Zitto, Makamba wautaka urais?

Ukiacha John Mnyika hao vilaza wengine akina Lema,Msigwa,Sugu et al Zitto ataongea nao nini? Apoteze muda kufuatana na mbumbu ili iweje sasa? Nafurahia sana Urafiki wa Zitto na January wote wako Smart Kichwani!

kaka acha matusi ina maana sisi wana mbeya tulichagua kilaza.?
au tukubali kweli n kilaza lakin ndyo chaguo letu..kila mtu ana tofaut katka kuchagua ndo maana kikwete kamuoa salma na slaa kamuoa josephine..ingekua kila mtu ana chaguo sawa na wengne tusingekua hapa leo..
 
Dr. Slaa, Mbowe na Tundu Lisu wakienda 'kunywa' chai ikulu na JK hiyo ni sawa, ila Zitto Kabwe akifanya press conference na January, na mhe. Kigwangalah, ni noma na Zitto anakuwa msaliti! Ama kweli mkuki kwa nguruwe. Go zitto go!
 
kaka acha matusi ina maana sisi wana mbeya tulichagua kilaza.?
au tukubali kweli n kilaza lakin ndyo chaguo letu..kila mtu ana tofaut katka kuchagua ndo maana kikwete kamuoa salma na slaa kamuoa josephine..ingekua kila mtu ana chaguo sawa na wengne tusingekua hapa leo..

Slaa kaoa lini? Dr. Slaa ana mchumba. Na ni mgombea urais, pekee aliyezunguka nchi nzima na mchumba!
 
zitto ni wa kumtilia shaka na hata viongoz wa chadema wanalijua hlo kama mnakumbuka jamaa alikuaga MESSI wa chadema ila kwa sasa wanamuona TORES tu(mnafatilia mpra mtaelewa na maansha nini)..
na msije mkajidanganya kuhusu juz alivoongozana na mnyika kwenda tanga,kumbuka alikua na ajenda yake binafsi(mkonge)..
na kifupi hata viongozi wa chadema washamsoma ndo maana hawampi kipaumbele kabisa kama zaman..
angekua anakitakia chama mazur asinge simama mwaka 2010 jimbon kwake na kuwambia wananchi wampigie kura kikwete wakat chama chake kinawakilishwa na slaa..alafu alipoulizwa akajitetea kwa hoja dhaifu kama vile ni mwanafunzi wa "DARASA LA PILI-D" ,eti "kikwete amelifanyia mengi jmbo langu"..
kwa hili CCM wamecheza kama pele walijua mshikaj atawasumbua sana,wakaanza kumlainisha taratibu na sasa kalainika kabisa,msije mkashangaa hata ndani CDM siku za uson wakamyima hata uongoz..

CHARACTERISTICS ZA ZITTO:-
1.mbinafsi..
2.mpiganaji wa uongo..
3.anafanya siasa kwa kukza jina lake,na sio kwa maslahi ya chama chake au taifa lake..
4.anajiona great kuliko mtu yeyote pale CDM..
 
Kuna tofauti za Kiitikadi, Kisera na Kimtazamo kama Zitto hakubaliani na viongozi wa Chadema kimtazamo lakini anakubaliana na January au hata baadhi ya wabunge au wabunge wote wa CCM haiwezi kubadilisha maana ya Itikadi, sera hasa ktk swala la posho..Wabunge wote wa CDM wanaweza kupendekeza posho zaidi na Zitto akapingana posho, haiwezi kumwondoa ktk msimamo wa chama kiitikadi. Hakuna mahala popote ktk upinzani wa kidemokrasia umeorodhesha chuki ama kutengana na vingozi wa vyama vingine.

Maadam nyie ni wapenzi wa Mpira basi nakuombeni fikirieni hivi hao wachezaji wa Yanga na Simba hawatakiwi kuwa marafiki au hata kufanya mazoezi pamoja beach?.. Wanaweza au sio?.. isipokuwa kumwona Zitto akifanya mazoezi kambi ya January ndipo mnaweza kusema yote haya. Kumbukeni tu kwamba mbunge yeyote iwe wa Chadema au CCM anaweza kupingana na mpango wowote ndani ya muswada wa serikali, hata mwana CCM anaweza tofautiana na wengine wote kimtazamo ktk mapendekezo ya mapato au matumizi na isimwondoe itikadi.
 
Slaa kaoa lini? Dr. Slaa ana mchumba. Na ni mgombea urais, pekee aliyezunguka nchi nzima na mchumba!

lakini ulishanielewa na maansha nini sio.?
na hoja ya msing hapa ni kuhusu hilo neno kilaza..
ukimtukana mtu aliyechaguliwa na wana mbeya kua ni kilaza unamaansha na sisi tulomchagua ni vilaza..
 
hivi kati ya Sugu na bi Kiroboto, kilaza ni nani?
 
