Endeleaaa
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 1,485
- 738
Zitto,
Nakuheshimu sana mdogo wangu.
Nasikitika sana ninapoona, kwa umakini wako wote ulionao, unaaandika kwa kubabaisha na kupotosha. Mimi sijaipitia bajeti yote, lakini hayo ulyoainisha hapo ya ama umefanya makusudi kupotosha katika maandishi yako ya ama hujui namna ya kuandika, hususan ikija kwenye namba.
1. Mstari wa kwanza umeandika "shilingi 537 Bilioni", mstari wa tatu na wa nne ukaandika "shilingi 402,402,071,000 milioni" na "shilingi 76,953,934,000 milioni" na "shilingi 325,448,137,000." halafu mstari wa nne ukarudia tena "Shilingi Bilioni 325".
Swali: Kwanini "shilingi 537 Bilioni" ziwe ni billioni? na kwanini "shilingi 402,402,071,000 milioni" na "shilingi 76,953,934,000 milioni" ziwe millioni? na kwa nini "shilingi 325,448,137,000." ziwe si millioni wala billioni? na halafu "Shilingi Bilioni 325" ziwe tena billioni?
shilingi 402,402,071,000 Equiv to 402.4bilioni kwamba kwenye hotuba ametamka Umeme umetengewa Bil 537 lakini kwenye vitabu, wizara ya nishati na madini imetengewa only bil 402.4
Matumizi ya wizara yatakuwa bil 76.9 matumizi ya kawaida na bil 325.5 maendeleo. [76.9 + 325.5 = 402.4] swali hapo bil 135 za ziada zimeingiaje kwenye hotuba ya Mkullo?
2) Unaeleza kuwa: kiasi cha shilingi 11.6 trilioni wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya shilingi 13.525 trilioni. Kati ya ya fedha hizo za mwaka 2011/2012, kiasi cha shilingi 1.901 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 14.06% ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la Taifa.
Halafu unasema: Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha shilingi trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011
Swali : Mbona hizo "shilingi trilioni 11.624" "za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 huoneshi ngapi kati ya hizo zililipa madeni?
3) Swali: Jee, bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 zilikuwa ngapi? mbona huoneshi?
4) Kauli ilikuwa baadhi ya posho zitafutwa na baadhi ya posho zitapunguzwa.
Jee, ni nini kilichozugwa hapo?
.
Na kauli uliyowekea "bold" haihusiani na kufutwa au kupunguzwa kwa posho, kauli hiyo inaongelea "kusamehe" kodi, sasa mdogo wangu Zitto huelewi maana ya kusamehe kodi? Kama huelewi, hiyo kauli inamaanisha zile posho ambazo hazijafutwa na ambazo zimepunguzwa na ambazo hazijapunguzwa, zitasamehewa kodi. Sasa nini unachoona hakiko sawa hapo?
5) Labda ili ueleweke vizuri, ungeweka hizo faini ambazo zitafikia 50,000/= na ambazo zitazidi zaidi ya 50,000 na kufikia 300,000/= Usitupotoshe na usiupoteshe umma kwa kuwaambia kuwa huku hivi huku hivi.
Kwa kukukumbusha tuu, ingawa faini za barabarani tunazijuwa kikawaida ni 20,000/= tuliona hata Chenge alichapwa faini ya 700,000/= kwa makosa hayo hayo ya barabarani. Nimekutajia ya Chenge kwa kuwa ndio kesi maarufu na ni wengi wanayoifahamu. Kwa mantiki hiyo, inabidi ufafanue kwa kina hiyo faini ya 300,000 na ya 50,000. Tafadhali usipotoshe watu.
Hapo hapo, sentensi yako hii haieleweki "kwa sababu serikali katika bajeti vyake rasmi vya bajeti imeamua kufanya marekebisho". sijui inamaanisha nini?
6) Jee, ulitaka serikali isilipe madeni? na Jee, ulitaka serikali isilipe posho?, kama hutaki serikali ilipe posho, kwanza onyesha mfano kwa kuzikataa posho zako kama mbunge, kwani mojawapo ya wenye posho kubwa katika watumishi wa serikali ni wabunge. Halafu onesha na takwimu za bajeti iliyopita, asilimia ngapi ililipa madeni na asilimia ngapi ililipa posho. Usiandikie mate na wino upo.
7) Tunaisubiri kwa hamu na kama ni nzuri tutaiomba serikali iifate, kwani upinzani ndio kazi yake kuu, kukosoa ili serikali ijirekebishe.
Kwa kusherehesha tu, ningeomba ajibu Zitto mwenyewe kama anavyonukuliwa kuwa ndio muandishi wa taarifa hii, nikimuomba mleta mada Regia Mtema ajibu ntakuwa sikutenda haki kwani yeye inaonesha kuwa ni kipaza sauti tu cha Zitto.
Nadhani hii taarifa ndio ina kusudio la kupotosha wananchi kwa kuandikwa ndivyo sivyo.
on red