku-judge kuliko kumhukumu kupitia vyombo vya habari.
 
Mugo"The Great";518797 said:
Hivi mnaosema hajafanya kitu jimboni kwake mna uhakika? Nadhani waulizeni watu vijiji vya Bitale, Mkongoro, Matyazo, Kalinzi n.k ndiyo wako kwenye position nzuri zaidi ya ku-judge kuliko kumhukumu kupitia vyombo vya habari.

Nimekupata mkuu 'MUGO',

Watu wasiandikie mate.......
 
Back
Top Bottom