Heshima kwenu wanajamvi,
Uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 CDM walishindwa kusimamisha wagombea katika majimbo mbali mbali hakuna ubishi wapo wabunge na madiwani wa CCM walishinda ubunge na udiwani bila kupingwa.Hali hii ilisababishwa na vyama vya upinzani kutkuwa na mitandao ya kichama iliyoenea Tanzania nzima.
Chama cha CDM kwa hakika kilibaini kasoro hii na kuamua kuanzisha program yake ijulikanyo kama M4C ikiwa na nia ya kuwafikia wapiga kura wengi kabla ya uchaguzi wa mwka 2015.Kabla ya hii program ilikuwepo opeshen sangara ambayo tunaaweza kusema kwa uhakika ilisaidia kukipatia chama matokeo mazuri katika uchaguzi 2010.
Wapo viongozi wa CDM ambao tumekuwa tukiwasikia wakihangaika huku na kule kuhakikisha M4C inafanikiwa bahati mbaya Zitto bila haya kaamua kuanzisha mtandao wake kama ule wa Kikwete kwaajili ya kuutwa ufalme wa magogoni.Mheshimiwa Zitto ni aina ya wanasiasa wanaotanguliza maslahi binafsi na kuyakanyaga maslahi ya chama chake.Tumekuwa tukisikia CDM ikisemwa ni chama cha kanda ya kaskazini, sijamsikia Zitto akikisaidia chama chake dhidi ya hizi propaganda hasa ikizingatiwa yeye anatoka ukanda mwingine.Tumekuwa tukisikia CDM ni chama cha kikristo Zitto kwa nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu angetakiwa kukisafisha chama chake kwakuwa yeye si mkristo.Propaganda hizi kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikitumiwa na CCM hasa baada ya kuishiwa hoja dhidi ya CDM.Naanza kuamini propaganda hizi pia zimekuwa zikitumiwa na Zitto au wapenzi wake kwa faida zake binafsi ndiyo maana hajawahi kukisaidia chama dhidi ya mashambuzi haya potofu.
Nilitegemea Zitto angejikita zaidi katika ujenzi wa chama chake na kupigania upatikanaji wa katiba nzuri badala yake anaunda mtandao wa wanasiasa wachovu ambao bila aibu wanatamka bungeni sasa ni zamu ya Kigoma.
Kweli nimeamini zitto ni tishio,na ni jembe la ukweli,maana asingewasghulisha hivi kila kukicha thread zake,mnajua ana madhara ndio sababu povu halikauki!
Kweli Zitto Ulivyokuwa unatetea Dowans inunuliwe na NSSF ulikuwa unajua.
Ulivyosimama chap chap na kusema lisijadiliwe bungeni, likatazamwe na kamati ya uongozi kumbe ulikuwa na agenda ya siri?
Angalieni hapa
Wafanyakazi, tuwe pamoja. Tupange maandamano kuanzia J3.
Bunge sasa limeshindwa.... Mungu yupo nasi
Wabunge ni wabinafsi sana, angalia wanavyojiongezea Posho, Kwanini wao wasisubiri hiyo miaka 55?
kama wameona ni habari kubwa wasiitumie kuwa kasema zitto au mbunge wa chadema?
mkuu anawatisha sana si unaona kila kukicha wafuasi waaminifu wa yule babu ambaye ni bachela mnavyopambana na zzk na mkimgusa tu chadema pinduuuuuzito ni kinyago tulicho kichonga wenyewe so atutishi.