Hawa watoto wanapagawa sana na umaarufu wa kisiasa koz ndo juzi juzi 2 wamebalehe kisiasa zasy majembe yenye hekima kam kamanda lema yanazidi kung'ara koz hayapagawi na umaarufu wa kijinga, chadema mkimuweka zitto Rais basi mjue mmekwisha.
 
Kuwa na mchumba ingekuwa kosa (Dr)Slaa asingeruhusiwa kugombea urais,ila 'bwana wenu' ana wake wangapi,hatangazi kama 'Zuma','Mswati'.jibuni(k-proffessional)basi@ritz,malaria sugu na members wenu
 
Kwani bado mna wazo lolote juu ya Mzito Kabwera?huyu jamaa hana tofauti na tiyara mwacheni apelekwe na upepo popote utakapomfikisha ni harari yake
 
Ndugu yangu Zito alianza maandalizi ya kuutafuta urais pale alipogombea uenyekiti wa CHADEMA ili aweze kuweka watu wake ktk vikao vya maamuzi wamlinde wakati wa kuteua mgombea urais. Aliposhindwa kwa njia hii, akaamua kumfadhiri na kumshauri kafulila ampindue Mbatia akijua dhahili Kafulila akiwa mwenyekiti NCCR, basi Zito kwake ingekuwa mteremko kukimbilia huko na kupitishwa kwa nafasi hiyo ya urais. Bado kakwama. Sasa njia pekee aloamua kutoka nayo ni ajenda ya umri. Yetu macho tutaona mwisho wake. Ila CDM ni makini wa kutosha make hawasemi ila wanabaini kila njama kabla ya athari zake. Nawapongeza!!!
 
RAIS KIKWETE ANAPOMPIGA VITA MWALIMU JULIUS NYERERE KABURINI LEO HII KWA KUHIMIZA 'DHANA YA URAIS WA VIJITOTO' ALILOTUKATAZA WATANZANIA LICHA YA MADHARA MAKUBWA TUNAYOYAVUNA HIVI SASA KWAKE MWENYEWE HIVI SASA, YOTE NI KWA FAIDA YA NANI?

Rais Kikwete kamwe hawezi kurusiwa kwa mara ya tatu kufanyia majaribio ya kimaabara maisha ya WaTanzania kwa misingi ya kukamatishwa mawazo ya kiayawani barabarani kila kukicha huku taifaa likiendelea kuangamia kwa kiasi kikubwa kwa kila Jaribio la Kisiasa analolifnya ama ndani au nje ya chama chake.

Mpaka hivi sasa, ni jambo lililo dhahiri kwa Watanzania waliowengi taifa limefikia hapa tulipofika kutokana na mambo matatu mazito ya kimajriobio hayo hayo.

Kwanza, madhara mazito yalioifikia taifa hili ilianza na jaribio la kwanza la kutumika dhna ya 'URAIS WA VIJITOTO' na matokeo yake tukampata Mhe Kikwete kuwa ndiye rais wa JMT licha ya Mwalimu Nyerere kuktalia jambo hili na kuonya kwa nguvu nyingi zaidi watu tusidhubuti kukumbatia jambo hili.

Kiukweli katika nchi hii hakuna hata mtu mmoja atakayeweza kusahau mambo gani ambayo yametupata na yanyoendelea kutupata kutokana na mtaji wa dhambi ya kwenda kinyume na ushauri wa Baba wa Taifa, Mwalimu J.K. Nyerere, kwa kukumbatia 'DHANA YA URAIS WA VIJITOTO' ambayo hivi sasa tena imempata dalali mpya kwa jina la Rais Jakaya M. Kikwete.

Sote hatuna shaka kwamba uongozi wa nchi si sawa na uongozi wa jimbo wala kata hivyo mtu gani akachaguliwe kuongoza WaTanzania zaidi ya milioni 48 si swala la kuchezea chezea.

Inasikitisha mno jinsi ambavyo urais wa nchi hii unavyoendelea kukosa thamani na hata kuanza kurahisishwa kiasi hiki kwa namna mbavyo hata Rais Kikwete anafika mahala anakwenda kujibana mahali kujadilian jambo linalogusa mustakabali wa nchi na vijitoto kwenye mazungumzo binafsi na akina Zitto Kabwe na Januari Makamba kwenye mgahawa na kisha kesho yake kuonelea kuwa sasa hizo ndoto binafsi sasa ziwe ni Mambo ya Ki-Katiba ambayo kila Mtanzania ataswa kuyafuata. Katu hatudanganyiki na mawazo ya barabarani ya aina hiyo.

