Zitto na Wabunge, Zitto na CHADEMA, Zitto na Urais...

ZITTO SIMWAMINI TENA.
zitto yupo kinyume na chama,yupo kinyume na wapenda mageuzi.
sipendi slaa arudi tena kwa tiketi ya chadema ila heri agombee said arfi kuliko zitto hata mdee yuko vizurikuliko huyu msaliti.
 
Siku zote kosa moja huondoa mazuri 100 uliyofanya ama kutenda,huoni utaratibu wa kiutawala.Huwezi kusamehewa kosa eti kwa sababu kuna mazuri, hakuna set off hapa kiongozi lazima siku zote uwe mwadilifu.

Nafikri tatizo siyo kutokuwepo kwa watu au viongozi wa kumuonya au kumshauri Zitto bali ni je, Zitto anashaurika? Kwa akili aliyo nayo Zitto, sidhani kama hafahamu yale anayoyafanya ambayo wananchi, wanachama wa CHADEMA na viongozi wa CHADEMA hawafurahishwi au kutounga mkono. Zitto anaendelea kufanya au kwa sababu haamini kama kuna mwenye akili, uwezo na ujanja kumzidi yeye au anafanya kwa manufaa na malengo maalum. Swali la kujiulizani, Je, Zitto anapenda mabadiliko ya mifumo ya kiutawala katika nchi hii au anataka mabadiliko ya kiuongozi ambayo yatamfanya yeye kuingia kwenye uongozi? Je, Zitto anaipenda CHADEMA kama taasisi ya utetezi wa maslahi ya nchi au kama taasisi ya kuitumia ili yeye afikie kutekeleza tamaa yake ya madaraka? Je, Zitto yupo CHADEMA kwa sababu anaiamini CHADEMA kama taasisi ya mabadiliko au kama taasisi pekee anayoiamini kuwa ni rahisi kwake kufikia utimilifu wa tamaa yake? Je, Zitto ni mwanachama thabiti wa dhamira wa CHADEMA au ni mtu ambaye yupo CHADEMA kwa mpango wa muda mrefu kwaajili ya manufaa ya CCM, TISS na watawala wa CCM? Je, Zitto ana mahusiano ya karibu na wakuu wa TISS kama mtu mnafiki au yeye mwenyewe ni TISS?
 
La kufanya chama kiwe imara ni la msingi sana. Mheshimiwa alitakiwa kuimarisha chama. Anakubalika mkoani kwao. kwa mshangao wangu nilikuja kushituka sana kuona Kigomaimekuwa Ngome ya NCCR Mageuzi tena ikishikwa na vijana waliotoka chedama miezi kadhaa tu kabla ya uchaguzi wa 2010. Ofcourse, we kno the whole story. Watu wabadilike tu kama anavyosema mtoa mada. ni mapema na tunawatakie heri.
 
Labda niseme tu, hawa wenzetu baadhi yao wakifikia viwango fulani katika uongozi na wakajua kuwa wanakubalika, basi hujiweka kabisa kwenye position fulani bila kujali kuwa wananchi nao wana analysis zao, kwamba kwa uwezo huu huyu anaweza kufit wapi na huyu anafit wapi.
Kwa mfano; mh. Zito ni kijana mwenye uwezo na ushawishi mkubwa tu katika jamii yetu na kweli anakubalika, ila swali tunavyomwona sisi ( tunavyo mu-weigh) uraisi anaweza? hapo ndipo angejua anafaa au vipi, na sio habari ya kutafuta vikundi vya ulaji/vya kupeana asante ya vyeo atakapoingia kwenye nafasi. hicho ndicho kilichom-cost mzee wetu lyatonga. alikuwa mzuri lakini sio urais kama alivyojiaminisha.
mi ningewashauri pia wanaotafuta nafasi hizo za juu wawe pia wanajiuliza kuwa wananchi pia wanawaamini katika hizo nafasi? badala ya kukimbilia vikundi au magazeti kwa kuwa mwisho wa siku kuna wapiga kura basi.
 
