Zitto Naibu katibu Mkuu hata vikao vya chama anaadimika?

MwanaHALISI limegundua.Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya idara hiyo zinaeleza kuwa vigogo hao wana mahusiano ya karibu na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe.
Anayetajwa rasmi kuwa na mahusiano na Zitto ni Naibu Mkurugenzi wa TISS, Jack Zoka.
Kufichuka kwa taarifa za kuwapo “uswahiba” kati ya Zoka na Zitto kumekuja katika kipindi ambacho CHADEMA kimekuwa kikituhumu maofisa wa juu wa usalama wa taifa kuvuruga uchaguzi mkuu uliopita.
Aidha, kuibuka kwa tuhuma hizi kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuchapisha taarifa mbalimbali za mawasiliano kati ya Zitto na Rais Jakaya Kikwete.
Baadhi ya mawasiliano hayo, ambayo Zitto ameyapeleka kwa rais, aliyapeleka pia kwa baadhi ya watuhumiwa ufisadi nchini.
Kwa mujibu wa mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ambaye alitangazwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Kikwete; viongozi wa TISS walihusika, kwa kiasi kikubwa, katika kile alichoita, “Kuchakachua matokeo ya uchaguzi.”
MwanaHALISI limefanikiwa kupata rekodi ya mshororo wa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka.
Kuna mwingiliano wa simu za mdomo na maandishi (sms) kutoka kwa Zitto kwenda kwa baadhi ya vigogo wa ngazi ya juu serikalini na TISS, hasa Zoka.

Nyaraka za mawasiliano zinaonyesha kuwa Zitto amekuwa akiwasiliana na naibu mtendaji mkuu wa TISS huyo zaidi ya mara tatu kwa siku.
Kwa mfano, Zitto na Zoka walifanya mawasiliano ya simu mara tisa hapo tarehe 8 Agosti. Simu iliyotumika katika mawasilino hayo, ni Na. +255756809535 ambayo hutumiwa na Zitto na +255754787550 ambayo hutumiwa na Zoka.
Wakati mawasiliano hayo yanafanyika, Zitto alikuwa katika maeneo tofauti.
Mawasiliano ya kwanza kati ya Zitto na Zoka yalipokuwa yanafanyika, simu ya Zitto ilisomeka kuwa alikuwa katika maeneo mbalimbali.
Mathalani, wakati mwingine simu ilikuwa ikisomeka kuwa yuko Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam, Kigoma Urban (Mjini), Kigoma Rural (Vijijini), Mtwara, Uwanja wa ndege-Ilala, Oyster Bay, Ukonga, Upanga na katikati ya mji.
Gazeti hili halikuweza kugundua mara moja undani wa mawasiliano ya Zitto na Zoka.
Kinachofanya baadhi ya wachunguzi wa mambo kujenga shaka ni kwamba mmoja ni mwanasiasa, tena kutoka chama kilichopo nje ya utawala; na mwingine ni mtumishi wa idara ya usalama inayolalamikiwa kukandamiza upinzani nchini.
Hata hivyo, taarifa zinaonyesha kuwa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka yalianza kupamba moto kuanzia tarehe 6 Agosti 2010, siku moja baada ya CHADEMA kuzindua kampeni zake za urais.
Kulingana na uchunguzi, siku hiyo, tarehe 6 Agosti, simu ya Zitto ilisomeka kuwa yuko Kigoma Urban.
Katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni, CHADEMA kupitia kada wake mashuhuri, Mabere Marando, iliibuka na lundo la tuhuma dhidi ya vigogo kadhaa wa serikali, CCM na idara ya usalama wa taifa.
Akizungumza na maelfu ya wananchi katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, Marando alisema wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu ya taifa (BoT), ulifanywa na serikali na washirika wake.
Miongoni mwa vigogo aliodai kuwa walihusika kufanikisha wizi huo, ni rais wa sasa, Jakaya Kikwete, rais mstaafu Benjamin Mkapa, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Edward Lowassa.
Akiongea kwa kujiamini, Marando alisema, “fedha za EPA ni wizi uliotiwa baraka na serikali ya CCM na ndio uliomsaidia rais Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005.”
Kuanzia hapo hadi sasa, Zitto na Zoka wamekuwa na mawasilino ya mara kwa mara, na karibu kila siku huzungumza kwa simu.
Mawasiliano mengine ya mara kwa mara yalifanyika tarehe 7 Agosti 2010, siku mbili tangu hotuba kali ya Jangwani. Yalianza saa 10:17 na kuendelea tena saa 10:50, saa 10:51:31, saa 11:46:13, saa 12: 14:46, saa 12:26:48 na saa 13:50: 21.
Lakini Zitto alipoulizwa kuhusu sababu ya yeye kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na vigogo wa TISS, alisema hajui na hakumbuki lolote kuhusu kuwapo mawasiliano hayo na Zoka au mkuu yeyote wa idara hiyo.

