JMakamba amepotea njia hapo bora atulie ila akitaka kwenda deep ataaibika tu kinachofuata.
Your the clear example of "POVERTY OF INTELECT".
Kigarama, hivi matakwa ya vijana wa Chadema ni yapi.Hivi kwani ni lazima vijana wote wa Tanzania waunge mkono matakwa ya vijana wa CHADEMA?
Kwa hiyo hawa vijana wanaamini;Wapo vijana hawafaidiki chochote kutokana na serikali iliyopo madarakani lakini nao wanayaona yanayotokea kama ni makosa ya kiutendaji na wala si uhalifu.
Kwa hiyo kuwa na mtizamo tofauti ni pamoja na kufumbia macho uozo unaotuzunguka. Sasa jamani hapo tutakuwa tunajenga taifa la namna gani? Kama hawa vijana wenzetu wenye msimamo tofauti si mbumbumbu kama unavyodai, tuwaiteje? Mbuni?Hawa wasichukuliwe kama ni mambumbu bali ni vijana wenzetu wenye mitizamo tofauti na sisi!!
Hii ndio JF,
kila mnayepishana mawazo MNAFIKI.
Kazi kweli kweli tanganyika
Kwanza Mag3 wengi wenu humu mnachanganya mambo na kutoka nje ya mada. Hapa hoja ni kuhusu ripoti ya CAG na wala si hayo ya Meremeta au Richmond na mengineyo. Kwa mfano hawa mawaziri si wao waliohusika moja kwa moja kwenye kuchota hizo fedha ila yametokea na kufanywa na watu wa chini yao.
- EPA haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
- KAGODA haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya utendaji!
- KIWIRA haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
- MEREMETA haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
- RICHMOND haikuwa uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
- WIZI si uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
- UFISADI si uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji!
- RUSHWA si uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji
- UHALIFU si uhalifu, ni makosa tu ya kiutendaji, duh!