Zitto, Makamba wautaka urais?

hapo kwenye red, kama ndio hoja zinazowafanya waanzishe chama chao basi wana uzee wa fikra hata kama wao ni vijana wa umri, ila kama ni mtazamo wako, basi uwezo wako wa uchambuzi umekukwamisha

Sijasema wanaanzisha chama kwa sababu ya hoja hizo mbili basi. Lakini kumbuka mkuu itikadi ndizo huwaunganisha wanasiasa. Kama itikadi dhidi ya posho haiwezi kutekelezeka ndani ya CDM ama CCM ni kwa nini wasitafute magala pa kwenda kuitekelezea?
 
Zitto has for long been implicitly identifying himself as a loyal backer of JK and effectually standing by CCM. His comments regarding presidential candidate age limit be reduced to 35 just insinuate that he is prepared to defy Slaa's 2015 presidential ambitions. Even as a non-Chadema partisan, I am very worried by his eccentric behaviour and his salient pridefulness which, in the end, will sunder the party if can not be early addressed.
 
Nadhani hoja ya kupunguza umri wa kugombea Urais ni hoja nzito na ya msingi. hakuna haja ya kuweka age limit bali waweke vigezo vya uwezo wa kiuongozi na pia kukubalika na wapiga kura. Kuna viongozi wengi sana ambao wameweza kuyaongoza mataifa yao wakiwa na umri mdogo tu. Nyerere ni mfano wa hapahapa Tanzania, aliongoza harakati akiwa na umri mdogo na kuleta uhuru akiwa 39 tu.
 
Mkuu najua kuwa Watanzania wengi wanapata take home chini ya hiyo na wanaishi. Kama nisemayo ni sawa basi ina maana Watanzania wanaopata take home chini ya 700,000.00 wote ni mafisadi? Mkuu kwa maana nyingine Taifa la Watanzania limejaa mafisadi?
Mkuu Kimbunga, maisha ninayoishi mm kapuku huku kijenge juu! huwezi linganisha na maisha ya suti wnayoishi wabunge kama akina zitto kabwe! hata kama wote tunalipwa laki saba!
Ufisadi wao unakuja hapa: Wanaishi maisha ya kifahari halafu kipato kidogo!
 
Zito Kabwe umepata ujumbe, jchunguze ktk wacwac huu cku iktokea hakika utalaaniwa abadan kwan ulziba maskio ulvokumbshwa mguu xawa!Angalia vema ndoto zko zid ya watz!Mungu yupo ataexpose UKWELI cku 1!
 
Tanzania kuna tatizo kubwa sana la kasumba ya baadhi ya vijana tena waliozaliwa na kukulia katika mfumo wa siasa shindani kuwa na ushabiki wa kipuuzi baadala ya kuwa vijana wanaohoji,kusikiliza,kufikiri na kudadisi.
Mtu anafanya umbea wa nani ni rafiki yake nani.nani ni adui yake nani.Kwa kuwa na vijana kama huyu hakuwezi kulisaidia taifa zaidi ya kuwa ni mzigo na aibu.
Ndo maana hata baada ya Uhuru ,pamoja na kwamba Nyerere alijua kwamba waafrika walikuwa katika daraja la tatu katika upataji wa huduma,huku wahindi wakiwa daraja la pili,wazungu la kwanza.Kilichoangaliwa katika uundwaji wa Serikali ni uwezo,uzalendo na uadilifu na siyo uafrika.
Tambua tunatambulishwa na Utanzania wetu na siyo Uchadema wetu au Uccm wako.Chama ni jukwaa tuu la kisiasa,kiitikadi ambayo ni imani juu ya vitu.
Hata unavyotumwa na baadhi ya watu wanaofikiri kama wewe tumia akili yako siyo yao,kwasababu hujii kwanini umetumwa.
Nakerwa na vijana wanapokuwa washabiki wa ujing.
To me this might be a Psychological phenomena and God is in witness for the time like this.
 
