Zitto,mwakyembe &ngereja wako wapi mgao wa umeme?

MkuyuMkubwa

Member
Sep 27, 2009
50
0
Nakumbmbuuka kipindi cha mgawo wa kwanza wa umeme, mjadala mkubwa ulibebwa na Zitto, Mwakyembe na waziri Ngereja...wengine walionekana zaidi nyuma ya hawa mpaka maamuzi yalipofikiwa...najiuliza kwanini sasa hawajitokezi kuchangia mjadala huu ilhali tatizo ni lile lile?....tunahitaji majibu....mpaka sasa, malima na shelukindo hawajatoa majibu....wamekubali tatizo tu....ufumbuzi bado....waziri Ngereja uko wapi wakati suala hili linatikisa nchi?....Mwakyembe uko wapi wananchi tunaumia bila majibu ya tatizo?...Zitto uko wapi?....nini mtazamo na misimamo yenu katika hali hii?....au mlikuwa viongozi wa kupingana tu bila kuwa na uwezo wa kupendekeza mikakati mbadala?
 
Wote wamesalimu Amri na sasa hivi wamebaki kama vile hawaoni kabisa. Zitto Kabwe alisema haya mambo mapema na tena kuna watu wakaja hapa na kusema kuwa amefidasiwa naye huku yeye alikuwa anatoa ushauri wa kiuchumi na tena Hata Mchumi mwingine naye alikuja na kusema mambo haya haya, Sasa Zitto, Lipumba, Idrissa wote walikosea au Vipi?? Hapana shaka kuwa hata Mwakyembe naye anaona hakuna jipya juu ya mambo ya ajabu kama mgao wa umeme katika Tanzania
 
Wakija ndio watatuletea umeme jamani...embu tutafute soln kwanza ndio tuwamulike watu.....
 
Wote wamesalimu Amri na sasa hivi wamebaki kama vile hawaoni kabisa. Zitto Kabwe alisema haya mambo mapema na tena kuna watu wakaja hapa na kusema kuwa amefidasiwa naye huku yeye alikuwa anatoa ushauri wa kiuchumi na tena Hata Mchumi mwingine naye alikuja na kusema mambo haya haya, Sasa Zitto, Lipumba, Idrissa wote walikosea au Vipi?? Hapana shaka kuwa hata Mwakyembe naye anaona hakuna jipya juu ya mambo ya ajabu kama mgao wa umeme katika Tanzania

mkuu asante sana.hapo kisu kimegusa mfupa..Zitto alisema wakapiga makelele akiwamo huyo kichwamaji Mwakyembe ,sasa nchi imeingia gizani wakae watulia hatutaki bughudha wenye hela zenu wekeni majenereta kama sisi..
 
Mwakyembe yuko jimboni Kyela, amesikia ushauri kwamba akae jimboni baada ya kutumia miaka minne kuwa mtalii huku kwake kunaungua.

Umeme ni kazi ya Tanesco na Ngeleja, hao wabunge mnawalaumu bure!
 
Zitto yupo Ujerumani anapiga degree chuo kikuu....tutafute umeme kwanza ili tutumie kuwatafuta viongozi wanao tuweka gizani hapo...
 
Mwakyembe yuko jimboni Kyela, amesikia ushauri kwamba akae jimboni baada ya kutumia miaka minne kuwa mtalii huku kwake kunaungua.

Umeme ni kazi ya Tanesco na Ngeleja, hao wabunge mnawalaumu bure!

Mkuu ungemalizia kwa kusema kuwa Wabunge kazi yao ni kukaanga mbuyu tu na kuwaachia Tanesco na Serikali kutafuna.
 
kweli umeme ni kazi ya tanesco, lakini kumbuka kwamba suala la umeme tanzania lina siasa nyingi zaidi ya utaalamu....wakati wa mjadala wa mgawo uliopita hata tanesco kupendekeza kununua mitambo ya dowans ilosababisha zogo kubwa....gwiji la masuala ya nishati katika benki ya dunia bwana Karhammar , akizungumza katika gazeti moja la nchini kenya la The east african , alisema "mjadala wa umeme tanzania na hoja ya kununua au kutonunua mitambo ya dowans imebebwa na siasa zaidi kuweza kuvuka mijadala wa kitaalamu"
 
mkuu asante sana.hapo kisu kimegusa mfupa..Zitto alisema wakapiga makelele akiwamo huyo kichwamaji Mwakyembe ,sasa nchi imeingia gizani wakae watulia hatutaki bughudha wenye hela zenu wekeni majenereta kama sisi..
__________________

we bado unatumia genereta ndugu pole...yaani mtu kama wewe ata umeme ukirudi usifike kabisa uko
 
Sikujua kama ni rahisi hivyo kutawala nchi ya Wadanganyika! kwani fikra zao ni sawa na viongozi wao.
Kukosekana kwa umeme Dar ni tatizo linaloundwa na sii ktk mahitaji yetu ya umeme. tupo kizani kwa sababu serikali imeshindwa kuanzisha vyanzo vya umeme... Period!
 
Inasikitisha sana kuona watu mahiri ndani ya JF wanashindwa kuunganisha dots.
Zitto kabwe alikubaliana kununuliwa mitambo ya kitapeli iliyotumika ya Dowans. Mwakyembe walikataa kwani kukubali kununua mitambo ya kitapeli, michakavu ni kukumbatia uozo na kuenzi rushwa na kukubali wezi kutuamulia mambo.

Kamati ile ilitoa mapendekezo ikiwa ni pamoja na tanesco kununua mitambo mipya kwa kipindi muafaka, na walisema kama tulikuwa tunatumia dola milioni 67 kununua mitambo iliyotumika ya dowans basi tunaweza kununua mitambo mipya kwa kiasi kama hicho na kutoa zaidi ya megawatt 100. Tanesco ilikuwa na muda wa kutosha wa kufanya hivyo na hawakufanya.

Dr idrisa aliahidi nchi kwenda gizani isiponunuliwa mitambo ya dowans kama vile viwanda vya kutengeneza jenereta vimefungwa, na kama fedha ilikuwepo ya kununulia mitambo ya dowans kwanini wasingelitumia fedha hizo kununulia mingine????

Zitto hakuwa sahihi na hawezi kuwa sahihi kuungana na akina Rostam kuwasaidia kufanikisha mbinu zao mbovu na uhujumu uchumi, Dr idrisa akiwa kama mdhamini wa mkopo wa mitambo ya richmonduli lazima afanye linalowezekana mitambo iende tanesco, sina uhakika Zitto anafaidika na nini?

Nchi kwenda gizani kamati ya akina mwakyembe ilifanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa, na tanesco wakisaidiana na wizara ya nishati na madini ndio wazembe na wahujumu uchumi, wanatakiwa wajiuzulu kwa kushindwa kuwa na uwezo wa kutatua tatizo la umeme.

Watanzania wenzangu muda umefika wa kuanza kutafakari na kutumia maono kuelewa nini kinachotengenezwa, ni uhayawani kuamini kutotumia mitambo ya dowans ndio chanzo cha nchi kuingia gizani. Huu ni wizi na ukosefu wa kufikiri.

Nina watakia kila la kheri watanzania na kumwomba mungu watanzania waweze kuelewa ni jinsi gani wanavyochezewa akili zao na wezi na watawala wanaotumia jasho lao, wakiwaacha gizani wakati kwenye nyumba zao kuna jenereta, solar, nk na kuwatisha bila ya dowans hakuna tanzania yenye mwanga.Wizi na uhujumu umekuwa ni mtindo wa biashara Tanzania.
 
Back
Top Bottom