Mimi sio mwanachama wa CDM, lakini hivi chama kinabomoka tu kwa zitto kutangaza kuwa raisi, wengine hakibomoki???
Kama CDM wanataka kuendelea vizuri waachane na tabia ya kuhamaki pale suala la zitto linapokuja mezani. Cha msingi waendelee kujenga chama itakapofika muda zitajulikana mbivu na mbichi
 
Nakuunga mkono 100% mkuu ,umeandika mambo ya msingi sana.Zitto amesemwa sana humu ila inaelekea yeye ni sikio la kufa.Makamanda walishamwandika kama mtu wenye tamaa na umimi ,walisema tabia hizi alizianza akiwa Tosamaganga .

sisi tuliyesoma naye tunamjua vizuri sana hatufai kabisa huyu..
 
siku zote kosa moja huondoa mazuri 100 uliyofanya ama kutenda,huoni utaratibu wa kiutawala.huwezi kusamehewa kosa eti kwa sababu kuna mazuri, hakuna set off hapa kiongozi lazima siku zote uwe mwadilifu.

isitoshe kufanya mazuri kwa kiongozi yeyote sio hisani ni wajibu na unapoharibu moja kwa makusudi na hasa kwa ubinafsi km anaouonyesha zitto basi watz wa sasa hawawezi kukusamehe kamwe...
Nimeamini kweli zitto janga la cdm na taifa
 
Kweli macomment Na nacomment .. Natumia kijichombo ambacho hakina kijitufe Cha like, but Leo kweli ningegawa like nyingi tu..hii wap mode waimodify..

Kuna asilimia ya raia ambayo wanapenda kujihusisha Na mambo ya kisiasa AMA Kwenye majukwaa ya kijamii au vikao visivyo rasmi.. Hii ni asilimia ndogo ya umati Wa Watanzania wote. Sosayati hii ya wapekuzi wanaweka bidii Za haki Na mawazo Yao kuhakikisha taifa linapata AMA viongozi bora au uongozi bora Na si utawala..

Sosayati hii ndiyo inakesha Kwenye majamvi haya ikiwarekebisha wale walioshika usukani wa uongozi. Na Kama kweli viongozi wetu wangeyatumia mawazo Mengi ya watanzania kupitia majukwaa ya wazi Kama haya wangefaidika sana. Lakini cha ajabu viongozi wengi Wanayaona majukwaa haya Kama mafundo ya uchungu kwao. Nimeona hoja Za William Malechela, Nape, Zito(mudymtoi) wanatumia jukwaa Kupost Maada zao Na kitimu a bila kujali majibu ya post zao Kwa Kuogopa mishale ya raia. Ukiwa mwanamasumbwi kwanini uogope nundu..

So viongozi hawa wamepuuza ushauri mzuri wa wananchi wengi kupitia majukwaa haya Na wameegemea sosayati kubwa ya raia wasiofuatilia chochote Na kuwahadaa wapendavyo kiasi Cha kuwachezea ngoma wakiwa wamevaa nusu Uchi .. Shame on de pipo zis kind..

Pia nadhani kuna upepo tu Wa uharibifu umewavamia ndugu hawa, kiasi kwamba kila mchongo Wa kujisafisha mbele ya Jamii unageuka mavi..
 
Mimi sio mwanachama wa CDM, lakini hivi chama kinabomoka tu kwa zitto kutangaza kuwa raisi, wengine hakibomoki???
Kama CDM wanataka kuendelea vizuri waachane na tabia ya kuhamaki pale suala la zitto linapokuja mezani. Cha msingi waendelee kujenga chama itakapofika muda zitajulikana mbivu na mbichi

kuna Mahali umeona CDM inahamaki? wanohamaki .ni nyinyi lakini chama karma taasisi kinasonga mbele. Havana mud wa kupoteza kufikiria ***** kama huu
 
CDM hawawezi kumzuia Zitto kugombea urais au hata kuwa rais,come 2015 tutakuwa na katiba inayoruhusu wagombea binafsi!
 
mpaka leo sijafahamu kwa nini mtu mwenye elimu kama ya zitto afanye mistakes za kitoto kwenye bajeti mbadala namna ile.Mbowe i think u need to do something, coz madhara yake ni kuwa huku kuzunguka nchi nzima mkikitangaza chama ni useless.
 