mgheni amani;

unachohitaji kusaidiwa wewe ni kufundishwa ama kujuzwa mambo haya elimu ya siasa, elimu ya uraia, na ya utaifa; na ufundishwe vile vile tofauti zilizopo kati ya siasa za jukwaani, siasa ndani ya bunge na siasa nje ya bunge, na ujue mahusiano ama ushirikiano wa watu binafsi dhidi ya vyama ama itikadi zao. Kuna wakati mnaenda beyond limit sasa halafu mnalaumu tuuuuu.......... Alisema malcom x "i know the essence of brotherhood and i know what it feels like fighting for the right of your people but i'll stand and fight for those who recognise my efforts and those who appreciates it and here i need not applying the sense of brotherhood but the sense of togetherness" sasa kama wengine hawatambui ama wanadharau juhudi zake ana haki naye ya kushirikiana na wale wanaoheshimu juhudi zake hasa katika kutimiza yale yawapasayo katika taifa hilli....

hatuna haja ya kuwa na haraka sana katika hili ila bado nadhani chadema bado kama chama wanayosababu ya kusimamia maslahi ya taifa kama chama peke yao huku wakionesha uwezo na dhamira yao itakayofuatwa ili taifa lisonge mbele sasa nilisema naweka kumbukumbu kwa kuhofu tu ukaribu ulee ila maana ya kuweka kumbukumbu ni juu ya kulinda matukio ya baadae na kubainisha dalili zake tahadhari ni kitu muhimusana kwenye siasa hasa kwakuwa zinagusa maisha ya watu pia nikumkumbusha zitto kuwa makini pia kwani watu hawatarajii unyume kwenye msimamo ila tusubiri kila kitu kitakuwa hadharani kabla ya 2015
 
Kukataa posho ni ITIKADI?? Mimi nitakuwa kilaza katika hilo........ Ila kama hiyo ni definition ya itkadi toka katika Angle ya POSHO basi wanafaa kufanya kazi pamoja....

Kwa upande wangu sina tatizo na hao watu kuwa pamoja katika kazi zao ila there is something racking on this relationship, let's wait and find out...

Lakini wanasiasa tuache waitwe wanasiasa tu.....
Mkuu kwenye itikadi hapo; Zitto na January wana itikadi moja in common: Wote wanapinga posho za vikao ila hao makamanda wengine unaosema hawana nia thabiti ya kuzipinga posho.
 
Jamani wadau mimi ninawasiwasi sana na ukaribu na utendaji kazi wa Zito Kabwe yaana urafiki aliokuwa nao na wanamagamba unatia wasiwasi suala moja lakujiuliza kwanini asishirikiane na watu
kamaMnyika,lema,msigwa,kasulumbayi,mbilinyi na makamanda wengine huu ukaribu wake na wakina January na kigwangala hatusemi wawe maadui ila tu kisiasa ukifanyakazi na watu mnaotofautiana itikadi hasa ikiwa wapo wenzako ambao mnaitikadi sawa wengi tu unaoweza kufanyanao kazi inatia sana mashaka lakini pia kuna dalili ya agenda ya chinichini kuunganisha nguvu hii ni kwa maslahi ya naani? NAWEKA WAZI MASHAKA YANGU ILI KUWEKA KUMBUKUMBU VIZURI JUU YA HILI

Siasa siyo uadui ni mchezo wa kunadi sera zako na jinsi utakavyozitekeleza kwa wananchi baada ya siasa,ujamaa na undugu ruksa bila shaka.
So usiwe na hofu sana.
 
Kwa sasa Tanzania ina Ombwe la uongozi!

Uchumi wa nchi unayumba

rasilimali za nchi zinaporwa na wageni

mfumuko wa bei unatisha

elimu tanzania imedorora

mgomo wa madaktari bado haujatulia kwani tarehe 3/3 unaanza tena

Sasa nashangaa hawa vijana wa wili Mmoja kutoka chama cha ukombozi (CDM) na mwingine Chama dola (SISM).

Badala ya kutafakari mustakabadhi wa tanzania, wao wanawaza uraisi. mnataka uraisi ili mukawanyie nini watanzania wakati sasa mnashindwa?

Tatueni matatizo ya watanzania.

Zitto ulikuwa kamati ya Jaji Mark Bomani--- what is outcome?