Hapa chini ni kijisehemu tu cha baadhi ya hatua za kimajaribio ya kimaabara ya Rais Kikwete kudiriki kucheza kamari na mchezo wa potea pata na maisha ya mamilioni y WaTanzania kwa namna isivyofaa hata tone:

1. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilijitokeza naa kamari ya kwanza kabisa ya kutuletea kitu walichokiita DAMU CHANGA (kwa maana ya Ndg Jakaya Mrisho Kikwete) kugombea kiti cha urais wa taifa letu.

Sote hivi sasa ni mashahidi jinsi gani kila kitu ndani ya nchi kimepuputika na tumebakiwa tu na janga la taifa kwa kukubaliana na uamuzi huo huo kufanya uchaguzi chini ya DHANA HIYO HIYO POTOFU LA 'URAIS WA NCHI KUKABIDHIWA VIJITOTO' ambao hata kusimamia tu mambo yao ya kimapenzi tu na visichana vyao yenyewe bado ni mtihani.

Kwa nini watu turudie kosa eti kwa jina tu la kuchagua UDOGO WA UMRI kama kigezo ki-kuu mtu kuongoza nchi??

2. Kwa mara nyingine Rais Kikwete mwenyewe, kwa mtiririko ule ule uliojaa MAWAZO YA KUKOMOA MAADUI WAKE, akaja na DHANA POTOFU nyingine kwamba bunge letu ambalo ni mhimili muhimu mno kikatiba kwa kazi ya kutunga sheria za nchi sasa kiongozi wake kwa maana ya spika ili apatikane ni sharti KILA MMOJA WAO AMA AVUE SURUALI AU SKETI KUMTAMBUA JINSIA ALIVYOUMBWA halafu eti kwa kigezo hicho tu ikawa ni leseni kwa baadhi ya washindani kuwashinda wengine kwenye kinyang'anyiro na kuibuka kuwa MA-SPIKA UBWETE AMBAO KILA SIKU UFANYAJI WAKE KAZI NI MADUDU MATUPU NA KAZI NYINGINE NI KUDAI TU POSHO.

Sasa hivi nako chaguo letu kwa kuzingatia DHANA POTOFU LA JINSI nalo linatutokea puani mpaka kinamma wanaharakati kulazimika kuingia barabarani kupinga jinsi gani Spika Anne Makinda anavyowadhalilisha kwa maamuzi yake ya ki-shabiki hata kwa masuala mazito kwa mustakabali mzima wa nchi.

Kweli Rais Kikwete bado tu huoni jinsi gani ulivyotuuza hadi hapo na bunge kuonekana kupwaya ajabu kutokana na mojawapo misururu ya mi-dhana yako yanayopingana na katiba ulioapa kulinda?

3. Kwa jinsi ambavyo Rais Kikwete amedhihirisha wazi kwa umma wa Tanzania kwamba yeye na MAFISADI nchini ni damdam, leo hii anapata wapi uhalali mbele ya uso wa jami na ujasiri uliomshinda kuwavua gamba mafisadi, eti kuja kuliambia taifa na wala si CCM yake kwamba Rais wa Tanzania ajaye atakua ni mtu wa aina hivi mara vile??

Mwenzetu huyu kwa jinsi alivyoongoza kwa KUKUMBATIA MAFISADI Tanzania na kutumia dola kuua wananchi kila kona ya taifa hili, moja kwa moja inamfanya awe ni mtu ambaye hana MORAL AUTHORITY kutuambia wananchi kwamba Rais ajaye atakua ni wa namna gani vile.

4. Isitoshe, masuala ya raia yupi mwenye umri gani ataweza KUWA NA HAKI YA KUZALIWA KUJITOKEZA KUCHAGUA AU KUCHAGULIWA kwa nafasi yoyote ya uongozi ndani ya mipaka hii ni SUALA NYETI NA LA MSINGI KI-KATIBA ya JMT hivyo hakuna mtu yeyote au taasisi itakayojifurahisha na njozi zake mwenyewe kulivibadilishia vichochoroni huko Magogoni kwa malengo yasio na faida kwa Umma wa Tanzania.

Hivyo, mabadiliko makubwa kama haya eti kwa ajili tu ya HIVI VIJITOTO FISADI ni sharti kwanza tuletewe wananchi kwenye REFERENDUM ILI TUKAIPITISHE KWENYE TNURI LA KIDEMOKRASIA halisi.

5. CCM ikitaka a political showdown wa aina yoyote eti kwa ghiliba hizo hizo wanazozitumia hivi sasa kuzuia baadhi ya watu wenye hamu kubwa ya kugombea urais ndani ya chama chao, na sasa waanze kuvusha ghiliba hizo hizo kwenda kwa vyama vingine kwa kutaka URAIS WA HIVO VITOTO VIWILI VIWAKILISHI NA VINARA WA MAFISADI NCHINI, CHADEMA kipo katika nafasi zuri mara 50 zaidi ya hapo kugeuza ghilib hii mpya kurojeka zaidi ya uji na tena nda ya kipindi kifupi haijawahi kuonekana.