Zitto amesema yeye, akiwa mwanasiasa na kiongozi, anazungumza na watu wengi kutoka katika taasisi na mashirika mbalimbali ndani na nje ya nchi, lakini hajui kitu kuhusu usalama wa taifa.

Alipobanwa kuhusu mazungumzo yake na Zoka, hasa yale ya 3 Novemba 2010, saa nne na dakika 56 asubuhi, siku mbili baada ya uchaguzi kumalizika, Zitto alisema, “Siku hiyo nilizungumza na watu wengi sana. Siwakumbuki ni akina nani hasa.”
Alisema, “Hicho ndicho kipindi ambacho matokeo ya uchaguzi nchini kote yalikuwa yakizuiwa ikiwamo kwetu Kigoma. Na ukumbuke mimi nilipigwa mabomu na polisi na usalama wa taifa. Nakumbuka viongozi wengi wa vyombo vya ulinzi na usalama walinipigia simu kunijulia hali na kupata taarifa ya kilichotokea,” anaeleza.

“Sasa kama Zoka naye alinipigia siku hiyo sikumbuki; lakini nilipigiwa na wengi…Naomba uniambie kitu, hivi mnachokitafuta hasa ni nini?” aliuliza.
Katika njia ya kujitetea, Zitto aliuliza, “Mwanasiasa kuongea na wakuu wa vyombo vya usalama ni kosa? Maana, hata kama ningekuwa nimezungumza naye, kosa langu liko wapi?” alieleza mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini.

Alipoelezwa kuwa haoni hiyo ni hujuma dhidi ya chama chake kwa kuzungumza na viongozi wa TISS na kile ambacho amekuwa akikizungumza kikiwa hakifahamiki kwa viongozi wake, Zitto alisema, “Sijawahi kukihujumu chama changu mahali popote, siku yoyote.”

Jitihada za gazeti hili kuzungumza na Zoka hazikufanikiwa katika kipindi chote
cha mwishoni mwa wiki, kwa vile kila alipopigiwa, simu yake ya mkononi ilikuwa haipokelewi.

Hata ujumbe mfupi wa maneno uliotumwa kwenye simu yake saa 2:53 asubuhi ya Jumapili; ukieleza sababu za gazeti kuzungumza naye, haukujibiwa.

Aidha, tarehe 2 Novemba, siku moja baada ya kuzungumza na Zitto, Zoka alinukuliwa akikana madai ya Dk. Slaa, kuwa TISS imesaidia kuvuruga uchaguzi.
Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Zoka alisema, “Dk. Slaa amekuwa akidanganywa na watu wanaojiita maofisa wa usalama wa taifa.”
Hata hivyo, kuna meseji mbalimbali kuhusu udini na uamuzi wa CHADEMA kususia hotuba ya rais Kikwete ambazo zilitumwa na Zitto kwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA ambazo zinadaiwa kuandaliwa na idara ya usalama wataifa.
Ujumbe huo unadaiwa kuandaliwa kwa ustadi mkubwa katika kukuza suala la udini na kuleta mtafaruki katika chama.
 
kwakweli hivi wnaCDM hatuna mambo mengine ya kujadili kuhusu chama zaid ya ZItto? tunajua kaenda nje kwenye mkutano sijui ni wa CPA vile sasa atawezaje kuwepo huku na huko? pia kama anaonekana ni msaliti basi mwambien kwenye vikao vya nidham vya chama na ikiweekana apewe karipio ama kufukuzwa kama akina shibuda walivyofukuzwa CCM. hivi kati ya shubuda na huyu zitto yupi huku CDM anautendaji wenye focus?

Ndugu yangu gfsonwin ninataka kukubaliana na mtazamo wako isipokuwa tu nikuweke sawa kuhusu shibuda. Hakufukuzwa ccm bali aliposhindwa kupenya kura za maoni za ubunge ndipo akaamua kucross kuja Chadema na akapewa nafasi ya kupeperusha bendera ya chama chetu.
 
Last edited by a moderator:
I'm afraid I cannot distinguish between an explanation and an excuse here.