January, umeme na gas vipi?

Acheni hizooo
 
I second this!!

halafu huu urafiki wao ni mashaka makubwa!!

Kabwe akumbuke siasa za kitaifa zinaweza zikampotezea jimbo.
 
si ni medani inayosimamia ushindani wa hoja miongoni mwa vyma na viongozi katika kujenga kukubalika kwa wanasiasa na vyama vyao.juu ya yote hayo msingi mkuu kwa makundi mbalimbali ya kijami ni uzalendo utii kwa nchi yao. hivyo basi urafiki wa watu wanaotoka makundi tofauti si haramu hata kidogo pale tu wanapokuwa na misimamo yenye maslahi mapana kwa wananchi na taifa kwa ujumla. kwa uono wangu makamba na zitto wamekuwa kwa nafasi tofauti watetezi wa wananchi katika majukwaa mbalimbali ambayo wamepata nafasi kushiriki katika midahalo au makongamano wakiwa pamoja au tofauti wamekuwa sauti ya wanyonge. waachane vijana wachangamane!
 
They scratch each others backs. Nothing more.

Huyo kijana wa GREEN BOOK anaona hana wa kumnyanyuwa sasa anamjaribu makamba na makamba anmjaribu kabwe.
 
Jamani wadau mimi ninawasiwasi sana na ukaribu na utendaji kazi wa Zito Kabwe yaana urafiki aliokuwa nao na wanamagamba unatia wasiwasi suala moja lakujiuliza kwanini asishirikiane na watu
kamaMnyika,lema,msigwa,kasulumbayi,mbilinyi na makamanda wengine huu ukaribu wake na wakina January na kigwangala hatusemi wawe maadui ila tu kisiasa ukifanyakazi na watu mnaotofautiana itikadi hasa ikiwa wapo wenzako ambao mnaitikadi sawa wengi tu unaoweza kufanyanao kazi inatia sana mashaka lakini pia kuna dalili ya agenda ya chinichini kuunganisha nguvu hii ni kwa maslahi ya naani? NAWEKA WAZI MASHAKA YANGU ILI KUWEKA KUMBUKUMBU VIZURI JUU YA HILI

Zitto keshapoteza mwelekeo.anatapatapa huku na kule kujaribu kupata attention.atazunguka CCM yote na kuhongwa na matajiri ili awasaidie kupayuka bungeni, lakini hamna kiongozi yeyote nje ya Chadema anayeweza kuwa rafiki au kumsupport.wanamtumia tu,wanamlipa then wanakula kona..January Makamba ni smart yule anamyeyusha tu zitto.Zitto kawa mpiga debe tu siku hizi.yuko against na kila kiongozi mwingine.kabakia kukimbilia media kila siku kupayuka.Juzi Mh Spika kaongelea issue ya posho za wabunge wakati akiwa jimboni kwa,Zitto wakwanza kutoa comments,Mh Raisi kaongea kidogo jana kuhusu wagombea Uraisi,Zitto huyoo katoa comments..lol..yuko against na kila issue ambayo viongozi wengine wanazipigania kwa maslahi ya wananchi.hii ni kwasababu Zitto yuko more after money na ushindani.Wakuu mwisho wa huyu jamaa hauko mbali..Naamini kabisa Chadema wanamjua ndo maana hatusikii hata siku moja viongozi wenzake wakilumbana nae.hata pale anapokuwa anawachokonoa ili wamjibu.wanampuuzia tu.Sifa kubwa ya kiongozi bora yeyote ni jinsi anavyoweza kushirikiana,kudumisha na kuimarisha umoja ndani yao.Ni kweli kabisa kwamba Zitto anauwezo wa kujenga hoja za maana lakini sio mtu wa kuweza kuongoza wengine.Team work kwake ni ziro.Ni mbinafsi,mwenye wivu,mchoyo,kigeugeu,anayependa siku zote yeye tu awe juu ya wengine..11
 
Tatizo kubwa la hii nchi kila mtu anawaza kuwa Rais na Mbunge..ukiangalia ukweli katika hawa wote wanaotaka hivyo vyeo hakuna Mzalendo hata mmoja wote ni watu wa Maslahi au la wachache sana wana uchungu na hii nchi!!! kwa kweli kuna shida kubwa sana tunayo sisi Watanznania...
 
zamani nilikuwa namwaminia sana zito lakini muda unavyo kwena naona hana tofauti na mzee wa kiraracha nahuko tunaekoenda atakuwa photocopy yake.
 