URAIS wa taifa hili kwa msururu wa dhana potofu kama vile JINSIA na au UMRI hauna nafasi hata kidogo kwa nchi hii mpaka mawazo ambayo ni HIGHLY CONTENCIOUS kama hayo yawe yamepitishwa kwenye KURA YA MAONI KITAIFA ikisimamiwa na Tume Huru ya uchaguzi ambalo si hili tume la huyu Jaji wa Mondo, Kondoa.

NOTE:
Na kama huu ndio mkondo mpya wa kutekeleza ile azma ya Rais Kikwete kwamba 'ninapoondoka madarakani uongozi wa nchi simuachii Mtanzania Mkristo ng'o' basi wenye mawazo haya mhesabu kula ya chuya kwa kuwa hamjafaulu bado katika hili la urais wa Januari Maakamba na na Zitto Kabwe!!!

Source: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015 « Zitto na Demokrasia

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015

KABWE ZUBERI ZITTO, MPKIGOMA KASKAZINI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015

Baadhi ya vyombo vya habari vimehusisha kauli yangu ya kutaka kupunguza umri wa kugombea urais na mimi ‘kuutaka urais'.

Mimi nikiwa mwanachama na kiongozi wa chama chama changu cha CHADEMA naelewa na kuziheshimu taratibu na kanuni tulizojiwekea za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo nafasi ya urais.

Nafasi ya uongozi ndani ya CHADEMA haiombwi kwenye warsha. Iwapo chama changu, wakati muafaka ukifika na kutokana na matakwa ya jamii, kikiona nipewe jukumu lolote sitasita kutekeleza wajibu huo niwe au nisiwe mgombea.

Kwa hivyo, nilichozungumza jana ni kutoa maoni yangu kwamba muda umefika kwa Taifa letu kupunguza umri wa kugombea urais. Maoni yangu haya yanatokana na ukweli kwamba hakuna sababu zozote za kisayansi zinazomfanya mtu aliye chini ya umri wa miaka 40 akose sifa za kuwa Rais.

Msimamo huu nimekuwa nao tangu zamani nikisoma shule na haujawahi kubadilika. Hakuna mahala popote katika maoni yangu niliyotoa jana niliposema kwamba nataka umri wa urais upunguzwe ili nipate fursa ya kugombea nafasi ya urais. Pia siwezi kutaka katiba iandikwe kwa ajili yangu.

Vilevile kamwe isionekane kwamba matakwa ya muda mrefu ya vijana ya kutaka umri wa kugombea Urais kupunguzwa yanalenga kunipa fursa mimi kwani mimi ni binaadamu naweza nisiwe na sifa za kuwa Rais lakini kukawa na vijana wengine wengi wenye umri chini ya miaka 40 wenye Uwezo na Uzalendo wa kutosha kushika usukani wa nchi yetu.

Ni maoni yangu kwamba tupate mabadiliko ya vizazi katika uongozi wa nchi yetu ili kukabili changamoto za sasa zinazokabili Taifa letu.

Tunapojiandaa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya ni vizuri vyombo vya habari vikajikita kutoa taarifa bila kuweka tafsiri au kuwatafasiria maoni ambayo wananchi na viongozi watakuwa wanayatoa kuhusu maudhui ya Katiba Mpya.

Dar es Salaam29 Februari 2012

I second this!!

halafu huu urafiki wao ni mashaka makubwa!!

Kabwe akumbuke siasa za kitaifa zinaweza zikampotezea jimbo.
 
Makamba ni Kuwadi mkubwa wa Lowasa fisadi wa kutupwa. uzalendo anaojivalisha ni wakuwachezea tu watanzania. kama ndo unaanza kumtilia mashaka ZITo umechelewa maana sisi wengine tulishamsahau ndani ya makamanda halisi wa chadema
 
sio mbaya kushirikiana watu wa vyama tofauti kwy swala lenye mtizamo mmoja! ... Utofauti wa vyama sio vitaa! Peoplzzzz Poweeeeeer!
 
mkuu "uwezo tunao" umeongea kwa sauti mpaka unatia uvivu. Kila mtanzania ana nafasi ya kutoa maoni yake juu ya katiba mpya, play your part.
 
Katika watu wa chache wamaana na wenye uwezo wa kujenga hoja chadema iliyonayo zito yupo tena top 3 .huwezi mlinganisha zito na lema hata siku moja .
 
Back
Top Bottom