Soon or later the excuses will dry-out, and we'll find Zitto as he really is.
 
zito ni msomi mwenye akili timamu. Hawezi kuhudhuria vikao vya kinafiki. Chama makini hakiwezi kutafuta picha za kwenye mitandao na kupoteza muda kuziangalia halafu na kutoa machozi kwa glaa uilty consiousness maana wao ndo wanawatuma watu, wakidhurika na polisi wanabaki kupiga usanii. Sasa wanalia nini?? Kama wangetii amri ya kusubiri sensa huyu mwandishi angekufa?? Ni kipi walichokiona ambacho walikuwa hawajakiona?? Mungu ataihukumu CHADEMA kwa unafiki na uzandiki. Huwezi kupoteza muda wa watu unawadanganya eti unataka kuwakomboa wakati unatafuta kula na njaa zako tu. Mshahara wa Slaa ni Mamilioni. Kwa nini asijilipe angalau hata milioni mbili tu?. Tusubiri uchunguzi wa Polisi habari itapatikana. Zitto wa watu mnamuonea bure mnamchinganisha, na hata kwenye hii jamii forum eti mnampambanisha na Slaa. Jamani acheni kuwagawa wa Tanzania. Ukwelo utawambua tu siku si nyingi. Mkamia maji hayanywi

Ahaa kweli zanzibar ni nchi kama hata sensa haikuwahusu hasa bububu ambako CCM walizindua kampeni.Zinduka ndugu acha kushadadia usiyoyafahamu.
 
Tuna mengi ya kujifunza toka kwa Mzee Madiba, kwani wachache sana wenye kuwa na moyo huo wa kuona nafasi zao kwa sasa zinawatupa mkono na kinachotakiwa ni kushika kipindi kimoja kuonyesha njia ya kupita ili wanaomfuata wasipotee njia.

Naamini kizazi cha leo inawezekana tu kama mfumo wa uongozi unabadilika kwa kutanguliza zaidi uwajibikaji na kujitolea badala ya kuzidi kuongeza mianya ya ulaji kivutio kinachokuwa urimbo kwa wengi hata kuwa tayari kuua ili mradi kulinda nafasi katika kiti chake.

Tungependa kujua kutoka kwako Zitto anakukera vipi au wewe ndiyo mwendesha propaganda za kuwahamasisha wapenzi wa CHADEMA kumchukia Zitto ili aonekane msaliti!

Kama umetumwa basi kajipange upya!
 
Kwa kuongezea yupo Colombo pamoja na spika wa bunge na ujumbe mwingine wa Tanzania

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo unaongozwa na Mhe. Spika ambaye pia ataongoza wabunge wengine kutoka tawi la CPA Tanzania ambo ni Mhe. Ziito Kabwe, Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mhe. Beatriace Shelukindo, Mhe. Hamad Rashid Mohamad na Mhe. Muhonga Ruhanya ambapo jumla ya mada 9 zinatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa katika mkutano huo

5.jpg

Kijana yupo na majukumu ya ujenzi wa taifa! Hebu tuache uchochezi!
 
Naamini hujitambui****
zito ni msomi mwenye akili timamu. Hawezi kuhudhuria vikao vya kinafiki. Chama makini hakiwezi kutafuta picha za kwenye mitandao na kupoteza muda kuziangalia halafu na kutoa machozi kwa glaa uilty consiousness maana wao ndo wanawatuma watu, wakidhurika na polisi wanabaki kupiga usanii. Sasa wanalia nini?? Kama wangetii amri ya kusubiri sensa huyu mwandishi angekufa?? Ni kipi walichokiona ambacho walikuwa hawajakiona?? Mungu ataihukumu CHADEMA kwa unafiki na uzandiki. Huwezi kupoteza muda wa watu unawadanganya eti unataka kuwakomboa wakati unatafuta kula na njaa zako tu. Mshahara wa Slaa ni Mamilioni. Kwa nini asijilipe angalau hata milioni mbili tu?. Tusubiri uchunguzi wa Polisi habari itapatikana. Zitto wa watu mnamuonea bure mnamchinganisha, na hata kwenye hii jamii forum eti mnampambanisha na Slaa. Jamani acheni kuwagawa wa Tanzania. Ukwelo utawambua tu siku si nyingi. Mkamia maji hayanywi
 
huyo mdosi nyuma ya slaa ni mzamini wa slaa na 2010 slaa alimpeleka huyo mdosi ashindane na kafulila ndipo kafulila alivyomgalagaza slaa na mzamini wake.
zitto hawezi kuhudhulia vikao vya cc vinavyoendeshwa kikoo yaani lema sio mjumbe wa cc ya cdm lakini anaingia kwa sababu ni binamu wa mbowe.
lema alikuwa mjumbe wa cc akiwakilisha wabunge wa cdm lakini toka aenguliwe ubunge amekuwa akiingia kwenye cc ya cdm kwa sababu ya undugu na mwenyekiti.
 