Jamani wadau mimi ninawasiwasi sana na ukaribu na utendaji kazi wa Zito Kabwe yaana urafiki aliokuwa nao na wanamagamba unatia wasiwasi suala moja lakujiuliza kwanini asishirikiane na watu
kamaMnyika,lema,msigwa,kasulumbayi,mbilinyi na makamanda wengine huu ukaribu wake na wakina January na kigwangala hatusemi wawe maadui ila tu kisiasa ukifanyakazi na watu mnaotofautiana itikadi hasa ikiwa wapo wenzako ambao mnaitikadi sawa wengi tu unaoweza kufanyanao kazi inatia sana mashaka lakini pia kuna dalili ya agenda ya chinichini kuunganisha nguvu hii ni kwa maslahi ya naani? NAWEKA WAZI MASHAKA YANGU ILI KUWEKA KUMBUKUMBU VIZURI JUU YA HILI
fundi wao ni mmoja , so kuvaa sare sare ni kawaida
 
Tanzania kuna tatizo kubwa sana la kasumba ya baadhi ya vijana tena waliozaliwa na kukulia katika mfumo wa siasa shindani kuwa na ushabiki wa kipuuzi baadala ya kuwa vijana wanaohoji,kusikiliza,kufikiri na kudadisi.
Mtu anafanya umbea wa nani ni rafiki yake nani.nani ni adui yake nani.Kwa kuwa na vijana kama huyu hakuwezi kulisaidia taifa zaidi ya kuwa ni mzigo na aibu.
Ndo maana hata baada ya Uhuru ,pamoja na kwamba Nyerere alijua kwamba waafrika walikuwa katika daraja la tatu katika upataji wa huduma,huku wahindi wakiwa daraja la pili,wazungu la kwanza.Kilichoangaliwa katika uundwaji wa Serikali ni uwezo,uzalendo na uadilifu na siyo uafrika.
Tambua tunatambulishwa na Utanzania wetu na siyo Uchadema wetu au Uccm wako.Chama ni jukwaa tuu la kisiasa,kiitikadi ambayo ni imani juu ya vitu.
Hata unavyotumwa na baadhi ya watu wanaofikiri kama wewe tumia akili yako siyo yao,kwasababu hujii kwanini umetumwa.
Nakerwa na vijana wanapokuwa washabiki wa ujing.
To me this might be a Psychological phenomena and God is in witness for the time like this.

Kumbuka Mwl nyerere aliyafanya yale kwa kuzingatia hali halisi ya wakati ule pamoja na mahitaji yake,pia wahindi na wazungu wa wakati ule walikuwa wazalendo.wa kweli.kumbuka wazee kama Habib jamal,Al noor kassum na Derek bryson.walikuwa wazalendo wa kweli kuliko wengi wa viongozi tulionao hivi sasa na hili halina ubishi.

Mimi binafsi namuona zitto kabwe kama Hamad rashid mwingine ndani ya CDM,na ianatubidi wana cdm tuwe makini naye sana.
 
By mgheni amani
Jamani wadau mimi ninawasiwasi sana na ukaribu na utendaji kazi wa Zito Kabwe yaana urafiki aliokuwa nao na wanamagamba unatia wasiwasi suala moja lakujiuliza kwanini asishirikiane na watu
kama Mnyika....

Acheni kumhukumu Zitto kwa hisia zenu za 'kichaga'. Juma lote lililopita mhe. Zitto alikuwa ziarani Tanga pamoja na mhe. Mnyika kwa juma zima. Hivi mnyika kawa CCM mara hii? Ni ushirikiano gani mnaoutaka nyie? Au mnataka zitto alale na mnyika ndo mseme, kweli sasa mhe. Zitto anatoa ushirikiano kwa wenzake? Shame on you!
 
Back
Top Bottom