Mkwawa
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,334
- 1,464
Kijana Zitto Zuberi Kabwe kapata umahiri mkubwa sana kwenye medani ya siasa, anayo mengi ya kujivunia mafanikio ya kisiasa kiuongozi na kiuchumi.
Zitto ameweza kuwa chachu ya vijana wengine kujiunga na siasa na kushiriki kwenye uongozi bila kujali ni chama gani wengi wa vijana walivutiwa na Zitto na kuona nao wanaweza.
Ndani ya CDM ameshawishi wengi na wengi wameshawishika kwa ajili ya kauli zake, vitendo vyake ndani na nje ya bunge uwezo wake wa kujenga hoja na mafanikio ya kijana mwenzao ambaye hajatoka kwenye jamii na familia za (Sliver spoon)
Mategemeo yamekuwa makubwa sana kwa Zitto kushika nafasi kubwa ndani ya chama yakiwa ni maandalizi ya kuandaa viongozi wa sasa na baadaye wa chama na Taifa.
Kinachotokea sasa mpaka kila mmoja anaogopa kauli za wenzake hata kama zilikuwa na nia njema tu ni hulka ya wanasiasa kupenda madaraka, kusahau wajibu na kujipenda zaidi ya wananchi wanaowafanya wawe hivyo walivyo. Binafsi sioni kwa nini Zitto au yeyote aogope au ashtuke kama Zitto ana nia ya kuwa Raisi wa Tanzania kwani hata mimi nina nia hiyo. Ni nani asiyependa kuwa dean kama yeye ni mhadhiri, ni nina asiyependa kuwa CEO kama yeye ni meneja wa kampuni husika?? Ni nina asiyependa mafanikio ??
Tatizo hapa ni jinsi ya kufikia malengo. Vijana wa leo hawako tayari kufanya kazi wanapenda vya kunyonga vya kuchinja hawavitaki. Vijana waliopo kwenye vyama vya siasa vinavyokuwa wanaotaka kuingia ikulu halafu hawajengi vyama vyao wanastaajabisha sana; unajiuliza watashinda vipi wakati chama kina sehemu kibao hakina mashina?? Kwa nini tusielekeze nguvu nyingi kujenga chama?
Unaponunua kundi la kukupigia debe nje ya utaratibu uliokubalika wa chama ulichokikubali unamaanisha nini?? Wakati huu viongozi wengine wakikijenga chama kwa kushughulika kufungua mashina matawi baadhi wanaelekeza nguvu kujipigia debe la Urais hii inasikitisha sana. Je ni kweli makamanda waliopo nyikani kila siku wangekuwa na Tamaa kama za vijana wa sasa chama kingekuwepo?? Kina mzee Mtei, Bob Makani nk walianzisha chama wakijua watakifikisha pahala fulani na wengine waendelee nacho, hawakuwa na tamaa kama za vijana wa leo. Wazee hawa wengi wao wamestaafu bila hata ya kuwa wabunge.
Kifo cha NCCR mageuzi ni uchu wa madaraka, kila mmoja alijiona ana akili sana kuliko mwenzeka.
Ni vyema kuwaambia vijana wa CDM waliopata madaraka, Taifa haliko tayari kuwaona wanalumbana kwa uchu wa madaraka na tamaa zao za maisha yao na wanaowatuma. Wananchi tunataka mabadiliko ya kiuchumi ili keki hii kila mtu aile.
Chadema waweke miiko ya viongozi iwe dira hata wakichukua dola. Leo serikali inayumba kwani ina viongozi wa ajabu wengi kila mmoja akiwa analake na maamuzi yake. Haiwezekani kila mara Tatizo ndani ya CDM lianzishwe na mtu yule yule kwa sababu zile zile.
Busara ya Zitto na hekima ya uongozi inampotea siku hadi siku, tamaa kubwa ya uongozi aliyonayo na makundi anayoyajenga akitumia wale aliowasaidia ama kufanikiwa kisiasa ama ushawishi wa aina zote inamfanya apotee na kujijengea maadui ndani na nje ya chama.
Naamini kabisa binadamu anabadilika na anaweza kufikia malengo yake akibadili mwelekeo. Zitto saidia kujenga chama wapiga kura wa kumtea mgombea wa Uraisi huanzia ndania ya chama. Ukishiriki kikamilifu kujenga chama wanachama watakupenda na kukuteuwa kupeperusha bendera, ila kama una nia nyingine endelea.
Zitto hatuhitaji Raisi anayetumia fedha, makundi, wahariri nk kushinda madhara ya Raisi kuingizwa ikulu na kakundi kadogo kwa watu tayari tunayaona. Utawalipa nini ?? Wanawekeza ili wapate nini??? Tamaa ikizidi huuza utu wa mwanadamu. Unaweza kuwatumikia watanzania bila kuwa Raisi.
AOGOPWE YEYOTE MWENYE TAMAA YA KUINGIA IKULU. IKULU HAKUNA BIASHARA IKULU NI PAHALI PATAKATIFU. KWA NINI KUTUMIA FEDHA NYINGI ILI KUINGIA IKULU MTAZILIPA VIPI?????
Chief Mkwawa wa Kalenga
Tamaa mbaya ndiyo inayoangamiza taifa langu Tanzania