Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Katika operation ya vuvuvuvu la mabadiliko, Zitto Kabwe haonekani kuandamana na makamanda wenzake, wakati akiwa Kaimu Katibu Mkuu ambaye ndiye kijana wa kuwa mstari wa mbele katika mapambano.
Isitoshe hata kikao hiki kilichofanyika Jijini Dar alitazamiwa kuwa katika picha, labda imekatwa alikaa pembeni, tukumbuke yeye ni kiongozi mwandamizi, lakini naona yuko makini kutokea katika picha za misafara ya kumsindikiza Kikwete kutalii. Hii imekaaje?
Tunahitaji Zitto aje kujibu haya, ndio uwajibikaji tunaohitaji sasa hivi. Tunahitaji viongozi wa chama wanaowajibika kwa chama na wananchi chama tunachotegemea kuchukua dola, na hivi kujihakikishia viongozi watakaowajibika kwa wananchi na wananchi wawe na haki ya kuwajibisha wasipowajibika kiutendaji.
Kiongozi anayefanya kazi kwa ujanjaujanja na kukwepakwepa magumu ni hatari kwamba siku yakitokea magumu anaweza kuwatelekeza wenzake na hata kukitelekeza chama chake.