Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,883
- Thread starter
- #101
Niliwahi ona video sehemu katika simu ya mtu..Gesture yake jukwaani wakati Mr II a kiperfom pale Arumeru katika kampeni za Nassari haikuwa nzuri.Hasa pale watu walipokuwa wamshangilia sana mh II wakija jukwaani kuwashika mikono makamanda.Zitto alionyesha dharau n akutokubaliana na hali ile ya kukubalika kwa Mr. II.Zitto alikuwa dettached sana na watu emotionally,hata yeye mwenyewe akiangalia video yake kama CDM wanazo ataona hili.
Ilikuwa hali ya kuhofia kuwa siyo pekee tena katika CDM+ ilikuwa hali kama vile wale watu si waelewa sana na zile shamrashamra na hisia ni za kipuuzi na si worth it.
Mheshimiwa usihofu kwani mimi ndivyo nilivyo nisione kitu.Kwani mara nyingi attention yangu kwa vitu vidogo ipo karibu sana.Ni mheshimiwa tuu akaangalie vizuri video za mikutano ya pale user river.Niliona hofu kama ya mtoto anayokuwa nayo anapozaliwa mdogo wake.Hii nilikuja thibitisha bunge lilipoanza Zitto alikuwa naive sana kuuliza maswali ya nyongeza kabla ya kuja stabilize baadaye.
Hilo nalo Nicholas ni jambo la kuangalia sana katika safu ya uongozi. Kuna udhaifu ambao viongozi wengi Tanzania katika siasa na hata sekta binafsi mmoja wapo au baadhi wanapofanya mambo mazuri au kuwa na dalili ya kuvutia hadhara hugeukwa kuwa adui kwa wale wanaotafuta kuonekana pekee ndio wajulikane. Kasoro hii inatokana na ubinafsi (selfishness, self-esteem, etc). Tunapokuwa na mmoja tu wa kumpitisha bila kupingwa kwa sababu ya kukosa mshindani au washindani wa kuwashindanisha katika nafasi hiyo, matokeo tunayajua, mambo haya siyapendi. Bora tuwe na wengi, anayepenya awe kweli amechujwa kwa kiwango cha mategemea kuwa atakuwa na kiwango cha uongozi.
Matokeo ya viongozi wa aina hii ni kutafuta zaidi popularity kwa wananchi badala ya uwajibikaji wa kweli. Tunaposhabikia popularity kwa viongozi badala ya kuangaliwa uwajibikaji ndipo jipu linapokuja kupasuka wakati wamepenya kwa popularity na kisha kuishia kuwa watalii muda wote wa uongozi wao.
Tusisubiri kipindi cha uchaguzi, tuwachambue sasa hivi, na wale wanaoona tunaonyesha kasoro nyingi ambazo zinaweza kuwakosesha sifa za uongozi watazifanyia kazi ili waingie kwenye ushindani wa kweli na wakiibuka ni kutokana na ukweli wa utendaji wao.
Tukumbuke daima usemaji mwingi mjengo si kiwango halisi cha uwajibikaji. Kikwete ninavyomkumbuka alivyookunjua kucha zake na kuvalia njua suala la hayati Kighoma Malima na kusababisha kujiuzuru uwaziri wa fedha, si Kikwete huyu wa leo, kwa nini? Hatukuangalia mambo mengi katika uwajibikaji, ila tuliangalia jambo moja moja tu kama ndio kigezo cha kuongoza nchi.