Ni haki ya kila mwanachama,shabiki na mpenda mabadiliko kutoa mchango wake au mtazamo juu ya Mh Zitto na siasa za ndani na nje ya CDM.Kwa mtazamo wangu nadhani tungejiuliza kwa nini cdm imefika hapa? tatizo liko wapi? kwa mtu mmoja mmoja au mfumo mzima wa uongozi na kupelekea makundi yenye maslahi tofauti kisiasa ndani ya chama.Ni mtazamo tu....
 
acheni unafkii huo wana CDM mna ajenda zenu za siri kwa zitto,kwanin ha mpendi kuwa wakweli?semeni tu kuwa zitto hapendwi kutokana na DINI yake na kabila lake,ndo mana zitto anafahamu ajenda zote khs hiki chama na malengo yake.Wakatoliki wamepanga mikakati kamambe ya kumchafua ZITTO ila hamta muweza kamwe huyu ni mpiganaji akiamua kuivunja na kuigawa CHADEMA anaweza time yyte ile.
 
mim ndo semtawa. nimefuatilia tuhuma za kipuuzi dhidi yangu kuhusu story ya zitto na urais, taarifa zote kuhusu mim asilimia 99 ni cooked! some stupid guys wanaotumiwa na mafisadi wanadhn wataniyumbisha! jukwaa hli si la great thinkers bali most of them are so stupid! the home of stupid thinkers-jf! haiwezikan jukwaa la great people lijadili watu na ktoa taarifa za uongo, kiwendawazimu na kipuuzi.
 
cdm wasipoangalia zitto atakuwa janga lao na taifa kwa ujumla.... Zitto huyu huyu hajishughulishi sana na kampeni za kukijenga chama kama watu wengine tunaowaona kila siku kwenye mikutano yeye kila wanapoonyesha kuwa bize kujenga chama yeye anaibuka na kauli tata za urai. Ebu atuambie nini malengo ya tamasha la kigoma? Imekuwaje liwe sasa hasa chama chake kinapokuwa kwenye kampeni za kujijenga huku yeye akiwa haonekani sana kwenye kampeni hizo?

ZITTO NI JANGA LA TAIFA...

Ni kweli kbs zitto huwa haonekani hata kwenye mikutano ya chama chake kama wenzake,hapo utasikia yupo kwenye shughuli nyingine za kichama!.kweli zitto 'huyu'siyo yule.
 
Zitto, nilimwamini sana, hata ikafika siku moja, enzi zile za kutolewa bungeni, nikabishana na kijana fulani, aliyekuwa na zitto chuoni akasema "Hivi ninyi mnamfahamu Zitto Kweli?" tuulizeni sisi tuliokuwa naye chuoni...Alieleza kisa fulani alichofanya akiwa kiongozi/safarini....nk kuhusu lack of integrity completely. Lakini kwa jinsi alivyokuwa ameni aminisha kuwa ni kiongozi mzuri, nilikataa. Lakini kwa sasa......Zitto amenitoka...kabisaa....Yaani sielewi anaanzaje kutaka watu wampigie debe eti anafaa urais....Kwani wananchi si watampa haki yake kama ni mtu safi???kwani Nyerere aliingiaje kwenye nafasi hiyo????Mkapa nk Na asitake kuona eti ana uwezo kupita wengine; wapo wengine walio uwezo pia...tena saana; Halafu Nasari na Mdee wakaingiaje kwenye mtego huo. Hao pia nawaamini, wasije wakatubadilisha mawazo wengine.
 
acheni unafkii huo wana CDM mna ajenda zenu za siri kwa zitto,kwanin ha mpendi kuwa wakweli?semeni tu kuwa zitto hapendwi kutokana na DINI yake na kabila lake,ndo mana zitto anafahamu ajenda zote khs hiki chama na malengo yake.Wakatoliki wamepanga mikakati kamambe ya kumchafua ZITTO ila hamta muweza kamwe huyu ni mpiganaji akiamua kuivunja na kuigawa CHADEMA anaweza time yyte ile.

Acha upuuzi wewe....wangapi ni waislamu chadema......??tena ana dada moto wa kuotea mbali toka huko huko Kigoma...SUNGURA....
 
Cdm,kuweni makini na huyu zitto huenda huyu akawa'kitanzi' chenu 2015 Mungu akitujalia kufka huko,kuna kipindi nilisikia mlimpigia kura ya kutokuwa na imani naye na kumsimamisha kwa muda kama naibu kub,angalieni sana mjue chama chenu angalau ndo watu wanakiona km mkombozi wa wanyonge.hivyo msikubali m2 avuruge mipango yenu hata km ni kiongozi ndani ya chama.narudia tena kuweni makini na huyu m2.
 
Back
Top Bottom