Kaka zomba umejawa na udini ambao hautakufikisha popote acha hizo tabia ndugu yangu hapa jamvini wewe hufai kila hoja lazima ukimbilie huko nini kinakusumbua ndugu yangu huwa nikisoma comment zako nasikitika sana halafu nafikiri hata Mods humu jamvin wanakulea sana

Sasa udini hapo ni mimi au wewe? nimesema nini zaidi hata uanzishe udini wako?
 
Kijana yupo na majukumu ya ujenzi wa taifa! Hebu tuache uchochezi!

Ni kweli alishafanya kazi yake kubwa kipindi chama kina wabunge watano na nadhani kutokana na kazi yake na misimamo yake ndio ikachangia hata idadi ya wabunge, wanachama na mashabiki wa chama hivyo basi hata hao wanaoonekana wachapakazi wa chama ni product za kijana. (kwa kifupi ni mgawanyo tu wa majukumu)
 
Mkifuatilia mtaona JK alipoingia Magogoni alipata afya fulani ya tofauti lakini ghafla suruali zilianza kumshuka na haikuchukua muda tulianza kumwona mvi zinaongezeka, sio mahala rahisi pale. Utabiri wangu ni kwamba Zitto alifurahia wakati alipokubali kwa mara ya kwanza kula hela za kuchonganisha jamii zetu, sasa kazi aliyonayo ni chungu sana. Aminini msiamini, Zitto yuko kwenye wakati mgumu sana na watu kama hawa wasipogeuka huishia ama kujimaliza au kumalizwa na utawala ulio madarakani itapoonekana anatetereka kwenye wajibu waliompatia. Msione jambo la ajabu usalama wa Taifa hao hao kummaliza Zitto mambo yatakapokuwa hayaendi kama walivyokubaliana. Kwa bahati nzuri sana muda huwa hausubiri, tuombe Mungu tuwe hai tuone mwisho wa sinema kama hizi wakati tukicheza naye kwa tahadhari.
 
Yupo nje ya nchi kwa kadri nilivyosikia kwenye majukumu ya kibunge
 
zito ni ndumilakuwili,yupoyupo tuu,hana msimamo kamili,usishangae cku mambo yakiwa mabaya zaid cdm ukasikia yuko ccm
 
attachment.php


Katika operation ya vuvuvuvu la mabadiliko, Zitto Kabwe haonekani kuandamana na makamanda wenzake, wakati akiwa Kaimu Katibu Mkuu ambaye ndiye kijana wa kuwa mstari wa mbele katika mapambano.

Isitoshe hata kikao hiki kilichofanyika Jijini Dar alitazamiwa kuwa katika picha, labda imekatwa alikaa pembeni, tukumbuke yeye ni kiongozi mwandamizi, lakini naona yuko makini kutokea katika picha za misafara ya kumsindikiza Kikwete kutalii. Hii imekaaje?

Tunahitaji Zitto aje kujibu haya, ndio uwajibikaji tunaohitaji sasa hivi. Tunahitaji viongozi wa chama wanaowajibika kwa chama na wananchi chama tunachotegemea kuchukua dola, na hivi kujihakikishia viongozi watakaowajibika kwa wananchi na wananchi wawe na haki ya kuwajibisha wasipowajibika kiutendaji.

Kiongozi anayefanya kazi kwa ujanjaujanja na kukwepakwepa magumu ni hatari kwamba siku yakitokea magumu anaweza kuwatelekeza wenzake na hata kukitelekeza chama chake.

kwa mtoa hoja hii .ukileta habari kamilisha .kama Zito hajahudhuria cc .je yupo wapi ??? .alafu ndio tiririka ,maana kidogo unatupa wasiwasi .usikute unafanya inside job kwa niaba ya .unajua mwenyewe
 
Swali la kuuliza ni je, katika mkutano wa kamati kuu Godbless Lema anakaa meza kuu kama nani?

Anajaribu kuendelea kujiweka mbele kutest labda zali la mentally litarudi tena 2015 wakati ameyamwaga mwenyewe kwa mambo yake ya hovyo yasiokuwa na busara
Hajui Kama ilikuwa ni game of chance and it always never came back"
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom